The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

chenge nenda usa na wewe,unasubili mpaka ukamatwe,mwanasheria wa zamani wa tanzania,du!!! nchi imeoza hiyo tanzania

Bora akajisalimishe polisi ajiandikie statement yake ya kweli, na akipelekwa mahakamani aplead guilty na awataje washkaji zake wote. Hii itamuepusha na ugonjwa hatari wa guilt conscious, ataishi maisha marefu huko segerea kwani atakuwa akiwahadithia wafungwa wenzie jinsi alivyotumia elimu yake kupora mali ya watanzania. Mwaya Chenge usikimbilie USA utaugua maradhi hayo niliyoyataja hapo juu.
 
-Pinda alishinikiza ‘asulubiwe!’
-Wabunge waliteta kumfukuza

SIRI ya kumtosa bilionea Andrew Chenge ni “kunusuru hadhi ya serikali inayotota” katika kipindi cha kilio cha wananchi dhidi ya ufisadi, MwanaHALISI limeelezwa.

Tayari imefahamika pia kuwa shinikizo la Chenge kujiuzulu limetokana na woga wa serikali ya Rais Kikwete kuja kushinikizwa na Bunge kumfukuza mwansheria mkuu huyo wa zamani.

Taarifa za ndani ya Bunge zinasema baadhi ya wabunge walikuwa wamejipanga kupeleka hoja binafsi, au kushinikiza kupitia kwa waziri mkuu, ili Chenge ajiuzulu.

Taarifa za Ikulu Dar es Salaam zinasema Rais Kikwete alikuwa tayari ana mawasiliano na Waziri Mkuu Mizengo Pinda juu ya “umuhimu” wa Chenge kujiuzulu.

Imeelezwa kwamba Pinda aliishamweleza rais kwamba “ni vema mtu wako akaondoka, akakupunguzia mzigo.”

Kauli hiyo inaendana na taarifa za awali kwamba Pinda alishasema hadharani kuwa yeye hakuomba kuwa waziri mkuu na kwa hiyo hatakubali kubeba mtu wa “kumchafulia.”

Hayo yanathibitishwa na kauli ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, aliyesema juzi kuwa rais alikuwa tayari anatarajia uamuzi wa Chenge kujiuzulu.

Chenge aliyekuwa Waziri wa Miundombinu alijiuzulu wadhifa wake Jumapili. Anakuwa waziri wa nne kujiuzulu katika mazingira yanayohusisha ufisadi ulioghubika taifa kwa takribani miaka kumi sasa.

Chenge anakabiliwa na tuhuma nyingi na nzito za kuwa na akaunti za benki katika nchi za nje ambazo MwanaHALISI hadi sasa limegundua kuna zaidi ya Sh. 25 bilioni ambazo upatikanaji wake unatiliwa mashaka.

Wachunguzi wa mambo wanasema kwa hali yoyote ile Chenge atakuwa hakutaja, katika fomu za wabunge za kutaja mali zao, utajiri wake ulioibuliwa na kuanikwa hadharani na vyombo vya habari.

Kama hivyo ndivyo, ukiukwaji wa maadili ulioambatana na utajiri wenye utata, unamwondolea Chenge uadilifu wote na unaweza kumgharimu hata ubunge wake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita baadhi ya mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Finland na Uholanzi walitembelea bungeni Dodoma ambapo, pamoja na mambo mengine, walikuwa wakifuatilia taarifa za ufisadi na hatua ambazo serikali inachukua kuukabili.

Kiongozi mmoja wa wa ngazi ya juu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameliambia MwanaHALISI kuwa chama chake hakiko tayari kumlinda Chenge na hivyo kuhatarisha sifa yake mbele ya wanachama na wananchi kwa ujumla.

Amesema, “Chama kipo tayari hata kupoteza jimbo lake kwa maana ya kuchukuliwa na upinzani, lakini kisipakwe matope kwa ajili ya mtu mmoja.”

Jimbo la Chenge, Bariadi Magharibi, lilipokonywa kwa United Democratic Party (UDP) ambacho mbunge wake alikuwa Isaack Cheyo.

Mawaziri wengine waliojiuzulu ni Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu, Dk. Ibrahim aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki na Nazir Karamagi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Wote hawa walikumbwa na kashfa ya upendeleo kwa kampuni feki ya Richmond iliyoingia mkataba na serikali kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 100. Ilishindwa kufanya hivyo kwa kutokuwa na uwezo kifedha na kiufundi.

