Kuhusu hilo la uraia mpaka nifuatilie mkuu na ukizingatia sheria za uraia zinatofautiana nchi na nchi. Hilo la mzee kuogopa kupanda ndege kubwa ni tatizo la kisaikolojia tu mkuu. Kuna wengine hawapandi kabisa. Kuna mchezi mpira sikumbuki exactly alikuwa wa nchi gani alikuwa anaogopa kupanda ndege.Sheria hizi zikoje!
(1)Eti mtoto aliezaliwa akiwa angani kwenye ndege Uraia wake unakuaje?
(2)kwanini unadhani Baba yangu anaogopa kupanda ndege kubwa!
Yerewiiiiiiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]2180km/h
Yaani kwenda mwanza inatumia dakika 15 tu
Dubai Masaa 2
Mkuu pole sana hii nilikuwa sijaiona.Mkuu unayo shule ndefu sana kichwan na unauelewa wa kutosha wa jinsi ya kujibu maswali. Tuendelee:
1. ndege zinazoruka sambamba chini na juu au ubavu kwa ubavu hua zimeondoka pamoja au wanabalansisha mwendo juu ili ziende sawa. Na je hiyo hailet madhara kwenye dostirbance ya windflow
2. Nieleze mfumo wa breki ya ndege ukoje (hasa hizi airbus)
3. Yale mahelikopta ya jeshi/UN au USA kwanini yanapangaboi laiini wameyawekea tairi (hua yanatua kwa kuserereka pia?
4. Ndege inapotua kwenye baharini, haizami? Na je hua wanazitoaje?
5. Anaewasiliana na uwanja husika kuomba ndege itue kwa dharula ni ruban au nan? Na je inawezekana kuishusha ndege kutoka say futi 38,000 ishushwe kibishi hafi atiboe wingu kama mawasiliano yakikatika yan ili ruban atafte uwanja manually?
Tupo pamoja mtaalam
Kula kile mkuu, umenijibu vzuri sanakuna maswali post namba 269 bado hujayajibu mkuu
Mkuu pole sana hii nilikuwa sijaiona.
Nianze na swali la kwanza kuhusu kuruka sambamba. Ndege zikiwa sambamba ubavu kwa ubavu au juu na chini haina shida ipo ikiwa moja ipo nyuma karibu sana. Hii ni kutokana na vortices ya ndege iliyoko mbele(vortices ni hewa inayozunguka kwa kasi, effect hii hutokea kwenye mabawa. Hewa huzunguka kuroka kwenye root ya bawa chini ya bawa kuelekea kwenye ncha ya bawa. Halafu juu ya bawa huanzia kwenye ncha kuelekea kwenye root ya bawa). Hii hewa inayozunguka itaharibu utaratibu wa hewa kuflow vizuri kwenye ndege iliyoko nyuma.
Kuhusu kutua majini haimaanishi kuwa haitazama ila ni kuondoa uwezekano wa kulipuka ikilinganishwa na ardhini.
Kuhusu helikopta kubwa kuwa na matairi hii ni kwa sababu ya kuhimili uzito wakati wa kutua si kwamba hukimbia ardhini.
Kuhusu mfumo wa brake wa Airbus ni multi disc. Nielezea vizuri siku moja kuhusu brake za ndege.
Kuhusu kuwasiliana kuomba kutua kwa dharura, anayeomba ni rubani.
Ndege huwezi kuishusha kibishi mkuu vinginevyo utaiangusha.
Autopilot nimeishia kuendesha kwenye gari tu
Asante sana kwa nondo hizi
Uraia wake ni wa kule alipotoka. Ili huesabiwe umeingia nchi nyingine ni baada ya ndege kutua.Sheria hizi zikoje!
(1)Eti mtoto aliezaliwa akiwa angani kwenye ndege Uraia wake unakuaje?
(2)kwanini unadhani Baba yangu anaogopa kupanda ndege kubwa!
