The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Na hakujua kuwa raisi atasumbuliwa alipojibu kuwa raisi ndio aulizwe mara baada ya uteuzi wake? CHENGE CLOSE YOUR STINKING BOWL
 
kuna mwanachama mwenzetu alijiita shetani mnamkumbuka na mnakumbuka alivyoueleza mwaka huu

yule kweli shetani maana mengi aliotabiri yameanza kuonekana naomba anaekumbuka ile link aniwekee nikachungulie nijiridhishe
 
Waziri aliyeachia madaraka asema hakuzaliwa ili awe waziri

SAA chache baada ya kutangaza kujiuzulu, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge amesema hakuzaliwa kuwa waziri hivyo, uamuzi aliochukua ni wa kawaida.

Akizungumza na gazeti hili juzi usiku muda mfupi baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kuthibitisha kujiuzulu kwake, Chenge alisema anashangaa watu wanaompa pole.

"Baadhi ya watu wananipa pole, pole ya nini, huu ni utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi za umma," alisema Chenge na kuongeza:,

"Mimi sikuzaliwa kuwa waziri, mtu anaponipa pole ana maana mimi nilazaliwa kuwa waziri, mimi sikuzaliwa kuwa waziri bwana," alisisitiza.

Chenge alifafanua kwamba, uamuzi wake wa kujiuzulu umeangalia maslahi ya taifa kutokana na kuona suala lake limechukua sura tofauti.

Waziri huyo wa zamani wa Miundombinu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alisema suala lake lilikuwa limeanza kumsumbua Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kwamba, ameona si vema Rais ajikute katika wakati mgumu kutokana na suala lake kutafsiriwa katika misingi tofuati na ukweli ndiyo maana ameamua kujiuzulu.

"Pia nimeona ni vema nijiuzulu kutokana na kuona watu wanataka kumsumbua Rais, ukilala ukiamka wanasema hivi, sasa si vema Rais asisumbuliwe," alisisitiza.

Chenge aliweka bayana kwamba, yeye hajawajibika bali amejiuzulu kulinda maslahi ya taifa.

Alisema si wakati wa kuzungumza mambo mengi, lakini amejiuzulu kwani kama ni kuwajibika kwa suala analochunguzwa atakuwa amethibitisha amekula rushwa kitu ambacho si kweli kwani uchunguzi unaendelea.

Je alizaliwa ili awe FISADI?
 
kuna mwanachama mwenzetu alijiita shetani mnamkumbuka na mnakumbuka alivyoueleza mwaka huu

yule kweli shetani maana mengi aliotabiri yameanza kuonekana naomba anaekumbuka ile link aniwekee nikachungulie nijiridhishe


Acha mambo ya pwani, fanya mwenyewe hii homework, ili kuikomboa Tanzania lzm tufanye kazi na sio kuagiza
 
Acha mambo ya pwani, fanya mwenyewe hii homework, ili kuikomboa Tanzania lzm tufanye kazi na sio kuagiza

samahani mkuu, nimeitafuta sijaiiona sasa kunisaidia si kosa au nimekose babu eeeeeeeeeeh

usimind kusaidiana kuko au vipi?
 
................"Mimi sikuzaliwa kuwa waziri, mtu anaponipa pole ana maana mimi nilazaliwa kuwa waziri, mimi sikuzaliwa kuwa waziri bwana," alisisitiza...............

I like the statement though........ "sikuzaliwa kuwa Waziri"........
 
I like the statement though........ "sikuzaliwa kuwa Waziri"........

At least analitambua hilo...
Baadhi ya wapambe wa CCM wanadhani ni wao walio na haki pekee ya kukalia uraisi...na wao waanze kutambua sasa kuwa CCM haikupewa haki pekee na Mungu ya kushikilia uraisi. Haki hiyo ni yetu sote na kuna wengine pia wenye uwezo tena mkubwa tu wa kuwa maraisi.
 
Kama hakuzaliwa kuwa rais angejiuzulu pale watu walipopiga kelele kupinga uteuzi wake katika baraza la mawaziri,mbona rais alisumbuliwa muda ule?Asitutanie kuzuga. Baba kubali yamekufika shingoni
 
Sheria ya Fedha Haramu itumike dhidi ya Chenge

Lula wa Ndali-Mwananzela Aprili 23, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo

TULISEMA Edward Lowassa hawezi kudondoka, akadondoka; tulisema Dk. Ibrahim Msabaha hang’oki, kang’oka; tulisema Nazir Karamagi hatoki, katoka; na tulisema Andrew Chenge hawezi kuanguka, na sasa kaanguka!