Chenge ambaye alikuwa ameanza kuitwa “bwana vijisenti” kutokana na kauli yake kuwa mabilioni yaliyokutwa kwenye akaunti yake Ulaya yalikuwa vijisenti tu, ameondoka kimyakimya baada ya kuwasiliana na rais wake.

Rweyemamu, akiongea katika kipindi cha BBC juzi Jumatatu asubuhi, alisema kitendo cha Chenge kujiuzulu kinaonyesha kile alichoita “ukomavu wa kisiasa na mfano wa kuigwa wa umakini wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete.”

Wki mbili zilizopita Kikosi Maalum cha Upelelezi wa Ufisadi Sugu cha Uingereza, kilinukuliwa na gazeti moja la Uingereza, The Guardian, kikisema Chenge ana zaidi ya Sh. 1.2 bilioni kwenye akaunti binafsi iliyoko kisiwa cha Jersy.

Hata hivyo taarifa za uhakika zilizochapishwa na MwanaHALISI zinasema akaunti hiyo ya Jersy ina Euro 3 milioni, sawa na Sh. 6 bilioni. Ni kutoka kwenye akaunti hii zilichotwa dola 600,000 kwenda kwenye akaunti ya “bosi” wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa shughuli ambayo haijafahamika.

Katika akaunti ya Uswisi, Chenge anamiliki dola 467,000 sawa na nusu bilioni, fedha ambazo zilichotwa kwenye akaunti ya kampuni ya TANGOLD iliyopo tawi la NBC Limited makao makuu.

Akiwa Mkurugenzi wa TANGOLD na mwidhinishaji malipo, Chenge anasimamia pia mabilioni katika akaunti mbili za kampuni hiyo zilizoko NBC Limited makao makuu.

Akaunti moja ya fedha za kigeni Na. 011105011782 ina akiba ya dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni. Katika akaunti nyingine ya fedha za ndani, Na. 011103024852 ya tawi hilohilo, kuna Sh. 1,379,359,367.37.

Kwenye akaunti yake ya fedha za Tanzania katika NBC Limited, makao makuu, Chenge anamiliki Sh. 25,794,805.89 hadi 11 Aprili mwaka huu.

Wachunguzi wa mambo wanasema kwa kadri Chenge alivyokuwa amekataa kujiuzulu, hatua hiyo aliyochukua siku tatu baada ya kung’akia waandishi wa habari wakati akitoka ziarani China, itakuwa imeshinikizwa na ikulu.

“Baada ya siri zake kuanikwa na yeye kushindwa kijitetea; na papo hapo kuonekana kuwa mzigo kwa utawala, wakubwa zake wameonelea wamtose ili kuepuka maswali mengi na magumu yanayohusu kwa nini anaendelea kukumbatiwa,” ameeleza mmoja wa wachunguzi.

Kuondoka kwa Chenge kunafungua mlango wa mawaziri wengine, naibu mawaziri na watendaji wakuu wa serikali waliohusika na kashfa za ufisadi kujiondoa kazini kabla ya kulazimishwa.

“Haileti maana yoyote kwa waziri kujiuzulu lakini Katibu Mkuu na wakurugenzi wakabaki kazini,” kimeeleza chanzo cha habari.

Hata hivyo imefahamika kuwa naibu mawaziri wawili huenda wakajiuzulu nafasi zao au kuondolewa wakati wowote kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

MwanaHALISI haikuweza kupata majina ya mawaziri hao.
 
...Hata hivyo imefahamika kuwa naibu mawaziri wawili huenda wakajiuzulu nafasi zao au kuondolewa wakati wowote kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

MwanaHALISI haikuweza kupata majina ya mawaziri hao.

Jamani hawa manaibu waziri wawili ni akina nani? na kashfa zao ni zipi? Mwanahalisi ameficha hapa!
 
Sasa wenzangu kuna haja ya kendelea na uchunguzi wa ile tume ya madini wakati matatizo yashajulikana mwnasheria mkuu anasaidia timu pinzani Tutafika kweli
 
La kuvunda halina ubani! Bado mafisadi chungu nzima wa mabilioni ya pesa za walipa kodi ambao hawajaguswa. Huyu Chenge kama alivyo Lowassa, Msabaha, Karamagi bado ni mbunge na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mafisadi.