Denis Berkamp wa Uholanzi utakuwa unamzungumzia.Kuhusu hilo la uraia mpaka nifuatilie mkuu na ukizingatia sheria za uraia zinatofautiana nchi na nchi. Hilo la mzee kuogopa kupanda ndege kubwa ni tatizo la kisaikolojia tu mkuu. Kuna wengine hawapandi kabisa. Kuna mchezi mpira sikumbuki exactly alikuwa wa nchi gani alikuwa anaogopa kupanda ndege.
huoni impact ya crash inakuwa ndogo ukifananisha na kuporomoka futi 24,000Sasa mkuu hata kama ni kutua itatua popote?
Upo NIT?Habari Wanajukwaa
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima bukheri.
Kuna tangazo moja la redio la malaria huwa linanivutia sana, mtoto anamuuliza baba yake kuhusu ndege inavyoweza kupaa angani. Mzee kutokuwa na elimu hata kidogo tu ya aviation anajitetea kwa kumwambia mwanaye hayo ni maarifa ya juu sana.
Ndege nini! Ndege ni chombo ambacho kinasafiri angani kwa kutumia kani mnyanyuo (Lift force) inayozalishwa hasa kwenye mabawa kutokana na uhusiano wa mwendo kati ya hewa na ndege yenyewe.
Ndege ina sehemu kuu tano, yaani; Injini (Power plant), bodi la ndege (fuselage), mabawa (wings), Mkia (Empennage) na Mfumo wa matairi (Landing gear).
1: POWER PLANT; hii ni sehemu ya ndege inayohusika na uzalishaji wa kani msukumo (Thrust force). Hii ndiyo kani (force) inayoisogeza ndege kutoka point A kwenda point B ikiwa angani.
2:FUSELAGE; Hii ni sehemu ya ndege ambapo sehemu zingine zimeunganishwa kwayo. Pia nyiyo sehemu ambapo abiria, wafanyakazi wa ndege na mizigo hukaa.
3:MABAWA; Hii ni sehemu ya ndege yenye umbo la "aerofoil" ambayo inahusika na kuzalisha kani mnyanyuo (LIFT FORCE). Hii ndiyo kani inayoifanya ndege ielee angani.
Aerofoil ni umbo ambalo huzalisha kani-mnyanyuo kutoka na tofauti ya mgandamizo wa hewa wa chini na juu ya umbo hili. Hii ni kutokana na utofauti wa ukubwa wa eneo la chini na juu. Eneo la juu huwa kubwa zaidi ya lile la chini, hivyo kusababisha hewa ya juu kusafiri kwa kasi zaidi ya ile inayopita chini ili kuweza kukutana pamoja katika muda ule ule (LAW OF CONTINUITY). Kasi ya hewa ikiongezeka basi mgandamizo wake hupungua (PRESSURE)
Hiki ndicho kinachotokea kwenye mabawa ya ndege. Mgandamizo wa hewa chini unakuwa mkubwa kuliko juu, hivyo kani-mnyanyuo kuzalishwa. Ikumbukwe kwambo umbo zima la ndege lipo katika aerofoil. Hivyo nalo huchangia kani-mnyanyuo japo kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ile inayozalishwa kwenye mabawa.
4:EMPENNAGE; Hii ni sehemu ya ndege kwayo kunapatikana maumbo yanayoipa ndege "U-stable" katika mihimili yake na vifaa vinavyoifanya ndege iweze kutembea (move) katika mihimili yake. (Tutaangalia huko mbele mihimili ya ndege ni nini). Katika sehemu ndipo kuna "horizontal na vertical stabilizers".
5:LANDIND GEAR; Huu ni mfumo mzima wa matairi ambao unaohusika na kuisaidia ndege kutembea juu ya njia ya kurukia (RUNWAY) wakati wa kuruka na kutua, vilevile wakati wa kwenda sehemu ya matengenezo (HANGAR)
Kwa leo tuishie hapo, sehemu itakayofuata tutaangalia kan (FORCES)i zilizopo kwenye ndege na mihimili ya ndege (MOTION ALONG AIRCRAFT AXES). Mwenye swali lolote kuhusu ndege unakaribishwa.