Sasa huoni kama hao ndio walipaswa kutukuzwa sana na kupigiwa mfano kuliko YESU ?Adamu na Hawa walikuwa binadamu wa kwanza hawakuzaliwa kwa kubebewa mimba ndio maana hawana wazazi
Sasa huoni kama hao ndio walipaswa kutukuzwa sana na kupigiwa mfano kuliko YESU ?Adamu na Hawa walikuwa binadamu wa kwanza hawakuzaliwa kwa kubebewa mimba ndio maana hawana wazazi
Kwanini aitwe bin Yussuf? hakumzaa wala hana nasaba nae. Kwanini umpe ubin ambao hauhusiki na yeye hata kisheria! hivi unaelewa maana ya Bin?Huyu ni Baba Wa kumlea, angalau mmgemuita isa bin Yusufu. Kama Leo tumekubaliana Yesu hana Biological father, Basi tukubaline baba ni Yule aliyekuwa akimuomba na anasema yuko naye siku zote yeye na Baba huyo ni ummoja, uungu una yeye 100% na Yesu sio Kiumbe ni Muumba pamoja Baba yake. Sasa rudi kusoma Yohana Moja uje ubatizwe
Mnashangaza sana mnaikataa biblia halafu mnaitumia kujibu maswali
Mbona hamjibu swali
Adam na Hawa, hawana Baba wala Mama. achilia mbali kuzaliwa, hawa ndio hawakuzaliwa kabisa lakini wamekuja duniani, kwanini basi hawa wasiwe Waungu? Naomba jibu.Sisi tunafahamu kwamba Yesu hakuzaliwa kwa namna ya kawaida inayofahamika kwa kuwa ni Mungu. Sasa tunawauliza wanaosema sio Mungu kwa nini basi yanamuita kwa jina la mama yake na sio la mume wa mama yake?
Unamjua ROHO anayezungumziwa na waislamu ? Huyu hapa ?
16. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki.
17. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.
18. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.
19. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.
20. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?
21. (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
23. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
24. Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
25. Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
26. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.
27. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
28. Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.
29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi. (Mariam : 16-29)
Huyo ndio ROHO na huo ndio uzao wa YESU.
17. Tukampelekea Roho wetu, HAWA wengi walikuwa kina nani maana inaonesha walikuwa mobu kubwa , Yesu na huyo issa sio wamoja wapo tofauti kabisa,
17. Tukampelekea Roho wetu, HAWA wengi walikuwa kina nani maana inaonesha walikuwa mobu kubwa , Yesu na huyo issa sio wamoja wapo tofauti kabisa,
@Khantwe hakuna muislamu anaekataa biblia, ila inapingwa kwasababu ya kuongezewa aya za kishetani..
Biblia ilikuwa sahihi hapo zamani kwa asilimia 100% ila kwa sasa wameongeza na kupunguza maneno
Kumbuka ule mkutano uliofanywa kule ulaya kwaajili ya kupiga kura vitabu gani viwepo na gani visiwepo
Nikisoma na kusikia habari za Quran na Biblia jinsi zilivyofanana huwa najua kabisa kuna uongo umefichwa katikati ya ukweli na ndio maana ni ngumu sana kujua usahihi wa maandiko kati ya dini mbili hizi. Mungu yupo ila kuna sehemu hizi habari zimekuwa twisted kumuhusu na ndio maana kuna madhehebu katika uislamu na ukristu.
Biblia ni kama maktaba ya vitabu na toka mwanzo kuna baadhi ya vitabu vilienguliwa kutokana na vigezo fulani ili kutengeneza biblia ya kwanza. Fuatilia historia ya utengenezaji wa biblia personally na uache kuyumbishwa na maneno ya kusikia. Unaruhusiwa kuwa na OPINION ila kama mtu muerevu yakupasa kutumia FACTS katika mambo muhimu. By the way hakuna mabishano ya kiimani yaliyowahi kuisha hivyo, focus kwenye kuwa mwema na kuamini imani yako
Sababu hapa tunaongelea elimu na elimu iko wazi,naomba uonyeshe huo uongo uliofichwa na umejuaje hilo ?
Pili,naomba uniambie wewe huwa unatumia njia gani kujua habari gani ya kweli na ipi ya uongo ? Jitahidi kuandika kielimu na usiandike kihisia.
Na hakuna kipengele chochote katika elimu ya mijadala kinachosema kwamba muafaka mwisho wa mjadala ni lazima.
Cha msingi katika mjadala ni hoja,na mwenye kuelewa ataona ukweli uko wapi,akiamua ataufata asipoamua hta ufata.
Tuendelee...
Kwa hiyo apo ww ukitaka kusema umepeleka kitu flani , utasema nimepeleka kitu changu au utasema nimepeleka kitu chetu embu weka sawaHuo ni ufasaha wa lugha,yaani wngi kumaanisha moja katika lugha ni maarufu sana hata kwa Waswahili.
Unspo kataa kuwa YESU si ISSA huku ni kuihujumu elimu na kuukata Ukweli wazi wazi. Na huwezi kapinga hili kielimu hata ukipewa miaka mia. Huwezi kumtofautisha YESU na ISSA kielimu zaidi ujinga na mapenzi ya upofu.
Anaezungumziwa ni mmoja bali kwa maelezo tofauti.
Mtu anauliza swali nawewe unauliza swali badala ya kujibu.Tupe ushahidi kuwa yesu ni mungu
Swali langu ndio mwanzo wa jibu la swali lake.Mtu anauliza swali nawewe unauliza swali badala ya kujibu.
Anzisha thread juu ya hilo lakwako na Inshaallah tutachangia
Kazaliwa kwa namna ipi bila ya Baba?Nani amekwambia Yesu baba ake ni Yusufu ? Sasa ndio utuambie Yesu baba ake Yusufu kimalezi au kinasaba ? Na kama kinasaba utupe ushahidi.
Kwetu sisi waislamu Yesu(Issa) kazaliwa pasi na baba,ndio maana ubini wake unarudi kwa mama,na kuitwa ISSA MWANA WA MARIAM.