Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Huu uzi upo ndani ya damu yangu, hongera sana kwa majibu mazuri.

Swali, kuna aina tofauti tofauti za ndege sijui Boeing 737, 747, 767, 787, Bomberdier sijui, ATR na kadhalika, hivi marubani wanaoendesha hizi ndege ana uwezo wa kuendesha ndege tofauti, leo anaendesha ATR, kesho anaendesha Boeing 747 au kuna marubani special kwa ndege specific?
Kuna kitu kinaitwa type rating. Lazima uwe na type rating ya ndege husika. Elimu ya ndege utasoma mpaka unastaafu. Kama ulikuwa ni rubani wa airbus, ukitaka kuhamia boeing fuani lazima ufanye type rating. Vile vile na uhandisi.
 
Vizuri sana mkuu kwa elimu:

Nilisoma physics kidato cha 5 nikaelewa kidogo sana nadhani kama 8 % tu hasa ukizingatia presha ya kufeli mitihani ikanilazimu nimeze tu baadhi ya mambo ila nilikiwa nikijua kabisa Nina ukakasi kuhusu mechanism ya Ndege kuruka angani na kutua..nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu mpaka leo miaka hii ila sikupata MTU kwa ufasaha wa kunielewesha vizuri ila leo hakika nimeelewa kwa 85% ..

Kilichobaki ni kutaka kujionea kila kifaa na uwezo kilionao hasa engines zake...kusema ukweli Ndege kupaa si jambo rahisi rahisi nadhani ndo sababu hata ya Engineering course zake gharama ni kubwa sana tofaut na Engineering hizi zingine...nimeelewa vizuri sana Bado real practical ila kwa wastani nimeelewa kabisa...
 
Kwa biashara ya ndege unatakiwa kuangalia soko lako lipo je na mazingira ya viwanja vyako vya maeneo ya biashara yako. Kwa viwanja vyetu hivi vingine ambavyo bado ni vya vumbi ndege kama airbus na Boeing hiyo biashara inaweza kukushinda lakini ndege kama ATR au Bombadier zinafanya vizuri. Kwa soko la kwenda nje huwezi kupeleka bombardier hapo lazima ushindanishe ndege kubwa. Ni swala la soko tu mkuu. Locally turboprop zinafanya vizuri.
asante mkuu

swali lingine,matairi ya ndege huwa yanajazwa upepo au tubeless,pia tairi ya mbele inapogoma kutoka pindi inapotua(japo sina hakika kama tukio hili lishawahi tokea) nini hufanyika ,pia ma engineer mnasafiri na abiria au kazi yenu inaishia uwanjani tu??
 
Vizuri sana mkuu kwa elimu:
Nilisoma physics kidato cha 5 nikaelewa kidogo sana nadhani kama 8 % tu hasa ukizingatia presha ya kufeli mitihani ikanilazimu nimeze tu baadhi ya mambo ila nilikiwa nikijua kabisa Nina ukakasi kuhusu mechanism ya Ndege kuruka angani na kutua..nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu mpaka leo miaka hii ila sikupata MTU kwa ufasaha wa kunielewesha vizuri ila leo hakika nimeelewa kwa 85% ..kilichobaki ni kutaka kujionea kila kifaa na uwezo kilionao hasa engines zake...kusema ukweli Ndege kupaa si jambo rahisi rahisi nadhani ndo sababu hata ya Engineering course zake gharama ni kubwa sana tofaut na Engineering hizi zingine...nimeelewa vizuri sana Bado real practical ila kwa wastani nimeelewa kabisa...
Nafurahi kusikia hivyo mkuu. Ni masomo ambayo unatakiwa utulize kichwa kwa sababu unasoma vitu vingi sana hiyo ni knowledge tu bado maintenance practices zina kusubiri. Na ujue ku-troubleshoot matatizo ya ndege.
 
asante mkuu

swali lingine,matairi ya ndege huwa yanajazwa upepo au tubeless,pia tairi ya mbele inapogoma kutoka pindi inapotua(japo sina hakika kama tukio hili lishawahi tokea) nini hufanyika ,pia ma engineer mnasafiri na abiria au kazi yenu inaishia uwanjani tu??
Yapo ambayo ni tube-type na tubeless type. Haya ambayo ni tubeless hujazwa nitrogen, yenye tube hujazwa air hayana shida.

