Sebago
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 224
- 280
sie tulikua tunaogelea upande wa wa kule Zizi la ng'ombe wanakofyatulia tofali...Mkuu ushawah kuogelea pale kigogoni kwny daraja la ruaha?
sie tulikua tunaogelea upande wa wa kule Zizi la ng'ombe wanakofyatulia tofali...Mkuu ushawah kuogelea pale kigogoni kwny daraja la ruaha?
Poleni!Hii komenti yako imenigusa sana nilimpoteza my brother miezi za sasa imepita. Sikuamini kama mtu mzima anaweza kufa kwenye swimming pool na mbaya zaidi alikuwa akiogelea peke yake.
Hahaha[emoji23][emoji23][emoji23] kaazii kweli kweli!Umezaa mapema sana. Kidato cha pili una watoto wa nne? Ni mapacha?
Hii imewahi kunikuta..Nilikuwa sijui vizuri kuogelea..Uogeleaji wangu ilikuwa siangalii ninapokwenda..Kichwa kipo ndani ya maji macho nimefumba..Nikaanza kwenda wrong direction naelekea kwenye kina kirefu bila kujijua..
Imefika stage nataka nisimame miguu haifiki chini then naanza kuzama..Nilidata..Nikianza kupiga mbizi kwa kasi huku sijui naelekea wapi..Hapo nishapanic..Mungu alikuwa upande wangu,nilikuwa naelekea kwenye kina kifupi..
Baada ya kuchoka kabisa na kuona siwezi tena kuendelea nikaamua nisimamame..Nikagusa chini..Maji yapo kifuani..Nilitembea hadi nje nikabeba nguo zangu na kusepa bila kuaga washkaji...
Hii siku siji kuisahau kamwe..
Ilikua pande za bahari beach kwa kando hivi.
niko na marafiki zangu wanapata msuba mi nikaona isiwe mambo ngoja nikapige mbizi.
Basi nikawa naogelea maji ya level yangu baada ya muda hivi nikawa narushrusha miguu na mikono nikawa naelea elea nikajiona yes nishajua kuogelea. Nikawa nafanya hivyo nikichoka nakanyaga chini. Sasa nilielea kwa muda mrefu kidogo kumbe maji yalishanipeleka kwenye kina kirefu. niliposema nishushe miguu nikanyage chini ndio balaa lilipoanza. Miguu haifiki chini na nishakunywa vikombe kadhaa. Nikaanza kutapatapa piga maji kama sina akili nzuri nilitoka niko hoi washkaji wanafurahi eti duh unayakata maji. kumbe mwenzao nimeponea tundu ya sindano.
Asante sana mkuu tushapoaPoleni!
Khaa... mkuu alikufa kwa kuliwa na mamba au?? Aisee na nini kilitokea siku hiyooMwaka 1996 miezi ya mwanzo mwanzo kabla MV Bukoba haijazama ilikuwa Tabora hiyo, mjinga mmoja akanidanganya tukaenda kuogelea bwawa lipo sehemu moja inaitwa igombe, halafu akanificha kwamba lile bwawa lina mamba na viboko wengi sana.........kwa kweli kilichotokea huwa sitaki kukikumbuka kabisa na yule mjinga bahati nzuri alikufa, maana tofauti na hapo ningefanya kitu kibaya sana juu yake
Hukunywa vikombe kadhaa??Mimi pia story yangu inafanania za kwenu.
Ni kitambo kidogo nakumbuka ilikua August 2010 tukaenda beach na washkaji.Nilikua sijui kuogelea vizuri.
Nikaanza mdogo mdogo kwenye kina kifupi, bwana nikanogewa baada ya kujiona ninaweza kuelea kwa mda mrefu.Basi nikaendelea kuelea kumbe nipo kina kirefu buana mda nimechoka nasema nisimame miguu haifiki chini.Nilipiga ukunga na kuanza kujiokoa bahati nzuri nikafanikiwa kurudi pafupi japokuwa washikaji hawakuamini kuwa nilikua nnazama wakadhani zile kelele ni geresha tuu ... niliishia kuangalia wenzangu hadi mwisho.maji ni mabaya sana ukiyakosea.
Hapana, nilipanick tuu ...Hukunywa vikombe kadhaa??
Aisee,Mwaka 1996 miezi ya mwanzo mwanzo kabla MV Bukoba haijazama ilikuwa Tabora hiyo, mjinga mmoja akanidanganya tukaenda kuogelea bwawa lipo sehemu moja inaitwa igombe, halafu akanificha kwamba lile bwawa lina mamba na viboko wengi sana.........kwa kweli kilichotokea huwa sitaki kukikumbuka kabisa na yule mjinga bahati nzuri alikufa, maana tofauti na hapo ningefanya kitu kibaya sana juu yake
Sio mzuri sana, baada ya kupona kifo matamanio ya kuendelea kuwa gwiji wa kuogelea yaliyeyuka ghafla, nikawa navizia vizia mara moja moja, ila yalizima kabisa baada ya kuogelea mara nasikia kitu chanigusa nikahisi mwanafunzi mwenzangu, kucheki vizuri kumbe maiti aisee[emoji22], nilitoka majini kama mshale[emoji23][emoji23][emoji23], ilipita miaka mi4 sijaogelea, hadi nilipoamua kuanza kuogelea tena mwaka 2015 mji kasoro bahari....Sema pumzi ipo ya kutosha.Hapana, nilipanick tuu ...
