The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

mawaziri wote waliokuwao kwenye utawala wa Benjamini mkapa wanahusika na ufisadi njia moja au nyengine.
JK atakuwa bado hana serikali mpaka pale atapowauzulisha wote waliotoka enzi zile. ikiwezekana na ubunge pia

Na yeye JK vipi hakuwa waziri serikali ya mkapa?
 
Si kama kawaida ya waandishi wetu wa habari na slogan yao "jina tunalo lakini tunalihifadhi"

Cha ajabu ni kuwa kwenye gazeti la majira wamemtaja Mwakyembe hajalipa bill ya maji...angalia hawa ma hypocrites

TANZANIA HAKUNA VYOMBO VYA HABARI.
 
Na yeye JK vipi hakuwa waziri serikali ya mkapa?

Inshort hatuna serikali tuna genge la wahuni tu JK pia alikuwa waziri wa JK na wizara yake ndio iliyoidhinisha malipo ya nyumba ya ubalozi Italy. Waliidhinishaje wakati hawakuuona mkataba? JK nae ni fisadi!
 
Mamilioni ya Chenge kutaifishwa

*Waziri Wakuu wa Jersey ateta na Majira Jumapili
*AG wao naye azungumzia 'vijisenti' vya Chenge
*Wasisitiza:Tukibaini, tutamfilisi kama Sani Abacha

Na Hassan Abbas

AKAUNTI ya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge iliyoko visiwa vya Jersey, Uingereza inaweza kutaifishwa na fedha hizo kurejeshewa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Majira Jumapili limebaini.

Msimamo huo dhidi ya akaunti ya Bw. Chenge yenye 'vijisenti' vilivyowekwa vikiwa kwenye pauni za Uingereza zipatazo 504,000 (zaidi ya sh. bilioni moja), umetolewa kwa nyakati tofauti wiki hii na viongozi waandamizi wa visiwa hivyo katika mawasiliano yao kwa njia ya intaneti na Majira Jumapili pekee.

Akizungumzia hatua zitakazochukuliwa na Serikali yake, Waziri Mkuu wa visiwa vya Jersey, Seneta Frank Walker alikuwa wa kwanza kulithibitishia gazeti hili kuwa sheria za nchi hiyo zitachukua nafasi katika suala la Bw. Chenge.

"Taasisi za fedha za Jersey kimsingi zinatakiwa kufuata misingi ya sheria za kimataifa kuhusu masuala ya fedha hasa zinazowahu wanasiasa," alisema Bw. Walker katika ujumbe wake aliolifikishia gazeti hili kupitia kwa Msemaji wa Ofisi yake, Bi. Cathy Keir.

Gazeti la The Guardian la Uingereza liliibua taarifa zilizovuja kutoka Taasisi ya Kupambana na Makosa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) zilizoonesha kuwa Chenge amehojiwa kutokana na akaunti hiyo, akihusishwa na fedha za rushwa katika ununuzi wa rada ambayo wataalamu Tanzania iliuziwa kutoka Uingereza ikiwa ni kuu kuu na iliyopandishwa gharama.

Kiongozi huyo wa Jersey amewahakikishia Watanzania kuwa mamilioni hayo ya Bw. Chenge yatataifishwa na fedha hizo kurejeshwa kwa Serikali ya Tanzania iwapo uchunguzi unaoendelea utabaini kuwa alizipata isivyo halali.

"Kiutaratibu taasisi zetu za fedha zinatakiwa kuchunguza fedha zozote zinazotiliwa shaka na kupeleka taarifa yao kwenye Kitengo cha Kuchunguza Shughuli za Fedha ambako hatua muafaka huchukuliwa," alidokeza.

Akathibitisha kuwa akaunti ya Chenge kutaifishwa halitakuwa jambo la ajabu katika harakati za visiwa hivyo kujinasua kutoka orodha ya maeneo yanayoonekana kuwa rahisi kwa wanasiasa na vigogo wengine kwenda kulimbikiza fedha walizozichuma kwa njia ya rushwa katika nchi zao.

Wiki iliyopita gazeti hili pekee liliibua habari ya uchunguzi iliyoonesha kuwa kwa mujibu wa ripoti moja ya nchini Marekani, visiwa hivyo vinarekodi mbaya ya kuwa moja ya maeneo ambako mafisadi hukimbilia kufungua akaunti za siri kwa sababu ya kinga nzuri za kisheria zilizoko visiwani humo.

Lakini Waziri Mkuu Walker amesisitiza kuwa Bw. Chenge anaweza kutaifishwa akaunti yake kama ilivyokuwa kwa aliyepata kuwa kiongozi wa Nijeria, Jenerali Sani Abacha.

"Mara nyingi sheria zetu zinaruhusu akaunti kufungwa na fedha kurejeshwa zilikotoka...Ushahidi wa hatua ambazo Jersey huzichukua inapobaini fedha husika ni za kifisadi unaweza kuonekana pale zilipotaifishwa akaunti za Jenerali (Sani) Abacha wa Nijeria," alisisitiza Bw. Walker katika taarifa yake hiyo.

