singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 769
- 4,442
MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU
2hours of memories.
By
SINGANO JR
Kopi halisi ya kitabu kimeandikwa mwaka 2020 na kupitiwa upya mwaka 2021.
Haki zote zimehifadhiwa
ONYO
Hauruhusiwi kunakili ama kusambaza kitabu hichi bila idhini ya mwandishi
Jatua kali za kisheria zitachukuliwa.
NB:SIMULIZI HII NI YA KUTUNGA HAIHUSIANI NA NA MATUKIO YOYOTE HALISIA
VITABU VINGINE VYA MWANDISHI
MY DREAM MY FAVOURITE
UMOJA NAMBA TISINI NASABA (WARAKA WA RAISI WA MWISHO )
UMOJA NAMBA TISINI NA SABA(BOOK OF ALL NAMES)
BAADA YA ATHARI(MASAA M AWILI YA KUMBUKUMBU)
DREAMSI OF CODES(NDOTO ZA KIKANUNI)
Ni tabia kwa jamii nyingi za Kiafrika kuchukulia baadhi ya matukio katika jamii kama jambo la kawaida pasipo kuzingatia athari zake katika wakati ujao .
Simulizi ya MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU ni simulizi ambayo itakwenda kukuonesha ni kwa jinsi gani kunakuwa na athari pale tunapochukulia kila jambo linalotokea katika jamii kuwa la kawaida. Ungana nami mwandishi SINGANOJR katika simulizi hii ya kusisimua kabisa.
UTANGULIZI
CIA(Central intelligence Agency) ni idara shirikishi ya kiusalama ndani ya taifa la Marekani, inayofanya kazi kwa kukusanya taarifa zote za kiintelijensia ulimwenguni , taarifa zote hizo baada ya kukusanywa na kufanyiwa uchambuzi wa kina zinapelekwa kwa DNI(Director Of National Intelligence)na huyu DNI anapeleka moja kwa moja kwenda kwa raisi.
Ushawahi kujiuliza tofauti kati ya NSA na CIA basi jibu ni kwamba NSA ni kirefu cha NATIONAL SECURITY AGENCY ni moja ya chombo shirikishi cha kiusalama ndani ya serikali ya Marekani kinachohusika na kukusanya taarifa za kiintellijensia kama ilivyo kwa CIA ila utofauti ni kwamba CIA inahusika na ukusanyaji wa taarifa katika mataifa ya nje (International Intelligence) ambazo ni husianishi , au kwa maneno mengine taarifa ambazo zinahusisha Marekani moja kwa moja au kwa njia isio ya moja kwa moja na hawa CIA wanafanya kazi kwa kusambaza mawakala(Agents) kila kona ya dunia , na hawa ndio wanakusanya taarifa hizo na kisha kuzituma makao makuu ya CIA ambayo yapo Lengley, Virginia na hawa mawakala wanaruhusiwa kushirikiana na vyombo vingine vya kiintelijensia katika kukusanya taarifa zao, kwa mfano MOSSAD, M16 na mashirika mengineyo.
Sasa ukija kwenye NSA ni kwamba misheni au kazi ya hii idara ni kuhakikisha kila intelijensia inayotumwa au inayotoka ndani ya CIA au nje ni ya uhakika, na wanahakikisha taarifa kwa kuvunja vunja kwa kutumia matarakishi yenye teknolojia ya hali ya juu kabisa ambayo yana ulinzi mkubwa.
Yaani ndani ya hiki kitengo mambo yote ya udukuzi wa taarifa na mengineyo husianishi na hayo yanafanyika , kwa hio kila taarifa inayofika hapa mara nyingi inahakikiwa na kutafsiriwa na baada ya hapo ndio inafanyiwa maamuzi .
Kwa hio hawa agent wa NSA sio wadhurulaji kama ilivyo kwa CIA agent, hawa kazi zao wanazifanya wakiwa wamejichimbia katika makao makuu yao yaliopo huko Fort Maede ,Meryland.
CIA hii yenyewe ilianzishwa mwezi wa Tisa mwaka 1947 huku NSA ikiundwa mwezi wa kumi na moja mwaka 1962.
NSA imegawanyika katika makundi mawili kutokana na misheni zao , kundi la kwanza linafahamika kwa jina la SID kirefu chake ni Signal Intelligence Directorate halafu kundi la pili ni IAD yaani Information Assurance Directorate , Kundi la kwanza yaani SID kazi yao kubwa ni kutengeneza taarifa zilizokuwa katika mfumo wa mawimbi ya kieletroniki au mfumo ambayo imetumika kama target, yaani kwa mfano mawasiliano, Rada na mifumo yote ya siraha sasa hawa SID ni kuangalia nia na matendo ya taarifa hizo zinahusianaje au zina athari gani kwa Taifa, yaani kwa mfano wanaweza wakapata taarifa yoyote ile kwa kutumia njia ya kimitandao yaani tuchukulie labda unapanga tukio la kigaidi halafu mawasiliano ya mipango unafanya kupitia mitandao , sasa hawa wajuba kazi yao ni kutafuta hizi taarifa.
Sasa baada ya SID kukamilisha kazi yao hawa IAD kazi yao ni kulinda mifuno ya nchi ya kitaarifa .yaani hawa wanazuia wadukuzi kwa kuboresha mifumo yao ya kitaarifa , na unaambiwa mifumo ya ulinzi wa taarifa ya kimarekani ndani ya NSA inakuwa updated kila baada ya sekunde ili kutoruhusu mwanya wowote wa leakage au udukuzi.
CIA yenyewe imegawanyika katika makundi makuu manne kutokana na misheni zao au kazi ndani ya kitengo kuna kundi la kwanza hili linadili na taarifa za site (sehemu husika)duniani kote kundi hili linafahamika kama Directorate of Intelligence, kundi lingine ni National clandestine kazi yake ni kuandaa lakini pia kuongoza misheni zote za siri, Directorate of support hili nalo kazi yake kubwa ni kutoa sapoti kwa makundi yote matatu na mwisho kuna Directorate of Science and Technology humu sasa ndio kuna maswala ya kiteknolojia katika janja zote .
Sasa hizi idara zinafanyake kazi , jibu ni kwamba kuna wakati hawa NSA wanapata intel(Taarifa) kupitia mitandao sasa baada ya kuipata tuchukulie labda intel hio wameipata katika mawasiliano ya Iraq na Pakistan , Sasa unakuta kuna muda wanataka kuihakiki hii taarifa au ifanyiwe kazi ndio hapo sasa watawahitaji CIA , kwa hio kuna muda hii NSA inashirikiana kwa ukaribu zaidi na FBI pamoja na CIA .
Sasa kama nilivyokuonesha muundo huu wa kiintelijensia wa taifa la Marekani turudi sasa kwenye simulizi yetu .
****
Lengley, Virginia CIA HQ, 2021 FEBRUARY 0800Am
Ilianza kama siku tulivu ndani ya makao makuu haya , ambayo yalikuwa na pilika pilika za kiusalama, kwani kila mfanyakazi alionekana kuwa bize kuhakikisha kila mtu anatimiza majukumu yake , kama ilivyokuwa moja ya falsafa kwa wazungu “muda ni mali” basi kwa pilika pilika hizo waliendana na falsafa yao hio .
Basi asubuhi hio ndani ya ofisi ya DCI`s(Director of the Intelligence Agency) alionekana bwana George crispian mkuu wa kitengo cha Directorate of science and Technology akiwa ameambatana na Jane Smith mkuu wa kiitengo cha Directorate of Intelligence , wote asubuhi hio walionekana kuwa na jambo la muhimu la kuripoti kwa mkuu huyo wa CIA bwana Luis Tenet .
