The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Viongozi wanatumia ujinga walionao wadanganyika wengi ili kujinufaisha, wanajua fika kuwa sio wananchi wengi wanasoma haya tunayoaandika, wapiga kura wengi ni wa kununuliwa hivyo wala hawakosi usingizi.

Kinachosaidia labda ni kuwa waandishi wengi wanapata cha kuandika humu, nao hawaandiki yote, naona the Citizen wanaanza kuja moto!

FD
 
Lakini je waandamanaji watajitokeza?? ngoja tusubiri maana watanzania kwa maneno hawajambo ukishawaambia twende sasa msitari wa mbele utasikia excuse kibao. Tusubirie tuone
 
Mzee Mwanakijiji.....upo? issue ya barua ya kuzungusha kwenye mtandao inaendelea ???? Sauti za wasiokuwa nchini itasikikaje au wasioenda kwenye maandamano...nipo nchini hayo maandamano siyo tishio hapa. Watu wanaendelea na mambo yao.The common man is busy looking for daily bread, sana sana naona yanaongeza foleni tu. Labda tuone kwenye vyombo vya habari jioni...God knows if they give us enough air time. Mimi naona kina Mnyika na Mbatias wamekuyrupuka hawaelewesha umma issue wanaanza kuandamana....kumbuka most of the Tanzanians are "in love with JK" unahitaji kuwa convice kwanza kwamba "mkombozi" anachemsha!
 
MMh mama lu kumbe na wewe Timu ya Taifa..Jk..maana serikali Ya JK imekua kama Timu Ya taifa Kila mtu anashangilia..sasa ndio wewe mama lu..nilidhania utatia Mkazo kwenye maandamano naona una bonda..usiwe hivyo mie mwenyewe nilikua namfagilia ila nishaona kaanza kukipaka haina haja ya kumfahilia tena..wee hebu angalia hawa viumbe hapa..utaamini kuna watu wanacheza na Fedha..?http://jambophotos.com/displayimage-1-301.html angalia hapo kisha fikiria jamaa wanavyotafuna hela..utalia mwanangu
 
Someni mwangalie wanao laumu magazeti ya Mengi ambayo mimi nasema ni Pro Govt . Yaani wanaandika kama vile habari hizi hazipo kabisa na zinatungwa UK . Tuna kaiz kubwa . Soma habari hii Ruksa wapinzani kuandamana`

2007-01-20 10:29:30
Na Romana Mallya


Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam, limeyabariki maandamano ya vyama vya upinzani yatakayofanyika leo yakiwa na lengo la kulaani wanachodai kuwepo kwa ufisadi serikalini na kashfa ya ununuzi wa rada.

Vyama vilivyopanga kushiriki maandamano hayo ni CUF, CHADEMA, UDP, TLP na NCCR Mageuzi.

Aidha, Jeshi hilo limevihakikishia ulinzi vyama hivyo wakati wote wa maandamano hayo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana, alisema maandamano hayo yataanzia Ubungo Maji saa 5:00 asubuhi kupitia Barabara ya Morogoro na kuishia viwanja vya Jangwani ambapo baadhi ya viongozi wa vyama hivyo, watazungumza na waandamanaji.

Aliwataka wananchi ambao hawahusiki na maandamano hayo kuendelea na shughuli zao bila wasiwasi wakati waandamanaji wakipita.

Pia, aliwataka watakaoshiriki maandamano hayo kutumia upande mmoja wa barabara ili kuruhusu upande mwingine utumike kwa shughuli za kawaida.

Maandamano hayo ni matokeo ya taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja la nchini Uingereza la The Guardian likidai kwamba, ununuzi wa rada hiyo ulikuwa na mianya ya rushwa.

Gazeti hilo lilidai kuwa, wakala mmoja wa mpango wa ununuzi wa rada hiyo alilipwa kwa siri dola za Marekani milioni 12 (sawa na Sh. bilioni 15) kwenye akaunti yake nchini Uswisi.

Gazeti hilo lilizidi kufafanua kuwa, malipo hayo yanahisiwa kwamba yalifanyika katika mazingira ya uficho ili kufunika mambo mengi yanayohusiana na mkataba wa ununuzi wa rada hiyo iliyoigharimu Tanzania zaidi ya Sh. bilioni 50 mwaka 2002.

Akizungumzia suala hilo katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, hivi karibuni, Rais Kikwete alisema suala la ufisadi linalohusiana na ununuzi wa rada hiyo, pia ni aibu kwa Uingereza na si kwa Tanzania peke yake kwa kuwa taasisi iliyohusika na mauzo hayo, ilikuwa ya serikali ya nchi hiyo.

``British Aero Space si kampuni binafsi, ni ya serikali...ni aibu kwa nchi kubwa kama Uingereza kuiibia nchi maskini kama Tanzania, `` alikaririwa Rais Kikwete alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) katikati ya wiki hii.

SOURCE: Nipashe
 
Shemzigwa....re read nilichoandika..Mimi sio shabiki wa JK.. Usijali.
 