Akalilidokeza gazeti hili kuwa uhalali wa kutaifisha fedha za Chenge na kuzirejesha kwa Watanzania wanaupata kupitia sheria ya nchi hiyo ya Kupambana na Makosa ya Usafirishaji wa Fedha Haramu (The Money Laundering [Jersey] Order, 2008).

Kufuatia uchunguzi ulioanza mwaka 2001 Serikali ya Jersey iliwahi kutaifisha na kurejesha nchini Nijeria kiasi cha dola milioni 180 (zaidi ya sh. bilioni 180) za Bw. Abacha. Mwaka 2004 Bw. Olusegun Obasanjo akiwa Rais mpya wa Nijeria alitembelea Jersey kushukuru kwa hatua hiyo.

Waziri Mkuu huyo wa Jersey pia ameeleza utayari wa Serikali yake kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Tanzania katika masuala yote yanayohusu sakata la Bw. Chenge.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu (AG) wa Jersey, Bw. William Bailhache alipotakiwa kueleza hatua zilizofikiwa katika kulichunguza sakala la Bw. Chenge, alisema kwa sasa hawezi kukana wala kukiri kuwa wanaendelea na uchunguzi, akihofia kile alichokieleza 'kuvunja sheria ya usiri.'

"Sheria za Jersey zinanizuia kuzungumzia suala lolote linalohusu uchunguzi wa rushwa, ufisadi au makosa ya usafirishaji wa fedha kwani kufanya hivyo ni kuingilia uchunguzi...Kwa jinsi hiyo siwezi kukana wala kukuthibitishia kuwa tunamchunguza Bw. Andrew Chenge," alisema na kuitaja sheria inayomzuia kufanya hivyo kuwa ni ile ya "Investigations of Fraud (Jersey) Law 1991."

Hata hivyo alikiri kuwa sheria za nchi hiyo zinaruhusu akaunti ya Bw. Chenge na mtu mwingine yeyote anayetuhumiwa kwa makosa ya jinai kuchunguzwa.

Naye Katibu wa Tume ya Kudhibiti Shughuli za Fedha ya nchi hiyo, Bw. Chris Renault, ambaye awali Waziri Mkuu wa visiwa hivyo aliliarifu gazeti hili kuwa Tume hiyo ndiyo inahusika na kuchunguza na hata kupendekeza hatua za kuchukua pale kunapokuwa na akaunti yenye fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali, naye alizungumza na gazeti hili.

Katika taarifa yake alithibitisha kuwa sheria za nchi hiyo ziko wazi juu ya kutaifisha akaunti husika iwapo itaonekana fedha zilizomo zina uhusiano na ufisadi.

"Kujibu swali lako, Serikali ya Jersey ina sheria ambayo inaruhusu kushirikiana na mataifa mengine katika kupambana na uhalifu wa fedha na pale ambapo uchunguzi unahusu kosa la jinai basi masuala hayo anayashugjhulikia Mwanasheria Mkuu chini ya sheria iitwayo The Criminal Justice (International Co-operation) (Jersey) Law 2001,ambayo naweza kukupatia nakala yake," alisema.

Hata hivyo Bw. Renaunt kama ilivyokuwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Jersey hakutaka kuingia kwa undani katika uchunguzi unaoendelea dhidi ya Bw. Chenge na kulishauri gazeti hili kuwasiliana na SFO ya Uingereza akisema wao ndio walianza kulifuatilia suala hilo.

"Kwa sasa hatuwezi kutoa jibu la moja kwa moja kuhusiana na Bw. Andrew Chenge. Ungewasiliana na SFO ambao ndio kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo," aliongeza.
 
Lowassa, Chenge, Karamagi, Msabaha achieni hata ubunge

Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BAADA ya 'nguvu ya umma' kuviangusha vigogo ambavyo havikutarajiwa kwa kasi ya ajabu na namna ya pekee, ni wakati muafaka kuwapa shime wananchi kushikilia uzi ule ule.

Haikuwa kazi nyepesi wala jambo lililotarajiwa kufanyika kama ilivyotokea. Lakini si hadithi wala dua la kuku, vigogo vimepukutika kama kupe kwenye mgongo wa ng'ombe.

Nani alidhani vigogo kama Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani; mawaziri, Nazir Karamagi, Ibrahim Msabaha, Andrew Chenge, Basil Mramba, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine wangeporomoka bila hata kufurukuta kama ilivyotokea?

Sasa imetokea na nguvu ya umma imebainisha makali na jeuri yake.

Tusibweteke na mafanikio haya kidogo tuliyopata dhidi ya ufisadi na mafisadi. Lazima tuzidi kuhoji na kushinikiza ili nchi yetu iwe safi na vikwazo vya maendeleo na utu wetu viangushwe.

Baada ya kuwatimua wahusika kwenye ofisi nono na kubwa, kuna haja ya kuwafuata hata huko kwenye ofisi za umma wanazoendelea kuzishikilia. Tusiwe na simile wala nini bali kufanya kazi moja tu-kuisafisha Tanzania.

