The Radar Scandal: Investigation & Progress

Kuna habari niliiweka hapa kuhusu Usalama wa Taifa, Sekretarieti ya Maadili kuhusu file la AC lakini Imehamishiwa kwenye sehemu nyingine. Kulikuwa na maswali mengi ya kujiuliza na habari hii nina i-paste hapa kama ifuatavyo:-

Habari ya baadhi ya utajiri wa Mh. Chenge ulioibuliwa na gazeti maarufu nchini Uingereza The Guardians imewashitua watu wengi wakiwemo cabinet members wenzake. Maneno mengi yataongewa sana lakini the bottom line huyu Chenge ndiye anajua ukweli kuhusu huo utajiri wake. Inabidi aje mbele ya wananchi na aeleze ni jinsi gani ameweza kujikusanyia hizo fedha.

Anyway nirudi kwenye mada. Ninaamini kuwa Kiongozi yeyote wa ngazi ya juu katika serikali kabla hajachukuwa madaraka huwa anafanyiwa uchunguzi kuona uadilifu wake. Utaratibu huu upo na unafanywa na Usalama wa Taifa, nina ushahidi kuwa utaratibu huu ulikuwepo kwa sababu niliwahi kufanya kazi katika ofisi ambayo ilikuwa inaomba ushauri kutoka Usalama wa Taifa ilipofikia wakati wa kuteua viongozi wa serikali kama vile mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara n.k
Usalama wa Taifa ulikuwa na jukumu la kuangalia uadilifu na rekodi za mtumishi ambaye alikuwa anatarajiwa kupata Presidential appointment. Baada ya kupata rekodi zake ndipo Rais ana decide either kumteua huyo mtumishi/mtu au la kulingana na rekodi yake.

Kitu ambacho kinanishangaza mimi ni kwamba Mh. Chenge amekuwa mtumishi wa serikali kwa muda mrefu. Na kila alipokuwa anapata Presidential appointment faili lake lilitakiwa lipitiwe na hawa jamaa wa Usalama wa Taifa ili kubaini kama kulikuwa na vitu ambayo vilikuwa ninakwenda kinyume na maadili ya mtumishi.Sasa within 3 years huyu jamaa kapata Presidential appointment mara 2 lakini still faili lake halikupata kuangaliwa kubaini kama kulikuwa na kasoro yoyote. Huenda liliangaliwa lakini wakaamua kuziba midomo yao.
Sasa watanzania tuelezwe ukweli kama ili faili lilichunguzwa na recommendation zikapelekwa kwa JK kuwa huyu jamaa anafaa kuchukuwa nafasi ya uwaziri. Kama walibaini hayo maburungutu huko Jersey je JK alishawishika vipi kumpa cabinet positions 2 times bila kuuliza maswali kuhusu hiyo account? Na kama alipewa maelezo kuhusu hiyo pesa aliridhika vipi kama hiyo pesa imepatikana kihalali?