Jambo walilokuwa wanazungumzia asubuhi hio ilikuwa ni juu ya misheni iliopewa jina la Dragon X Trail , misheni ambayo ilikuwa ikienda kufanyika nchini Tanzania.
Mbele ya meza hio kubwa iliokuwa imezungukwa na watu wa tatu juu yake kulikuwa na fomu ama bahasha tatu ambapo kila bahasha ilikuwa na taarifa iliokuwa jumuishi juu ya misheni Dragon X, bahasha namba moja ilikuwa na taarifa kutoka NSA , fomu hii au bahasha ilikuwa imebeba taarifa ya picha, hapa nazungumzia picha kama picha, na picha hizo zilikuwa zikizionyesha ubongo wa binadamu , lakini pia zilikuwa zikionyesha pia Screenshot ya jumbe za meseji kupitia mtandao wa Watsapp, jumbe hizo zilikuwa zikitoka kwa Profesa au daktari ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenda kwa mkuu (CEO) wa kampuni ya kitehama ifahamikayo kwa jina la EARTH TECH INC, kampuni iliokuwa na makazi yake ndani ya Taifa la Tanzania mkoani Arusha.
Fomju ya pili ambayo hii sasa haikutoka NSA bali ilikuwa imetoka ndani ya CIA na ilikuwa imewasilishwa kwa DCI na mkuu wa kitengo cha Directorate of intelligence yaani Bi Jane Smith, Fomu hii ilikuwa imejaa nyaraka zenye taarifa kutoka kwa Undercover Agent(wakala) kutoka Tanzania(jina halikutajwa).
Fomu ya tatu hii ilikuwa ipo kwenye meza ya mkuu wa CIA ndani ya fomu hii juu kabisa ya ukurasa wa kwanza kulikuwa na maandishi ya DRAGON X TRAIL MISSION APPROVAL ikiambatana na neno Confidential , fomu hii ilikuwa imetoka kwa Raisi wa USA kupitia ofisi ya DNI kwenda kwa CIA.
Sasa basi ndani ya ofisi watu hao walionekana kujadili jambo , lakini baada ya kama nusu saa hivi , waliongezeka watu wawili watu hawa walikuwa ni wakuu wa vitengo viwili yaanni Directorate of support pamoja na ile ndogo kabisa ya Directorate of clandestine .
Walikuwa wote ni wanaume na baada ya kuungana , walionekana kuwa katika kikao na mwisho wa kikao walionekana walikuwa wakijadili mtu ambae anakwenda kuiongoza misheni hio ya DRAGON X TRAIL.
Lakini kati ya wale watu wawili walioingia ndani ya ofisi hio kwa kuchelewa mmoja alionekana kutoa faili na juu ya hilo faili likuwa na nembo kubwa ya alama ya UMOJA NAMBA TISINI NA SABA yaani U-97 na faili hilo lenyewe likiambatana na neno CONFIDENTIAL
Hii misheni ni nini haswa , kwanini ifanyiwe ndani ya Taifa laTanzania , jibu la jambo hilo linakuja kupitia tukio ambalo ndani ya Taifa lilionekana ni tukio la kawaida kabisa kutokea katika jamiii , lakini kumbe ni jambo ambalo lilikuwa limebeba athari kubwa kwa jamii ..
Tukio hilo linakwenda kwa jina la MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU ni tukio la kusisimua lililotengeneza sababu ya kuundwa kwa misheni iliofahamika kwa jina la DRAGON X TRAIL.
Lakini ni tukio ambalo lilipelekea kufichuka kwa siri kuu ya UMOJA NAMBA TISINI NA SABA siri ya kitabu cha BOOK OF ALL NAMES
Huo ni utangulizi wa kitabu changu kinacho enda kwa jina la MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU.
Sasa kwa wewe ambae ushakwisha kusoma UMOJA NAMBA TISINI NA SABA (waraka wa raisi kabla ya kifo ) basi nakuomba usome na tukio lililotokea katika kitabu cha MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU ili upate maana halisi ya ya code name U-97 je ni nini maana halisi ya hilo neno , je kuna umoja huo kwenye jamii au duniani kwa ujumla wake basi usisite kusoma.
Mambo makuu mawili utakayo yapata kuyajua katika kitabu hiki ni pamoja na jinsi gani mashirika makubwa ya kimitandao yanavyokagua mawasiliano ya wateja wao wote dunia nzima .
Utapata kujua nini nini kiligunduliwa katika BLUE BOOK project, pia utakuja kugudnua namna projekti hio ilivyo changia uundwaji wa project ya TOP ON FILE project iliokuwa ipo chini ya STAR LABS pamoja na IBM .
Je, unataka kujua ni nini kilichonyuma ya DRAGON X TRAIL MISSION hakikisha haukosi kusoma
NB kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa njia ya softcopy (PDF,DOC and EPUB) kina season 1&2 kila season ina vipande 50 kila episode inapatikana kwa bei ya ofa 4000 tu mpaka kesho kutwa ambappo itapatikana kwa kila season 6000
Lipia kupitia namba 0687151346 jina ISSAI SINGANO ukishalipia nitumie
SEHEMU YA 01
Ni siku ya ijumaa , siku ambayo Ilikuwa imetawalia na jua kali sana ndani ya wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga ,wilaya hii ilikuwa imetawalia na eneo la tambarare kwa ukubwa wake , licha ya baadhi ya maeneo kuwa na misitu na baadhi ya miti ,lakini kwa maeneo ya mjini hayakuwa na miti mingi sana masalani katika pembe ya barabara kuu iliokuwa ikiunganisha mkoa wa moshi –Arusha na Pwani – Dar es salaam .
Wilaya ya korogwe ni wilaya ya pili kwa kuwa na maendeleo ya wastani , ukiachana na wilaya ya Tanga mjini ambako ndio makao makuu ya mkoa .
Pembezoni mwa barabara hiyo iliyokuwa ikiunganisha mkoa wa Tanga ,Arusha na Dar es salaam alionekana kijana mmoja akiwa anatembea kwa unyonge sana huku akionekana akiwa amechoka sana ukizingatia na jua lilivyokuwa kali ilikuwa ni zaidi ya taabu mbele ya barabara hio huku mgongoni akiwa amebeba mfuko mmoja mdogo ambao ulionekana kuwa mifuko ya zamani sana , mifuko hii ilikuwa ukiubeba mgongoni huku ukiwa na kamba ambazo zilitumika kama mikanda ya begi na ndani ya mfuko huo alionekana akiwa amebeba nguo .
Licha ya kijana huyu kuonekana akitembea barabarani lakini hata mavazi yake yaliwakilisha kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake , alitembea kwa umbali mrefu kidogo mpaka akafika sehemu moja iitwayo Mwembeni sehemu ambayo ndio anaingia mjini Korogwe.
"Hapa sina hata hela ila lazima nifike jijini Dar kwa njia yoyote ile , pia nitakula nitashiba ngoja uone, kwanza nikale kwenye kibanda kile mgahawani pale”.
Aliwaza yule kijana huku akikisogelea kibanda kwa kujiamini kabisa na wakati huo hakuwa hata na shilingi mia mfukoni zaidi ya mfuko wake wa kubeba mgongoni.
Baada ya kufika ndani ya mgahawa ule alitafuta meza ambayo kuna mzee mmoja nae alikuwa akipata chakula .
"Mzee shikamoo!"
