Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,290
- 5,767
Tahadhali : huu si mjadala wa mashambulizi ya Kidini. Ni mjadala qwa kisomi wa kujenga Hoja. Kelele za Dini zenu pelekeni kwingine. Hapa tunataka hoja na uelewa. Sisi wengine hatuna Dini.
1. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini huyu Nabii kwenye Quran anatambulika kama Issa Bin Mariam. Kwa jina la Mama yake ni si ukoo wa Baba yake kama wengine wote waliosalia.
2. Je wenye Quran wanamwamini ktk namna gani? Kuwa ni mtume. Je ni mtume kama Mtume mwingine?
3. Je wasiotumia Quran wanamfaham na wanamkubali kuwa ni mmoja ya manabii?
Naomba tujadiliane kwa utulivu kwa nia ya kujifunza. Mimi naifaham Quran na ninaifahamu Biblia. Kwa kuwa nmekulia katika mazingira yote mawili.
Mimi nikupe majibu kwa ufaham wangu
1. Nabii issa Anatambulika kwa jina la Issa Bin Mariam kwa kuwa amezaliwa na Mama Bila baba.
2. Kwenye Uislam Isa Bin Mariam ni mtume kama mitume wengine aliyetumwa na Mungu kwa kazi maalum (kila mtume alikuja kwa jukumu maalum kuendana na changamoto mbalimbali ikiwepo kuamini vitu tofauti na mungu, magonjwa, machafu, nk
3. Sasa ukisema wasio tumia qurani watamtambua kama mtume wao; kama unarefer Quran maana yake unaongelea Waislam sasa sijui nikusaidieje?