Hivi karibu kuna swali liliulizwa bungeni na hilo swali lilielekezwa kwenye ofisi ya Rais kuhusu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Na hilo swali liliuliza ni watumishi wa Umma wangapi ambao wamewahi kutuhumiwa au kugundulika na hiyo Sekretarieti kujipatia mali isivyo halali. Na hilo swali lilijibiwa kuwa hakuna hata mmoja. Sasa sielewi hii Sekretarieti inakwenda how much deep kuwachunguza viongozi wa Umma kuhusu mali wanazotaja. Maana Mh. Waziri katika ofisi ya Rais ambaye yuko responsible na hiyo Sekretarieti hiyo alidai hakuna kiongozi aliyedanganya katika kutaja mali zake. Leo hii tena Waziri wa nchi (Utawala Mtamu) anaonyesha mshangao kuhusu hiyo account. Hapa kuna mashaka kidogo kwamba kuna mtu au taasisi haifanyi kazi yake ipasavyo. NI NANI WA KUWAJIBIKA HAPA????? Usalama wa Taifa hilo hamkuliona kabla JK hajamteua kwa mara ya kwanza kuwa Waziri, Sekretarieti hamkuweza kuchunguza kwa undani zaidi ndani na nje ya nchi kujua kama mtumishi yeyote wa umma na akiba kupita income yake. Kama mlikuwa hamjui ukweli basi MMEPIGWA BAO SI TU NA CHENGE BALI KUNA WENGINE ZAIDI.
Huyu ni mtu mmoja kawapiga bao kwa account moja tu, maana hatujui anazo ngapi huko nje. Kwa hiyo alikudanganyeni, na huyo ni Chenge tu sasa je wengine vipi kama akina Mgonja, Mramba, Mkapa, Yona na wengineo???? Na kama mlijua ukweli kwa nini mlinyamaza? Na kama hamkunyamaza, mlimshauri vipi Rais kuhusu huyu jamaa. Hapa lazima watu wawajibike. Mambo yanakwenda tu kiholela, nakumbuka FS kabla hajawa PM faili lake lilipitiwa na watu wa Usalama kama ilivyo desturi lakini kwenye term yake ya pili faili liliteleza tu wakati kuna upupu tayari alikuwa ameshaanza kufanya. UCHAFU UMEKITHIRI KUPITA KIAMA.

Sasa katika hili nani wa awajibike hata kabla ya AC kuondoka maana dhis taimu AC haz no choisi dhan tu liv bifo hi get kicked aut. Nani awajibike? Usalama wa Taifa, Sekretarieti ya Maadili au Rais mwenyewe. Mie nilikuwa nafikiria wote mnatakiwa kuwajibika, Rais pamoja na taasisi zake za kisanii ili tuanze upya.
 
Waache uhuni, wanashtuka utajiri wa Chenge au wanashtuka umewekwa peupe?
Wakati wanakomba za EPA hawakushtuka, Wakati wanakomba za Richmond hawakushtuka, wakati wanakomba za Twin Towers hawakushtuka, wakati wanakomba Buzwagi hawakushtuka...
 
Hawakushtuka bilioni 133 na bilioni 155 zilizokupuliwa na mafisadi toka BoT ambao mpaka leo hii hakuna hata mmoja wa hao mafisadi aliyeguswa na mkono wa sheria! eti sasa ndio wanashtuka! Kikwete acha usanii nchi inakushinda!

Posted Date::4/14/2008
Utajiri wa Chenge waishitua Ikulu

*Ni kuhusu kumiliki akaunti ya Sh 1 bilioni

*Yasema inasubiri taarifa rasmi sheria ichukue mkondo

*Profesa Lipumba kuuzungumzia leo

Ramadhan Semtawa, Dodoma na Muhibu Said, Dar
Mwananchi

SIKU moja baada ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kudaiwa kumiliki dola 1 milioni nje ya nchi, serikali imesema sheria itachukua mkondo wake kuona fedha hizo amezipataje.

Hatua hiyo itafanyika baada ya taarifa rasmi kuhusu utajiri wa waziri huyo kufika serikalini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alisema taarifa rasmi zikifika, sheria itachukua mkondo wake kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria. Simba alisema hata yeye hayuko juu ya sheria.

Waziri Simba aliongeza kwamba, taarifa zikifika itaangaliwa katika kumbukumbu za Chenge katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma.

Alisema Chenge kama viongozi wengine, amejaza fomu za kutaja mali zake hivyo kama amedanganya, itajulikana.

Simba alipoulizwa anachukuliaje taarifa za waziri kumiliki fedha nyingi kama dola 1 milioni, alijibu: "Hata mimi nashangaa kama wewe iwapo alizipata kihalali au la."

Alisema hadi sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi nchini Uingereza.

"Ni vema watu wakawa na subira katika jambo hilo. Lakini kuna mtu nimemwambia, labda kauza ng'ombe wao wote ndio akapata hizo pesa, labda watu hatujui, au ana biashara nyingine," alisema Waziri Simba.