"Marhaba kijana" Aliitika huku akiendelea kula na hakutaka maongezi zaidi kwani kwa muonekano wa yule kijana aliona kabisa kaja eneo lile kwa ajili ya kumuomba hela ili na yeye apate chakula ,kwani mara nyingi alizoea kuona vijana wengi wenye tabia hiyo kuja sehemu ile na kuomba hela.
“Karibu kaka nikuletee chakula gani?"Aliongea muhudumu.
“Weka msosi kama anao kula huyu mzee " Aliongea vile makusudi maana aliona huyu mzee kama alikuwa akidhania kuwa atamuomba hela kwa hio aliagiza vile ili kumkomoa.
“Kaka chakula chake hicho ni elfu kumi utaweza kulipa?"
“We muhudumu mteja si kakuagiza ,we lete kama alicho omba unahoji maswali ya nini" Aliongea yule mzee huku akitaka kuona kweli kama atamudu bei ya chakula.
Ndani ya muda mfupi muhudumu aliweka chakula kwenye meza na jamaa huyu bila ya kupoteza muda aliamka na kunawa mikono na kuanza kula msosi huu kwa mbwembwe zote mpaka akamaliza , huku yule mzee aliekuwa akila chakula bado alikuwepo pale pale kwenye ile meza akichati na simu yake kubwa na yote alifanya vile kutaka kuona kama huyu kijana ataweza kulipia kile chakula , maana ukizingatia jinsi mavazi yake yalivyo chanika chanika halafu ale chakula cha zaidi ya elfu kumi ilikuwa nikichekesho na alitaka kuona mwisho wake.
Kijana baada ya kumaliza kula chakula kile aliagiza maji ya buku ya uhai na kisha akanywa kidogo na pale pale yule muhudumu alikuja kwa lengo la kuchukua hela .
Lakini kabla hajakaribia meza waliokuwepo aliitwa na mteja mwingine kwa ajili ya kuchukua hela . "Mzee " Aliita yule kijana na yule mzee akaangalia na kuitika lakini cha kushangaza yule kijana alifumba jicho moja kwa sekunde mbili na kisha kuliachia .na bila ya kuongea chochote alinyanyuka na kuchukua maji yake na kutoka ndani ya ule mgahawa lakini wakati anakaribia kutoka mara yule muhudumu alimwita.
"Wee kaka mbona hujalipia na unataka kuondoka?"
" Nishamwachia yule mzee hela na inayobaki tumia mrembo ee"Basi yule dada alimfuata yule mzee na kumuomba ampe hela alioachiwa na kumbuka kijana hakutoa hela yoyote pale zaidi ya kula na kuondoka.
"Anhaa kweli kaniachia elfu ishirini na inayobaki kasema.. inayobaki tumia mremboo" Aliongea yule mzee huku akitoa walleti kitu kilichomshangaza yule muhudumu maana hela katoa kwenye walleti lakini hakutaka kujihangaisha sana zaidi ya kupokea na kufurahia kwani yule kijana alikuwa ametumia elfu kumi na moja kwa hio ilio baki ilikuwa elfu tisa .
Yule mzee baada ya masaa mawili kupita alijikuta akiwa amekaa pale pale hotelini lakini ni kama mtu alierudiwa na kumbukumbu.
"Duuh! hivi yule kijana alilipa ?" alijiuliza huku akinyanyuka na kumfata yule muhudumu na kumuuliza. " Ndio alilipa mbona tena hela alikuachia wewe au ushasahau na kanipa mpaka chenchi".
"Unasema hela nimetoa mimi?" Aliuliza yule mzee kwa mshangao "Mhmh ndio mzee tena hela si umetoa kwenye walleti yako wewe?"
Yule mzee bila kujiuliza alitoa waleti yake na kuanza kuhesabu hela zake lakini alijikuta akipagawa maana ni kweli kuna upungufu wa shiringi elfu ishirini.
"Umesema ameondoka saa ngapi?"
"Muda mrefu kama masaa mawili yaliopita "
"Duuh! ..basi asante kwa chakula " Alisema yule mzee huku akijikuta akipata mfadhaiko kwani hela yake kamlipia yule kijana huku akiwa hana kumbukumbu ya aina yoyote ile .
"Daah! leo nimeumbuka yule dogo lazima atakuwa mchawi yule sio bure , ila siku nitamkamata tuu hela yangu haiendi buree , ila atakuwa yupo vizuri maana kama ni chuma ulete asingeniweza nimezindikwa vya kutosha na pia hirizi yangu ipo kiunoni iweje ameniweza?"
Yule mzee alikubaliana na yalio mtokeo na kuondoka zake ...... yule kijana ni nani ? swali hilo likabaki kwenye kichwa chake.
**********
1995 -DAR ES SALAAM 1800hours PM
Katika moja ya maeneo ambayo yanasifika kama sehemu(Neighbourhood) ambazo matajiri wengi huishi ndani ya jiji la Dar es salaam ni Masaki na Osterbay , na hili sio kwa hapa Tanzania tu lakini pia kwenye nchi nyingi na majiji makubwa huwa na maeneo ambayo yamejitenga kama maeneo ambayo wanaishi walio nazo kwa mfano tu China kuna Central park hii ni moja ya sehemu ambayo inaaminika matajiri wengi wanaishi , kwa hio sio jambo la kushangaza sana ,nijambo la kawaida kwa watu kuonesha uwezo wao wa kipesa pale wanapokuwa nazo , yapo maeneo mengi ndani ya majiji tofauti makubwa duniani ambayo matajiri wengi wamejitenga na watu wa vipato vya chini.
Ndani ya eneo hili la Masaki wakati familia nyingi zikiwa ndani ya mageti yao katika maeneo haya tulivu ,kuna familia moja ambayo haina muda mrefu tangu ihamie maeneo hayo alionekana dada mmoja ambae alikuwa akisukumiwa nje na mlinzi wa nyumba hio baada ya kupata maelezo kutoka kwa bosi wake huyo ambaye alifunga ndoa hivi karibuni na kuhamia maeneo hayo ya ushuani, kwani baba yake alikuwa tajiri mkubwa aliekuwa akihusika na biashara za usafirishaji wa mizigo (Cargo Transit And Swift Logistic Company) kampuni ambayo ilikuwa ikisifika sana kwa usafirishaji wa mizigo ambayo makao yake makuu yalikuwa maeneo ya mikocheni nyuma kidogo kabla hujakaribia jengo la Airtel ambalo kwa miaka hio ya tisini jengo hilo halikuwepo.
Na moja ya wafanyakazi wa kampuni hio ni kijana Samiri ambae alikuwa ndio CEO(Mkurugenzi mtendaji ) wa kampuni hio huku baba yake akiwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hio kubwa Africa Mashariki.
Tukirudi huku Masaki baada ya mwanadada yule kufukuzwa alijikuta akilia sana huku akianza kukumbuka siku alio kutana na Samir katika biashara zake za uchangudoa lakini kutokana na matakwa ya mteja wake kutotumia kondomu basi alijikuta akibeba ujauzito bila mategemeo .lakini kama ilivyokuwa kwa wadada wengi wapatapo ujauzito wa kutotarajia basi huwa wanachukua maamuzi ya kutoa mimba hizo na wazo hilo lilimjia Irene mwanadada ambae alipata ujauzito kutoka kwa Samir lakini kilicho muhuzunisha na kuchukua maamuzi ya kuicha mimba ikue ni baada ya kuambiwa na daktari wakati akitaka kutoa mimba hio kwamba kama atatoa mimba hio kuna aslimia tisini za kutoweza kupata ujauzito tena na asilimia kumi za kupata ujauzito tena ndipo daktari alipo mshauri kwenda kujifikiria kwanza kama atoe ujauzito huo asipate mtoto maisha yake yote ama auche ..ulikuwa ni uchaguzi mgumu sana kwake ukizingatia na hali ya maisha alio kuwa nayo, alijikuta akilia sana usiku mpaka alipo kuja kuamka na kupata wazo la kumtafuta mtu alie mpa ujauito huo kuona kwamba ni kipi atamwambia , kama angeweza kukubali uja uzito huo.japo alikuwa na uhakika mdogo sana wa kukubaliwa na huyo mwanaume alie mjua kwa jina la Samir kwani alijulikana sana kwa utajiri alio kuwa nao pamoja nakupenda maisha fulani ya kuonekana pamoja na kununua dada poa kila anapojisikia .
