Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Kuna uzi wa kifaa cha kutunza taarifa za ndege nataka kuuanzisha, vipi wadau ni uchanganye humu au nifungue thread mpya?
Weka tuu hapa hapa ili maswali yawe pamoja yote. Na uzi uwe mnono
 
Habari wadau

Baada ya kuangalia sehemu muhimu za ndege, nimeona ni busara tuangalie kifaa kimojawapo ambacho ni muhimu katika uchunguzi wa ajali. Ni baada ya kuwa nimeona kimetajwa sana kwenye comment kwa lake ambalo ni maarufu japo kwa lugha ya kindege kinafahamika kwa jina jingine. Hiki ni kifaa cha kuhifadhi taarifa mbalimbali za ndege iwapo safarini. Kifaa hiki kinaitwa Flight Data Recorder (FDR) maarufu kwa jina la " Black Box".

Histtoria yake:
Kizazi cha kwanza cha kifaa hiki inaanzia miaka ya 1950 ndipo kilianza kutumika kufuatia uhitaji wa wana anga kuwa na kifaa ambacho kinaweza kutoa angalau abc za ajali husika, kutokana na nature ya ajali za ndege mara nyingi hupoteza watu wote wanaokuwepo kwenye ndege. Hivyo kukosa hata kujua chanzo cha ajali nini! Mpaka mwaka 1965 kifaa kilikuwa kikihifadhiwa kwenye kisanduku chenye rangi nyeusi, ndiyo sababu ya kujulikana kama "Black box". Mwaka 1965 shirika la kusimamia mambo ya anga la dunia (International Civil Aviation Organization) liliamuru kifaa hiki kiwekwe kwenye kisanduku cha rangi ya njano angavu au rangi ya orange angavu (bright yellow or bright orange) ili kurahisisha uonekanaji wake wakati wa kukitafuta pindi inapotokea ajali.
Katika kizazi hiki cha kwanza ilikuwa ni tape ambayo ipo katika mfumo kama ule wa redio ya kanda.

Kizazi cha pili cha kifaa hiki kilianza miaka ya 1970. Hapa tape iliboreshwa kidogo ikawa na urefu wa futi 300-500, inaweza kurekodi data kwa takribani masaa 25 na ikiwa ni magnetic tape. Vifaa vya kizazi hiki bado vinatambuliwa na ICAO, hivyo bado vinaweza kutumika kwenye ndege.

Pamoja na kuboreshwa kwa uwezo wa kuweza kurekodi data kwa muda mrefu, bado FDR hii haikuweza kuhimili data zinazotoka kwenye sensor mbalimbali kwenye ndege kwa wakati mmoja. Hivyo miaka ya 1980 kuligunduliwa kifaa kingine ambacho kinasaidia kupokea data kutoka kwenye sensor mbalimbali. Pia wakati huo FDR ilikuwa imeboreshwa na kurekodi data katika mfumo wa digital. Kifaa hicho ni Flight Data Acquisition Unit (FDAU).

Hadi sasa teknolojia ya kifaa hiki ni kizazi cha tatu ambayo ni Solid State Technology, yaani maana ni kwamba kifaa hiki utunzaji wake wa kumbukumbu upo katika solid memory storage. Hii ni kama unavyoona hizi memory cards na flash disks. Hiyo ndiyo solid state memory storage.
Uwezo wake sasa hivi ni mkubwa sana, kinaweza kupokea signal kutoka kwenye sensor mbalimbali takribani 88 kwa wakati mmoja.

JINSI KINAVYOFANYA KAZI:
Flight Data Recorder ikisaidiwa na Flight Data Acquisition Unit ambayo inafanya kazi kama interface (kiunganish) hupokea na kuhifadhi taarifa mbalimbali kutoka kwenye sensor za vifaa vya ndege. Taarifa hizi ni kama;
Uelekeo wa ndege, speed ya ndege, mwinuko wa ndege, power ya injini na position ya vifaa vinavyotembea vya ndege vinavyosaidia ndege kupata kani-mnyanyuo (lift force). Endapo ndege itapata ajali basi taarifa hizi zilizohifadhiwa zitasaidia kujua chanzo cha ajali ni nini. Kama ni makosa ya rubani, matatizo ya mifumo ya ndege ama ni sababu kutoka nje, kama vile upepo mkali na vinginevyo.

Pamoja na kifaa hiki pia kuna kifaa kingine ambacho pia husaidia uchunguzi wa ajali. Kifaa hiki hurekodi sauti za mazingira ya cckpit. Kifaa hiki kinaitwa Cockpit Voice Recorder (CVR). Vifaa hivi huweza kuwa vimehifadhiwa katika kisanduku kimoja ama tofauti. Mbali na uchunguzi wa ajali, pia FDR husaidia kujua hasa injini imefanya kazi kwa muda gani. Kifaa hiki kila mwaka lazima kikaguliwe na mamlaka ya anga.

SIFA ZA KIPEKEE ZA FLIGHT DATA RECORDER;
Kifaa hiki kimehifadhiwa kwenye " enclosure" ambayo ina sifa hizi:
1: Kinaweza kuhimili moto mkubwa wenye jotoridi 1100°C, kikiwa 100% kwenye moto huo, kikahimili kwa dakika 30. Endapo enclosure itakuwa na kiwango cha ED 56 Test protocol (Hiki ni kiwango cha juu sana cha material kuhimili joto), basi kinaweza kudumu katikati ya moto huo kwa saa 1 yaani dakika 60.
Kwenye moto wa kiwango cha chini 260°C (Oven test), kinahimili moto huo kwa masaa 10
2: Athari za kuanguka kwa kishindo; Kinaweza kuhimili impact shock ya kiwango cha 3400g(g ni kipimo cha shock) yaani kiwango hicho ni kikubwa sana cha shock. Kifaa hiki kipo strong.
3:Kifaa hiki kina life span ya kukaa ndani ya maji ya bahari kwa siku 30 bila matatizo.
Ili kurahisisha upatikanaji wake, kifaa hiki hakitafutwi kwa macho tu, hivi sasa kimeboreshwa, kikiwa popote hata majini kinatoa frequency ambazo zinaweza kupokelewa na receiver.