Huwa siachi kujiuliza mantiki ya kumfurusha mtu uwaziri tukambakizia ubunge. Kufanya hivi ni kuendelea kufuga ndwele na kutoa nafasi kwa wahusika kurejea tena kutuguguna kwa kasi ya ajabu.

Tusimwachie Rais jukumu hili. Maana Rais hana anachokosa kuanzia usingizi hadi maslahi yake. Tunaoumia ni sisi tunaowagharimia wakwasi hawa wasio na udhu wala lengo la kututumikia bali kututumia.

Hapa ndipo hitaji la kuwataka wahusika waachie na ubunge wetu linapokuja.

Ubunge ni uwakilishi wa umma sawa na uwaziri. Ofisi ya waziri na nafasi ya ubunge ni mali ya umma. Sasa anafukuzwa uwaziri anabakiziwa ubunge kwa lipi na kubakia kwa lipi?

Kwangu ubunge ndiyo mama wa vyote. Hivyo kuna haja ya kuangalia namna ya kuwawajibisha watu hawa ambao wamebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu za utumishi katika nchi yetu.Kuna haja ya kujiuliza. Kama mtu ameweza kuiibia taasisi yenye wataalamu lukuki, inakuwaje inapokuja kwa wananchi maskini wengi wa vijijini wanakotokea hawa wabunge?

Nafahamu. Chama Cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kuwatetea na kuwalinda wahalifu hawa wa kisiasa. Lakini ikubalike. Nchi hii si ya CCM wala Rais. Ni mali na nchi ya watanzania.

Ingawa kuna sheria chafu zilizotungwa na kupitishwa na watu hawa zinazowalinda watu wabovu kama hawa, bado wananchi wakijua uzito wa nguvu yao wanaweza kuwang'oa licha ya kuwapo sheria chafu zinazowalinda.

Tusiogope mamlaka ya Rais na dhamana ya CCM kama vinatumika vibaya.

Rais yupo kwa ajili ya wananchi lakini wananchi hawapo kwa ajili yake. Yeye ni mtumishi wao. Si ndivyo alivyotwambia wakati akituomba tumchague? Sasa inakuwaje anapoingia madarakani awe mtumikishaji badala ya mtumishi?

Nani anataka kumwajiri mtumishi mwenye kiburi na mamlaka kupita yake muajiri?Hapa ndipo Rais anapopaswa kuwa makini.

Kama umma utajua haki na wajibu wake na jinsi ya kuvitumia vitu hivi hatakuwa na lake. Na hii ndiyo silaha iliyowakomboa wenzetu kwenye nchi tunazoziita zimeendelea.

Kitu muhimu ni kuelewa kuwa nguvu ya umma huwa haiji kwa kubembeleza au kupewa na watawala bali hujitokeza na kuziba ombwe.

Mapinduzi tunayopigia mifano kama yale ya Urusi (1903-05 na kuendelea) na yale ya wafanyakazi wa Ufaransa (1789-1799) hata ya hivi karibuni ya Poland (Septemba 1980) na ya Romania (Desemba 1989) hayakushushwa kutoka mbinguni.

Yalisababishwa na dhuluma ya watawala kwa watawaliwa. Yalianzishwa na kuchochewa na ufisadi na kiburi cha watawala waliowaona watawaliwa kama vyombo vyao vya kuneemekea na kutanulia kama ilivyo kwetu.

Mapinduzi haya yalikiuka imani na itikadi za kisiasa na kidini kiasi cha kujichimbia kwenye ukombozi wa kweli kiuchumi. Hakuna anayekula itikadi ya dini wala chama chake bali mkate. Je, bila kuwa na haki mkate ambao ni keki ya taifa utaipata wapi?

Hii ndiyo siri ya heshima na ustawi wa nchi tajwa, hasa mwananchi wa kawaida mitaani-msukuma mkokoteni, omba omba wa kutengenezwa, mwanafunzi, mjamzito maskini asiye na pa kwenda kutibiwa.

Chuki dhidi ya wale waliokuwa wakiishi maisha ya uhakika na wale waliokuwa wakiishi ‘bora liende' ndicho chanzo na chachu ya wenzetu kufanya mapinduzi hasa kuanzia kwenye fikra na malengo yao kama jamii.

Leo Watanzania wamegeuzwa kunguru kula vya kudandia na kudokoa! Haya si maisha ni kiama.

Si maisha anayostahili kuishi mtanzania juu ya nchi yenye kila neema na utajiri.

Kuendelea kujiweka utumwani kwa watawala ni ukondoo na ukuku.

Haya si majaliwa ya binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe. Haya siyo majaliwa wala maisha yanayomfaa Mtanzania.

Kwa nini kwa mfano Watanzania tuishie kuwa makapuku huku hata wakimbizi wa kiuchumi kutoka India na China wakiishi vizuri miongoni mwetu?Sina haja ya kuleta ubaguzi wala hisia zake.