Irene hakupata shida kupajua sehemu anayoishi Samir alifanikiwa kufika nyumbni hapo na aliruhusiwa na kuingia ndani na kumkuta Samir na mke wake shani ambae licha ya kuwa wachumba wa muda mrefu ndio walioana siku chache tuu zilizo pita ,baada ya Irene kumkuta Samir, Samir kwanza alishtuka kwani anamkumbika vizuri Irene japo hakumfahamu jina ila alimkumbuka kwa kumnunua na kulala nae hotelini.
"Samahanini jamani kwa kuwaingilia na jioni hii " Aliongea Irene
"Hakuna shaka karibu" Walimkaribisha Irene aliekuwa akiendelea kushangaa mandhari ya kuvutia ya nyumba hio na kujisemea kuwa kuna watu wanaishi sehemu nzuri sana.
" Ninamazungumzo na wewe kaka "
" Okey hapa au nje ya hapa " Aliongea Samir
"Hata hapo nje tafadhari" Basi Samir alitoka na irene mpaka nje kwa ajili ya mazungumzo huku mke wake japo alitamani kusikia kilichokuwa kinakwenda kuongelewa ila alijikuta akikubaliana na mume wakekuongea na Huyo mwanamke.
" Nadhani unanikumbuka vizuri ?" Alianzisha maongezi Irene
" Ndio sura yako inakuja kuja hivi "
"Sitaki kwenda mkato mkato nimekuja sio kwa ajili ya kukubebesha hili swala ila nimekuja unipe ushauri na kama utapata moyo wa kunisaidia maana hapa nilipo nimwchanganyikiwa sijui cha kufanya ."
"Mbona unanitisha dada jambo gani hilo?"
"Siku ile ulivyokuja kupata huduma kwangu kama unakumbuka ulikataa kutumia kondomu na mimi sikutarajia lakini nimepata ujauzito wako"
"Whaat!!!.., wewe dada una kichaa?" Aliongea Samir kwa mpayuko ulio sababisha hata mke wake alie kuwepo sebuleni kuja kuangalia kinacho endelea .
"Mume wangu nini tena?"
"Shania hakuna kitu mke wangu kuna jambo limenishangaza hapa”
" Mhmh haya " Shania alirudi ndani na kuwaachaa
Lakini samir pale pale alienda mpaka getini na kumuita mlinzi aitwae Juma
"Wewe juma unaruhusu je watu wa ajabu ajabu wanaingia nyumbni kwangu " alisahau kama yeye mwenyewe ndo alimruhusu”.
" Bosi samahani sitorudia tena " Juma alijibu na kuomba msamaha japo hakufanya kosa
" Sasa sikia nenda kamtoe pale kimya kimya mke wangu asijue haraka sana , usilete watu vicha vichaa ndani kwangu"
Juma bila kupinga oda ya bosi wake alikwenda kumburuza Irene kimya kimya na kumsukumia nje ya getii"
Samir alijikuta akipata hasira na wasi wasi juu ya jambo lile haraka haraka aliingia chumbani kwake na kuvuta droo na kutoa kiasi cha pesa huku mke wake akimuangalia tu
" Mume wangu unapeleka wapi hizo pesa ?"
"Subiri nakuja kukuhadithia mke wangu “ huku akitokà nje
" Juma yuko wapi?"
“Nishamtoa nje "
"Sikia hebu nifungulie haraka haraka " Juma alifungua na na Samir akatoka nje na bahati ni kwamba Irene hakwenda mbali.
"Sikia we kahaba naomba usije ukakanyaga nyumbani kwangu kuanzia leo sitaki kujua unacho ongea ni cha kweli ama uongo , shika hii pesa utajua mwenyewe cha kufanya " Aliongea Samir na kumtupia zile hela chini.
"Irene alijikuta akilia sana ila upande mwingine alipata nafuu baada ya kupata zile hela kwani pia haikuwa nia ya yeye kwenda kukubaliwa kwa mimba ile ila alitaka tu kubahatisha kama anacheza mchezowa bahati nasibu,maana ni naninagekubali mimba ya mwanamke anajiuza.
“Samahani sana kaka kwa kusababishia mawazo na kukukosesha amani lakini jisikie huru kabisa sikuja kukuambia tulee hii mimba ila nimekuja unipe msaada wa kimawazo , lakini nakuhakikishia hii mimba nitaelea lakini hakika mwanangu hatokuja kujua kama wewe ndio baba yake japo huo ndo ukweli kama hii mimba ni yako naomba usahau kuhusu hili nitaitumia hii pesa kama moja ya matumizi kwa mwanao atakapo zaliwa kwaheri" Aliongea Irene maneno hayo na akaondoka zake huku Samir nae baada ya kumwangalia mwanadada huyo mpaka alipo yokomea ndipo akaondoka zake.
SEHEMU YA 02
Irene baada ya kurudi kwenye chumba chake alicho panga maeneo ya Sinza alifungua zile hela na kuanza kuzihesabu na kuzikuta ni milioni mbili na hamsini kwanza alishukuru sana kwa hela ile na kuona ni msaada mkubwa sana ambao amepata , ndipo alipoamua kuacha biashara yake ya kujiuza na kuanzisha biashara ya kuuza mkaa katika eneo la Tegeta mbuyumi biashara ambayo ili muwezesha kujipatia kipato huku kiasi kidogo alicho kuwa akipata akitunza benki kwa ajili ya mwanae atakae jifungua ,basi hatimae baada ya miezi tisa alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume aliempa jina la Peter.
Mtoto Peter maendeleo yake ya ukuaji hayakuwa mabaya na hatimae alifikisha umri wa miaka sita alianzishwa shule darasa la kwanza, siku zilizidi kusonga hatimae Peter alifikisha darasa la saba ndipo mama yake Irene alipopata ajali ya kugongwa na gari ilikuwa ni ajali moja yakusikitisha sana kwani alifia hapo hapo lakini kilicho washangaza wengi ni mazingira halisi ya ajali hio kwani ni kama mgongaji alidhamiria kumgonga mama Peter kwani baada ya ajali hio kutokea gari halikusimama na wala namba za gari hakuna alieweza kuziona .
Ilikuwa ni ajali mbaya sana ajali ambayo ilimfanya Peter kuwa yatima kwani mama yake alishawahi kumwambia kuwa baba yake alikwisha kufariki , mtoto Peter alilia sana na kuhuzunika kumpoteza mama yake hasa kwa wakati huo ambao bado alikuwa bado akimuhitaji sana kwani ndo kwanza alikuwa darasa la saba , majirani walimuonea sana huruma Peter , walijitahidi sana kumfariji lakini kumfariji huko hakukuzaa matunda ,lakini haikuwa na jinsi kwani tayar mama amekwisha kufariki.
Basi baada ya siku chache Irene au Mama Peter alipumzishwa katika makabuli ya Sinza.