Kauli hiyo ya Waziri Simba imetolewa siku moja, baada ya Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza, katika toleo lake la juzi, kueleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya Waziri Chenge, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini humo, ijulikanayo kwa jina la Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa, wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajia kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Waziri Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey, zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada hiyo kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.

The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.

Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba, fedha hizo ni mali yake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika serikali ya awamu ya tatu.

Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Waziri Chenge katika orodha ya vigogo 11, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini, wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.

Baadaye, Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa, walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleke katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.

Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo inamilikiwa na serikali na kwamba, hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.

"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wa wakurugenzi hadi sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge na kuongeza:

"Lakini kama mtu ana ushahidi wa tuhuma za ufisadi, jamani tunavyo vyombo vyetu, si wapeleke zikafanyiwe kazi," alisema Chenge.

Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.

Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.

Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanasheria Mkuu katika serikali ya awamu ya pili na ya tatu.

Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005, hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba, suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye aliyemteua.

Chenge alisema hayo mara tu baada ya kuapishwa na Rais Kikwete kuendelea kuiongoza wizara hiyo katika sherehe za kuwaapisha mawaziri katika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma Februari 13, mwaka huu.

Akizungumzia taarifa hizo, Dk Slaa alisema ni habari za kutisha kwani mshahara na posho zake haziwezi kumfanya kuwa na akiba kubwa kiasi hicho.

"Huyu Waziri wa Tanzania ambaye mshahara wake tunaujua, posho zake zinajulikana lazima aeleze alipata wapi fedha hizo," alisema.

Dk Slaa alisema SFO wanafanya uchunguzi wa kwao na kwamba Chenge ni shahidi tu.

"Nilishamuomba Rais Kikwete amwondoe uwaziri na uchunguzi wa kina ufanyike, yatagundulika ya ajabu," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, leo atakutana na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuzungumzia tuhuma hizo za umiliki wa fedha nyingi dhidi ya Chenge.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani, aliliambia gazeti hili jana kuwa, Profesa Lipumba atakutana na waandishi wa habari, kuzungumzia suala hilo katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam wakati wa asubuhi.

"Kesho (leo) saa 5:00 Profesa (Lipumba) atakuwa na press conference (mkutano na waandishi wa habari) makao makuu Buguruni, kuzungumzia hilo suala la (Waziri) Chenge," alisema Bimani, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa.

Ikulu ipi imeshitushwa ? Wameshitushwa na kitu gani ? Nani hapo Ikulu kashituka hasa ? Maana ikulu ina wengi pale .Kuna Rostam , JK nk .Nani hasa kashituka utajiri huu ?
 
Ndugu yangu we! fisadi ana muda wa kuangalia faili la fisadi mwenziye! Hayo yalikuwa wakati wa Mwalimu Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi ~AMEN. Ili mradi akishajua kwamba jamaa ni fisadi mwenziye na anaweza kumtumia kwa ufisadi wao na kuficha madhambi yao basi mara moja anapata uteuzi. Mafisadi wanajuana kwa ufisadi wao kama vile waarabu wa pemba wanavyujuana kwa vilemba!
 
unashutuka kitu ambacho ukui lakini hii habari hipo jambo forum zaidi ya mwezi sasa, so its not new, huyu jamaa hawezi kuondolewa kwenye serikali ya CCM kwa kuwa ana skendo nyingi za CCM lazima waendelee kumuifadhi, lets wait Vasco dagama arudi kutoka ughaibuni tuone
 
JK anatakiwa avunje baraza lake lote na yeye akiwemo na uitishwe uchaguzi mwingine, yaani kote unapogusa ni ufisadi tu. Tangu Mwl JKN aage dunia SISIEMU wamekuwa wakikimbizana mbio za Marathoni za UFISADI. Nani zaidi, nani kakusanya mali nyingi kwa kipindi kifupi, katumia masaa mangapi kumaliza hiyo FISADIZ' MARATHON. Yaani ni aibu tele na wakati wa masoo haya wanajifanya kusafiri abroad ili kupulizia. Mmmh mmeunywa uji wa ulezi bila sukari kwani uzi ni uleule. Hanyamazi mtu mpaka fisadi wa mwisho ajulikane na kachukuliwa hatua za kisheria. JK nakuhurumia sana maana there r honest people in ur administration wanakuangalia tu huku wakiangalia saa zao zinavyo-tick. Mie naamini bado una muda mzuri to come CLEAN before Tanzanians. Be serious... man, this is not MDAKO.
 
