The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Sam,
Ooh by the way who are CorpWatch?
Logo yao inasema CorpWatch - Holding Corporations Accountable kisha mission yao ni hii:-
CorpWatch investigates and exposes corporate violations of human rights, environmental crimes, fraud and corruption around the world. We work to foster global justice, independent media activism and democratic control over corporations.
 
Mzee Mwanakiji...hii barua iwe na maelezo ya kina kuhusu huu "uozo". Magazeti ya bongo hayaelezei hizi details kama humu yenyewe yanakuwa ni watu wa "headlines " ili wauze at the same time ...wapendwe na serikali.In simple terms watu waelewe kuwa "tumeibiwa, tumedanganywa na kuna rushwa imeendelea!". Tu waambie wananchi hizi pesa zingewezaje kutumika vizuri zaidi nchini(examples).Na tuseme what we need...waliohusika wawe put to task! NDIO MAANA YA UTAWALA BORA!!!!!!!!!PUT PRESSURE TO THE PUBLIC.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Vyama vya siasa vya CUF, CHADEMA, TLP, UDP na NCCR Mageuzi kwa kushirikiana na kambi ya upinzani Bungeni vimendaa maandamano na mkutano wa hadhara jumamosi ya tarehe 20 Januari 2007.

Maandamano hayo yataanzia Ubungo (mkabala na TRA/ubungo maji) kuanzia saa 5 asubuhi kupitia barabara ya Morogoro mpaka uwanja wa Jangwani na kufuatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara.

Lengo kuu la maandamano hayo ni kuunganisha nguvu ya umma kulaani ufisadi uliokithiri katika serikali inayoongozwa kwa utawala mbovu na CCM unaojitokeza katika nyanja mbalimbali ambao ni chimbuko la kuendelea kwa umaskini miongoni mwa watanzania.

Maandamano hayo pia yatatoa ujumbe wa mshikamano (political support) kuunga mkono jitihada za wabunge wa upinzani za kukabiliana na vitendo vya rushwa vinavyoendelea kufumbiwa macho na serikali pamoja na tuhuma zingine za kuingiliwa kwa shughuli za Bunge.

Katika maandamano hayo masuala yenye mazingira ya rushwa kubwa yatawekwa wazi na athari zake kwa wananchi zitawekwa bayana ili watanzania waweze kuelewa athari za vitendo hivi vya ufisadi kwa mustakabali wa taifa.

Baadhi ya masuala yatakayozungumziwa ni kashfa ya ununuzi wa Rada, Tuhuma ya rushwa kwa wabunge na mhimili wa serikali kuingilia bunge kama ilivyoibuliwa na Mheshimiwa Ndesamburo na Kashfa ya mikataba katika sekta ya nishati ikiwemo Richmond na IPTL.

Mambo mengine yatakayozungumziwa ni pamoja na mazingira ya rushwa katika mikataba ya madini, ujenzi wa jengo la gharama kubwa la BOT na matumizi ya pesa za mifuko ya hifadhi za jamii(NSSF/PSPF) nk.

Maandamano na mkutano huo wa hadhara vitaoongozwa na viongozi wakuu wa vyama na wabunge wa kambi ya upinzani.

“Tunawaomba watanzania wote bila kujali itikadi kufika kwa wingi katika maandamano na mkutano huu kujua siri zilizomo katika masuala haya na athari zake kwa maisha ya wananchi ya kila siku. Katika mkutano huu maazimio maalumu yatafikiwa kuhusu mwelekeo wa kukabiliana na ufisadi nchini”.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na mratibu wa maandalizi- Wilfred Lwakatare 0713 237869.

