The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

unashutuka kitu ambacho ukui lakini hii habari hipo jambo forum zaidi ya mwezi sasa, so its not new, huyu jamaa hawezi kuondolewa kwenye serikali ya CCM kwa kuwa ana skendo nyingi za CCM lazima waendelee kumuifadhi, lets wait Vasco dagama arudi kutoka ughaibuni tuone

wewe unacheza kweli, vasco dagama atafanya nini? ameshindwa hata ku-address issue ya maadili (ethics) kule kwenye kikao chao butiama halafu unategemea aseme kuhusu chenge, oooooh anamuogopa kama ukoma akimgusa tu anawaumbua wote dagama na chama cha mafisadi, huyu rais wetu bure kweli.
 
Sikupata taharifa ya Pro. Lipumba hivi amesema nini kuhusiana na hili updates please
 
Kwako Mramba, now you are a mute!!I bet you never thought kuwa utakuwa kijiweni this soon, well,just to let you know that nyasi hazina ladha mbaya sana and in that sense join the club!!
 
Mimi katika kufikili kwangu nilijua atatangulia Mramba kabla ya wengine sijui whats happened mpaka Chenge akasurface mapema zaidi au inawezekana yeye ni kinara zaidi.
 
Kumbe politics zinalipa kiasi hiki? Wakuu nisome kozi gani ili nami niwe mwanasiasa?
Mh.Chenge tuwasiliane nikupe account details zangu uhamishe kamshiko kabla soo halijawa kubwa!A friend in need.....
 
Wala hauitaji shule KKN bali unahitaji kujipendekeza kwa wakubwa wa CCM ili uweze kupitishwa kwenye NEC kugombea ubunge halafu watakuchagua kuwa waziri. Lakini kumbuka Jambo forums bado hipo tutakujadili usiku kucha hapa
 
yaani kuna mtu humu aliwahi kusema kuwa maovu wanayoyafanya CCM hata shetani anayachukia...
haya sasa hapo ndo naungana na wahenga waliosema ukistaajabu ya musa.............halafu sasa watu wote wenye akili timamu walishasema kuwa huyu chenge ni galasa, lakini kikwete akamchagua na tena alishaambiwa huyo jamaa ndiye aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali kipindi cha mkapa, na uharo wooote wa serikali ya mkapa ye ndo alikuwa mwanasheria lakini mzee akang'ang'ania...sasa kiko wapi?
 
Lakini kumbuka Jambo forums bado hipo tutakujadili usiku kucha hapa

Nikiwa waziri ufisadi wangu wa kwanza ni kuizima hii JF kama kibatari ili niwezefanya mambo yangu kwenye giza. MMK,MWK na wengine wote ambao mna credits zaidi ya 100,000 mtaozea Segerea,tena kimyakimya.
 
Nikiwa waziri ufisadi wangu wa kwanza ni kuizima hii JF kama kibatari ili niwezefanya mambo yangu kwenye giza. MMK,MWK na wengine wote ambao mna credits zaidi ya 100,000 mtaozea Segerea,tena kimyakimya.

Nimekupata lakini kumbuka hata miezi sita haijaisha wenzio wameshindwa tena kwa gia kubwa ya ugaidi, siju utatumia strategy gani
 
Nikiwa waziri ufisadi wangu wa kwanza ni kuizima hii JF kama kibatari ili niwezefanya mambo yangu kwenye giza. MMK,MWK na wengine wote ambao mna credits zaidi ya 100,000 mtaozea Segerea,tena kimyakimya.

Nikunongoneze wengine wasisikie,
kuwa makini isije ikawa ya hadithi za mashariki ya kati ambazo Mfalme alikuta watoto wanacheza kama mahakama ya kuamua kesi iliyokuwa mbele yake na akagundua busara za wale watoto na kuchukua uamuzi wao.
 
Nikiwa waziri ufisadi wangu wa kwanza ni kuizima hii JF kama kibatari ili niwezefanya mambo yangu kwenye giza. MMK,MWK na wengine wote ambao mna credits zaidi ya 100,000 mtaozea Segerea,tena kimyakimya.

kana-ka-nsungu hawa jamaa CCM hawana aibu hata chembe, unaweza kusikia kesho wanaanza kufuata njia hiyo ambayo we utaitumia siku ukibahatika kuukwaa uwaziri.
 