Ikulu kushtushwa na kusikitika si ndo kawaida siku hizi.ripoti ya EPA iliposomwa Muungwana kaepa kuisoma mwenyewe kampa Luhanjo.Hili la Chenge mpaka Serious Crime Office (SFO) ndo wamesema.Then ndo ikulu inashtushwa.

Mi mtizamo wangu ni kwamba kama Prime Minister EL anajiuzulu kwa kashfa ya rushwa.The whole cabinet should have gone and we start a fresh.Maana if u are surrounded by flies huitaji kuambiwa unanuka.JK serikali yake imeundwa na wala rushwa wenzake tu.ndo maana hana uwezo wa kuwatoa.Kuna sababu gani ya msingi kuendendelea kuwa na kina Mgonja,Chenge,Mnyika,Hosea,na vibaraka kibao wa RA/EL kama Ngeleja,Buriani,Malima,Masha etc kwenye kabinet.
Kumbe kauraisi ka JK kana ubia.Na siku zote wanazuoni husema mwangalie adui wako anatumia mbinu gani kujaribu kukuangamiza.Ukishajua ujue kuwa hivyo ndo vitu anavyoogopa zaidi.Hivyo JK anaogopa mno ubia,lakini hana ubavu wa kuuondoa na kubaki kuweweseka.
 
Mbona wako WaTz wengi wanamiliki hizo fedha ,yaani kama kutaanza kupekuliwa basi inawezekana kabisa hizo si lolote si chochote , hivi kuna mali za asili ambazo kijidonge kidogo tu kinakupatia feza kiwera ,sasa hao nao mmewachunguza au kutuma wachunguzi wa kimataifa wakague kague huko majuu ,yaani mnabaka tu tena huko wala sio nyinyi mliotisua hilo guruneti ,ila mmeruka na kuwa kama nyie ndio mmeona hiyo ela ,uyo simba ni wivu tu ndio unampa tabu , hao akina takukuru na kukurika mbona awajafichua kitu ,au ndio tuamini hawana wanaemjua na hawana ubavu wa kupata ushahidi na badala yake kama tunavyosikia wanawaonea wauza gongo na kujidai kuwakamata polisi wa usalama barabarani ,huyo mkubwa sijui anaitwa hosia nae amesemwa kuwa ni bepari au ndio kunagojewa mzungu aseme halafu iwe kipofu ameona jogoo.
Maana nilisema uko uhitaji wa kuajiri wazungu ikiwa sisi tunaajiriwa kwenye nchi za watu na tunatumika vizuri na kuaminiwa kikamilifu.
Leo Mtanzania anarudi kutembea kwenye nchi yake anapekuliwa pale airport kila kitu na kusachiwa hata mifukoni na pengine apelekwe kwenye chumba cha upekuzi ,lakini pembeni anawaona wazungu wanapita na kuheshimiwa vizuri kabisa wala hawaambiwi weka begi lako pembeni wakati mambo yote yameshachekiwa kwa machine sa kisasa,mtanzania ambae amekusanya vidola vyake kidogo ili kuja kusaidia ndugu na jamaa pamoja na malafiki zake japo kama kuwazawadia vitu vyote vinaporwa pamoja na kutolewa upepo airport ,kutoikoromea tabia hii ndio imewafanya hata viongozi nao wawe wenye kwiba bila ya kuoneana huruma.Sasa kelele za nini wakati wale wa aiport wanaiba kwa kiwango walichofikia na hao wakubwa nao wanakwiba kwa hapo walipo.
kama tunahitaji kuzuia wizi basi hata haya mambo madogo madogo nayo yasemewe kwa kina ili kuwe kusafi kila kona ya serikali na vyombo vyake.Wizi ni wizi ukiwa mdogo au mkubwa maana moto mkubwa huweza kuwa umeanzishwa na cheche ndogo tu.
 