Imetolewa 18 Januari 2007 na :

John Mnyika
Mjumbe
Kamati ya maandalizi
0754 694 553
 
Jamani kwa mtu yeyote mwanaforum aliyoko Dar bongo aturekodiye yayo maandamano ya kesho na mkutano tutaweka humu kwenye forum tutatuma wakala wetu hapo dar ajekuchukua hiyo tape record kwenye min div cassete umoja wa watanzania waishio EU,USA,ASIA, tuliondoka nyumbani kwa sababu ya chama Tawala CCM tutarudi tukipata chama kingine

Tutaijenga Tanzania kwenye Internet kwa kusema ukweli bila uwoga,na kujiamini,

Mungu ibariki nchi yetu Tanzania inayo zulumiwa na wachache

asanteni
 
Jasusi/Tabasamu/Lunyungu

Natumaini baada ya kunipinga kuhusu vyama vya siasa kuandaa maandamano kupinga rushwa zinazoendelezwa nje nje, hatimaye vimekubaliana na mawazo yangu ya kuandaa maandamano. Huu ni mwanzo tu na natumaini WTZ walio nyumbani watajitokeza kwa wingi kupinga vitendo viovu vya wachache wanojilimbikizia mali.

Nawatakia mafanikio makubwa wenzetu nyumbani.
 
Wacha sina kumbukumbu kama kuna siku nimepinga maandamano ya aina hii . Kama nilifanya basi nitakuwa akili zangu zilikuwa kama za Mzee wa London ama Mtetezi . Tuna watakia kila jambo jema wale ambao tutakuwepo kwenye maandamano
 
Lunyungu

Wewe alisupport kwa kusema Tabasamu anipe mimi darasa kwa sababu mimi ni CCM jambo ambalo nilikwambia at the moment sina chama. kubali makosa ulifanya data zipo hapa in black and white.
 
Well, Maandamano na naona ni hatua moja nzuri lakini inatakiwa shinikizo zaidi baada ya watanzania kuelewa nini wanachodhulumiwa.Lazima wamwambie JK kuwa wanataka kuona kama alivyofanya kwenye mauaji ya wafanyabiashara kule Sinza.Nini kinafanya kashfa hii ya rada na umeme visichunguzwe??Migomo ndo lugha inayowafaa ili waelewe tunamaanisha nini.It is time to say enough is enough.Serikali ya Tanzania ni jeuri sana hawaelewi lugha ya maneno.
 
Nyangumi wanaogopa sana kwa kuwa Wooooooooooote JK , EL , Mkapa wote hawa wamo sasa wanaweza kweli kujishitaki? Sinza jamaa aliwatoa kafara wale maaskari lakini kama yale mauaji yangalitokea leo hii sijui kama uchunguzi ungalifanyika .Sina hakika sijui .
 
Jasusi/Tabasamu/Lunyungu

Natumaini baada ya kunipinga kuhusu vyama vya siasa kuandaa maandamano kupinga rushwa zinazoendelezwa nje nje, hatimaye vimekubaliana na mawazo yangu ya kuandaa maandamano. Huu ni mwanzo tu na natumaini WTZ walio nyumbani watajitokeza kwa wingi kupinga vitendo viovu vya wachache wanojilimbikizia mali.

Nawatakia mafanikio makubwa wenzetu nyumbani.

Wacha,
Bado nasimamia palepale. Maandamano and then what!? Kesho vyama vitaandamana na kisha watahutubiana hapo halafu sasa nini kitatokea baada ya hapo? Sehemu sahihi ya suala hili kushughulikiwa ni bungeni na mahakamani hizi zingine ni ngonjera tu.
Bungeni tuchukulie kwa mfano wabunge wetu wangeshupalia kama lile suala la Kitine na matibabu hewa, bila shaka hili lingepata ufafanuzi na watu kushughulikiwa lakini aa wapi, tuna watanzania ambao hawana dhamiri (conscious) kabisa kwa maneno mengine ni sawa na hayawani tu.
 