Basi maisha kwa mtoto Peter yaliendelea na uzuri ni kwamba mama yake alikuwa alimuwekea pesa benki basi Peter hakupata shida sana ya matumizi na baada ya miezi kadhaa kupita Peter alifanikiwa kumaliza darasa la saba ndipo alipo anza kuendeleza biashara ya mama yake ya uuzaji mkaa huku mara nyingi pesa alio kuwa akiipata aliitunza kwani bado alikuwa na safari ndefu ya kusoma na kutokana na msaada wa majirani zake basi walimfanya Peter asijisikie kuwa mpweke sana.
Basi baada ya miezi kadhaa matokeo ya kidato cha kwanza yalitoka huku Peter akiongoza katika somo la hisabati na sayansi kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kupata A kwa kila somo ilikuwa ni habari njema sana kwa kijana Peter na kwa wale ambao walikuwa wakimpenda, lakini bahati pia ikamwangukia Peter kwani wanafunzi wote ambao walifanya vizuri katika masomo ya sayansi walipata ufadhili chini ya kampuni ya R&J foundation kwa kuwalipia ada wanafunzi hao pamona na matumizi kwa kipindi chote cha masomo, na moja ya wanafunzi walio pata ufadhili wa masomo hayo alikuwa ni Peter huku sheria ya mkataba huo ni kusomea katika shule za serikari ama za jeshi kwa shule yoyote ile yenye bweni.
Kwa upande wa Peter baada ya kwenda ofisini kwa ajili ya kukamilisha usajili wa ufadhili huo alikutana na mwanamama mrembo ambae japo umri umeenda lakini alionekana kama kijana kwa uzuri wake pamoja na mavazi aliovaa yalikuwa ya bei ghari.
Basi Peter alikaribishwa vizuri na kujieleza pamoja na historia yake , na baada ya hapo alichagua shule ya Makongo sekondary lakini akikataa kukaa hostel kama sheria za ufadhili huo.
“Kukaa hostel za shule ama kutokaa bado hakutakuwa na mantiki kama tui mwanafunzi mnae mfadhili hatafanya vizuri katika masomo yake , mimi naona nitafanya vizuri zaidi kama nitakaa nyumbni na kwenda shuleni asubuhi"
“Okey ni sawa lakini lazima uelewe kwamba kama itatokea umefanya vibaya katika masomo yako basi tutaacha kukufadhili "
" Hakuna shida " Peter alifurahi sana na hatimae mwezi wa kwanza alianza kusoma katika shule hio ya Makongo shule ya jeshi iliopo kati ya Mbezi beach na Mwenge ndani ya eneo la Lugalo. .
********
Tukirudi kwa kijana tuliemuona Korogwe baada ya kutoka mgahawani pale alichukua barabara kuu huku akidhamiria kutafuta stendi ya mabasi ,kwani alipo uliza aliambiwa stendi utaipata mbele huko, ndipo alipoamua kunyoosha pasipo kujali jua ambalo lilikuwa likimuwakia alitembea huku akipoozea na maji alio chukua pale mgahawani
"Japo Mungu hakunijaalia uwezo wa akili lakini alichonipa namshukuru Asante Mungu nimeshiba"Aliongea huku akizidi kusonga mbele mpaka akafikia eneo moja liitwalo Majengo ndipo alipo msimamisha mtu na kuuliza stendi ya mabasi .. baada ya kuelekezwa alifuata barabara hio hatimae aliingia stendi, lakini wakati anatembea aalikuwa akiyafikiria mausia alio kuwa akipewa na mama yake kabla hajafariki.
"Mwanangu najua una uwezo wa kumpumbaza mtu kwa muda mfupi na kumfanya afanye kile ukitakacho lakini isiwe chanzo cha wewe kuanza kuwadhulumu watu mali zao na kufanya uhalifu , hakikisha unajipatia kipato kilicho halali , shida zako zisikufanye ukiuke sheria za ulimwengu kumbuka hiko ulicho jaaljwa na Mungu ni kama zawadi ila sio siraha ya kuwachapia watu "
Hayo ni maneno ambayo kijana huyu ambaye bado hatujapata kumjua jina akiyakumbuka maneno ambayo aliusiwa na mama yake kipenzi kabla ya kupatwa na umauti.
"Mama nisamehe sana ila sina jinsi lazima ni utumie uwezo wangu nilio nao ili nifikishe Dar kutafuta maisha."
Aliongea kijana huyu na wakati huo akiingia stendi hapo,moja kwa moja aliinyoosha kwa wakata tiketi na kudhamiria kukata tiketi lakini wakati huo hakua hata na shilingi mia mfukoni zaidi ya mavazi yake yaliochakaa huku baadhi ya sehemu zilionekana zimechanika.
"Dogo unaelekea Dar?, njoo nikukatie tiketi chapu gari linafika sasa hivi" Aliongea moja ya watu wanao kata tiketi kama unavyojua mbwembwe zao , lakini kilicho mfurahisha kijana huyu ni mkataji tiketi yule kutombagua kutokana na mavazi yake.
"Dogo unaitwa nani?
"Unasema?"
"Jina lako nani?"
"Naitwa bahati masumbuko"
" Dogo kweli wewe kwa muonekano wako masumbuko kakuzaa kwa bahati "
"Hata mimi naona broo”
"Poa toa hela chapu tiketi yako hii hapa na gari lile ndo linaingia"
"Broo.." Aliita kijana huyu ambae jina lake ni Bahati masumbuko na pale pale akachezesha jicho lake kwa staili ya ajabu kama vile anakukonyeza
"Dogo shika tiketi yako nilisahau kumbe ulianza kutoa pesa"Aliongea yule jamaa huku Bahati akipokea tiketi yake na kwenda kupanda gari.
"Nisamehe sana broo mimi sio mchawi ila inanibidi kufika Dar kutafuta maisha nitakuja kukulipa" Alijiongelesha mwenyewe Bahati huku akiingia ndani ya basi.
Baada ya Masaa mawili yule mkata tiketi alijikuta kama anatoka usingizini kwani ndo anakumbuka kuwa yule dogo hakutoa pesa na gari ishaondoka
"Yule dogo nilimuachia achia je au mchawi , ngoja nimpigie Ayubu achukue hela aache uhuni( Ayubu ni konda) au alilinipa sikumbuki” Huku akitoa simu na kuanza kupiga .
Simu ilimshtua Ayubu ambae alikuwa bize akiangalia movie ya Majuto kwenye Tv ya gari aliichomoa na kuweka sikioni baada ya kuona ni rafiki yake
"Oya mzee kuna dogo sijui nimemuachia achia vpe nimemkatia tiketi lakini hela hajatoa anaitwa Bahati Masumbuko hebu fanya mpango uichukue"
"Una uhakika hajatoa au umesahau. Kama ametoa?"
"Nina uhakika ila sikumbuki vizuri"
"Sasa una uhakika halafu hukumbuki vizur jibu sahihi ni lipi ,ndo maana nakwambia uache kuvuta bangi mchana wewe"
"Oya Ayubu hebu muulize tuu kama amenipa au hajanipa? "
"Poa ngoja nimcheki"
Konda wala alikuwa anamkumbuka vizuri bahati kutokana na muonekano wake wa mavazi halafu isitoshe kapanda gari ya Luxury
"Dogo vpe eti ulipo kata tiketi ulitoa hela?"
"Wewe konda na wewe sasa kaingia je humu kama hajatoa pesa au kisa anamavazi yalio chakaa ndio kinachokutia wasi wasi?" Alijibu mama mmoja aliekuwa akionekana na rafudhi ya kitanga Tanga .
"Mama mimi nimeuliza tu maana aliempa tiketi kanambia ana uhakika ila hakumbuki vizuri kama alitoa hela"
"Sasa ushasema ana uhakika na hakumbuki vizuri jibu ni kwamba kijana ametoa pesa mfyuu..".