Utajiri wa Chenge waishitua Ikulu
*Inasubiri taarifa rasmi sheria ichukue mkondo

...Alisema Chenge kama viongozi wengine, amejaza fomu za kutaja mali zake hivyo kama amedanganya, itajulikana.

Simba alipoulizwa anachukuliaje taarifa za waziri kumiliki fedha nyingi kama dola 1 milioni, alijibu: "Hata mimi nashangaa kama wewe iwapo alizipata kihalali..."

"Ni vema watu wakawa na subira katika jambo hilo. Lakini kuna mtu nimemwambia, labda kauza ng'ombe wao wote ndio akapata hizo pesa, labda watu hatujui, au ana biashara nyingine," alisema Waziri ...

Viongozi wa Tanzania hawajui kutoa matamko hadharani hata kidogo. Kama Ikulu ina mashaka na utajiri wa Chenge ina maana Rais hana imani kamili na mteuliwa wake. Kwa hiyo hawezi kuendelea na kazi mara tu itakapo tamkwa hivyo.

Lakini kama mashaka yenyewe sio ya uhakika, yanasubiri kubainishwa, na Simba mwenyewe anaamini inawezekana Chenge ana biashara au kauza ng'ombe (kama nilivyosema kwenye tundiko langu la "Hakuna Smoking Gun" basi Waziri Simba hatakiwi kuongelea lugha za 'kama amedanganya.' Jibu pale ni: sheria itachukua mkondo wake, sina la zaidi kwa sasa. Mwisho wa hadithi. Ni kama Pinda alivyo jitosa kujibu maswali ya Majeshi ya Afrika Zimbabwe. Hawa watu vipi jamani?
 
Posted Date::4/14/2008
CCM yajivua kuhusu utajiri wa Waziri wa Miundombinu Andrews Chenge
*Chiligati asema utajiri wake ni suala binafsi
*Adai kuihusisha CCM kutaivuruga nchi
*Shibuda amtaka aeleze alivyozipata
*Mramba asema ameishiwa maneno

Na Ramadhan Semtawa, Dodoma
Mwananchi

SAKATA la Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kudaiwa kumiliki dola za Marekani milioni moja (zaidi ya Sh1.2 bilioni), zilizoko kwenye akaunti yake katika benki moja nchini Uingereza limepokewa kwa hisia tofauti, huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikijivua kwa kusema kuwa hilo ni suala lake binafsi.

Wakati CCM ikijivua kwenye tuhuma hizo, Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), alisema tatizo si Chenge kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, bali njia zilizotumika kuzipata.

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Uenezi na Itikidai wa CCM, John Chiligati alisema ni vema suala hilo likatenganishwa na chama.

Alifafanua kuwa, ni makosa kukihusisha chama hicho na suala hilo la Chenge kwa kuwa linamhusu yeye binafsi.

Alisema chama kina mambo yake, lakini suala hilo kama ni kweli ana fedha hizo au hana, CCM haihusiki; na kuongeza kwamba sheria itatoa maamuzi ya haki.

“Kwanza naomba jamani mtende haki na mtenganishe haya mambo, vinginevyo mtaivuruga nchi bure,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Chiligati alipoulizwa ni vipi chama tawala kisihusike katika sakata hilo ambalo linamgusa mwanachama wake ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na waziri wa serikali inayoongozwa na chama hicho; alijibu: “Jamani hili ni suala binafsi, linamhusu Chenge mwenyewe.”