Hiyo ndiyo Flight Data Recorder Al-maarufu Black Box.
 
naomba kujua kuhusu concorde, utofauti wake na ndege zingine, usalama wake, na sababu za kuzuiwa kutumika
Concord ilikuwa inasafiri kwa spidi kubwa sana ambayo ilikuwa ni ngumu kwa rubani kuicontrol. Baada ya ajali zake kuonesha makosa ya marubani kushindwa kuicontrol ilibidi izuiliwe.
 
Ahsante sana mkuu. Umeielezea FDR (Black Box/Yellow Box) vizuuuri sana kiasi ambacho umekata kiu yangu. Ahsante sana na Mungu akuwezeshe kufanya vizuri sana kwenye kazi yako na akupe afya njema na hata promotion itapendeza zaidi.
Asante mkuu
 
Zile ni Jumbo jets. Ni pure Gas turbine jet engine. Thrust(kani inayosababisha mwendo) hutokana kutoa hot exhaust gases kwa kasi kubwa kwenye exhaust( wabongo tumezoea kuita eksozi). Zinapita juu sana kwa sababu ya mfumo wake wa engine una kelele sana.
Kumbe Jumbo jets engine zinatoa kelele nilikuwa sijui, nakumbuka ndege za ATC Boeing 737 zilikuwa na kelele sana, engine zake ndo Jumbo?
 
Mkuu nna swali lingine, kuna mahali niliwahi kusoma nadhan ni humu humu JF. Iliandikwa kuwa ndege aina ya Boeing ina teknolojia inayoweza kumfanya pilot asiweze kui-control, hii hufanyika pale ambapo itaonekana ndege inakuwa na muelekeo wa kuleta ajali na kuanzia hapo ndege inakuwa kwenye autopilot remotely. Kama zilivyotumika zile ndege zilivyogonga yale majengo WTC, sept 11. Je hili likoje mkuu, kuna ukweli katika hilo?
 
Mkuu nna swali lingine, kuna mahali niliwahi kusoma nadhan ni humu humu JF. Iliandikwa kuwa ndege aina ya Boeing ina teknolojia inayoweza kumfanya pilot asiweze kui-control, hii hufanyika pale ambapo itaonekana ndege inakuwa na muelekeo wa kuleta ajali na kuanzia hapo ndege inakuwa kwenye autopilot remotely. Kama zilivyotumika zile ndege zilivyogonga yale majengo WTC, sept 11. Je hili likoje mkuu, kuna ukweli katika hilo?
Mkuu kwa hili nisikudanganye sina ufahamu nalo. Labda niambie ni aina gani ya Boeing ili nicheck na watu ambao wamefanya kazi na hiyo aina ya ndege. Lakini kwa knowledge yangu ya ndege nabaki najiuliza swali; kama itajiweka kwenye autopilot halafu pilot asiwe na command nayo tena, ni nani ataitoa ili kuendelea na maneuvre?
 
Mkuu kwa hili nisikudanganye sina ufahamu nalo. Labda niambie ni aina gani ya Boeing ili nicheck na watu ambao wamefanya kazi na hiyo aina ya ndege. Lakini kwa knowledge yangu ya ndege nabaki najiuliza swali; kama itajiweka kwenye autopilot halafu pilot asiwe na command nayo tena, ni nani ataitoa ili kuendelea na maneuvre?
Ngoja niutafute ule uzi uliokuwa unaelezea hiyo ishu naweza kufahamu aina ya Boeing, nnavyokumbuka mtoa mada alidai kuwa ikiwa kwenye autopilot inaongozwa na walioiweka kwenye autopilot mpaka inatua. Maana yake inakuwa haiko tena kwenye comand ya pilot mpaka inatua.
 
Mkuu kwa hili nisikudanganye sina ufahamu nalo. Labda niambie ni aina gani ya Boeing ili nicheck na watu ambao wamefanya kazi na hiyo aina ya ndege. Lakini kwa knowledge yangu ya ndege nabaki najiuliza swali; kama itajiweka kwenye autopilot halafu pilot asiwe na command nayo tena, ni nani ataitoa ili kuendelea na maneuvre?
3c8835a3ee3e4d11a916c78abb0c02e4.jpg

Nime-screenshot sehemu ya maelezo kuhusu autopilot, pitia pitia mkuu
 
Sawa mkuu, Bermuda ina maajabu yake mpaka ilipewa jina la Bermuda triangle mystry. Kuhusu ndege kupita Juu ya mlima Kilimanjaro hiyo ni kutokana na sababu ya hewa maeneo ya inaweza kuwa haina flow nzuri kwa sababu ya yale mashimo ya volcano.
Nitaomba Hiyoo triangle uielezee mkuu kama unaifahamu kivyovyote vile please shebbydo. Then kuhusu mlima wa Kilimanjaro nitoe ka sapoti kadogo kuna Uzi wa Kilimanjaro kuna mtu alisema ndege inapita pembeni kidogo na watu huwa wanaona lile shimo na mandhari yake,so in short haipiti katikati Bali pembezoni kidogo,na mfano ukatolewa air Kenya hufanya hivo.
Tuko pamoja
 
Back
Top Bottom