"Wewe dogo ulitoa hela "
" Nilitoa ndio" Alijibu Bahati Masumbuko na kumfanya konda atulie nakurudi zake mbele huku safari ikiendelea
"Hapa nikifika kwanza niitafute milimani city niingie, kisha niitafute Kariakoo ndio mambo mengine yaendelee"Aliwaza Bahati Masumbuko huku akijikuta anafurahi kwani ndoto zake ya kulioana jiji la Dar muda si mrefu zinaenda kutimia hayo yalikuwa ndio mawazo ya n bwana Masumbuko hakuwaza nani atampokea atakaa kwa nani au atalala wapi na kuishi vipi.
Ndani ya muda wa saa moja kuelekea na nusu ndio muda ambao basi alilo panda Bahati Masumbuko ndio lilikuwa likiingia stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani yaani Ubungo basi ilijiegesha kwenye eneo lake na kuruhusu abiria watoke kwani walikuwa wamefika .
Bahati nae aliamshwa kutoka usingizini kwani alikuwa amesinzia tokea muda mrefu na hata gari lilivyo fika hakujua limefika mda gani
"Wewe amka gari lishafika Ubungo" Aliongea mama aliekuwa amekaa pembeni yake huku akichukua begi lake na kutoka nje .
Bahati alijikuta akianza kushangaa baada ya kuona upande wa pili taa zinawaka kwenye jengo lililopo hapo ubungo , alichukua kijimfuko chake na kutoka haraka mpaka nje ya basi na kuanza kuendelea kushangaa.
******
Peter alianza shule kidato cha kwanza na siku kadri zilivyokuwa zikisogea alijikuta akifahamika haraka sana kutokana na uwezo wake wa akili darasani huku akionyesha ubingwa wake zaidi katika somo la .Mathematics(hesabu) na komputa(Tarakishi), ndani ya miaka miwili tu Peter alikuwa moto sana kwenye somo la komputa na hisabati kwani alikuwa ameshajua kila kitu kuhusu komputa
"Vipi Peter "
"Safi niambie kaka"
"Vipi baadae nataka nije getoni kwako unisaidie kunielekeza maswala ya Excel na Publisher yananizingua kinoma " Aliongea jamaa mmoja afahamikae kwa jina la John ambae yeye alikuwa kidato cha nne na Peter cha pili.
"Poa hakuna shida wewe njoo " Alimjibu huku wakitembea mpaka walipo fikia eneo la Smart area .eneo ambalo hapo shuleni hauruhusiwi kutembea zaidi ya kukimbia.
Peter wakati buo yeye alikuwa akiishi Mbezi Beach ambako alipangishiwa Apartment(nyumba) na wafadhili wake baada ya Peter kuonyesha uwezo mkubwa darasani, japo Peter alikuwa akilipiwa kila kitu lakini hakuacha kufanya biashara yake ya mkaa ambauo ilikuwa ni kama urithi kutoka kwa mama yake Irene. Na kila pesa aliokuwa akiptata kwenye biashara hio nusu alikuwa akiweka benki na nusu alikuwa akitumia kwenye matumizi yake madogo madogo
"Baada ya muda wa jioni kukaribia John alikuja nyumbni anapoishi Peter
"Mzee ndio maana uko vizuri kwenye komputa kumbe una madesktop himu ndani"
"Ndio mzee naanza maandalizi ya kozi nitakayo soma nikimaliza shule tuu maana sina mpango wa kusoma kidato cha tano na cha sita nataka nipitie diploma kwanza"
"Unataka usome kozi gani sasa mzee"
"Nataka nipige Computer science "
"Duuh kweli mzee we fuata kipaji chako kitakutoa kimaisha "
Basi John alielekezwa na Peter mpaka pale alipoelewa ndio aliondoka.
Baada ya miaka saba kupita Peter alikuwa ni kichwa cha kuotea mbali sana katika maswala ya komputa na wakati huo alikuwa chuo kikuu akimalizia kuchukua degree yake ya Computa sayansi katika chuo cha Dar es salaam .
Siku moja ikiwa ni wikiend Peter alikuwa maeneo ya mlimani city ambapo yeye alikuwa upande wa nje kwani tayari alikiwa ashanunua kilichomleta pale ,kwani siku bio alikuja kununua simu ya ndoto yake simu aina ya Sumsung galaxy note 10 ila wakati yupo anajiandaa kuondoka mara aliona gari moja zuri sana likiingia mahali hapo na kwenda mpaka kupaki mita kadhaa kutoka miguuni mwake alijikuta akiliangalia gari hilo lakini alijikuta akipata kushangaa zaidi baada ya kumuona moja ya msichana mrembo sana alievalia gauni jekundu akishuka kwenye gari hio ,wakati anaendelea kushangaa alishuka mwanaume ambae Peter alimjua kwani alikuwa maarufu sana ncbini ambae watu walipenda kumuita bosi Samir.
"Huyu mtoto atakuwa wa huyu bosi , huyu demu nitafanya jui chini nilale nae"
"Aiyaaa...mamaaaa simu yanguu jamani mwiziii..." Peter alijikuta akiropoka kwani simu alio kuwa amenunua muda sio mrefu uliopita imepakuliwa kwa kushangaa kwake.....
SEHEMU YA 03
Bahati Masumbuko baada ya kufika stendi ya mabasi muda ule wa saa moja alijikuta akikosa uelekeo wa kwenda kwani hakujua achukue njia ipi atokee wapi.
"Nitalala hapa hapa hadi kesho" Alijiongelesha huku akiangalia namna ya kulala hapo stend.
"Wewe dogo bado uko hapa tuu ?" Aliongea konda aliekuja nae
"Ndio broo nataka nilale hapa ila nina njaa kweli nisaidie elfu moja"
" Yaani uweze kupanda gari la Luxury ,ushindwe kupata hela ya kula , na ndugu wako wako wapi?
"Broo sijaja huku kwa ajili ya ndugu nimekuja kutafuta maisha ,kama unanisaidia hio buku nisaidie"
"Siwezi kukupa kwanza nina uhakika hela ya nauli hukutoa ..tambaa ..endelea kutafuta maisha" Aliongea yule mchaga huku akiondoka zake akimuacha Bahati Masumbuko palepale pale .
"Haja kubwa imenibana sijui napata wapi choo ..ingekuwa kuna hata sehemu ilio jificha kama kichaka ningeenda kuutua" Bahati aliongea huku akitembea huku hajui hata anaelekea upande gani.
"Wewe dogo unapitaje hapa bila kutoa tiketi wala hela" Aliongea mzee mmoja ambae alikuwa amekaa kwenye kiti na vijana wawili waliokuwa wakikusanya hela kwa anaeingia na kutoka pale Ubungo kwenye geti la kutokea "
"Tiketi ya nini na kwa nini nitoe hela?"
" Wewe dogo ndio unaanza kuja Dar au unajifanya huelewi"
" Ndo nimekuja leo natafuta sehemu ya kujisadia "
"Sasa toa hela upite "
"Sina hela yoyote hapa "
"Pita lakini siku nyingine huwezi kupita hapa bila hela au kuonyesha tiketi "
"Sasa najisaidia wapi?"
" Una muuliza nani nenda kule utaona choo dogo pisha wenzako wapitee"
Bahati alitembea huku akizungusha shingo kila mahali alitembea na kukiona choo na kwakuwa hajui kusoma hata kusoma kitu kinacho endelea aliingia ndani ya choo kile nakujisaidia alivyomaliza alifunga mshipi wake na kutoka.