Alipobanwa zaidi, kwamba vipi chama makini chenye kuzingatia misingi ya utawala bora na maadili ya viongozi, kinaweza kujitoa kwenye suala ambalo waziri katika serikali yake ametajwa kuhusika na kiasi kikubwa cha fedha, alijibu: “Hapana, hili si suala la chama.”

Alisema wakati mwingine CCM inahusishwa katika mambo ya watu binafsi na kuongeza kwamba, hiyo inalenga kukichafua chama na kuivuruga nchi. Aeleze alizipataje!

Kwa upande wake, Shibuda alisema, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivyo kama kweli ana kiasi hicho cha fedha ni vema ajitokeze hadharani na kuwaeleza Watanzania alivyozipata.

Alifafanua kwamba, inawezekana Chenge ni mfanyabiashara, kwa sababu kuanzia enzi ya utawala wa awamu ya pili, tatu hadi sasa, viongozi waliruhusiwa kufanya biashara.

Hata hivyo, alisema hizo ni fikra za kuhisi na ni vema mwenyewe akaweka bayana alipataje kiasi hicho kikubwa cha fedha, kama kweli anazo.

Mbunge huyo anayependa kuzungumza maneno kwa misemo na methali za Kiswahili, alisema haipaswi kuwepo fikra za kuhisi katika suala hilo.

“Mimi sina ugomvi kwa yeye kuwa na fedha nyingi, lakini awathibitishie Watanzania alizipataje,

hii itaweza kuondoa fitina za uzushi na hisia, ikizingatiwa kwamba alikuwa Mwanasheria Mkuu, aonyeshe uadilifu aeleze alipataje fedha hizo,” alisisitiza Shibuda.

Alisema si vibaya kwa Mtanzania kama Chenge kuwa na fedha nyingi kwa sababu uamuzi wa kuwaondoa wakoloni ulikuwa ni kuleta ustawi wa jamii na kuhakikisha uchumi unashikwa na wazalendo.

Hata hivyo, alisema dhana na nia nyingine ya kupigania uhuru ilikuwa kuondoa, unyonyaji, hivyo isiwe kigezo cha wazalendo Waafrika kuwa matajiri kwa kunyonya wenzao.

Alisema unyonyaji ulipigwa vita huko nyuma, ikiwa ni pamoja na Ukaburu nchini Afrika Kusini, lengo likiwa ni kujenga ustawi wa jamii yote, si pato la taifa au matajiri.

“Wanyonyaji tuliowapiga vita si wenye rangi nyeupe tu, bali hata sisi Waafrika tusije kutaka kuanza kujitajirisha kwa kuhujumu au kunyonya wengine,” alisisitiza.

Alisema Chenge ni ndugu yake na kuongeza kwamba, inawezekana pia anafanyiwa fitina na baadhi ya maadui, hivyo njia sahihi ni kueleza ukweli kwa umma wa Watanzania.

Naye Waziri wa zamani wa Fedha, Basili Mramba, alipoulizwa maoni yake kuhusu suala hilo la Chenge, alikataa kuzungumza kwa madai ameishiwa hoja.

Alisema ni vigumu kwake kuzungumzia suala hilo, kwani yeye siku hizi ni bubu na ameishiwa maneno ya kusema.

“Mimi siwezi kuzungumzia hilo, siku hizi sizungumzi nimekuwa bubu, nimeishiwa maneno,” alisema Mramba huku akicheka na kupunga mkono akiashiria kukataa kuendelea na mazungumzo.

Hata hivyo, Mramba na Chenge wamo kwenye orodha ya wapinzani ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaja kwenye baraza jipya la mawaziri Januari, wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini walilalamika wakihoji ni kwa nini, kwa madai kuwa hakufaa kuwemo katika baraza hilo.
 
CCM bwana, very opportunistic. Yaani wakipata upenyo wa kujikweza wanajikweza kweli (uvunjaji wa nyumba tabata dampo) na ikifika wakati wa kukunana wanakanana hasaaa. Hii inanikumbusha ule wimbo 'nakila mtu atauchukuaaaaa, mzigo wake mwenyewe' itafikia wakati mwana anamkana baba au baba kumkana mwana. Hivi jamani mlio huko nyumbani....huyo Chenge bado hajajiuzulu tuu? au anasubiri kufukuzwa kazi?
 