Ndiyo ukweli tunaopambana nao kila siku mitaani. Rejea Wahindi kuwa karibu katika kila kashfa ya wizi wa mabilioni yetu walipa kodi.

Rejea kuanza kuongezeka kwa idadi ya wabunge wafanyabiashara wa Kihindi ili kulinda maslahi yao ambayo kimsingi yanaua maslahi yetu.

Hapa ndipo ilipo siri ya akina Jeetu Patel kutuibia. Wanatumiwa na watawala kwa kujua fika mambo yatakapoharibika watawatorosha. Rejea kwa mfano kuwa vigumu kuwatorosha akina Maregesi na Lukaza. Hawa wangekuwa Wahindi kisingepatikana kitu.

Tukirejea kwa walengwa wa makala hii, ni wakati muafaka kuwatendea na kujitendea haki kwa kuwataka waachie ubunge kama taasisi ya umma.

Wakikataa tuandamane kuwazuia wasiingie kwenye Bunge letu. Maana watalitia najisi kutokana na kuendekeza ulafi na maslahi yao binafsi kinyume na yale ya umma.

Vita hii ni ‘do or die' au kufa na kupona. Kuondokana na watu kama hawa kwenye taasisi hakutupi hasara bali kurejesha haki zetu za kuishi kama watu.

Si chuki wala chuiu.Watawala wabovu wamekuwa chanzo kikuu cha umaskini wetu kuliko hata majanga ya kimaumbile kama vile ukame.

Hebu rejea kitendo kichafu cha Rais wa zamani na walafi wenzake kuleta, kwa mfano, kampuni ya Kikaburu kuja kuua TANESCO lililosababisha kupandishiwa umeme.

Rejea hata hili sakata la Richmond ambapo tunalazimika kulanguliwa umeme kuwalipa matapeli wanaoshirikiana na baadhi ya watawala wetu.

Hatuwezi kama nchi kuendelea na jinai hii na tukajidanganya kutakuwa na maisha bora kwa Mtanzania.

Sasa ni miaka mitatu tangu tuambiwe maisha bora kwa Mtanzania. Nini kimefanyika zaidi ya kuishia kuwa usanii wa kisiasa?

Kuna haja ya kuanza hata kupambana na rais wetu kwa kumbana atimize tuliyokubaliana na kama atashindwa hata mwaka 2010 asiruhusiwe hata katika chama chake kugombea tena kiti cha urais maana amefeli vibaya sana.

Tuhitimishe.

Wakati sasa umefika kuwataka ‘kiutu mzima' watajwa na wengine wanaofanana nao kujitoa haraka kabla ya umma kuwachukulia hatua ambazo matokeo yake hayatakuwa mazuri kwao.

Hapa ni kuwaomba wabunge wenye uchungu na nchi kutokubali kuburuzwa na chama kilichokwisha onyesha wazi kuishiwa na kupoteza mwelekeo.

Mungu ibariki Tanzania.

mpayukaji@yahoo.com
 
Lowassa, Chenge, Karamagi, Msabaha achieni hata ubunge

Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BAADA ya 'nguvu ya umma' kuviangusha vigogo ambavyo havikutarajiwa kwa kasi ya ajabu na namna ya pekee, ni wakati muafaka kuwapa shime wananchi kushikilia uzi ule ule.

Haikuwa kazi nyepesi wala jambo lililotarajiwa kufanyika kama ilivyotokea. Lakini si hadithi wala dua la kuku, vigogo vimepukutika kama kupe kwenye mgongo wa ng'ombe.

Nani alidhani vigogo kama Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani; mawaziri, Nazir Karamagi, Ibrahim Msabaha, Andrew Chenge, Basil Mramba, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine wangeporomoka bila hata kufurukuta kama ilivyotokea?

Sasa imetokea na nguvu ya umma imebainisha makali na jeuri yake.

Tusibweteke na mafanikio haya kidogo tuliyopata dhidi ya ufisadi na mafisadi. Lazima tuzidi kuhoji na kushinikiza ili nchi yetu iwe safi na vikwazo vya maendeleo na utu wetu viangushwe.

Baada ya kuwatimua wahusika kwenye ofisi nono na kubwa, kuna haja ya kuwafuata hata huko kwenye ofisi za umma wanazoendelea kuzishikilia. Tusiwe na simile wala nini bali kufanya kazi moja tu-kuisafisha Tanzania.

Huwa siachi kujiuliza mantiki ya kumfurusha mtu uwaziri tukambakizia ubunge. Kufanya hivi ni kuendelea kufuga ndwele na kutoa nafasi kwa wahusika kurejea tena kutuguguna kwa kasi ya ajabu.

Tusimwachie Rais jukumu hili. Maana Rais hana anachokosa kuanzia usingizi hadi maslahi yake. Tunaoumia ni sisi tunaowagharimia wakwasi hawa wasio na udhu wala lengo la kututumikia bali kututumia.

Hapa ndipo hitaji la kuwataka wahusika waachie na ubunge wetu linapokuja.

