Kuna mtu anajua watu maarufu waliozaliwa ktk ndege ili tujue na uraia wao ulikuwaje thereafterUraia wake ni wa kule alipotoka. Ili huesabiwe umeingia nchi nyingine ni baada ya ndege kutua.
Big up sn kaka. Mi ntakuwa nakuita Shebbymandege.Mkuu kile kitundu kinaitwa "bleed hole" hakitokei mpaka nje ila kipo kwenye "pane" (Pane naweza kusema ni tabaka) ya katikati. Ipo hivi
Dirisha la ndege lina pane tatu, ambazo ni pane ndani ambayo unaweza kuigusa ukiwa ndani ya ngege, pane ya katikati na pane ya nje. Sasa hiki kitundu hakipo kwenye pane ya nje. Kitundu hiki kipo kwa ajili ya usalama wako. Kivipi? Nifuate hapa chini:
Unapozidi kwenda juu zaidi density ya hewa hupungua, yaani hewa inazidi kuwa nyembamba, hivyo pressure yake nayo huzidi kupungua kadri unavyozidi kwenda juu. Pressure ya hewa dhidi yetu ndiyo hutufanya sisi tujisikie vizuri hivi tunavyojisikia tukiwa hapa chini. Sasa kutokana na pressure kupungua unapozidi kwenda juu, ili ujisikie sawa kama upo hapa ardhini, ndani ya ndege huingizwa hewa ili kuleta mgandamizo wa hewa kama huu unaousikia hapa ardhini (Cabin pressurization). Hali hii husababisha tofauti kubwa ya mgandamizo wa hewa wa ndani ya ndege na nje ya ndege. Hivyo hutokea hali ya msukumo fulani kuelekea nje ambako kuna mgandamizo mdogo wa hewa. Ili kuweza kuleta msawazo (equilibrium) wa gap lililopo kwenye hizo window pane ndiyo kukawa na hivyo vitundu (bleed holes). Vile vile vitundu hivyo husaidia madirisha kutoweka ukungu (fogging).
Umesomea chuo gn mkuu! Ada bei gn!Aircraft maintenance engineer.
Duuh.... Bonge la dude! Lilivyokaa kaa kama vile Eagle akiwa kwenye mawindo ya vifaranga .nimeingia kuangalia hiyo concord aisee kwa muonekano huu ni haki yake kufungiwa inaonekana kabisa inakimbia sana![]()
Nafikiri huwa wanavuka hili anga kwa escape velocity, ambako hufikia anga ambalo G yake sio 9.8,tena.Mkuu...
Miaka kama mitano hivi tumesikia ndege za abiria zimepotelea angani mfano kama ile malasia, je nini kinasababisha ndege inapotea? Je kwanini kesi kama hizi zinatokea? je kwanini mpaka leo hawajafanikiwa hata kuona kile kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege wanaakiita "something,,, box"!
Asee hiyo hutegemea na rubani, rubani mwingine huwezi sikia uo upuuzi, ana balance kila kitu, au sijui inategemea vyuo.Ndege inapokaribia kutua kuna hali flani inatokea, sijui ni kitu gani husababisha hiyo hali. Hali hiyo hufanya masikio yazibe na kunakuwa na kelele flani kama mruzi mkali sana, na hiyo hali abiria hutangaziwa na wahudumu kuwa rubani amefungua kitu flani ili ndege iweze kutua. Mkuu hii ni kitu gani, na je inatokea kwa ndege zote zinapokaribia kutua au baadhi.
Mi niliwahi msikia yule mdada mtz rubani akisema ivo kuwa, hizi ndege za kisasa ni rahisi, unaweka auto to una relax.Mkuu kwa hili nisikudanganye sina ufahamu nalo. Labda niambie ni aina gani ya Boeing ili nicheck na watu ambao wamefanya kazi na hiyo aina ya ndege. Lakini kwa knowledge yangu ya ndege nabaki najiuliza swali; kama itajiweka kwenye autopilot halafu pilot asiwe na command nayo tena, ni nani ataitoa ili kuendelea na maneuvre?
Huwa zinapita pembeni tena karibu kabisa na rubani huwaamsha na kuanza kuwaelezea. Ni kama utalii wa ndani vile.Nitaomba Hiyoo triangle uielezee mkuu kama unaifahamu kivyovyote vile please shebbydo. Then kuhusu mlima wa Kilimanjaro nitoe ka sapoti kadogo kuna Uzi wa Kilimanjaro kuna mtu alisema ndege inapita pembeni kidogo na watu huwa wanaona lile shimo na mandhari yake,so in short haipiti katikati Bali pembezoni kidogo,na mfano ukatolewa air Kenya hufanya hivo.
Tuko pamoja
[emoji23][emoji23][emoji23]![]()
Hii ndege ya abiria kwenda kwa mtindo huo inawezekana au tulidanganywa kwenye movie?
Mkuu dunia huzunguka pamoja na anga(atmosphere) lake kwa hiyo helcopter inakuwa siyo stationary bali inazunguka pamoja na atmosphere at the same speed!Kama dunia inazunguka mbona helcopta huganda angani may point A na kutua eneo hilo hilo bila kujikuta iko point B!!sikokatka matani nijibu kisayansi nielewe
Mkuu kwa elimu hii unayogawa bure ubarikiwe sana.Asante mkuu
Nianze na swali lako la kwanza ambalo unataka kujua nini maana airspeed na True airspeed.