Mramba bubu mwenzangu...🙂 acha usanii! mbona hukuwa bubu ulipokuwa ukilazimisha ununuzi wa rada hiyo? unakumbuka kauli yako,"hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe."

Je, na wewe una bank account ngapi nchi za nje? zina balance kiasi gani?

Twambie unayoyafahamu kuhusiana na madhambi mliyoyafanya katika deal hiyo.
 
Hawezi kusema, Mkapa amewalisha yamini/amini. Wote wamekaa kimya hawawezi kujibishana na watu wanaonuka umaskini kama watanzania. Wawajibu ili iweje kwani? wenyewe wala vyao bwana wengine tutabakia kunawa tu.
 
Mramba bubu mwenzangu...🙂 acha usanii! mbona hukuwa bubu ulipokuwa ukilazimisha ununuzi wa rada hiyo? unakumbuka kauli yako,"hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe."

Je, na wewe una bank account ngapi nchi za nje? zina balance kiasi gani?

Twambie unayoyafahamu kuhusiana na madhambi mliyoyafanya katika deal hiyo.

Mwaka huu watakimbia hadi vivuli vyao wenyewe!

Mimi hapa nimetoka kuchukua "madiaba" ya pepsi maana hii movie inaonekana itakuwa ndefu kuliko nilivyotegemea.
 
Kama vile namuona Dr. Watson, meno nje, akikusanya vidhibiti fresh kabisa kutetea nadharia yake...
 
Hata vitu vibaya hawajui kuvifanya vizuri.

Of all places, unaenda kuweka hela ulizokwiba Tanzania kwenye a British Crown dependant island barely 100 kms from the shores of England.Despite all the extradition treaties and Commonwealth ties?

Smart lawyer indeed, hakusikia kilichompata Professor? Hakuwa hata na hesabu za kujua Liechenstein, Luxembourg Switzerland au Monaco ambako sheria za privacy ni ngumu zaidi ya UK?

Ujinga wake ndoyo faida yetu, maana sasa waingereza wamemuaibisha kashindwa hata kukataa imebaki anasema hizo pesa sio za BAE.

With AG's like these, no wonder we have such horrible contracts.
 
Looh! tayari wanaanza kurukana. Muhimu ni kuendelea kumvizia mmoja mmoja.
 
Viongozi wa Tanzania hawajui kutoa matamko hadharani hata kidogo. Kama Ikulu ina mashaka na utajiri wa Chenge ina maana Rais hana imani kamili na mteuliwa wake. Kwa hiyo hawezi kuendelea na kazi mara tu itakapo tamkwa hivyo.

Lakini kama mashaka yenyewe sio ya uhakika, yanasubiri kubainishwa, na Simba mwenyewe anaamini inawezekana Chenge ana biashara au kauza ng'ombe (kama nilivyosema kwenye tundiko langu la "Hakuna Smoking Gun" basi Waziri Simba hatakiwi kuongelea lugha za 'kama amedanganya.' Jibu pale ni: sheria itachukua mkondo wake, sina la zaidi kwa sasa. Mwisho wa hadithi. Ni kama Pinda alivyo jitosa kujibu maswali ya Majeshi ya Afrika Zimbabwe. Hawa watu vipi jamani?

Mazee,

Ukiona hivyo ujue Ngurdoto inahitaji Ngurdoto.
 
Hawakushtuka bilioni 133 na bilioni 155 zilizokupuliwa na mafisadi toka BoT ambao mpaka leo hii hakuna hata mmoja wa hao mafisadi aliyeguswa na mkono wa sheria! eti sasa ndio wanashtuka! Kikwete acha usanii nchi inakushinda!