Habari za siku wazee wa kazi..niko nyumbani Tz baada ya kuwa ughaibuni kwa muda kidogo. Juwa lianwaka kwelikweli. Waandamanaji ndo wanajikusanya kuelekea kwenye viwanja vya jangwani na punde viongozi wa walioandaa maandamano watatoa mihadhara. Nitakupeni the very updated na lates kadri nitakavyozipata. Kazi njema wanaforum.
 
mzee Kingwee Tunazisubri..Hizo nyeti Au sio babake..Usisite kutudokezea
tunahamu ya kujua jamaa wako fiti au maneno tu..Mama lau usiwe na wasi nimekuelewa!!!
 
Sasa hapa lazima mtu atolewe kafara kusevu ngoma.Hivi Sumaye yuko wapi?
 
Alnadaby,
Sumaye anatanua Marekani. Kajiandikisha kusoma chuo kikuu cha Harvard.
 
they paid R1billion as bribe!, GOD.........! WITHER AFRICA!!!
-----------
NPA agrees to work with UK in probe of SA’s BAE arms deal
JONATHAN KATZENELLENBOGEN


SIX months after the first request, the National Prosecuting Authority (NPA) has agreed to co-operate with the UK Serious Fraud Office’s (SFO’s) investigation of BAE Systems’ involvement in SA’s multibillion-rand arms deal.

This came just days after mounting political pressure on British Prime Minister Tony Blair to let the probe of BAE’s dealings in SA and Tanzania go ahead.

An investigation of BAE’s dealings with Saudi Arabia was controversially dropped last month, with “national security interests” being cited as the reason. It has been alleged that BAE Systems operated a slush fund to pay members of the Saudi Royal Family.

The Saudis had reportedly threatened to cancel arms purchases from the UK if the investigation went ahead.

NPA spokesman Makhosini Nkosi said on Friday that “we are in the process of effecting the process” of co-operation with the SFO investigation. However, he would not be drawn on what information the SFO had requested from SA.

The NPA’s willingness to co-operate comes six months after the initial request for information in the investigation that began two-and-a-half years ago. Earlier in the week SFO spokesman David Jones said the “SFO is seeking co-operation from SA. That co-operation has yet to be executed.”

The SFO is said to be looking into allegations that BAE Systems paid R1bn in commissions to individuals in SA who were in a position to influence the arms package. SA has agreed to buy a package of 24 Hawk fighter trainers and 28 Gripen fighters from BAE Systems.

This week the leader of the UK’s Liberal Democrats, Menzies Campbell, insisted that the SFO be allowed to complete its investigation of BAE Systems’ dealing with SA.


The Organisation for Economic Co-operation and Development added to pressure on the UK government to press ahead with the probe, when its working group on the Anti-Bribery Convention voiced “serious concerns” about the decision to halt the Saudi investigation.






The working group will discuss the issue further in March.

This week, Blair strongly defended his decision to drop the corruption probe, saying it would have “materially damaged” the UK’s relationship with Saudi Arabia, which was “vital” in fighting terrorism.

But Britain’s attorney-general Lord Goldsmith said on Thursday that the decision to call off the probe was an uncomfortable one. “It is very important to make it clear that dropping the investigation into alleged bribes paid by BAE Systems — and it was not an entirely comfortable decision — doesn’t mean we are backing off in any way from our commitment to tackling international corruption.”
 
Masikini Africa we sometimes need people like Mugabe japokuwa si kwa kila jambo .
 
It's about TIME!....

Safi sana baada ya kilio cha miaka kuwa JF tunapiga makelele hali vyama vya upinzani wamekaa chini wakishuhudia haya machafu yote. Walishindwa hata kunyoosha kidole kazi kupongeza na kusubiri hizo deal za kisiasa baina yao.

Mkandara,
Kweli unaamini haya maandamano yataisaidia kuimarisha vyama vya upinzani? Au mimi nakosa kile unachotaka kusema?
Wakati inaweza kuwa njia moja ya kuhamasisha wananchi maandamano hayana impact yeyote kwa siasa za Bongo. Kwanza ukiona maandamano yameruhusiwa ujue watawala wameshagundua kuwa hayana kitu cha kuwafanya wahofie mkate wao.
Ziara za Mbowe mikoani zina impact kubwa mno kuliko hayo maandamano. Changamoto ya Ndesamburo inachachu kubwa sana ndani yake kuliko hayo maandamano.
 
Home News
Opposition decries graft in government
KILASA MTAMBALIKE
Sunday News; Sunday,January 21, 2007 @00:08

‘BLUE guards’ form a security wall ahead of leaders of the Opposition during their demonstration in Dar es Salaam yesterday.(Photo by Bernard Rwebangira)

OPPOSITION parties said yesterday that they were not always against the government, promised to support it where it does well and criticise it when it errs.

National Chairman of the Civic United Front (CUF), Prof Ibrahim Lipumba told a rally at Jangwani grounds in Dar es Salaam yesterday after a demonstration that the Opposition only had the best interests of the nation at heart and wanted to see action taken against perpetrators of graft.