Kwa maoni yangu huyu bado hajatoswa ameondolewa tu uwaziri ataendelea kupata mshahara na marupurupu manono kama Lowassa, Msabaha na Karamagi ambayo hawastahili.
 
Jamani hawa manaibu waziri wawili ni akina nani? na kashfa zao ni zipi? Mwanahalisi ameficha hapa!

Ni vizuri tukapata majina ya hawa mapema ili tuone kama kweli wanasitahili kujiuzuru, na makatibu wa wizara je inakuwaje maana nao kuna ambao wana kashifa kubwa tu.
 
Wangeipata hiyo ya vijisenti ingekuwa vizuri zaidi ili nchi wafadhili waone na kushinikiza huyu mtu ashitakiwe.
 
Sasa wenzangu kuna haja ya kendelea na uchunguzi wa ile tume ya madini wakati matatizo yashajulikana mwnasheria mkuu anasaidia timu pinzani Tutafika kweli

haja ya kuendelea na uchunguzi ipo, we unafikiri alipokuwa anaiba aliiba mwenyewe? unamaanisha kuwa huyu ni bangusilo? hiyo tume tunaisubiri kwa hamu ilete matokeo
 
-Pinda alishinikiza ‘asulubiwe!’
-Wabunge waliteta kumfukuza

...............Wiki mbili zilizopita Kikosi Maalum cha Upelelezi wa Ufisadi Sugu cha Uingereza, kilinukuliwa na gazeti moja la Uingereza, The Guardian, kikisema Chenge ana zaidi ya Sh. 1.2 bilioni kwenye akaunti binafsi iliyoko kisiwa cha Jersy.

Hata hivyo taarifa za uhakika zilizochapishwa na MwanaHALISI zinasema akaunti hiyo ya Jersy ina Euro 3 milioni, sawa na Sh. 6 bilioni. Ni kutoka kwenye akaunti hii zilichotwa dola 600,000 kwenda kwenye akaunti ya “bosi” wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa shughuli ambayo haijafahamika.

Katika akaunti ya Uswisi, Chenge anamiliki dola 467,000 sawa na nusu bilioni, fedha ambazo zilichotwa kwenye akaunti ya kampuni ya TANGOLD iliyopo tawi la NBC Limited makao makuu.

Akiwa Mkurugenzi wa TANGOLD na mwidhinishaji malipo, Chenge anasimamia pia mabilioni katika akaunti mbili za kampuni hiyo zilizoko NBC Limited makao makuu.

Akaunti moja ya fedha za kigeni Na. 011105011782 ina akiba ya dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni. Katika akaunti nyingine ya fedha za ndani, Na. 011103024852 ya tawi hilohilo, kuna Sh. 1,379,359,367.37.

Kwenye akaunti yake ya fedha za Tanzania katika NBC Limited, makao makuu, Chenge anamiliki Sh. 25,794,805.89 hadi 11 Aprili mwaka huu.....................

Wajameni ma vijisenti yote hayo....huyu si fisadi tu ni mhujumu uchumi.....hukumu yake inatakiwa haraka sana.Ndio maana lilikuwa na kiburi hivi. Anaringia pesa zetu
 
Jamani hawa manaibu waziri wawili ni akina nani? na kashfa zao ni zipi? Mwanahalisi ameficha hapa!

Si kama kawaida ya waandishi wetu wa habari na slogan yao "jina tunalo lakini tunalihifadhi"

Cha ajabu ni kuwa kwenye gazeti la majira wamemtaja Mwakyembe hajalipa bill ya maji...angalia hawa ma hypocrites
 
Bwana Vijisenti Chenge kama alikuwa registered mwanasheria Tanzania au hata nje ya nchi, Uanasheria wake ufutwe mara moja kwani ameshindwa kabisa kutekeleza maadili ya kazi yake mbali ya yale ya wadhifa aliokuwa nao.

Tunaomba bodi inayosimamia mamlaka ya wanasheria Tanzania imuondoe huyo FISADI CHENGE mara moja.
 
Kinachonishinda kuelewa ni pale hawa aMafisadi wanapoendelea kushika nafasi zao za Ubunge bila kuwauliza wananchi waajiri kuhusiana na viongozi hao.
Hivi kweli kesi za hawa mafisadi zinaishia kujiuzuru kwao, hata kama wananchi hawataki kuwaona wezi waliowaibia wakiendelea kushika wadhifa wa Ubunge na kuendelea kulipwa mabillioni ya fedha zao mbali na zile walizokwisha iba.
Hawa mafisadi kwa lugha nyepezi ni WAHARIBIFU.... inakuwaje waruhusiwe kuendelea kuharibu mipango ya maendeleo ya ambayo ni pamoja na utunzi wa sheria pamoja na mabadiliko yoyote ya katiba ambayo yanaweza kuwabana..
 
mawaziri wote waliokuwao kwenye utawala wa Benjamini mkapa wanahusika na ufisadi njia moja au nyengine.
JK atakuwa bado hana serikali mpaka pale atapowauzulisha wote waliotoka enzi zile. ikiwezekana na ubunge pia
 
Mkataba ulikuwa unahusu sehemu gani ya Miundo mbinu na ni kitu gani "Wakina" walikuwa wafanye?
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameelezwa kukerwa na jinsi mawaziri wa serikali yake wanavyofanyakazi bila uangalifu. Watu waliokaribu na Rais Kikwete na walioongozana naye katika ziara ya India, China na Marekani, waliliambia gazeti hili kuwa kukwerwa huko kulitokana na baadhi ya mawaziri kuharibu mkataba.
Walisema kuwa mkataba huo uliokuwa kwa upande mmoja usainiwe na waziri wa Tanzania na upande mwingine waziri wa China, uliharibika baada ya kusainiwa na mawaziri wawili wa Tanzania, hivyo kuharibu itifaki.
Wakizungumza kwa sharti la kutokutajwa majina gazetini, walisema kuwa mkataba huo ulikuwa batili baada ya kusainiwa na mawaziri hao waandamizi, hali iliyomfanya Rais Kikwete kuja juu kutokana na uzembe huo.
Vyanzo hivyo vya habari vilidai kuwa mkataba huo ulisainiwa na mawaziri hao wawili kutokana na jinsi ulivyokuwa umeendaliwa licha ya ukweli kwamba ulikuwa ukihusu zaidi wizara moja.
Walidai kuwa mkataba huo uliokuwa ukihusisha masuala ya wizara ya miundombinu, katika mazingira yasiyoeleweka ulianza kusainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na kisha kusainiwa na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge.
Vyanzo hivyo vilidai kuwa Waziri Membe alisaini mkataba huo baada ya kuwepo kwa sehemu yake ya kusaini, huku nyuma kukiwa na sehemu ya kusaini Chenge.
Kulingana na vyanzo hivyo, inadaiwa kuwa baada ya kusainiwa, mkataba huo ulikuwa batili kwa kuwa ulipaswa kuhusisha waziri mmoja wa Tanzania na mwingine wa China.
Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja aliyehusika na uzembe huo katika mkataba huo ambao unadaiwa uliandaliwa mapema tangu kuwapo kwa taarifa ya safari ya Rais Kikwete nchini China.
Pia haikuweza kufahamika hatua ambazo Rais Kikwete anaweza kuzichukua dhidi ya mawaziri wake hao kutokana na uzembe wa kuandaa mikataba kama ilivyojitokeza.

Ndio wateule wa Kikwete hao, na anaandamana nao kwenda kuuza nchi kwa Wakoloni wapya! Hata mkataba wa Buzwagi ulisainiwa na Karamagi akiwa katika ziara ya Kikwete.
 
Kazi kubwa kwani Chenge si mwanasheria au msomi wa UDSM?
 
mawaziri wote waliokuwao kwenye utawala wa Benjamini mkapa wanahusika na ufisadi njia moja au nyengine.
JK atakuwa bado hana serikali mpaka pale atapowauzulisha wote waliotoka enzi zile. ikiwezekana na ubunge pia

Wanahusika ndio! maana maamuzi hufanywa na baraza la mawaziri kwahiyo hata JK anahusika. Wenye akili finyu humtoa huyu jamaa.
 
Je Raisi Kikwete Ni lini wananchi watathibitika na kuthibitishwa kama walikuwa wahujumu Uchumi waliokubuhu.
 
Back
Top Bottom