Posted Date::4/14/2008
Utajiri wa Chenge waishitua Ikulu

*Ni kuhusu kumiliki akaunti ya Sh 1 bilioni

*Yasema inasubiri taarifa rasmi sheria ichukue mkondo

*Profesa Lipumba kuuzungumzia leo

Ramadhan Semtawa, Dodoma na Muhibu Said, Dar
Mwananchi

SIKU moja baada ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kudaiwa kumiliki dola 1 milioni nje ya nchi, serikali imesema sheria itachukua mkondo wake kuona fedha hizo amezipataje.

Hatua hiyo itafanyika baada ya taarifa rasmi kuhusu utajiri wa waziri huyo kufika serikalini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alisema taarifa rasmi zikifika, sheria itachukua mkondo wake kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria. Simba alisema hata yeye hayuko juu ya sheria.

Waziri Simba aliongeza kwamba, taarifa zikifika itaangaliwa katika kumbukumbu za Chenge katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma.

Alisema Chenge kama viongozi wengine, amejaza fomu za kutaja mali zake hivyo kama amedanganya, itajulikana.

Simba alipoulizwa anachukuliaje taarifa za waziri kumiliki fedha nyingi kama dola 1 milioni, alijibu: "Hata mimi nashangaa kama wewe iwapo alizipata kihalali au la."

Alisema hadi sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi nchini Uingereza.

"Ni vema watu wakawa na subira katika jambo hilo. Lakini kuna mtu nimemwambia, labda kauza ng'ombe wao wote ndio akapata hizo pesa, labda watu hatujui, au ana biashara nyingine," alisema Waziri Simba.

Kauli hiyo ya Waziri Simba imetolewa siku moja, baada ya Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza, katika toleo lake la juzi, kueleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya Waziri Chenge, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini humo, ijulikanayo kwa jina la Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa, wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajia kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Waziri Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey, zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada hiyo kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.

The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.

Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba, fedha hizo ni mali yake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika serikali ya awamu ya tatu.

Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Waziri Chenge katika orodha ya vigogo 11, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini, wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.

Baadaye, Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa, walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleke katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.

Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo inamilikiwa na serikali na kwamba, hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.

"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wa wakurugenzi hadi sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge na kuongeza:

"Lakini kama mtu ana ushahidi wa tuhuma za ufisadi, jamani tunavyo vyombo vyetu, si wapeleke zikafanyiwe kazi," alisema Chenge.

Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.

Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.

Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanasheria Mkuu katika serikali ya awamu ya pili na ya tatu.

Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005, hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba, suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye aliyemteua.

Chenge alisema hayo mara tu baada ya kuapishwa na Rais Kikwete kuendelea kuiongoza wizara hiyo katika sherehe za kuwaapisha mawaziri katika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma Februari 13, mwaka huu.

Akizungumzia taarifa hizo, Dk Slaa alisema ni habari za kutisha kwani mshahara na posho zake haziwezi kumfanya kuwa na akiba kubwa kiasi hicho.

"Huyu Waziri wa Tanzania ambaye mshahara wake tunaujua, posho zake zinajulikana lazima aeleze alipata wapi fedha hizo," alisema.

Dk Slaa alisema SFO wanafanya uchunguzi wa kwao na kwamba Chenge ni shahidi tu.

"Nilishamuomba Rais Kikwete amwondoe uwaziri na uchunguzi wa kina ufanyike, yatagundulika ya ajabu," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, leo atakutana na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuzungumzia tuhuma hizo za umiliki wa fedha nyingi dhidi ya Chenge.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani, aliliambia gazeti hili jana kuwa, Profesa Lipumba atakutana na waandishi wa habari, kuzungumzia suala hilo katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam wakati wa asubuhi.

"Kesho (leo) saa 5:00 Profesa (Lipumba) atakuwa na press conference (mkutano na waandishi wa habari) makao makuu Buguruni, kuzungumzia hilo suala la (Waziri) Chenge," alisema Bimani, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa.

Wamchunguze Lowassa, huenda hata ana pesa nyingi zaidi ya Chenge.
 
Back
Top Bottom