Prof Lipumba said the government should form a committee of prominent and ethical people, to look into all past government contracts that seem dubious.

The demonstration was organised by an umbrella of opposition parties to protest what they termed as controversial acquisition of a radar system by the government in 2002.

It was a calm demonstration escorted by police officers that started at Ubungo, through Morogoro Road to Jangwani grounds where leaders addressed a crowd of between 400 and 500 people, who were later in the evening scheduled to have a communal meal.

On their opinion about the new draft bill on corruption, all the opposition leaders present at the rally said that they had not read the document as yet, so they could not comment.

Opposition leaders who were present were Mr Augustine Mrema of Tanzania Labour Party (TLP), Mr John Cheyo of United Democratic Party (UDP) and Mr James Mbatia of NCCR-Mageuzi. There were also Members of Parliament from Opposition parties.


HABARI ZA GAZETI LA SERIKALI
 
Tabasamu,

Hakuna Kiongozi yeyote duniani asiyeogopa maandamano hasa yale yanayoihusu serikali moja kwa moja. Kwa sababu maandamano huwashirikisha hata wale waliolala kuamuka na kuuliza - KUNANI?..
nadhani unakumbuka maandamano ya China, Poland na hata Ukraine kwa uchache jinsi yalivyoweza kusambaza habari na harakati za mapinduzi yao ya kifikra.

Kweli inawezekana Mbowe kwenda kwake huko mikoani ilikuwa na impact kubwa lakini hizi ni siasa hazina ushahidi na zaidi ya hapo wewe na mimi hapa hatufahamu alichofanikisha mbali na kuziwekea maanani hizo hutuba.

Maanadamo haya Dar nzima wanaipata na imeanza kutangazwa hata nchi za nje!... Hili ni tishio kubwa kwa utawala na lazima JK itamkosesa usingizi. na kama ingekuwa uwezo wangu hawa jamaa wangeahidi maandamano mengine makubwa zaidi (Mjini -Mnazi mmoja) hadi hapo JK atakaposimama kuhakikisha kuwa haki yao haipotei bure.
 
Well said Mkandara, watanzania nyumbani bado ni waoga lakini polepole wataanza kuona na kujiuliza. Leo mkutano wa EAC Temeke wamekataa jumuiya ya afrika mashariki kwa wajumbe wa kamati na hivyo hivyo itaendelea hadi nchi nzima watasema hatutaki.

Mwanzo mzuri na mafanikio yatatokea.
 
Jamani habari ya Maandamano mbona haipatikani ? Jambo forum hakuna hata mmoja aliyepata bahati kuwepo jangwani ? Naona magazeti ya Mengi hayana habari hii kabisa kama vile hili tukio halikuwepo. Je mwenye habari zaidi ?
 
kuhusu maandamano haya, kwa maoni yangu yameharakishwa. Ili uweze kufanya maandamano yenye nguvu zaidi unahita mambo haya:

a. Jenga kesi ya kwanini mnaandamana. Hoja tulizozitoa humu kuhusu shilingi bilioni 40 zilizotumiwa kununua rada na hizo bilioni 12 (toka ya hizo 40) zilizotumika kumlipa dalali, zingefafanuliwa kwa wananchi wa kawaida na kuonesha zingeweza kuwaletea mabadiliko kiasi gani. Kesi ingejengwa vizuri kuhusu suala la Lowassa na Mengi. Kufanya hivyo wangenunua matangazo radioni, magazetini na kwenye televishini kuonesha ubovu huo (siko nyumbani sasa sijui kama walifanya hivyo). Unachofanya ni kuwafanya watu waelewe ni nini kinaulizwa? Lengo ni kuwafanya watu wa kawaida, (gengeni, sokoni, shambani, kwenye ulabu n.k) waanze kuzungumzia rada kama radi iliyotuunguza!

b. Watu wakishaanza kuzungumzia, la pili ndio unawaambia lazima tupinge na tutake maelezo, na njia pekee ya kufanya hivyo (kwani Bungeni hatuna ubavu) ni kuonesha kwa kutumia wingi wetu kuwa tunataka maelezo na hatua za dhati. Hivyo unaanza kuwahamasisha watu (siyo kwa kutoa tangazo kwa waandishi wa habari - hiyo ni kwa wasomi na vyombo vya habari) bali kwa kupita mitaani na kuwafikia watu mitaani waliko. Hebu fikiria Lipumba anatembea Mitaa ya Manzese, Mnyika Ubungo, Mbatia Kinondoni, n.k wakipokezana kwa wiki nzima na kuhamasisha watu wajitokeze kwenye maandamano ya siku ya jumamosi.

Sasa ni kweli maandamano yameshafanyika, lakini next time nawasihi wapinzani wasiharakishe kufanya hivyo. CCM inanufaika kwa hilo. Anyway, bora kufanya hivyo na watu kidogo kuliko kukaa kimya na kuendelea kutanua!
 
Back
Top Bottom