Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Kwani Biblia ni kitabu kitukufu ? Je ni kitabu cha mtume gani ?

Halafu hii hoja yako dhaifu ya kutaka upewe "manuscript" ya Qur'aan nikishakujibu mara kibao lakini unaonekana umekaa kubisha bishana na si kujifunza. Nilikwambia hivi sisi tuna sanadi mpaka kufika kwa mtume,na Qur'aan tangu mtume yuko hai maswahaba walikuwa wanaihifadhi vifuani mpaka leo watu wanaihifadhi Qur'aan vifuani na elimu huenda kwa kuridhishana,leo hii mpaka kiama kinasimama hakuna hata wale walio muona Yesu walio hifadhi Injili yote vifuani,Yesu aliondoka na Injili yake.

Ajabu sasa nataka wewe uniambie iko wapi ile Injili aliyokuja nayo Yesu hata kipande cha nusu ukurasa ? Sababu Musa alikuwa na Torati,Daudi alikuwa na Zaburi. Sasa hapa ndipo utakapo kujua dhamiri ya kitabu sio mpaka kiwe cha kushikika mkononi.

Usinieletee habari za kina Luka,Mathayo,John na Marko ambao kati ya wawili hao hawakumdiriki Yesu vipi tuwaamini lwa yale wayasemayo ?
Nimewahi kukuambia na naendelea kukusisitizia.
Bibilia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na mitume, manabii na watumishi wa Mungu walioongozwa na Roho mtakatifu wasiopungua 30.

Imeandikwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1500 katika mazingira tofauritofauti kwa mfumo tofautitofauti mfano mashairi, mithali, hadithi, unabii, masimumulizi, etc. Quran ni kitabu kimoja tu ambacho kinataka kufuta kazi njema aliyoiasisi Mungu kwa miaka zaidi ya 1500 wakati chenyewe kikibaki kinaacha shaka jingi na kubwa sana hata uhalalinwa uwepo wake na mamlaka yake kama inatokana nanMungu maana kinapingana na Mungu aliyeongea na watu mbalimbalia miaka zadi ya 4000.

Hilo hoja ya Quran, ntaomba niianzishie mada tuchimbe kwa kina, nitakutag ila uje na hoja usije na evidenceless arguments. Kama ulikuwa unacopy na kupaste zile articles za ELEMA anza kusoma. Ila ukiniruhusu na kamamukiwa tayari kujifunza.

Kwa sasa naomba ushahidi wa huo mnyororo wakati kama ulikuwa ujui chanzo cha kuandika quran ilikuwa ni baada ya kila mtu kuwa anasema lake. hadi leo kila mmoja anatafsiri lwake.
 
Ina maana hamna Injili aliyokuja nayo Issa mwenyewe bali mna vitabu vya historia ya Yesu na miujiza yake. Sasa ndio mtuletee ile Injiki ya Yesu mwenyewe.
naomba ushahidi kuwa Yesu alikuja kuandika Injili. '' Kusema quran imesema sio ushahidi maana, injili ipo kabla ya quran''.
Yesu hakuja kuandika alikuja kuileta hiyo injili '' Uweza wa Mungu uletao wokovu''.

Sasa wewe unaposema Injili imekuwa corrupted huwa unamaanisha ipi, maana sijawahi kuona kitabu kilichoandikwa na Ywsu ambacho kiko corrupted angalau. kama unacho unipe.

Mtume aliposema Injili alikuwa anamaanisha agano jipya au zile injili nne maana ndizo zipo miaka yote hadi wakati yupo. Na Ushahidi upo kuwa tunachosoma sasa ndio hichohicho kilichoandikwa na eye witness wa uwepo wa Yesu na kuandikwa kabla ya 100AD.

Ila wewe nikikupa miaka 100000000 uniletee ushahidi wa alichokiandika mtume, au basi maswahaba waliokuwa wanacopy wahaya zake katika maandishi huna na hutakaa ulete, maana tumeshakubaliana na wewe ukaleta ushahidi kuwa Zilichomwa Moto. Utaaminije kitu ambacho hakina ushahidi wa maandishi wa uwepo wake asili.
 
Kwangu mimi hii sio elimu bali ni ujinga na uongo ulio wazi kabisa.

Kabla sijasema yaliyo sahihi,je unaweza kunipa andiko kutoka katika kitabu chenu linalo thibitisha ya kuwa hao ni malaika ?
Malaika waovu hao wote mkuu. utajua siku wakikuchenjia.
2 Cor 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
 
Mtume lazima aamini hilo bali sisi wafuasi wake tuna amini hilo,ila hapa inazungumziwa Injili aliyo pewa Issa na sio Injili ya Mathayo,Marko,Luka wala John.
naomba injili aliyopewa isa, au nionyeshe hiyo aliyopewa alafu sisi tumeichakachua. au majini wameeiba hata hiyo potofu.
mkuu kuwa serious huoni kuwa hizo ni propaganda.
wakristo hawajawahi kusoma kitu kinaitwa injili ya Yesu, Bali ni injili hizo nne zilizoandikwa kabla ya 100AD na hazijawahi kubadilishwa popote. Ukisema zimebadilishwa tutaenda kwenye greek manuscripts kuzikosoa.

Nashangaa mbona waislam wengine walishatoka kwenye ubishi huo wakipropaganda kuwa kumewahinkuwa na injili iliyoandikwa na Yesu. Injili ni hizo nne zinamuelezea Yesu ambaye ndiye mzizi wa injili.

Naomba ushahidi wa hiyo ya Yesu, Usiniambie mimi ninayo ndio nitoe mimi nakuhakikishia 100% Yesu hakuwahi kuandika hiyo bali ni hizi mnazozikataa na mtume alimaanisha hizohizo aliposema wakristo wahukumiwe wa injil wanayoiamaini. Hakujawahi kuwepo mkristo duniani ambaye anatembea na kitabu kilichaondikwa na Yesu. Hiyo ni historically false argument with 0 evidence.
 
hilo hoja ya Quran, ntaomba niianzishie mada tuchimbe kwa kina, nitakutag ila uje na hoja usije na evidenceless arguments.

Kama ulishindwa kujenga hoja huko nyuma,hutaweza kujenga hoja hata ukianzisha hiyo mada na kuijadili. Anzisha mada kisha uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.

Sijawahi kuja na "Evidenceless" ndio maana mpaka leo unaendelea kubisha bisha ili kujifariji.
Kama ulikuwa unacopy na kupaste zile articles za ELEMA anza kusoma. Ila ukiniruhusu na kamamukiwa tayari kujifunza.

Kwa ufupi tu zile makala nilikuwa nazi copy na kupaste na ndio msimamo wangu uko vile vile kama nilivyokuwa na copy na ku paste na uzuri makala zile ni za kielimu na zina marejeo,kama ulishindwa kujenga hoj na kuzikosoa zile makala,hutaweza kufanya hivyo tena na mimi nimesoma elimu ya Qur'aan na historia yake kwahiyo wewe anzisha mada kisha tuijadili kielimu.

Ruhusa umepewa wala usiwe na shaka.
kwa sasa naomba ushahidi wa huo mnyororo wakati kama ulikuwa ujui chanzo cha kuandika quran ilikuwa ni baada ya kila mtu kuwa anasema lake. hadi leo kila mmoja anatafsiri lwake.

Qur'aan ilianza kuandikwa tangu mtume yuko hai na mtume amakufa hali ya kuwa Qur'aan imekamilika.
Nimewahi kukuambia na naendelea kukusisitizia.
Bibilia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na mitume, manabii na watumishi wa Mungu walioongozwa na Roho mtakatifu wasiopungua 30

Unakubali kama Yesu hakuliacha jili tamko "Biblia" vipi ina maana nyinyi mnajua sana kuliko Yesu ?

Na nani aliwaambia mvifanye Taurati,Zaburi kufanya kama muongozo wenu ?

Hao mitume na manabii huo utume na unabii walikuwa wanapewa na nani ?
Imeandikwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1500 katika mazingira tofauritofauti kwa mfumo tofautitofauti mfano mashairi, mithali, hadithi, unabii, masimumulizi, etc.

Ndio utuambie ilikuwaje mpaka ikawafikia nyinyi leo hii,yaani nataka utupe chain ya wapokezi mpaka ifike kwa Yesu bila kukatika.
 
Malaika waovu hao wote mkuu. utajua siku wakikuchenjia.
2 Cor 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Ila nyinyi mlinyimwa kweli maarifa,hivi kiumbe kikijigeuza mfano wa kiumbe fulani ndi hicho kiumbe chenyewe halisia ?

Huna ushahidi wa kuonyesha ya kuwa Majini,mapepo na mfano wake ni malaika au walikuwa malaika.
 
naomba injili aliyopewa isa, au nionyeshe hiyo

Injili aliyopewa Issa iko kwenye Lawhul Mahfoodh,sisi hatuko nayo,ila tunasadikisha ya kuwa kweli alipewa Injili na tunaamini hivyo sababu tumetajiwa kwenye Qur'aan.

Na sio tu mimi nikupe au sisi tukupe,yaani hapa duniani hakuna menye Injili ya Issa,hata nyie mnakiri ya kuwa wale walioandika hiyo iitwayo Injili waliandika juu ya maisha ya Yesu na harakati zake pamoja na miujiza aliyoitenda.
 
Kama ulishindwa kujenga hoja huko nyuma,hutaweza kujenga hoja hata ukianzisha hiyo mada na kuijadili. Anzisha mada kisha uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.

Sijawahi kuja na "Evidenceless" ndio maana mpaka leo unaendelea kubisha bisha ili kujifariji.

Kwa ufupi tu zile makala nilikuwa nazi copy na kupaste na ndio msimamo wangu uko vile vile kama nilivyokuwa na copy na ku paste na uzuri makala zile ni za kielimu na zina marejeo,kama ulishindwa kujenga hoj na kuzikosoa zile makala,hutaweza kufanya hivyo tena na mimi nimesoma elimu ya Qur'aan na historia yake kwahiyo wewe anzisha mada kisha tuijadili kielimu.

Ruhusa umepewa wala usiwe na shaka.

Qur'aan ilianza kuandikwa tangu mtume yuko hai na mtume amakufa hali ya kuwa Qur'aan imekamilika.

Unakubali kama Yesu hakuliacha jili tamko "Biblia" vipi ina maana nyinyi mnajua sana kuliko Yesu ?

Na nani aliwaambia mvifanye Taurati,Zaburi kufanya kama muongozo wenu ?

Hao mitume na manabii huo utume na unabii walikuwa wanapewa na nani ?

Ndio utuambie ilikuwaje mpaka ikawafikia nyinyi leo hii,yaani nataka utupe chain ya wapokezi mpaka ifike kwa Yesu bila kukatika.

1: asante kwa ukubali. nitakutag nipe nafasi ila lazima ujue hizi imani zetu lazima tufungue ubongo hadi ambako hukuwahi kudhani ulipaswa kufikiri.
Mungu akubariki sio leo wala kesho ila wiki hii haipiti.

2: Naomba hata ushahidi wa kipande cha karatasi kilichoandikwa wakati mtume Yuko hai. Nitakutumia 10,000 ya Bundle mkuu bure.
hakipo duniani pote.

3:Mitume na manabii, walipewa na Mungu, na waliandika, ila habari za Torati, zaburi zote zipo ndizo hizo unazozisoma kwenye Bibilia. Hakuna kilichopotoka kama kipo nionyeshe, na kilipotoka lini na kwa ushahidi upi. Imefika wakati tuache kibishana tuelimishane kwa shahidi mbalimbali.

4:Hii unayoipinga, angalau uanze kunionyesha hiyo unayodaiiliandikwa na Yesu sisi tumeichakachua. Hii ni tuhuma kubwa unatakiwa uithibitishe kwanza hata angalau kwa kuionyesha hiyo iliyochakqchuliwa mkuu
 
Injili aliyopewa Issa iko kwenye Lawhul Mahfoodh,sisi hatuko nayo,ila tunasadikisha ya kuwa kweli alipewa Injili na tunaamini hivyo sababu tumetajiwa kwenye Qur'aan.

Na sio tu mimi nikupe au sisi tukupe,yaani hapa duniani hakuna menye Injili ya Issa,hata nyie mnakiri ya kuwa wale walioandika hiyo iitwayo Injili waliandika juu ya maisha ya Yesu na harakati zake pamoja na miujiza aliyoitenda.
naona umeanza usanii wakati unataka tujadili kielimu mkui.
Huku kwwnye Lawhul Mahfoodh (Preserved tablets)
aliziweka nani?
lini?
kwa nini?
zilizhakachuliwaje?
mbona ulianza kusema sisi tumeichakachua? naomba uliiona wapi tulioichakachua?

mtume akiwa hai, nimetoa hapo haya ya Surah 5: 46-47 mtume anathibitisha wakati yupo hai, ilikuwepo, na anawataka wakristo wahukumiwe kwa hiyo kama aya ya 43 ( alitoka kwenye kiti cha hukumu ikawekwa torati ili imuhukumu myahudi, akasema myahudi atahukumiwa kwa torati).

naona unaendeleza propaganda ninazozipinga mkuu.
 
Ila nyinyi mlinyimwa kweli maarifa,hivi kiumbe kikijigeuza mfano wa kiumbe fulani ndi hicho kiumbe chenyewe halisia ?

Huna ushahidi wa kuonyesha ya kuwa Majini,mapepo na mfano wake ni malaika au walikuwa malaika.
nimekupa Fungu la ziada Ufunuo 12
Shetani/ Ibirisi alitupwa na 1/3 ya malaika wote wa mbinguni waliomuunga mkono juhudi zake uovu.
Kumbuka mbinguni kwa hesabu za kadikio la chini kuna malaika zaidi ya trilioni ( 1000*1000*10000*10000*)
kuna mabilioni ya malaika wachafu mkuu.
hao unapowaita majini unawapa nafasi ya kukudanfanya zaidi.
hawana nia njema Yesu anasema wakiisha kutumia wanataka ufe hukohuko hata kama anakuletea fedha.
 
Injili aliyopewa Issa iko kwenye Lawhul Mahfoodh,sisi hatuko nayo,ila tunasadikisha ya kuwa kweli alipewa Injili na tunaamini hivyo sababu tumetajiwa kwenye Qur'aan.

Na sio tu mimi nikupe au sisi tukupe,yaani hapa duniani hakuna menye Injili ya Issa,hata nyie mnakiri ya kuwa wale walioandika hiyo iitwayo Injili waliandika juu ya maisha ya Yesu na harakati zake pamoja na miujiza aliyoitenda.
naona unayumba kila hoja inavyoyumba mkuu.
leo umesema duniani hakuna injili.
juzi injili imeharibiwa mliyonayo.
kingine mungu alilinda quran tu hizo zingine hazikulindwa wanadamu waliziachafua.
Tukiendelea hivi mkuu zurri utaona kuna mchezo mnachezewa katika belief system yenu bila kujua.
 
: Naomba hata ushahidi wa kipande cha karatasi kilichoandikwa wakati mtume Yuko hai. Nitakutumia 10,000 ya Bundle mkuu bure.
hakipo duniani pote.

Una kichwa kigumu sana,sisi tuna "sanadi" na nyinyi hamna sanadi,baada ya zoezi la ukusanyaji wa Qur'aan kukamilika,makaratasi hayakuwa na haja tena,yaani yawepo ili iweje ? Wakati watu walikuwa wana Qur'aan vifuani na wanaendelea kurithishana ?
Mitume na manabii, walipewa na Mungu, na waliandika, ila habari za Torati, zaburi zote zipo ndizo hizo unazozisoma kwenye Bibilia. Hakuna kilichopotoka kama kipo nionyeshe, na kilipotoka lini na kwa ushahidi upi. Imefika wakati tuache kibishana tuelimishane kwa shahidi mbalimbali.
Nipe ushahidi wa utume na unabii wao kutoka kwa Mungu ?

Safi kabisa,mimi kwanza ukosoaji wangu kwenye Biblia uko wazi na huu ukiushindwa tangu kipindi kile,iko hivi,nitajie chain ya walio andika Bibli mpaka ifike kwa Yesu,ukiweza mimi nakuwa Mkristo.
:Hii unayoipinga, angalau uanze kunionyesha hiyo unayodaiiliandikwa na Yesu

Sijasema Yesu aliandika,na bora hata kama angekuwa ameandika kidogo mngepata pa kuegemea,yeye alifikisha ujumbe kisha akaenda zake. Ndio mtuambie Injiki ya Yesu mnayo na kama mnayo mmeipata wapi ?
 
Una kichwa kigumu sana,sisi tuna "sanadi" na nyinyi hamna sanadi,baada ya zoezi la ukusanyaji wa Qur'aan kukamilika,makaratasi hayakuwa na haja tena,yaani yawepo ili iweje ? Wakati watu walikuwa wana Qur'aan vifuani na wanaendelea kurithishana ?

Nipe ushahidi wa utume na unabii wao kutoka kwa Mungu ?

Safi kabisa,mimi kwanza ukosoaji wangu kwenye Biblia uko wazi na huu ukiushindwa tangu kipindi kile,iko hivi,nitajie chain ya walio andika Bibli mpaka ifike kwa Yesu,ukiweza mimi nakuwa Mkristo.

Sijasema Yesu aliandika,na bora hata kama angekuwa ameandika kidogo mngepata pa kuegemea,yeye alifikisha ujumbe kisha akaenda zake. Ndio mtuambie Injiki ya Yesu mnayo na kama mnayo mmeipata wapi ?
Ubarikiwe ntaanzia hapa.
ila suala la injili ya Yesu unahaingaika hadi nakuonea huruma mkuu.
 
naona umeanza usanii wakati unataka tujadili kielimu mkui.
Huku kwwnye Lawhul Mahfoodh (Preserved tablets)
aliziweka nani?
lini?

Unakataa kwamba hakuna Lawhul Mahfoodh au ?
Sasa hii ndio Lawhul Mahfoodh,Anasema Allah aliye juu :

70. Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. (al Hajj : 70)

Yaani huko kuna kila kitu,mpaka matendo yako yapo huk yameandikwa.

Aliziweka Mola muumba na kuhusu lini anajua mwenyewe Allah.
zilizhakachuliwaje?
mbona ulianza kusema sisi tumeichakachua? naomba uliiona wapi tulioichakachua?

Una kubali Yesu alikuja na Injili ? Kama unakubali je hii mliyonayo ni kama ile ? Maana umekiri ya kuwa Walioandika injili wameandika habari za Yesu na matukio yake,sasa habari za Yesu ndio Injili ?
mtume akiwa hai, nimetoa hapo haya ya Surah 5: 46-47 mtume anathibitisha wakati yupo hai, ilikuwepo, na anawataka wakristo wahukumiwe kwa hiyo kama aya ya 43 ( alitoka kwenye kiti cha hukumu ikawekwa torati ili imuhukumu myahudi, akasema myahudi atahukumiwa kwa torati).

Nacheka sana,bado huu uhuni wa kunakili nusu nusu bado unao,kwanza ulitakiwa uanze aya ya 43 uje mpaka aya ya 40. Lakini hapa ngoja nikuwekee mpaka aya ya 48 ili ujue kulikuwa kunazungumizwa nini.

Anasema Allah aliye juu :

46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu.
47. Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.
48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. (al Maidah : 46-48)
 
Hawa ni binadamu na waliumbwa na Mungu kama ni msomaji wa biblia kitabu cha mwanzo “ basi tumuumbe kwa sura na mfano wetu” means Adam na Hawa waliumbwa Mungu na kesi yao ni tofauti na ya Yesu ndo maana tunasema ni wazazi wa kwanza sio miungu wa kwanza
Sasa wewe huoni kuwa Adam na Hawa wameumbwa kwa mfano wa Mungu?
 
Back
Top Bottom