Posted Date::4/14/2008

Serikali isisubiri taarifa imchunguze Chenge

Mwananchi

SIKU chache baada ya gazeti la The Gurdian la nchini Uingereza kuchapisha habari kwamba uchunguzi umeanza kufanyika dhidi ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kuhusiana na akaunti yake iliyoko katika benki moja ya nchini humo kukutwa na dola za Marekani zaidi ya 1 milioni (Sh1.2 bilioni), serikali imeahidi kuchukua hatua za kisheria kupata uhakika wa jinsi fedha hizo zilivyopatikana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba, wakipata taarifa rasmi juu ya suala hilo, taratibu za kisheria zatafuatwa kwa kuangalia kwenye kumbukumbu za Waziri Chenge, kama alijaza fomu za viongozi za kutaja mali zao, kikimwemo kiasi hicho cha fedha na kuonyesha jinsi alivyozipata.

Kauli hiyo ya serikali inatia moyo kama kweli hatua hizo zinachukuliwa na kusimamiwa vizuri kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni njia mojawapo muhimu ya kukabiliana na ufisadi wa viongozi wa umma hapa nchini.

Ni jambo la ajabu sana kwa kiongozi wa umma, tena wa ngazi za juu serikalini kuwa na kiasi hicho kikubwa cha fedha katika benki za nje ya nchi, wakati uchumi wa nchi yetu unaendelea kudorora.

Hata kama alizipata fedha hizo kwa njia halali, kwa nini azifiche nje ya nchi yetu wakati hapa nchini kuna benki zinazoweza kumtunzia vizuri na wakati huo huo kuwasaidia Watanzania kutokana na kodi na riba zinazokatwa kwenye fedha hizo pamoja na kutumika kwenye miradi mingine kwa njia ya mikopo inayotolewa na benki kwa watu na mashirika mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu?

Kama tatizo ni la thamani ya fedha ya nchi yetu kutokuwa imara kutokana na hali ya uchumi kuwa mbaya, karibu benki zote hapa hapa nchini zina akaunti za fedha za kigeni ambazo angeweza kuzitumia na bado zikawanufaisha Watanzania na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, inadaiwa kuwa waziri Chenge alikiri kuwa na kiasi hicho cha fedha kwenye akaunti ya benki moja iliyoko kwenye kisiwa cha Jersey na kufahamisha kuwa hakuzipata kwa njia ya ufisadi.

Hata hivyo, kauli ya serikali haijatoa picha maalumu juu ya hatua itakazochukua katika suala hilo, hivyo kuifanya jamii kuwa na hofu kwamba huenda kale katabia ka kulindana kanapewa nafasi kama inavyokuwa kwenye mambo mengine yanayohusiana na masuala kama hayo ambayo humalizwa kimyakimya.

Si hivyo tu, badala ya serikali kusubiri taarifa ya uchunguzi kutoka kwa taasisi maalumu ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini Uingereza ya Serious Fraud Offence (SFO), inafaa kwa kutumia vyombo vyake nayo ifanya uchunguzi wake wa kina ili kujiridhisha na suala hilo.

Tusema hivyo kwa sababu, hata kama suala hilo linamhusu Chenge binafsi, ni wazi tuhuma hizo ni kashfa kubwa kwa serikali kwa sababu ni mmoja wa mawaziri wake mwenye dhamana ya kuiwakilisha nchi kwenye maeneo mbalimbali, kwani kwa wadhifa wake huo anaweza kuingia mikataba na mashirika ya nje kwa niaba ya Watanzania.

Inashangaza kuona kwamba serikali inashindwa kubaini viongozi wake wanaoficha fedha zao nje ya nchi badala ya kuzihifadhi hapa nchini, ili zitumike kuimarisha uchumi wa nchini yetu.

Kwa ujumla, tunalaani kitendo cha viongozi wetu wa ngazi za juu serikalini kuficha fedha zao nje ya nchi, ikimaanisha kwamba wanahamisha utajiri wa nchi yetu na pia wanaonyesha kwamba hapa nchini mambo si shwari, hivyo kuwafanya wananchi kuwa na hofu na mwelekeo wa taifa lao kiuchumi.