Ile miti mitakatifu isiyokatwa katika Tanzania imeanza kuanguka mmoja mmoja na milio yake imeanza kusikika kila kona ya nchi.

Ile miti ambayo ilijulikana kama “migogo” imeanza kuporomoka kama kuporomoka kwa ukuta wa udongo upigwapo na mvua kali. Tulidhani ni wagumu kama saruji kumbe ni udongo; tena udongo mbichi si wa mfinyanzi. Taratibu wameanza kuanguka na kuangushana.

Kuanguka kwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge (CCM – Bariadi Magharibi) hakukuja kwa bahati mbaya na si kwa kushtusha. Kuanguka kwake kumekuwa kwa kujitakia zaidi baada ya kuamini kuwa yeye ni “kigogo” asiyeng’oka na kwa namna fulani aliamini kuwa alistahili nafasi aliyokuwa nayo. Vigogo wameanza kuanguka vijiti na vikae chonjo!

Kuna watu ambao wameridhika na kujiuzulu kwa Chenge, na hao wanaweza kufikiria kuwa basi huo ndio uwe mwisho wa sakata la Chenge na “vijisenti” vyake vilivyoko huko mafichoni katika kisiwa cha Jersey.

Binafsi naamini kuwa kujiuzulu kwa Chenge kuwe ni mwanzo tu wa hatua kali, dhahiri na za makusudi za “kumshughulikia” ili liwe funzo kwa watu wengine wenye nafasi kama yake.

Katika kufanya hivi naomba nikumbushe sheria dhidi ya Usafirishaji wa Fedha Haramu (Anti-Money Laundering) ya mwaka 2006.

Sheria hii iliaanza kuandikwa na kupitiwa tangu Mwanasheria Mkuu akiwa ni Andrew Chenge na ilitiwa sahihi na Rais Kikwete Januari 5, 2007.

Kwa maneno mengine tunayo sheria ambayo inaweza kabisa kutumika kushughulika na suala la Chenge endapo Mwendesha Mashaka atakuwa tayari kuitumia.

Sheria hii ilikuja hasa baada ya matukio ya Septemba 11 na mojawapo ya malengo yake makubwa ni kukata njia za maghaidi kuweza kutumia mifumo yetu ya benki kupitisha fedha zao ambazo zingeweza kutumika katika ughaidi au uhalifu mwingine. Ni mojawapo ya sheria ambazo tulipewa shinikizo na “wakubwa” tuweze kuzipitisha na kupita kwake kulikuwa ni hatua mojawapo ya kupambana na ughaidi na uhalifu wa kimataifa hasa ule unaohusu fedha.

Hata hivyo, bila ya shaka Chenge hakuwa anafikiria kuwa sheria hii inaweza kutumika dhidi yake au aliamini kuwa yeye hiyo sheria haimhusu.

Lakini kwanza tuweke mambo kadhaa ambayo tunayajua japo kwa juu juu na ambayo ndio msingi wa hoja yangu ya leo.

Kwanza tunafahamua kuwa Chenge alihusika katika mchakato wa ununuzi wa rada ya kijeshi na ni ofisi yake iliyokubali Mkataba wa ununuzi wa rada hiyo (kwa maana ya vipengele vyote pamoja na bei).

Hivyo, ingawa yeye mwenyewe anasema nafasi yake katika mchakato huo ilikuwa ni kidogo lakini kwa mtu makini ataona kabisa kuwa kama mkataba ulikuwa ni mbaya ni mbaya kwa sababu Mwanasheria Mkuu aliuacha uwe mbaya.

Pili, tunafahamu kuwa dalali aliyehusika na mkataba huo akiwa katikati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya BAe alikuwa na mkataba wa udalali uliompa makato fulani na malipo fulani kutokana na nafasi yake hiyo.

