Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,285
9,920
TRA leo wamafanya mazungumzo na wawakikishi wa Mitandao hiyo ya kijamii kuona namna Mitandao hiyo inaweza kulipa kodi kutokana na hiduma wanazotumia wananchi.

=====

DARESSALAAM: Timu ya Wataalam wa Kampuni ya meta inayomiliki mitandao ya @facebookapp instagram pamoja na Whatsapp leo 21 Aprili, 2022 imefanya mazungumzo ya awali na TRA kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.

Pia soma;


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wake wa huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa ufafanuzi baada ya TRA kukutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini.

"Mkutano kati ya TRA na kampuni ya META ulikuwa ni mkutano wa awali wao kuweza kuelewa mazingira ya sheria za kodi za Tanzania na pia kuweza kutupitisha katika jinsi wanavyofanya biashara yao na wanavyotozwa kodi katika Nchi nyingine.

"Lengo ni kufikia mahali huko mbeleni ili kampuni hiyo ichangie kodi kwa pesa inayopata kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao, Wananchi hawatakiwi kuwa na hofu yoyote kwasababu hii inahusu biashara inayofanyika na kampuni hiyo katika Nchi mbalimbali.

"Na hili sio jambo geni lipo dunia nzima, tumesikia Kenya tayari hilo lipo, Benin, Cameroon na Nchi za Ulaya ambako kampuni hizo kubwa za mitandao duniani zinachangia kodi kwa kufuata sheria za nchi husika na taratibu za kimataifa," - Kayombo

20220421_155335.jpg
20220421_155332.jpg
20220421_155329.jpg
20220421_155324.jpg
 
Back
Top Bottom