Ubunge ni uwakilishi wa umma sawa na uwaziri. Ofisi ya waziri na nafasi ya ubunge ni mali ya umma. Sasa anafukuzwa uwaziri anabakiziwa ubunge kwa lipi na kubakia kwa lipi?

Kwangu ubunge ndiyo mama wa vyote. Hivyo kuna haja ya kuangalia namna ya kuwawajibisha watu hawa ambao wamebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu za utumishi katika nchi yetu.Kuna haja ya kujiuliza. Kama mtu ameweza kuiibia taasisi yenye wataalamu lukuki, inakuwaje inapokuja kwa wananchi maskini wengi wa vijijini wanakotokea hawa wabunge?

Nafahamu. Chama Cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kuwatetea na kuwalinda wahalifu hawa wa kisiasa. Lakini ikubalike. Nchi hii si ya CCM wala Rais. Ni mali na nchi ya watanzania.

Ingawa kuna sheria chafu zilizotungwa na kupitishwa na watu hawa zinazowalinda watu wabovu kama hawa, bado wananchi wakijua uzito wa nguvu yao wanaweza kuwang’oa licha ya kuwapo sheria chafu zinazowalinda.

Tusiogope mamlaka ya Rais na dhamana ya CCM kama vinatumika vibaya.

Rais yupo kwa ajili ya wananchi lakini wananchi hawapo kwa ajili yake. Yeye ni mtumishi wao. Si ndivyo alivyotwambia wakati akituomba tumchague? Sasa inakuwaje anapoingia madarakani awe mtumikishaji badala ya mtumishi?

Nani anataka kumwajiri mtumishi mwenye kiburi na mamlaka kupita yake muajiri?Hapa ndipo Rais anapopaswa kuwa makini.

Kama umma utajua haki na wajibu wake na jinsi ya kuvitumia vitu hivi hatakuwa na lake. Na hii ndiyo silaha iliyowakomboa wenzetu kwenye nchi tunazoziita zimeendelea.

Kitu muhimu ni kuelewa kuwa nguvu ya umma huwa haiji kwa kubembeleza au kupewa na watawala bali hujitokeza na kuziba ombwe.

Mapinduzi tunayopigia mifano kama yale ya Urusi (1903-05 na kuendelea) na yale ya wafanyakazi wa Ufaransa (1789-1799) hata ya hivi karibuni ya Poland (Septemba 1980) na ya Romania (Desemba 1989) hayakushushwa kutoka mbinguni.

Yalisababishwa na dhuluma ya watawala kwa watawaliwa. Yalianzishwa na kuchochewa na ufisadi na kiburi cha watawala waliowaona watawaliwa kama vyombo vyao vya kuneemekea na kutanulia kama ilivyo kwetu.

Mapinduzi haya yalikiuka imani na itikadi za kisiasa na kidini kiasi cha kujichimbia kwenye ukombozi wa kweli kiuchumi. Hakuna anayekula itikadi ya dini wala chama chake bali mkate. Je, bila kuwa na haki mkate ambao ni keki ya taifa utaipata wapi?

Hii ndiyo siri ya heshima na ustawi wa nchi tajwa, hasa mwananchi wa kawaida mitaani-msukuma mkokoteni, omba omba wa kutengenezwa, mwanafunzi, mjamzito maskini asiye na pa kwenda kutibiwa.

Chuki dhidi ya wale waliokuwa wakiishi maisha ya uhakika na wale waliokuwa wakiishi ‘bora liende’ ndicho chanzo na chachu ya wenzetu kufanya mapinduzi hasa kuanzia kwenye fikra na malengo yao kama jamii.

Leo Watanzania wamegeuzwa kunguru kula vya kudandia na kudokoa! Haya si maisha ni kiama.

Si maisha anayostahili kuishi mtanzania juu ya nchi yenye kila neema na utajiri.

Kuendelea kujiweka utumwani kwa watawala ni ukondoo na ukuku.

Haya si majaliwa ya binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe. Haya siyo majaliwa wala maisha yanayomfaa Mtanzania.

Kwa nini kwa mfano Watanzania tuishie kuwa makapuku huku hata wakimbizi wa kiuchumi kutoka India na China wakiishi vizuri miongoni mwetu?Sina haja ya kuleta ubaguzi wala hisia zake.

Ndiyo ukweli tunaopambana nao kila siku mitaani. Rejea Wahindi kuwa karibu katika kila kashfa ya wizi wa mabilioni yetu walipa kodi.

Rejea kuanza kuongezeka kwa idadi ya wabunge wafanyabiashara wa Kihindi ili kulinda maslahi yao ambayo kimsingi yanaua maslahi yetu.

Hapa ndipo ilipo siri ya akina Jeetu Patel kutuibia. Wanatumiwa na watawala kwa kujua fika mambo yatakapoharibika watawatorosha. Rejea kwa mfano kuwa vigumu kuwatorosha akina Maregesi na Lukaza. Hawa wangekuwa Wahindi kisingepatikana kitu.