"Wewe!"
"Unaongea na mimi?"
" Ndio hujatoa hela"
" Hela ya nini”
" Soma hapo ukutani”
“Nilipasoma si pameandikwa choo"
"Malizia kusoma maneno yote" Hapo ndio bahati kiwewe kilimshika maana kusoma alikuwa hajui na hata maneno alio tamka kuwa ni choo alibahatisha tu kwa sababu hapo ni choo.
"Nishamaliza kusoma"
“Toa sasa "
"Nitoe nini??"
"Hivi wewe hujui kusoma si umeona hapo kumeandikwa choo cha kulipia”
"Mimi sina hela”
"Bwana eeh hebu ondoka tuu na unabahati leo niko vizuri ningekudekisha humu ndani"
" Yaani huku kila kitu unaambiwa toa hela , hata kujisaidia"
Bahati baada ya kutoka eneo lile nakuona , alitembea tembea pembezoni mwa vibanda ambavyo vingine ndio vilikuwa vinafungwa kwa kuwa muda umeenda sana lakini kuna wengine bado hawajafunga aliendelea kushangaa huku na kule na kujikuta tayari ashafika barabarani ,huku njaa ikimsumbua maana chakula alicho kula Korogwe kilikuwa kishaisha.
" Broo vipi?"
"Poa" Alijibu jamaa mmoja ambae alikuwa akichoma mahindi pembeni kidogo na barabara inayo elekea Mawasiliano
"Mlimani city iko wapi"Yule jamaa alimwangalia Bahati kwanzia mavazi
"Vipi dogo ndio unaanza kuja Dar leo nini?"
" Kwa nini broo?”
"Dogo hii Dar kwa hayo mavazi yako ungekua chokoraa au mtu anaeishi Dar asiekuwa na maisha mazuri angekuwa analijua jiji lote kwa kurandaranda"
"Anhaa..ndio broo mimi ndo nimekuja ndo nimeingia usiku huu "
"Sasa Mlimani city unataka mwenda kufanya nini?"
"Nataka nikaangalie Mlima city ulivyo nyumbani watu wanahadithia sana”
"Wewe sasa utaenda kesho pale huwezi kuruhusiwa saizi unaweza kuitwa kibaka pale ila na hayo mavazi sijui kama watakukubalia kwani ndugu zako wako wapi?".
"Sina ndugu yoyote mimi nilikuwa na mama tu kafariki kaniacha mwenyewe ndio nimekuja kutafuta maisha na historia yangu ya mama kuwa na ndugu sijui"
Bahati alikaa pale na yule kijana wakiendelea kupiga stori mpaka yule jamaa alipomaliza kazi yake ya uuzaji mahindi huku vikibaki vipande vichache na kwakuwa bahati hakula alimuomba vile vilivyo baki kwani alikuwa na njaa na yule kijana akampa huku akiondoka zake.
"Wewe dogo mbona unanifuata?"
"Broo si tunaenda wote nyumbani au umesahau kuwa mi mdogo wako " Aliongea Masumbuko huku akimkimkonyeza kwa staili flani hivi ili ampumbaze akili yake.
" |Poa twende mdogo wangu "
Bahati alitabasamu na kufuata nyuma mpaka wakapanda daladala kuelekea maeneo ya Mwenge ndani ndani huko sehemu moja ambayo ilikuwa ikisifika sana kutokana na Mamantilie mmoja ambae anafanya biashara zake hapo alifahamika kwa jina la Mama mchafu , ni katibu na kota za jeshi, basi baada ya kijana yule kushuka huku nyuma akifuatiwa na Bahati Masumbuko.
"Dogo ingia ndani acha kusimama nje mbu wanaingia”
"Aliongea yule muuza mahindi"
Baada ya Masumbuko kuingia yule kijana au muuza mahindi aliwasha jiko lake la gesi ndani ya chumba chake hicho ambacho alipanga kwenye nyumba hio yenye wapangaji wengi.
"Unapika ugali?”
“Ndio chambua hizo dagaa tupike chapu"
Baada ya kupika ugali na kumaliza walikula na kushiba na kisha wakalala kifupi walitumia muda mchache sana kumaliza mambo yote hayo kwanzia kusafiri kwenye daladala mpaka kufika na kupika haikuzinidi masaa mawili.
"Huyu akija kushtuka kumbukumbu nilizo muwekea zitakuwa zimeisha atanitoa nduki huyu” Aliwaza Masumbuko huku akitafuta usingizi mpaka pale alipopitiwa na kulala.
Wakati wamelala yule muuza mahindi alishtuka kutoka usingizini kutokana na haja ndogo iliombana ,lakini alijikuta akishtuka baada ya kugusa mwili wa mtu , alijikuta akikimbilia taa na kuiwasha, jamaa alijikuta akipatwa na mshangao na kuanza kuangalia mlango kama alisahau kifunga lakini alijikuta akiwa amefunga kabisa.
"Huyu dogo si nilikutana nae kule ubungo kapafahamu vipi hapa nyumbani kwangu na kaingiaje humu ndani sikumbuki kama nilimfungulia mimi wala kuja nae" Jamaa alianza kujiuliza maswali kibao huku hata mkojo ulio mbana ulikata ghafla alianza kumuasha Bahati ambae alionekana kanogewa na usingizi kweli kama yupo nyumbani kwake.
"Wewe toka ndani kwangu , nani karuhusu kuingia hapa ndani si nilikuacha Ubungo wewe na umepajuaje hapa au uliniangalia kwenye darubini zako za kichawi".
"Broo wewe si ndio ulio niruhusu kuja hapa au ushasahau hata ugali tulikula wote" Aliuliza Bahati huku akijisahau kuwa alimpumbaisha akili yake.
"Unasema hata ugali ...huku akiangalia sufuria alio pikia ugali alijikuta akizidi kuchanganyikiwa maana sio sufuria ya kawaida aliokuwa akiitumia kupika labda kuongezeke mtu mwingine ndio hubadilisha.
"Bwana ee.. we toka bhna utakuwa mchawi wewe sio bure kama sio jini "
" Broo sasa usiku huu nitaenda wapi"
"Utajua mwenyewe we umekujaje hapa shika mfuko wako ondoka bwana tafuta ungo wako urudi kwenu bwana " Huki akimsukumia nje na kufunga mlango na kupanda kitandani lakini alikaa kidogo tu mkojo ukaanza kuuma tena maana ni kawaida kwa binadamu yoyote pale apatwapo na mshtuko mara nyingi hata ulikuwa unanjaa inapotea kwa kuwa damu nyingi hukimbilia ubongoni na kupunguza kazi upande wa tumbo na kwenye mfumo wa utoaji wa taka mwili hii kwa kingereza inaitwa (Sympathetic na Parasympathetic ) hii ndo inaweza kukufanya kuruka hata ukuta ukiwa kwenye hatari lakini baada ya kutulia ile sehemu ulioruka huwezi tena kuruka.
Aliamua kutoka aende chooni lakini ile anafungua mlango alimkuta Bahati kaegamia ukuta huku akiwa amekaa na usingizi uliisha kutokana na mbu walivyo kuwa wakimsumbua.
"Wee mchawi sijui jini bado upo hapa tuu??."
"Broo.."Aliita Bahati na kisha yule muuza mahindi alimuangalia usoni na hapo hapo Bahati alifumba macho na kufumbua kwa staili ya kukonyeza.
"Dogo ingia ndani ulale mbona upo hapa nje kuna mbu unashindwaje kugonga mlango” Aliongea yule kijana huku akielekea chooni kisha akakojoa na kurudi Masumbuko alirudi zake ndani na kuendelea kulala.
