Na Roho mtakatifu ni Nani? Au ndio huyohuyo Yesu?
Sent from my CPH1803 using
JamiiForums mobile app
Ndio huyo huyo Yesu Kristo. Unahitaji kufundishwa ulimwengu wa Roho na wa Mwili.
Roho Mtakatifu ambaye ndiye Neno alifanyika mwili akaja duniani akajitambulisha kwetu kama Mwana wa Mungu.
Zama za Agano Jipya.
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Mnao angalia mwili ni ngumu kidogo kulielewa hili.
Mgekuwa na macho ya Kiroho mngejua kuwa.
Mungu wa Wakristo anaongea na sisi kama Baba, kama Mwana na Kama Roho Mtakatifu.
Hili limetoka kwa Neno la Kinabii
Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; (Mwana wa Mungu) Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.
Isaya hajasema ataitwa majina yake, bali
Ataitwa Jina lake. Yaani hayo majina yote ni jina moja la Mungu mmoja.