Tukirejea kwa walengwa wa makala hii, ni wakati muafaka kuwatendea na kujitendea haki kwa kuwataka waachie ubunge kama taasisi ya umma.

Wakikataa tuandamane kuwazuia wasiingie kwenye Bunge letu. Maana watalitia najisi kutokana na kuendekeza ulafi na maslahi yao binafsi kinyume na yale ya umma.

Vita hii ni ‘do or die’ au kufa na kupona. Kuondokana na watu kama hawa kwenye taasisi hakutupi hasara bali kurejesha haki zetu za kuishi kama watu.

Si chuki wala chuiu.Watawala wabovu wamekuwa chanzo kikuu cha umaskini wetu kuliko hata majanga ya kimaumbile kama vile ukame.

Hebu rejea kitendo kichafu cha Rais wa zamani na walafi wenzake kuleta, kwa mfano, kampuni ya Kikaburu kuja kuua TANESCO lililosababisha kupandishiwa umeme.

Rejea hata hili sakata la Richmond ambapo tunalazimika kulanguliwa umeme kuwalipa matapeli wanaoshirikiana na baadhi ya watawala wetu.

Hatuwezi kama nchi kuendelea na jinai hii na tukajidanganya kutakuwa na maisha bora kwa Mtanzania.

Sasa ni miaka mitatu tangu tuambiwe maisha bora kwa Mtanzania. Nini kimefanyika zaidi ya kuishia kuwa usanii wa kisiasa?

Kuna haja ya kuanza hata kupambana na rais wetu kwa kumbana atimize tuliyokubaliana na kama atashindwa hata mwaka 2010 asiruhusiwe hata katika chama chake kugombea tena kiti cha urais maana amefeli vibaya sana.

Tuhitimishe.

Wakati sasa umefika kuwataka ‘kiutu mzima’ watajwa na wengine wanaofanana nao kujitoa haraka kabla ya umma kuwachukulia hatua ambazo matokeo yake hayatakuwa mazuri kwao.

Hapa ni kuwaomba wabunge wenye uchungu na nchi kutokubali kuburuzwa na chama kilichokwisha onyesha wazi kuishiwa na kupoteza mwelekeo.

Mungu ibariki Tanzania.

mpayukaji@yahoo.com

Chama chetu hakina mpango wa kuwafukuza wabunge wetu maarufu na wakaribu na waadilifu toka ndani ya CCM.
 
Mwenye Kutaka Kuwatoa Ubunge Watu Hawa Ni Wananchi Walio Wachagua Kwa Kura Nyingi Sio Mwingine Wowote Yule
 
Mwenye Kutaka Kuwatoa Ubunge Watu Hawa Ni Wananchi Walio Wachagua Kwa Kura Nyingi Sio Mwingine Wowote Yule

Hayo ni mojawapo ya mapungufu ya katiba na sheria ambayo yameachwa wazi ili kuweza kuwalinda walafi wachache. Sheria na kanuni ambazo lengo lake ni kumlinda mnyonge zinatakiwa kuweka wazi mambo kama hayo.Iwapo kiongozi ameishanuka rushwa na kupelekea kutuhumiwa, basi apoteze pia sifa ya kuwa kiongozi, ama mtendaji wa serikali. Hii inaweza kupelekea kupunguzia walipa kodi mzigo mkubwa sana wa gharama za kutunza baadhi ya viongozi wastaafu..ambao wameishanuka rushwa..pia inaweza kutuhakikishia viongozi bora hapo baadae..
 
Lula wa Ndali-Mwananzela

Huko ndiko tunasema kumkoma nyani haswa na sasa JK tuone usanii wake kama utafanya Kazi. Maana kwa DITO ameponea chupu chupu baada ya Dua la kuku kumpata Mwewe na Balalis ametoweka kiajabuajabu ingawa marekani wamesema kama tunamtaka wako radhi kumrudisha.

Huyu ni lazima tule naye hii keki hadi mwisho bila kusahau aliyekuwa waziri mkuu wake EL na pesa zake za richimonduli.
 
Je Atarudisha Pia Majumba Aliyomnunulia Mkewe Christina Na Wadogo Zake ?

Christina Nae Atarudisha Pesa Anazomuhonga Yule Dogo Dogo ?
 
Hata Hivyo Hii Nchi Sio Ya Democrasia Huru Kwahiyo Vitu Hivyo Ni Bado Sana Kuwa Kama Sheria Kwa Sababu Hata Wananchi Wenyewe Hawajui Haki Zao
 
Hata Hivyo Hii Nchi Sio Ya Democrasia Huru Kwahiyo Vitu Hivyo Ni Bado Sana Kuwa Kama Sheria Kwa Sababu Hata Wananchi Wenyewe Hawajui Haki Zao

Ni kweli..suala la uelimishaji wa raia kuhusu haki zao linakuwa gumu sana.. hii katika nchi yetu inatumika kama mojawapo ya mbinu ya utawala..nadhani ipo wazi sana kwamba ni rahisi sana kumtawala mjinga..tujiulize je ni mara ngapi watu wamekuwa wakutana na sheria ambazo hawazifahamu, pindi wanapotiwa mbaroni ama, wanapojikuta kizimbani?
Kuna fungu pia ambalo hutolewa na sirikali kwa ajili ya uelimishaji wa raia juu ya haki zao ikiwa ni jitihada za kuimarisha utawala,(UTAWALA bora/BORA utawala?)..na vile vile kuna NGO's ambazo zinafadhiliwa kwa kutekeleza kazi hizo..wanapopeleka hizo hela nadhani wengi wetu..kama mie hatufahamu...na wala hatuelewi kwamba tutaenda kuhoji wapi na kumhoji nani kuhusu ufanisi wa zoezi hilo,matumizi yake na vyombo dau pia...
 