Kwenye cockpit (ndani kwa marubani) kuna vifaa vinavyosoma parameters mbalimbali. Sasa kuna hivi ambavyo vinaitwa basic pitot-static instruments. Yaani; Airspeed Indicator, Altimeter na Vertical Speed Indicator. Ni muhimu Rubani kuwa taarifa hizi; spidi ya upepo ambayo ndiyo airspeed ili asije akazidisha spidi ambayo inaweza kuzalisha shock waves ambazo zinaweza kuleta madhara kwenye ndege hasa ndege ambayo haina sifa ya airflow kuzidi spidi ya sauti. Hizi shock waves huanza kupatikana pale ambapo airflow(uhusiana wa spidi ya hewa na ndege yenyewe) inazidi spidi ya sauti. Kitu kingine ni umbali kutoka usawa wa bahari ili kuweza kufuata maelekezo anayopewa kutoka Aircraft Tower Control kuhusiana na ndege zingine ili kuepuka kugongana. Pia lazima ajue wakati wa kupanda anapanda na spidi kiasi gani(Vertical Speed). Hivyo Air Speed Indicator, Altimeter na Vertical Speed Indicator ndizo zinafanya kazi hii ya kumbpa taarifa.
Jibu la swali lako la kwanza ni kwamba Airspeed ni spidi ya airflow na True Speed ni spidi halisi ya ndege.
Swali lako la pili umeuliza jinsi gani speed ya ndege inapimwa na kifaa cha kupimia speed kipo wapi.
Mlolongo wa kupima speed ya ndege ni mrefu kidogo, nifuatilie hapa chini:
Nje ya ndege sehemu za ubavuni(Ndege zingine huwa ni kwenye mabawa) kuna matundu ya namna mbili; PITOT TUBE-hii ni tube yenye tundu mbele na STATIC VENT- hivi ni vitundu vidogo vipo kwenye fuselage( bodi la ndege). Matundu haya yapo katika mfumo unaoitwa Pitot-Static System ambapo zile instrument tatu yaani; airspeed indicator, altimeter na vertical speed indicator zinapatika ili kumwezesha rubani kusoma zile parameter nilizozieleza pale juu.
Ili kuweza kusoma speed ya ndege ambayo ndiyo True Airspeed, mchakato huu hufanyika:
Hewa ambayo inaingia kwa speed kupitia Pitot tube na ile ambayo inakuwa ni hewa iliyotulia (Static) kupitia Static vent hukutana sehemu moja ambapo kuna kiwambo (Diaphragm). Kiwambo hiki hutanuka na kusinyaa kutokana na speed ya hewa inayoingia kupitia Pitot tube , ambapo hewa tuli kupitia Static vent huwa imekizunguka kiwambo hiki. Kutokana na mchakato huo, hivyo basi Air Speed Indicator (ASI) ambayo imeunganishwa katika mfumo huu huweza kusoma Airspeed.
Airspeed siyo kipimo halisi cha speed ya ndege kwa sababu bado kuna kuwa na makosa (errors) kutokana na position ya ndege ilipo na instrument yenyewe, hivyo basi calibration ya hizo errors hufanyika ma kupata speed nyingine inaitwa Calibrated Air Speed (CAS).
Hii CAS nayo bado inakuwa na makosa kutokana na Compressibility ya hewa katika speed 300 knots na kuendelea. (Watu wa physics wanajua compressible na Incompressible fluids). Hivyo error ya Compressibility inaondolewa na kupata speed nyingine inaitwa Equivalent Air Speed (EAS).
Speed halisi ya ndege ni True Air Speed(TAS) ambayo inapatikana kwa formula hii hapa chini;
TAS= EAS/√relative air density
Swali lako jingine umeuliza kuhusu umbali kutoka ardhini(altitude)
Altitude hupimwa na Altimeter ambayo ni miongoni mwa vile vifaa vitatu vya Pitot-Static.
Altimeter yenyewe hufanya mlinganisho wa density ya hewa ambayo hupimwa kupitia Static vents, ambapo ndani ya mfumo kuna Aneroid (kipima pressure ya hewa) na ile pressure ya hewa katika usawa wa bahari ambayo huchukuliwa kama referece. Lakini kutokana na variation ya pressure ya hewa kutokana na hali ya hewa, ndege nyingi sasa hivi zina altimeter ambayo inaweza kuwa adjusted na rubani ili kuingiza reference pressure anayopewa na vituo vya karibu vya hali ya hewa. Hii hutoa pressure halisi na kuifanya altimeter isome umbali halisi kutoka ardhini. Altimeter hii inaitwa Kollsman Window kufuatia jina la mgunduzi wake somebody Kollsman.
Nahisi mfumo wa ndege za kivita unaendana na mfumo wa ndege hiiDuuh.... Bonge la dude! Lilivyokaa kaa kama vile Eagle akiwa kwenye mawindo ya vifaranga .
Dude limesimama, linavyoonekana likiamsha hukamati.
Fungua mwingine ila huu bado unamaisha mkuu.Kuna uzi wa kifaa cha kutunza taarifa za ndege nataka kuuanzisha, vipi wadau ni uchanganye humu au nifungue thread mpya?
Zilikuwa zinaendaje kwa saa..?Concord ilikuwa inasafiri kwa spidi kubwa sana ambayo ilikuwa ni ngumu kwa rubani kuicontrol. Baada ya ajali zake kuonesha makosa ya marubani kushindwa kuicontrol ilibidi izuiliwe.
Au labda alimaanisha pilot anaweza kuiweka auto endapo kuna hali imemkuta labda ya kiafya au uvamiz.Mkuu kwa hili nisikudanganye sina ufahamu nalo. Labda niambie ni aina gani ya Boeing ili nicheck na watu ambao wamefanya kazi na hiyo aina ya ndege. Lakini kwa knowledge yangu ya ndege nabaki najiuliza swali; kama itajiweka kwenye autopilot halafu pilot asiwe na command nayo tena, ni nani ataitoa ili kuendelea na maneuvre?