Kwa kuongezea, niliwahi kuambiwa kwamba kuna spidi ya chini (minimum speed) ambayo inaiwezesha ndege kueleaa hewani na ndio maana ili iweze kupata, ni lazima ikimbie hadi ifikie hiyo speed ndio dude linanyanyuka. Hivyo hivyo kwenye kutua, hawezi kupunguza speed chini ya hiyo vinginevyo ataidondosha kabla haijagusa chini.
Tofauti ya pressure (msukumo) wa chini ya mabawa (flat) na juu ya mabawa (curved) ndio unaozaa kani mnyanyuko (uplift) na hutegemea speed ya upepo inayopita kwenye mabawa kutokana na speed ya ndege yenyewe. Kama sikosei nadhani ndege nyingi huanza kunyanyuka zinapofikia speed ya 150km/hr na kuendelea.
Hili suala brother wetu Shebbydo ningeomba ikimpendeza, aliweke vizuri. Natanguliza shukrani.