Kwa vile mkataba kati ya dalali na Serikali ya Tanzania nao lazima upitie ofisi ya Mwanasheria Mkuu si mbali sana na ukweli kuwaza kwamba Sailesh Vithlani alifanya majadiliano ya mkataba ili umnufaishe kiasi cha mkataba huo kuwa tayari kumlipa Shs. bilioni 21. Hili linachukulia kuwa Vithlani alifanya mjadala na Tanzania.

Hata hivyo, kama haikuwa upande huo ni wazi kuwa BAe ndio walioingia mkataba na Vithlani. Hili ndilo ambalo linajulikana sana na liliibuliwa mwaka jana na gazeti la Guardian la Uingereza.

Hata hivyo, BAe isingiweza kuingia mkataba wa karibu bilioni 50 na Serikali ya Tanzania pasipo nafasi ya Vithlani na uhusiano wake na maafisa wa Tanzania. Ni kwa sababu hiyo ofisi ya SFO (Uchunguzi wa Utapeli wa Hali ya Juu) iligundua kuwa Vithlani alikatiwa bilioni 21 na kampuni ya BAe (kwa kutumia kampuni yake ya pembeni) na kutoka kiasi hicho akagawa kiasi cha fedha kwa maafisa fulani wa Tanzania.

Jambo la tatu ni kuwa SFO katika kufuatilia mtiririko wa fedha wamegundua kutokea kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti ya Chenge na pia mtiririko wa fedha kuingia na kutoka ambao unasababisha shuku.

Kuonekana kwa dola milioni moja kwenye akaunti ya Chenge baada ya malipo ya rada kulipa, kumewafanya waamini kabisa kuwa fedha hizo zinahusiana na malipo ya Vithlani toka BAe.

Jambo la nne ni kuwa Chenge hajakana kuwa na fedha hizo na hajakana moja kwa moja kuwa hizo fedha hazihusiani na rada au mapato yoyote haramu. Kimsingi ametaka watu waache SFO wafanye uchunguzi ili lolote litakalokuwa na “liwe”.

Ni kutokana na mambo hayo manne ninaamini kabisa kuwa sheria ya fedha haramu yaweza kutumiwa dhidi ya Chenge. Kuna sababu.

Chenge aliamua kuweka fedha hizi katika kisiwa cha Jersey ambacho kinajulikana kwa utaratibu wake wa “usiri” katika mambo ya kibenki na hasa pia katika kuepesha ulipaji wa kodi.

Ni kwa sababu hiyo kisiwa hicho na mamlaka nyingine 36 vilitajwa katika muswada wa Bunge la Marekani ulioamua kutangaza maeneo ambayo yanakwepesha kodi kinyume na sheria za Marekani.

Chenge alikuwa na sababu ya kuweka fedha hizo Jersey na si nchi nyingine yoyote au hata hapa nyumbani. Kwa mtu yeyote mwenye lengo zuri benki zetu zina uwezo wa kuhifadhi “vijisenti” vya dola milioni moja kwani wapo Watanzania na mashirika kadhaa ambayo yanafedha hizo za kigeni katika benki zetu.

Kimsingi naamini pasipo shaka kuwa Chenge aliamua kuweka fedha hizo Jersey kwa sababu kubwa mbili. Kwanza kuzificha ili zisijulikane kwa mtu yeyote hasa vyombo vya ndani vya Tanzania na pili ili asilipie kodi yoyote na hivyo kuendelea kubakia na kiasi kikubwa cha fedha mahali fulani.

Kwa mujibu wa sheria hiyo Ibara 12🙁a) na (b) mtu ambaye anasafirisha na kuficha fedha ambazo anajua ni haramu au kinyume cha sheria atakuwa amevunja sheria hiyo hasa akiwa anajua, anapaswa kujua au alikuwa katika nafasi ya kujua kuwa kufanya hivyo ni kosa. Chenge ni Mwanasheria aliyesomea Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani, ambacho kinaheshimika sana, na anaijua sheria hiyo.

Pamoja na nguvu ya sheria hiyo sina budi pia kuhoji kamakile kitengo cha Ujasusi wa Fedha (Financial Intelligence Unit) ambacho kiliundwa na sheria hii kikiwa Wizara ya Fedha kilikwisha kuanza kazi na kimefanikiwa kwa kiasi gan? Kitengo hiki ambacho kina wajumbe kutoka sehemu mbalimbali pamoja na Usalama, wa Taifa kimejua kwa kiasi gani kuhusu fedha za Chenge?

