Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 130
Hii habari inafurahisha sana na inasikitisha sana. Katika habari hii ndio mtaona uzuzu wa viongozi wa CCM. Aliyoyasema Shibuda yalitakiwa yasemwe na Chiligati maana yeye ni Katibu wa Uenezi na Itikidai wa CCM. Au na yeye hana nguvu kama katibu wao?au hajijui kama yeye ni Katibu wa Uenezi na Itikidai wa CCM? Au anadhani watanzania tumelala statment yake iatufanya na sisi tuwe mazezeta?Kuna mtu aliwahi kuniambia ukiwa CCM inakubidi uwezuzu ndio utakaa ndani ya CCM sasa naamini maneno yake. Wewe ni Katibu wa Uenezi na Itikidai wa CCM na Waziri wa Serikali tena ya chama chenu! hujui kama ni kosa kwa kiongozi kushutumiwa?nilitegemea ungesema inabidi Chenge ajiuzulu ili ufanye uchunguzi huo ndio uwajibikaji. Huo ndio utawala bora. Lakini badala yake mnatufanya sisi mazuzu. Jueni hizo zama zimeshapitwa na ndio maana mnazomewa!