..wananchi wa Bariadi,Kibaha,Bukoba Vijijini, ndiyo wenye haki ya kuwavua Ubunge kina Chenge,Msabaha,na Karamagi.

..wananchi kumkataa mbunge wao siyo jambo la ajabu Tanzania. miaka ya 1980 wananchi wa same walimshitaki mbunge wao Chediel Mgonja kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa wakati wa uchaguzi.

..asiyewataka Karamagi,Chenge,na Msabaha, aandae hoja ya kikatiba kwa kushirikiana na wananchi wa Bukoba,Bariadi, na Kibaha, na aipeleke mahakamani kwamba hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge.
 
Mbunge ni mwakilishi na anayepelekwa kwa wananchi kupitia chama husika. Chama kikimfukuza mbunge anakuwa automatically amepoteza kiti chake bila kujali kama amechaguliwa na wananchi wake au la.

Hawa waheshimiwa ni MAFISADI hii haina shaka. CHama chochote cha siasa kiko kwa ajili ya maendeleo ya taifa na siyo MAFISADI. Chama chochote chenye viongozi ambao ni MAFISADI(ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa) hakifai na kinaweza kutafsiliwa kuwa ni chama cha mafisadi.

Chama cha mapinduzi kina watu ambao tayari wamethibitika kuwa ni mafisadi. Ni jukumu la chama cha mapinduzi kuhakikisha kinaondoa uozo ktk bunge letu.

Bungeni ni mahala patakatifu, mahala pa kutunga sheria sheria ambazo zinatakiwa ziheshimiwe na kufuatwa na mtanzania yeyoyte bila kujali anatoka Bukoba vijijini, Mto wa Mbu, Shinyanga, mara au wapi.

Mojawapo ya sheria ni pamoja na sheria za uadilifu.

Mbunge ambaye ni mwizi wa mali ya umma atatungaje sheria inayokataza wizi?. Huu ni mgongano wa MASilahi. Tunaomba vyama husika viweze kuondoa wote waliohusika ktk kashifa za ufisadi.

Vinginevyo ni jukumu la wananchi kuhusisha UFiSAdi na vyama husika.
 
..asiyewataka Karamagi,Chenge,na Msabaha, aandae hoja ya kikatiba kwa kushirikiana na wananchi wa Bukoba,Bariadi, na Kibaha, na aipeleke mahakamani kwamba hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge.

Katiba ina mapungufu mengi mojawapo ni hili la waziri ambaye ni fisadi anajiuzulu uwaziri lakini anaendelea kuwa mbunge. Mishahara na marupurupu yao inalipwa na Watanzania wote sio wale wa majimbo ya waliowachagua tu.

Warioba ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu amaeshatamka kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuandika katiba mpya na kipengele ambacho ni lazima kiwekwe ni kile kinachosema kwamba ukijiuzulu au kufukuzwa uwaziri moja kwa moja unapoteza na ubunge wako.
 
Mkuu kama sikosei warioba alishiriki katika kuandika katiba iliyopo sasa hivi kama ameona hili kwa hiyo hili suala halina mjadala.

Tunatakiwa tuweke nguvu kuhakikisha katiba inaandikwa upya kabisa kulingana na experience na challenges tunazozipata sasa hivi na kuangalia challenge zinazokuja siku za usoni.
 
The Anti-Money Laundering ACT 2006 was enacted and is inforce. The Tanzania Financial Intelligence Unit (FIU) has also been established and the President has also appointed one BOT Fisadi by the name of Herman Mark Kessy as its first Commisioner. As I write this, the FIU is busy recruiting albeit not in a so open and competitive manner(apparently, personnel for the unit are appointed and they will only come from the public sector) this in my view is a recipe for failure.

Every so often the Tanzanian government comes up with some profound plans to tackle this or that, they enact laws and establish agencies but then implementation is usually carried out so horribly that everything fails in the end. This FIU is a classic example! Why appoint people? I belive the FIU will be better served if they advertised job positions competitvely, that way they stand a chance of getting the best and brightest.