Ingawa bado ni kitengo kipya Watanzania wana haki ya kujua kama kitendo hiki kimeanza kazi na Kamishna wake ni nani ili watu wajue wapi pa kuanzia.

Kwa vile sheria hii ya Fedha Haramu inaeleza pia utaratibu wa kufuatilia kesi hizi basi ofisi ya Mwendesha Mashtaka na ofisi ya Upelelezi wa Makosa zifanye kazi zao na wasisubiri hadi Rais awaagize.

Kwa mujibu wa sheria hiyo ibara ya 28 inasema kuwa utaratibu wa kukamata wahusika wa fedha haramu na kuwafikisha mahakamani ni ule ule unaotumiwa katika sheria ya “Kuhujumu Uchumi” ya Mwaka 1984 (na mabadiliko yake) basi kina Robert Manumba watueleze wanangoja nini kumfanyia uchunguzi Chenge na kuhakikisha anafunguliwa mashtaka ya kuvunja sheria ya fedha haramu.

Maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa kwa muda sasa kuwa “uchunguzi unaendelea” ni maelezo finyu kwani hakuna uchunguzi wetu wenyewe tunaoufanya kuhusu fedha za Chenge. Hatuwezi kusubiri uchunguzi wa SFO ambao wao wanaufanya kwa ajili ya nchi yao.

Sasa kuna tetesi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza anataka SFO wasitishe uchunguzi huo na wakifanya hivyo Chenge anaweza kupona. Sasa SFO wakisitisha uchunguzi wao na sisi tufanyeje? Tukubali yaishe?

Maelezo mengine pia kuwa TAKUKURU inafanya uchunguzi ni geresha kwa sababu karibu wote tunajua ni jinsi gani taasisi hiyo imelala kitanda kimoja na mafisadi na ya kuwa haina rekodi yoyote ya kujivunia kuhusu rushwa au ufisadi mkubwa zaidi ya kutuambia “wameanza kuchunguza”.

Hadi hivi sasa tukianza kuuliza yale yote waliyosema wanachunguza yamefikia wapi tunaweza kupatwa na kichefuchefu. Si walisema wanachunguza juu ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na mikopo hewa kwa wanafunzi hewa, hadi leo wametuambia wamefikia wapi?

Kwa vile sheria ya dhidi ya Fedha Haramu ina ruhusu kushirikiana na vyombo vingine kama FIU yetu, basi serikali ya Rais Kikwete iiombe SFO ifanye uchunguzi wa mawaziri wote na manaibu wao ili kuona kama ni Chenge tu ambaye ndiye kondoo mwenye doa jeusi au kuna wajanja wengine waliojaza “vijisenti” vyao kwenye visiwa mbalimbali vya fedha za kifisadi kama Bahamas, Bermuda, Belize, Cayman, Isle of Man na Barbados.

Kimsingi ninachosema ni kuwa Chenge achunguzwe na vyombo husika na sheria yetu dhidi ya fedha haramu itumiwe dhidi yake mapema inavyowezekana kabla jaribio lolote la kuharibu ushahidi halijafanyika.

Wakati huo huo ninaamini kabisa kuwa ingawa Chenge amejiuzulu uwaziri wake, bado hastahili kushika nafasi yoyote ile ya uongozi na kwa vile ameonesha uwajibikaji basi aendelee kujiwajibisha yeye mwenyewe kwa kuamua kujiondoa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM na zaidi ya yote, ajiuzulu ubunge kwani amekiletea Chama cha Mapinduzi (CCM) fedheha kubwa na kwa kweli amemuaibisha Mwenyekiti Jakaya Kikwete.

Zaidi ya yote Chenge ajiuzulu Ubunge ili wananchi wa Bariadi waweze kupewa nafasi ya kumchagua mtu mwingine ambaye ataenda bungeni kuwawakilisha kweli kweli na si kuwakilisha mifuko yake.

Kama CCM wanafikiri kwamba kwa kujiuzulu uwaziri basi inatosha watafanya makosa. Kama wanatafaka kujisafisha kweli, basi huu ndio wakati muafaka.