Tunaomba serikali isingoje taarifa za wakaguzi wa nje juu ya suala hilo, bali ishiriki kikamilifu kufuatilia suala hilo nchini Uingereza na mahali pengine na lisiishie kwa Chenge tu, bali hata kwa viongozi wengine pia.
 
kana-ka-nsungu hawa jamaa CCM hawana aibu hata chembe, unaweza kusikia kesho wanaanza kufuata njia hiyo ambayo we utaitumia siku ukibahatika kuukwaa uwaziri.

Inabidi nianze kuweka sawa masuala ya hati miliki sasa kama idea yangu inauzika.
 
Jamani Tanzania ni nchi masikini sana kwa mtu mmoja tena mtumishi wa serikali kuwa na dola mil moja ni jambo la kutisha kama si kuogopesha.

Mshahara na malupulupu ya muheshimiwa huyu kwa miaka yake yote ya utumishi katika serikali bado hayawezi kufika kiwango hicho, na hata kama akiunganisha mshahara wa mke wake. Hizi ni pesa za wizi alizotuiibia Watanzania kwa kutumia nafasi aliyokuwa nayo.

Ndugu wana JF, huu ni mwanzo tu wa kujua ukweli kuhusu mapesa yetu yanavyoliwa na kuhamishwa na hawa mafisadi kwa kutumia kivuli jinamizi CCM.

Huyo ni mtu mmoja tu ndani ya CCM ana miliki dola mil moja, sasa tukichukulia mtu kama Mkapa, Yona, Mramba, Mgonja, Kikwete, Rostam Azizi, Mzindakaya na wengine wengi huko nje ya nchi wana mapesa kiasi gani?. Nina amini kabisa hawo niliowataja hapo juu kama watarudisha pesa walizozificha nje ya nchi, basi hatutakuwa na bajeti tegemezi tena katika Tanzania. Tutaweza kuwa na barabara safi, huduma bora za afya, elimu nk.

Huyu Chenge ni mwizi na hana la kutuambia. Mapesa hayo yarudishwe haraka iwezekanavyo na muhusika apelekwe ukonga kunyea debe.
 
Mpaka sasa sina data za uhakika kwamba Waziri Chenge anakosa gani? Nadhani kilichoonekana ni hela... source bado haijajulikana tusubiri tutajua. Tunajenga taifa la kipumbavu sana kwa mtu kama Chenge kuwa/kumiliki TZS 1.2 Billion ni hela ndogo sana!!! Huu umaskini ndio unatusumbua...

Of course nikifa bila kumiliki utajiri usiozidi hapo... nitakuwa nimekufa nikiwa maskini...

Mkuu Kasheshe,

Heshima mbele, najua kuwa wewe ni mmoja wa vichwa hapa JF, lakini kwenye hili acha uchuro ndugu yangu, Mungu hapendi maneno ya namna hii bro, kuwa na huruma kidogo, unafikiri wale watoto wadogo wanaozurura humu mjini wakiomba omba wanahitaji dola ngapi kwa siku kuweza kula na kulala vizuri kwa maisha yetu ya bongo?

Hivi unajua Mwalimu, aliyekuwa rais for 23 years, hakuwa na hela kiasi hicho? Huyu Chenge, according to dataz amezipata hizi hela na nyingine zaidi akiwa Mwanasheria na waziri wa Miundo mbinu, sasa akiwa rais ambalo ndilo hasa lengo lake itakuwaje?

Jamani maneno mengine mnasema msalieni mtume kidogo!
 
ishu iko wazi kabisa, ila sasa chekini hawa CCM jinsi watakavyolizusha jingine na kulipoza kama si kulisahaulisha hili la chenge...sasa umefika wakati mkimkuta mtoto wa fisadi mnamsulubisha kisha mnakula kona...life goes on
 
Simba alipoulizwa anachukuliaje taarifa za waziri kumiliki fedha nyingi kama dola 1 milioni, alijibu: "Hata mimi nashangaa kama wewe iwapo alizipata kihalali au la."

Unaona mpaka waziri mwenziwe anamshangaa, sasa sisi wananchi walalhoi itakuwaje?
 
Jamani Tanzania ni nchi masikini sana kwa mtu mmoja tena mtumishi wa serikali kuwa na dola mil moja ni jambo la kutisha kama si kuogopesha.

Mshahara na malupulupu ya muheshimiwa huyu kwa miaka yake yote ya utumishi katika serikali bado hayawezi kufika kiwango hicho, na hata kama akiunganisha mshahara wa mke wake. Hizi ni pesa za wizi alizotuiibia Watanzania kwa kutumia nafasi aliyokuwa nayo.