Pia mbinguni huwezi kwenda tu kwa sababu umekufa. Matendo yako hapa duniani yataamua uwe wapi
 
bravo ,saa ya ukombozi imewadia,.

wajameni kama ni kashfa hii serikali imezidi ,mzee mwanakijiji nimekusikiliza ,safi sana kwa kujitoa kufichua maovu tupo nyuma yako ,sasa angalia Wakati wa kutimiza mwaka mmoja wa rais ikulu,palitokea habari kuwa RICHMOND walifanikiwa kuingiza kwenye grid ya taifa kw20,sasa leo TANESCO wanaibuka kusema kuwa RICHMOND inauzwa haikupata kuuza au kuzalisha hata grid moja ya umeme zaidi ya tests...[citizen ,friday 19jan 2007] sasa hapa napata hisia kuwa hiyo habari ya richmond kufanikiwa kuwasha umeme siku moja kabla ya jk kuadhimisha mwaka itakuwa ilipenyezwa na wanamtandao ili isiharibu sherehe zao ,sasa basi kama walidiriki kupindisha ukweli kuonyesha richmond wamewasha umeme,..kwa nini tusiamini kuwa hii kampuni ni aibu yao....
nategemea maandamano ya kesho yatatoa mwanga ,naomba watanzania wote twendeni tukapinge nchi kuendeshwa na wasanii...
 
Laiti ningekuwa nyumbani... naandika hotuba ambayo ningeitoa kesho.. mko ruhusa kuitumia jinsi mtakavyo!!
 
Wengi wamekubaliana na mawazo yangu ya maandamano yafanyike ili iwekwe rekodi ambayo haijawahi kutokea Tanzania. Rais wa nchi aliyechaguliwa kwa kishindo kuonyeshwa kwamba rushwa imekithiri. Mawazo yako wengi hawakubaliani nayo hilo ndio la maana. Mengine yote ni alinacha, maandamano yanafanyika mahali popote ulimwenguni kuonyesha ishara ya kutokubaliana na mwenendo wa serikali yoyote. Yatakayofuata baada ya hapo ni historia nilitoa wazo la msingi ambalo wengi wameafiki.

Nategemea kuona mawazo na michango yako vilevile ambayo wengi wataafiki.
 
mwana ,si hiyo tu mifuko ya hifadhi ya jamii ina kashfa wanatumia fedha zetu kwa kampeni na kuwagawia kina manji ,hapo wameweka masharti magumu eti kuchukua pesa mpaka ufike miaka sitini,wakati maisha ya mtanzania ni miaka arobaini..sasa sisi tuliopunguzwa kazi ni tabu ...hii wameweka ili watu wafe kabala hawajadai pensheni zao.
KALI YA YOTE kuonyesha haya mashirika yamejaa pesa za bure na dhuluma moja ya haya mashirika limekamilisha taratibu za kujenga MSIKITI dodoma kwa hiyo pesa ya dhuluma..mkumbuke ni kampuni ya umma na serikali haina dini ,sasa sijui tunakoelekea kuanza kujengewa misikiti na pesa za N .. Kwani wanachama si kuna wakiristo,waislamu ..na wasio na dini..kwanini kuleta choko choko...kama mtu anataka kutoa sadaka atoe mfukoni mwake na asitumie michango ya wanachama...
 
Sisi watanzania kama tusipopigania haki zetu hatutafika mbali!!Lazima hawa wahuni wa CCM wawekwe ndani.
 
It's about TIME!....

Safi sana baada ya kilio cha miaka kuwa JF tunapiga makelele hali vyama vya upinzani wamekaa chini wakishuhudia haya machafu yote. Walishindwa hata kunyoosha kidole kazi kupongeza na kusubiri hizo deal za kisiasa baina yao.
 
Viongozi wote wa sasa wa Tanzania wamesoma bure kwa pesa za walipa kodi, na wakati wakisoma hamna hata mmoja aliyekaa chini kama hawa watoto kwenye hii blogu: http://www.blog.co.tz/mrocky

Wakati umefika wa kuchukua hatua, sikumbuki hata siku moja niliyokaa chini wakati wa kusoma kwangu, AIBU HII ITAISHA LINI WAKATI TUNATUMIA RASILIMALI KUTAJIRISHA RICHMONDULI NA WAGENI WACHACHE.
 
Back
Top Bottom