Lakini zaidi ya yote, Chenge ataweza vipi kuendelea kushiriki shughuli za Bunge wakati anakabiliwa na tuhuma nzito kama hizi? Binafsi nimemsamehe kauli yake ya “vijisenti” baada ya kuomba radhi maana amefanya kile ambacho Basil Mramba alishindwa kufanya baada ya kututukana kwa kutuambia “tutakula hata nyasi” ili Rais wetu apate ndege mpya.

Kwa vile ameonyesha uungwana wa kuomba radhi, naamini wakati umefika aonyeshe pia uungwana wa kujiuzulu ubunge ili mkondo wa sheria uweze kufuatwa bila kiwingu chochote kile au kivuli chochote cha madaraka. Endapo, atakutwa hana hatia au hana kosa lolote basi itakuwa ni gharama ya kisiasa aliyoilipia wakati huu na sitoshangaa chama chake kikimpitisha tena mwaka 2010 na wananchi kumrudisha bungeni.

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk
 
Daily Mail

Andrew Chenge: Resigned after more than £500,000 was found in his off-shore bank account
A minister in Tanzania accused of taking bribes from Britain's largest arms manufacturer has resigned.


Andrew Chenge quit after being accused of pocketing a backhander when his country bought a £20million military radar system from BAE Systems.


More than £500,000 was found in an offshore account belonging to the infrastructure minister, which is believed to be linked to the 2002 deal.


The company is already under scrutiny over claims it paid illegal "commissions" to win lucrative defence contracts.


The Serious Fraud Office is investigating the Tanzanian deal, which went ahead even though the east African state is one of the world's poorest countries.


Mr Chenge, a Harvard-educated lawyer, was attorney general at the time.


An earlier SFO inquiry into a record £43billion BAE arms deal with Saudi Arabia was stopped by the UK Government. Two weeks ago, the High Court ruled that this had been unlawful.


In Tanzania, President Jakaya Kikwete accepted Mr Chenge's resignation on Sunday. A spokesman for the president said: "Mr Chenge said that in addition to the allegations, the love for his country and party had forced him to step aside."


Local media said the resignation was sparked by reports that Mr Chenge had $1million in the offshore account.


He caused outrage last week when he referred to it as "a small amount of money".

Critics said the radar system was costly, obsolete and unnecessary for such a poor country.


A spokesman for BAE Systems said: "We continues to fully cooperate with the SFO investigation, which includes Tanzania."
 
🙂
mwaka huu mafisadi hawana pakupumzikia....

mie naona hata maana kamili ya vijisenti hawajaipata hao wazungu....au hawakuweza amini hiyo maana yake halisi 🙂
 
Nani kumfuata Chenge?

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KUNA kila dalili kwamba, mkakati maalum wa kuwasafisha kwa zamu mawaziri wanaoandamwa na tuhuma za kifisadi ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete unaendelea.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo kadhaa vya habari ndani ya serikali na miongoni mwa wanasiasa zinaeleza kwamba, bado kuna mawaziri wengine zaidi ndani ya serikali ambao wataanza kushughulikiwa na kufuatiliwa nyendo zao baada ya kuanguka kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.

Tayari majina ya mawaziri ambao wataingia katika mkumbo huo wa ‘tuhuma nzito za kifisadi’ yameshaanza kuandaliwa na kinachosubiriwa sasa ni mabadiliko ya mawaziri yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima waliyataja majina ya baadhi ya mawaziri ambao iwapo watarejeshwa katika Baraza la Mawaziri atakaloliunda tena Rais Kikwete, wanaweza wakakabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi ambazo hatimaye zitawalazimisha kujiuzulu.

Pamoja na kuendelea kuwapo kwa hofu ya mawaziri wengine kufuata mkumbo wa kuanguka, viongozi kadhaa waliozungumza na gazeti hili wameeleza kwamba, hali hiyo imesababisha kuanza kwa mapambano makali ya kisiasa miongoni mwa makundi ndani ya CCM na serikalini katika kuiangalia hali hiyo na namna ya kukabiliana nayo.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima kwa siku kadhaa sasa wameanza kueleza wasiwasi wao kuhusu mtazamo wa Rais Kikwete katika kukabiliana na mwenendo huo wa mambo ambao kwa kiwango kikubwa unaonekana kuitikisa serikali na kuanza kuwatia hofu baadhi ya wanasiasa.