Ndugu wana JF, huu ni mwanzo tu wa kujua ukweli kuhusu mapesa yetu yanavyoliwa na kuhamishwa na hawa mafisadi kwa kutumia kivuli jinamizi CCM.

Huyo ni mtu mmoja tu ndani ya CCM ana miliki dola mil moja, sasa tukichukulia mtu kama Mkapa, Yona, Mramba, Mgonja, Kikwete, Rostam Azizi, Mzindakaya na wengine wengi huko nje ya nchi wana mapesa kiasi gani?. Nina amini kabisa hawo niliowataja hapo juu kama watarudisha pesa walizozificha nje ya nchi, basi hatutakuwa na bajeti tegemezi tena katika Tanzania. Tutaweza kuwa na barabara safi, huduma bora za afya, elimu nk.

Huyu Chenge ni mwizi na hana la kutuambia. Mapesa hayo yarudishwe haraka iwezekanavyo na muhusika apelekwe ukonga kunyea debe.
 
Chenge aibua mjadala

Shadrack Sagati
Daily News; Monday,April 14, 2008 @18:01

TAARIFA kuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge ana akaunti ya fedha za kigeni nje yenye akiba ya zaidi ya Sh bilioni moja imeibua mjadala na shinikizo la kutaka ajiuzulu na achunguzwe na vyombo vya dola.

Kutokana na kutolewa kwa ripoti magazetini juzi kwamba vyombo vya upelelezi vya Uingereza vimefuatilia uhalali wa Chenge kuwa na akaunti yenye dola milioni moja ( takriban Sh bilioni 1.2), mjadala huo uliendelezwa kwa kasi katika magazeti na redioni jana na pia kuchukua sura ya siasa kwa kushinikiza kuwa ajiuzulu.

Katika mlolongo huo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana aliitisha mkutano mahsusi wa vyombo vya habari kuzungumzia suala hilo huku akisema kutokana na kiasi kikubwa cha fedha zilizo katika akaunti ya Waziri Chenge, inatosha kumfanya Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha kwa kumwondoa kwenye Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, kwa mujibu wa sheria mpya ya rushwa kifungu cha 29, Waziri huyo anapaswa kufuatiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na kuchunguzwa alikopata fedha hizo. Profesa Lipumba alisema kwa fedha za mshahara wa mtumishi wa serikali na posho, Chenge hawezi kuvuna na kutunza hadi kufikisha Sh bilioni moja na kuziweka kwenye akaunti nje ya nchi.

Alinukuu kifungu cha 29 cha sheria ya Takukuru kinachosema; "mtumishi wa umma atakuwa ametenda kosa la jinai iwapo ataishi na kuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chake cha sasa na cha nyuma. Na iwapo atakuwa na mali ambayo haionyeshi namna alivyoipata kihalali.

Taarifa za akaunti hiyo ya nje ya Chenge ziliibuliwa na gazeti la Guardian la Uingereza toleo la Jumamosi. Gazeti hilo liliripoti kuwa Waziri huyo anachunguzwa kuhusiana na rushwa ya dola za Marekani milioni 12 zilizolipwa na kampuni ya BAE System ya Uingereza iliyoiuzia rada Tanzania.

Gazeti hilo liliripoti kuwa Chenge anachunguzwa na Taasisi ya Kuchunguza makosa makubwa ya rushwa ya Uingereza (SFO) na kuwa Chenge alilieleza kwamba hakupata fedha hizo kwa kupokea rushwa ya rada.

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia rushwa (Takukuru) ambayo nayo imekuwa inachunguza suala hilo haikuwa tayari kusema lolote kuhusiana na tuhuma hizo dhidi ya Chenge. "Siwezi kujibu swali lako kwa sasa naomba uniletee maswali," alisema Mkurugenzi Msaidizi Lilian Mashaka alipohojiwa na mwandishi wetu jana.

Wakati ununuzi wa rada unafanywa Mwaka 2002, Chenge alikuwa mwanasheria mkuu wa Serikali cheo alichokaa nacho hadi mwaka 2005 baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi na baadaye akateuliwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri wa Miundombinu.

Ununuzi wa rada iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 65 ulifanywa na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na mkataba ulisainiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na ulipingwa na wanasiasa wa upinzani wakidai kuwa kulikuwa na harufu za rushwa.
 
Back
Top Bottom