Kesi za matairi kugoma kutoka kwa hizi retractable landing gears hutokea. Ikitokea hivyo basi rubani inabidi aangalie sehemu ya kwenda kuishusha ambapo impact haitakuwa kubwa lakini si kwenye runway.

Swala la injinia kusafiri na ndege na ndege sasa hivi limepungua kwa sababu ndege za sasa haziitaji position ya flight engineer. Labda ndege yenu iwe spanner mkononi.
 
Ahsante sana mkuu kwa ufafanuzi unaoutoa. Je napenda kujua kuhus namba kwenye majina ya ndege:

Mfano Q300, Q400
Boeing 767

1. Je, hizi namba zinatokana na nini?
2. Utarabu wa kuita namba na mfuatano wa namba hizi ukoje?
3. Je, ndege yenye namba kubws ndiyo yenye uwezo mkubwa kuliko ndogo? Mfamo Q400 ina uwezo mkubwa kuliko Q300?

Nawasilisha.
Huo ni utaratibu wa manufacturer kuname series za matoleo ya ndege zake.
 
Niliwai kusikia kwa wanasiasa huko bungeni mbunge mmoja akishutumu Ndege za ATCL kuwa alipanda Ndege alafu mvua ilikuwa inanyesha na Ndege ikawa inavuja kwa maana ya kulowa na mvua
Bahati nzuri waziri alimjibu vizuri akasema hicho kitu hakiwezi kutokea Ndege ni sayansi ya hali ya juu sana..akaendelea kusema kuwa ndo tatizo la sifa ya mbunge kujua kusoma na kuandika tu ...hajui lolote lile kuhusu Force wa pressure ..[emoji1] [emoji1]
 
Niliwai kusikia kwa wanasiasa huko bungeni mbunge mmoja akishutumu Ndege za ATCL kuwa alipanda Ndege alafu mvua ilikuwa inanyesha na Ndege ikawa inavuja kwa maana ya kulowa na mvua
Bahati nzuri waziri alimjibu vizuri akasema hicho kitu hakiwezi kutokea Ndege ni sayansi ya hali ya juu sana..akaendelea kusema kuwa ndo tatizo la sifa ya mbunge kujua kusoma na kuandika tu ...hajui lolote lile kuhusu Force wa pressure ..[emoji1] [emoji1]
Nilicheka sana mi mwenyewe kabla ya majibu
 
hivi uzito wa juu kabisa kubebwa na ndege ni uzito gani? Na kwanini wakati wa kuruka au kutua cabin crew wanaomba madirisha yafunguliwe ndani ya ndege na viti viwe upright?je speed ya ndege angani ni constant au pilot anaweza kuamua kwenda slow au speed?
 
Hizo ndege uzito wake mpaka niangalie kwenye manual zake sina figure halisi. Sifa ya ndege ni kuwa imara lakini nyepesi. Lakini siyo nyepesi kwa kiwango cha chinii sana kwa sababu component nazo ni nyingi.
Mkuu...

Miaka kama mitano hivi tumesikia ndege za abiria zimepotelea angani mfano kama ile malasia, je nini kinasababisha ndege inapotea? Je kwanini kesi kama hizi zinatokea? je kwanini mpaka leo hawajafanikiwa hata kuona kile kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege wanaakiita "something,,, box"!
 
Ndege ivuje? Na bado ifanye kazi?
Ndege inapokaribia kutua kuna hali flani inatokea, sijui ni kitu gani husababisha hiyo hali. Hali hiyo hufanya masikio yazibe na kunakuwa na kelele flani kama mruzi mkali sana, na hiyo hali abiria hutangaziwa na wahudumu kuwa rubani amefungua kitu flani ili ndege iweze kutua. Mkuu hii ni kitu gani, na je inatokea kwa ndege zote zinapokaribia kutua au baadhi.
 
Back
Top Bottom