Second, based on what I gathered from the ACT establishing the FIU, the FIU will be pretty much a toothless organization.They are only empowered to "recieve" "analyze" and "desseminate" information. This in my view will make the FIU a very passive agency.If we are serious about fighting economic and financial crimes,we need to take a "foward-leaning approach " The ACT should have given the FIU a more proactive role. How about amending the legislation so that it empowers the FIU to not only receive information, but also look for information, go after information, collect information,"Gather" information? How about amending the legislation so that it empowers the FIU to prosecute/institute criminal proceedings against offenders? The way things are right now is, if after analysis of recieved information, the FIU deems the information collected importatnt, the FIU can then disseminate the "recived" infomation to relevant law enforcment agenices so that the enforcemnt agencies can act upon it if they so wish/at their discretion. This is total BS!!. It seems like a deliberate loophole!This I say because, it gives the enforcement agencies the luxury of choosing not to prosecute eg. for political reasons.

Mr "Bubu ataka Kusema" the issue is that, the FIU does not have powers to prosecute offences listed under the Anti money laundering ACT 2006.If the FIU or any other law enforcement agency for that matter, such as the PCCB have evidence of Chenge's wrong doing, the only way Chenge anaweza kushitakiwa ni if the Directore of Public Prosecutions (DPP) does it himself or gives his "permission" either to the PCCB or some state attorney to do so.

Personally, I can speculate on a number of offences Chenge might have committed under the Anti-Money laundering Act. I am doing my reserch and will post it here shortly. The main issue though is, Je who is ready and willing to prosecute? I have reasons to seriously doubt if the DPP's office will allow any proceedings against Chenge.DPP could simply call "Nolle Prosequi" on the whole thing, and kill it instantly!
 
A legal opinion by the Tanzania Attorney General’s Chambers on the purchase of a 28 million British pounds air defence radar system from BAE Systems in 2001 is central to the scandal that has led to the resignation of the former Attorney General.

Mr. Andrew Chenge, who resigned from government last week, is a former Attorney General and had been promoted to cabinet to head the ministry for infrastructure development. The multi-million pound sterling scandal is under both local and international scrutiny. Chenge was Tanzania’s Attorney General when the radar deal was sealed. East African Business Week has learnt that at the time the deal was negotiated, Tanzania had no money so it had to look for other sources to finance the project.

Reliable sources say the Tanzania government sought a legal opinion about the deal at which point the Attorney General office advised “to continue with the project and above all advised the government to borrow money from a British bank, Barclays.” According to a source within the ministry of legal and constitutional affairs, that legal opinion was by itself illegal because such a commercial debt was uncalled for as the World Bank and the International Civil Aviation Organisation had said the purchase was “unnecessary and overpriced.”

He said the Attorney General’s Chambers advised the government to borrow a huge amount of money well knowing that the price was on the higher side. “Apart from an inflated price, Tanzania being a HIPC country was not supposed to enter such a debt burden with a two-digit interest rate,” he said. “The Serious Fraud Office (SFO) has shown concern after discovering that such a legal opinion was itself illegal, and could have been pushed by personal interests because the deal was wildly expensive,” he said.

Although reports that Chenge is under investigations came out recently, East African Business Week has established that the SFO started a follow up on the matter three years ago. The radar was manufactured by Siemens Plessey, which then had become a BAE subsidiary. The local Siemens agent then negotiated the sale with the Tanzanian defence ministry. The radar deal has a long history. It all started in 1992 during President Ali Hassan Mwinyi when negotiators had put the price tag at 11o million pound sterling.

The deal was blocked on reasons that it was unaffordable and the first Tanzanian President, Julius Nyerere played a great role in discouraging it. However, when Nyerere died in 1999, the scheme was resurrected, with a smaller phase to be followed by the rest but both the World Bank and the International Civil Aviation Organisation were against the deal. In the UK, the then Development Secretary, Ms. Clare Short, temporarily blocked aid payments in protest and said openly that she suspected corruption.

“It stank and was always obvious that this useless project was corrupt,” she was quoted as saying. Short also made an attempt to prevent the sale by arguing that a British arms export license be withheld but was overruled in cabinet by the then Prime Minister Tony Blair. Britain’s Foreign Secretary then, Mr. Robin Cook and current prime minister Gordon Brown were also against the deal. The reasons put forward by both Short and Cook were that because Tanzania is one of the poorest countries in the world, there were no substantive reasons to enter into such an expensive deal.

Chenge, resigned on April 20, 2008 after the Guardian newspaper of the UK said the minister has stashed away $1 million in an offshore account and that the team investigating the sale of the military radar to Tanzania was tracing the account. Also discovered, was a $ 500,000 transaction shown to have been made (from Chenge’s offshore account) to one of the senior officers of the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco). Two weeks ago SFO conducted an in-depth search at both Chenge’s offices and residence in Dar es Salaam.

Chenge is now the fourth minister to resign in a period of two months. Edward Lowassa (Prime Minister), Nazir Karamagi (Minister for Minerals and Energy) and Ibrahim Msabaha (EastAfrican Cooperation) resigned in February after they were implicated in the irregular awarding of a multi-billion shilling tender to generate emergency electricity in 2006. The tender was awarded to a shadowy American company, Richmond.
 
Back
Top Bottom