"Wewe chriss wee chrisssii….!" Ilisikika sauti kutoka nje ikiita kwa sauti na kumfanya Chriss ambaye alikuwa usingizini kushtuka , lakini kilichomshangaza na kumpandisha hasira ni baada ya kumuona Masumbuko tena ndani hapo kalala tena kajiachia.
“Wee chrisss zamu yako ya kusafisha choo leo wewe jishaue tu umelalala hapo nakuita hauitiki"
Chriss alimsikia Pamela ambae ni mpangaji mwenzake ambae mara nyingi ndio alikuwa kama kiongozi ndani ya nyumba hio aliwakumbusha wapangaji wenzake ambao walikuwa hawatimizi wajibu wao kama vile kudeki choo na kulipa kodi ya umeme.
Sasa huyu kijana ambae ndio tumejua jina lake anaitwa Chriss aliamuamsha Masumbuko kwa kumsukuma na mguu.
"Wewe dogo jana si nilikufukuza wewe ikawaje tena upo umelala hapa ndani , na nilihakikisha kabisa baada ya kukufukuza nilifunga mlango , sasa sitaki kujua wewe ni mchawi ama ni nani nataka uchukue vitu vyako uondoke na usirudi hapa nikikuona tena nakuitia mwizi"
Aliongea huku akimpa mfuko wake Bahati Masumbuko aliekuwa akifikicha macho na kumsukumia nje na kisha kufunga mlango.
"Huyu dogo si bure huyu lazima atakuwa mchawi , ni aibu hii watu wakijua nimelala na jini , wanaweza wakasema nimelala na popo bawa, hajanipasuia mayi kweli huyu ." ?Huku akijigusa gusa gusa akjihakiki kama yuko salama sehemu zake za nyuma.
Masumbuko baada ya kutolewa nje kwa kusukumwa hakuona haja tena ya kukaa pale pale zaidi ya kutembea huku akipania kweli kwenda mlimani city , alitembea kwa kushangaa shangaa akipita vichochoro ,wakati akitembea ndani ya vichochoro hivyo alishuhudia baadhi ya vijana wakipokonyana kitu kama kijibegi na vijana hao walionekana kama mateja au vibaka na ni kweli walikuwa ni vibaka na hapo palikuwa ndio chimbo lao na maeneo yao ya kazi yalikuwa Ubungo yote mpaka Mawasiliano na Mlimani city na kila walichokwapua walikuwa wakirudi hapo kwa ajili ya kupeana mawazo jinsi kuviuza vile walivyo iba ,lakini kwa Bahati hakulijua hilo kwani ndio kwanza kaingia jijini aliwakariri sura huku akipita zake mpaka akaja kutokezea Mwenge alitembea katikati ya mabanda ya nguo na kuja kuibukia kwenye barabara ya Samunujoma na wakati wote huo alikuwa akishangaa mataa ya Pale mwenge.
"Broo vipii?"
"Poa"
"Naulizia huko Mlimani city ni wapi maana sioni mlima nikaufuatisha "
Jamaa alimwangalia na kisha kumjibu kuwa aendelee kwenda na hio barabara ataona mlima mkubwa huko mbele , wakati anatembea mara wale vijana ambao walionekana kuwa ni wavutaji bangi na vibaka walimpita huku wakiongea kwa kubishana , Bahati alianza kuwafuatisha . , aliwafuatisha huku pasipo sababu ya msingi ya kuwafuata ,alitembea umbali mrefu lakini kutokana na kushangaa kwake alijikuta akiwapoteza wale vibaka ..alitembea ndipo alipo kuja kupita eneo ambalo ni zuri na watu mbali mbali pamoja na magari yalikuwa yakiingia alisimama pembeni ya geti ..lakini wakati akishangaa mara alijikuta akishikilia kichwa na kudondoka karibu na geti ambapo magari huingia na kutoka huku akitingisha miguu kama mtu nwenye kifafa , wale walinzi ilibidi wamuwahi na kumsogeza pembeni na baada ya muda kidogo alitulia na kushtuka jambo ambalo liliwashangaza hata wale walinzi.
"Baba shikamoo .. nina njaa naomba unipe chochote nile au hela"
"Kwa hio we kijana ukiwa na njaa ndio unadondoka na kuamka halafu unaomba hela”
"Hapana huu ni hali nimezaliwa nayo mzee wangu "
Yule mzee alienda na kutoa kisha akampa ule mkate.
"Sikia kijana hii ni Dar tumia akili upate pesa usipende kuomba omba na wakati una afya njema , kwanza una miaka mingapi? "
"Kumi na saba sasa"
"Sasa kumi na saba ni mingi sana , ngoja nikufundishe jinsi ya kupata hela , ni hivi sikiliza ..angalia ni kitu gani mwenzako hawezi kufanya na wewe unaweza kukifanya ukishakipata mwambie huyo mtu umsaidie kukifanya ila mwambie akulipe”
"Anhaa... kwa hio nifanye halafu niombe hela, hlafu mzee hapa mbona watu wanaingia na kutoka hapa ni wapi"
"Wewe kijana kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Bahati masumbuko”
“Sasa Masumbuko si umeona pale pameandikwa Mlimani city na hapa ni mlimani city”
"Mzee mbona sasa hakuna mlima na sioni hayo magemu ya kuvaa miwani kama watu walivyokuwa wanasema"
"We dogo hata sikuelewi ngoja kwanza nifungulie watu wenye pesa zao , aliongea huku akivuta kamba kuruhusu gari lipite pale na kulionyesa sehemu ya kupaki , huku akiona moja ya mdada ambae kapendeza kweli kweli akiwa amevalia gauni jekundu na baada ya kushuka, alishuka tajiri mmoja maarufu Samir.
Lakini mzee yule akifunga uzio yule huku nje ndio kijana Peter alikuwa anatoka kununua smartphone yake huku akiishikilia kwakuwa alikuwa haamini kama angekuja kumiliki simu kama hio , lakini alijikuta akishangaa gari ambayo iliingia kwani ilikuwa ni nzuri sana lakini kilichomfanya ajisahau kabisa ni baada ya kumuona msichana mrembo hatari na kujikuta akisahau kama yupo barabarani kwani wakati anashangaa wale vibaka waliikwapua simu na kisha kutimka kuelekekea mafichoni kwao, huku tukio hilo likishuhudiwa na Bahati na yule mzee ambae alisharudi alipo Masumbuko. Peter hata sauti haikutoka alijikuta akikaa chini huku haamini kilicho mtokea simu ya milioni moja na nusu imekwapuliwa alijikuta akichanganyikiwa.
"Kaka vipi .. naenda kuileta ila unipe hela" Peter alisikia sauti ilio mfanya ainue uso wake na kumwangalia huyo anaemuongelesha "
" Oya chalii hebu toka tuu hapa usinivuruge mimi , wewe ni wale wale ondoka bhn" Aliongea Peter kwa hasira huku akitaka kuondoka kwani aliona ameshapoteza kila kitu alianza kutembea na kujikuta akigeuza na kumfata yule kijana ambae amesimama pale pale maana alichukia kuambiwa yeye ni wale wale wa kuiba.
" Wewe unawajua wale ?"
" Wewe nipe hela nikakiletee simu yako "
"Poa nenda nitakupa laki moja ukiirudisha"
" Hio hela mpe huyu mzee hapa anishikie mpaka nitakapo rudii"
" Mzee nafanyia kazi mbinu yako ya kutafuta pesa"
" Wewe kijana sijamaanisha hivyooo" Lakini mzee alichelewa kwani Masumbuko alikuwa amekwisha kimbia