Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Duh! Pole sana...Hayo maji ya kupwa na kujaa yanahitaji timing, vinginevyo ni habari nyingine.
Kweli mkuu... ..nilishikwa pabaya siku ile....naelea kwa mateso ya kusubiria..kuzamishwa na wimbi...masaa..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]; Fadhila nitalipa tu maana kama Mungu alimuwezesha kuniokoa ndivyo atakavyonitengenezea mazingira ya mimi kukutana na mkeo[emoji3].
Jambo zuri...
 
Sio vizuri ila nimecheka mpaka machozi yamenitoka bro kwa namna ulivyosimulia. Maji nayaheshimu kwa heshima zote aisee
[emoji23][emoji23][emoji23], usicheke bro.
 
7 April 2012
Jioni Beijing China
Sitasahau
Tokea siku hiyo swimming naoga upande wa juu kule kwa watoto au siingii
 
Nilikua Zanzibar mwaka 2007 tukaenda kuogelea, yule Mpemba Mungu Ampe maisha marefu! Sitaki kukumbuka
 
Duuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana

Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.

Mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.

Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..

Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa

Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi

Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah

Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"

Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..
[emoji28][emoji28][emoji28] vipi mzungu ulitoombaaa
 
Ilikuwa Nairobi Miaka ile ya 98/99 ku mto unaitwa River Nairobi... Kipindi hicho nipo Standard 6

Huo mto unapitisha maji machafu kwa kua unapita pembezoni mwa soko, maji ya mochuari sijui na mauchafu kibao...


Ufinyu wa ardhi ukawafanya wakenya wafanye diversion ya mto ili wapate eneo la kujenga..

Wakafaniikiwa kuchimba diversion huku wakiwa wameblock maji yasipite njia yake ya awali... Kwenye huo mto palijitengeneza kama ka dimbwi na chem chem basi pakawepo maji... Vijana tuona fursa sio kila siku kwenye Uhuru Park au City Park

Mara tukanza kuogelea tukiwa kama watu 7 huku nguo tumevua tumezitega kwa pembeni na vikengele vyetu vinaninginia....

Kumbe majj huwa yanafuata mkondo..... Tupo tunajirusha kwenye maji mara ghafla tukasikia makelele... Muda huo ule mto ulikuwa umefurika na yale maji yaliyokuwa blocked yakarudi kwenye mto wa zamani...

Asikuambie mtu nguvu ya maji... Tulizolewa ila tunamshukuru Mungu watu walikimbia kuja kutuokoa... Maji yalibomoa kwa kasi yupo mwenzetu alipiga glasi za kutosha mpaka akapewa LAST KISS ndio akazinduka...

Tangu siku hiyo mimi na maji sina mazoea hata kuoga dakika tatu nyingi... Huwa nawashangaa wanaongangania mabondeni...

Kama hayajakukuta, simuliwa kisha uone ni mambo ya kwaida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom