Umeongezea hoja nyingine ambayo inamtofautisha Yesu na ISSA.
7. Yesu anasifa ya uungu Kwa mujibu wa maandiko na Utabiri aliotabiriwa nao. Lakini ISSA ni mtume kama mitume wengine, kina Daudi, Muhammad, Hosea n.k.
Rejea;
Mt 1:23 SUV
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Isaya 9:6 BHN
Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”. “Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba wa Milele”, “Mfalme wa Amani”.
Yesu kwa mujibu wa maandiko anasifa ya uungu, kama Unabii unavyomuelezea hapo,.
Msikie mwenyewe,
Yohana 9
39 Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.”
Huyo ni Yesu, ndio maana nimeeleza Yesu na Issa ni Watu Wawili tofauti. Wakati Yesu akija kuhukumu Ulimwengu, ISSA atakuja kuoa