Wewe ni mwogeleaji mzuri?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]apaaaaa womiiiiiAiseee... nimeponea scenario 2. Sitakaa nisahau.
Sisi wachagga mito yetu ilivyo na mawe kuogolea wapi na wapi kwamfano?
1. Enzi hizo tukienda moshi likizo bwana kila actuvity hutaki kumiss. Kuna vibarua walikua wanaenda shamba Ibukoni huko. Sina hata kilo za nyama enzi hizo kadogo tu. Bibi alibikataza sana kwani naelewa. Nataka nikale maembe huko mwai. Wooi, tukaenda na binamu yangu haooo tukafika shamba. Miye nahangaika tu huku na huku. Binam yangu alikua na mdogo wake pia mdogooo tena kunizidi. Binamu alikua mkubwa na ana mwili. Muda wa kurudi ukafika. Uuwuuii, mvua iliyokuja utasema huko mbinguni malaika wa zamu alibet mkeka ukachanika. Barabara zote zimejaa maji. Kumbuka hiyo ni kupanda. Nikawa naona kizunguzungu. Tukafika mahali kuna mfereji unaenda kuunganisha na bonde ni kama mto hivi linapeleka maji kenya. Mdogp wake binamu akavuka kwanza, huyoo akachukuliwaa, nikawa nayadharau yale maji. Na mimi nikavukaa. Weeee, nikajikuta hata kusema maa siwezi napambana kujiokoa. Aisee yule binam yangu kwa hofu alirukia kwenye maji akaanza nitoa mimi, then later akamtoa mdogo wake. Yaan angechelewa tukafija kwenye lile bonde ndo basi wangesubiria miili yetu kenya iletwe tena tz kutuzika.
2. Hii nilienda marangu mtoni kwa mamdogo wangu ameolewa huko. Ule mto na kwake pamepakana. Hata maji enzi hizo wanachota huko kuna mifereji ndo huchota maji yake. Siku moja wakawa wanaenda kuogelea. Watu woote wanaogelea. Mimi peke yangu ndo nimebaki kwenye jiwe nawaangalia wanavyodive. Hapo pia kadogo kweli. Nikasema jaman si na mimi naweza? Wooiii si na mimi nikajidumbukiza1[emoji23][emoji23][emoji23] nilikunywa maji apaaaa womii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa kuna binamu akiwa yuko ndani ya maji akahisi kama ameshika mtu maana miye hapo nasubiria kukata roho tuu[emoji23][emoji23] ila akawa anasita asije akamtoa nguva bure ila akajikaza kisabuni akasema liwalo na liwe, akaninyakua paaaap, kufika nje ya maji si huyu hapa fulani mungu wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] msaada wa chap chap. Since then sitaki tabia mbaya na maji. Yaan hata uniue. Lama ni kuogelea natbeaga tu kwenye yale maji mafupu ya wet en world ama popote mahi mafupi
Apaaaa ndengAaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]apaaaaa womiiiii
nimecheka sana ila sikucheki kaka bali ulivyoelezea maana aje ulijitosa kwa sababu ya sifa kwa watasha hahahahahah uuu wiiii mbavu zang jaman,kwamba maji sio uhai hahaDuuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana
Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.
Mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.
Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..
Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa
Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi
Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah
Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"
Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..
hahahahaha uwiiiii jamani jf humu, ni noma kuna watu mnachekesha kweli bwana uwiiii sina mbavu mie,vip sasa uliwahi kurudia tena?Mimi naziheshimu sana swimming pool za kwenye mahoteli makubwa, nilikuwa nafikiri ni fupi, sasa siku moja nikasema ngoja na mimi niogelee kwenye swimming pool, aisee nilikunywa maji mpaka nikajamba na kauharo kidogo na kamkojo kidogo kakatoka, siku ile ndiyo nilijua maji ya swimming pool sio masafi kama yanavyoonekana
Apaaaa wamaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimekumbuka mbaliiApaaaa ndengAaaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahahaha wapiApaaaa wamaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimekumbuka mbalii
Moshi kwa bibi yangu.Hahahahaha wapi
Hahaha mbona ni mshangao wa kichaga huo?Apaaaa wamaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimekumbuka mbalii
Hahahaha naupenda pia ila nimepunguza mnoMoshi kwa bibi yangu.
Huwa anapenda hii misemo
Hahahaha ndiyo, umejuajeee???Hahaha mbona ni mshangao wa kichaga huo?