Chanzo cha kuaminika cha habari kutoka Ofisi ya Rais Ikulu kinaeleza kwamba, kundi moja ndani ya serikali limefikia hatua ya kumtaka Kikwete kuanza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo inayoweza kuimaliza na kuiyumbisha kabisa serikali yake.

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Rais Kikwete aliyezungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita alisema, baadhi ya viongozi serikalini wameanza kuwalaumu wanasiasa na wanahabari kuwa chanzo kikuu cha kumegeka kwa Serikali ya Kikwete kutokana na tuhuma hizi za kifisadi.

“Unajua kinachoonekana sasa ni kwamba, ninyi waandishi mmeacha kabisa kuandika mambo mengine ya msingi yanayohusu uchumi na maendeleo ya kijamii, na mmekazana kuwatafuta watu uchawi na kuandika madhambi yao. Hali hii ni lazima idhibitiwe. Uandishi wa aina hii haupo duniani kote zaidi ya hapa,” alisema ofisa huyo wa juu serikalini.

Alipotakiwa kueleza iwapo tuhuma dhidi ya mawaziri na baadhi ya wanasiasa hazimgusi Kikwete mwenyewe moja kwa moja, ofisa huyo alisema takriban masuala yote mazito yanayohusu ufisadi yanayozungumzwa katika siku za hivi karibuni, ukiacha sakata la Richmond yalitokea wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

“Leo hii mnamtuhumu Chenge kwa mambo yaliyotokea zama za Mkapa. Ukiacha suala la Richmond, tuhuma takriban zote dhidi ya ufisadi wenu huu haziigusi Serikali ya Kikwete leo, ni za watangulizi wake. Sasa kwanini mnamhusisha rais?” alisema ofisa huyo.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kuhusu mwenendo huo wa mambo hivi sasa, alisema tayari baadhi ya makada wa chama hicho na watu walio karibu na Kikwete wameshamuonya kuhusu haja ya kuanza kuchukuliwa kwa hatua za dharura za kukabiliana na wimbi la mawaziri kujiuzulu kutokana na kashfa.

Mwana CCM huyo ambaye kwa miaka mingi amekuwa karibu kikazi na Kikwete, alipoulizwa msimamo wa rais kuhusu matukio haya ya mawaziri wake kubebeshwa tuhuma nzito za ufisadi, alikataa kueleza lolote zaidi tu ya kusema:

“Hali hii kwa kweli imeanza kututisha baadhi yetu, na tuna wasiwasi ambao tayari tumeshamfikishia Jakaya, tukimtaka achukue hatua za kuzuia hali hii ya watu kuchafuana.

“Tumemueleza JK waziwazi sisi kama taifa hatujafikia hatua ya kutoa uhuru mpana wa namna hiyo ambao ni jambo la hatari, kwani baadhi ya wenzetu wameanza kutumia uvumilivu wa rais kujenga uzushi dhidi ya wenzao. Unajua huyu mtu siku zote ni liberal,” alisema mwana CCM huyo.

Hata hivyo, mwana CCM mwingine aliyezungumza na Tanzania Daima kuhusu matukio haya ya viongozi kulazimishwa kujiuzulu alisema, baadhi ya makada wenzao wameshaanza kujiuliza iwapo matukio haya hayana baraka za Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa taifa wa CCM na rais mwenyewe.

“Tumeanza kupata hofu kwamba, kuna uwezekano kuwa Bwana Mkubwa (rais) amekuwa akiunga mkono na kushangilia kuanguka kwa marafiki zake na mawaziri wanaokumbwa na kashfa mbalimbali katika siku za hivi karibuni,” alieleza mwana CCM huyo ambaye alifikia hatua ya kuuliza iwapo kulikuwa na mawasiliano kati ya wanahabari na Ikulu.

Hata hivyo, mwanasiasa mmoja ambaye ni kiongozi wa juu Umoja wa Vijana wa CCM aliye karibu na Chenge, alilieleza Tanzania Daima kwamba, mwanasiasa huyo alikuwa ameshaanza kujiandaa kutoa ufafanuzi kuhusu dola za Marekani zaidi ya milioni moja zilizokutwa katika akaunti yake katika visiwa vya Jersey nchini Uingereza.

Kada huyo wa CCM alisema pia kwamba, tayari mwanasiasa huyo alikuwa ameshaanza kuwasiliana na kiongozi mmoja wa juu wa dini ambaye ndiye anayehusishwa na fedha hizo kama hatua ya mwanzo ya kujisafisha dhidi ya tuhuma hizo nzito.

“Mzee ameshaanza kuwasiliana na mtu ambaye aliziingiza fedha hizo katika akaunti yake mwaka 2002 kwa malengo mahususi, kabla ya kuwatangazia Watanzania ukweli kuhusu akaunti hiyo ambayo imeshaanza kuchunguzwa iwapo ina uhusiano na fedha zinazoaminika kutolewa kwa rushwa wakati serikali iliponunua rada ya kijeshi kutoka Uingereza,” alisema kada huyo wa CCM.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Chenge kwa simu jana alasiri kuzungumzia kuhusu suala hilo, alimtaka mwandishi kumpa muda wa kupumzika na kumwacha atulie kutokana na uzito wa masuala anayokabiliana nayo.

“Ndugu yangu sasa hivi ninakabiliwa na majukumu mazito, siwezi kuzungumza chochote kuanzia leo, kesho, kesho kutwa au mtondogoo kwa vile siko katika nafasi nzuri… nawaomba mniache... Sasa hivi niseme nini? Muda ukifika sawa... lakini ungekuwa wewe ungeweza kujibu nini katika kipindi kama hiki, niacheni tu ndugu zangu,” alisema Chenge.

Alipoelezwa na mwandishi wa habari hizi kuwa kulikuwa na taarifa kuwa alipanga kukutana na waandishi wa habari hivi karibuni kutoa ufafanuzi wa fedha zilizokutwa kwenye akaunti yake, alikana na kusema hana mpango wa aina yoyote wa kukutana nao kwa sasa.

“Nani kakwambia nakutana na waandishi wa habari? Sina mpango wa aina hiyo na wala hakuna kitu kama hicho kwa sasa… nipeni muda ndugu yangu, nakutakia kazi njema,” alisema Chenge.

Akizungumza na Tanzania Daima kuhusu kujiuzulu kwa Chenge na tuhuma za ufisadi, Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya vyombo mbalimbali vya habari kumweka kando Kikwete katika tuhuma hizi.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, alisema ni jambo lisilowezekana kwa Kikwete ambaye ana vyombo vya usalama kuwateua watu wenye tuhuma nzito, na yeye mwenyewe akaendelea kubakia kuonekana mtu safi.

“Ndege wenye mbawa zinazofanana huruka pamoja. Kikwete hawezi kutenganishwa na ufisadi huu. Angekuwa si mmoja wao asingekubali kukaa meza moja na watu ambao wanakabiliwa na tuhuma nzito za rushwa,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisema, iwapo Kikwete angekuwa safi, basi asingesubiri mpaka watu watuhumiwe ndipo akubali kujiuzulu kwao kabla yeye mwenyewe hajachukua hatua ya kuwafukuza kazi.

Mbowe anatoa kauli hiyo, ikiwa ni siku moja tu baada ya viongozi wa ushirika wa vyama vinne vya upinzani kuandamana hadi katika Tume ya Maadili ya Viongozi na kutaka kupata maelezo kuhusu mali alizonazo Rais Kikwete na viongozi wengine kadhaa wa juu.
 
That's good. Kila kona wanabanwa mbavu sijui watakimbilia wapi? inabidi waende misitu ya Congo wakafiche nyuso zao.
 
Baada ya Chenge next is Mwandosya na Mkapa ni wa mwisho kabisa .Kama huniamii tulia uone.Ndani ya CCM kila mmoja ni majeraha wameamua kufa wote ili wazaliwe upya .Watch out
 
UFUNUO WA YOHANA;181369]That's good. Kila kona wanabanwa mbavu sijui watakimbilia wapi? inabidi waende misitu ya Congo wakafiche nyuso zao.

hah....hah...ahh iseh hii kali sana umenivunja mbavu, ufunuo.
 
Just imagine AC anaacha hekalu lake kule Bariadi na kuanza Maisha mapya na mbilikimo wa Congo, sasa sijui atakuwa anakula Nyani? Na sijui pombe yao ya kienyeji ni ipi huko?
 
chenge nenda usa na wewe,unasubili mpaka ukamatwe,mwanasheria wa zamani wa tanzania,du!!! nchi imeoza hiyo tanzania
 
Back
Top Bottom