The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Haya hapa napo akipona basi nitaona kweli SISI NDIVYO TULIVYO, JK kweli nitamwona bonge la Fisadi akikwepesha na hii, ambayo iko wazi sasa kabisaaaaaaa

Huo ni mrija mwembamba sana ukilinganisha na mirija minene waliyonyonya yeye na Mkapa wake. JF tulisema, hizi kelele zetu si za mwendawazimu. Watu wanapokuwa wanatoa hoja hapa zina ukweli ndani yake na hata kama zisipokubaliwa kwa muda mfupi zinapotolewa. Tulisema ya Chenge yatakuja kweupe, sasa yako wapi. Na tulisema kuwa Mkapa atatinga mahakamani, IT'S JUST MATTER OF TIME.

Na mie siamini kama JK alikuwa hajui haya, sijui kuna kasoro fulani kwenye ubongo au ni kiburi cha ufisadi. Tunashuhudia kuona mafisadi walivyo na viburi, kiburi cha kung'ang'ania madaraka i.e Mwanyika, Chenge, Hosea......++++++++++ etc. Mwingine kuyumbisha Bunge na chama chake tawala. Pamoja na hayo yote siku yenu inakaribia, ni pale kila mwananchi MZALENDO mwenye uchungu na nchi yake atakapokuchapeni bakora. Mawaziri nyie wenyewe mmeshuhudia mlivyozomewa huko mikoani mkitetea bajeti wakati wananchi wengine wanalalia mlo mmoja na si ajabu wa maembe mabichi.

Sasa tusubiri kinara wa wasanii atoke huko ughaibuni, sijui atafanya nini. Yetu masikio.
Pinda naye kaanza kupindisha mambo, kwa nini msimuache RA na yeye atumie haki yake kujitetea mbele ya wananchi wakiwakilishwa na wabunge wao?????????? Naamini hilo lilikuwa ni shinikizo toka kwa Pinda kwenda kwa Sitta. Imani yangu yaanza kunitoka juu ya Pinda (Sorry kwa kutoka nje ya mada). Hii inakera sana but malipo yenu ni hapa hapa. MUWASHO unaomsumbua Mugabe utakuwa mara 60 kwa SISEMU. Naye Mkapa na Mramba wakae wakae mkao wa kufuturu maana kuna kitu fulani kinakuja kwenu nacho ni....chagua hapo chini wee Mkapa na wenzako:-
(a): UTAJO
(b): UTAMBI
(C): UTAMU
(d): ULAJI
Mafisadi kazi kwenu chagueni jibu sahihi, atakayepata jibu sahihi tutamhurumia kwa kumtandika viboko 20 mbele ya wananchi, kufilisi mali yake na kisha kwenda Segerea miaka 21 na akimaliza kifungo anafanya community Services for 2 months. Now do maths, ambao mtakaokosea jibu mtapata nini!!!?
 
Naona watu hapa hamzingatii ukwelikamba wachunguzi wa wa hii so siyo Takukuru bali ni wenyewe wajanja wa shughuli hii ya kunusa.

Kuna kitu inaitwa "Account Foresinc"

Hiyo kitu achana nayo wanafuatilia Trail ya fedha yako mpaka pale zilipoanzia.

Kama Chenge angetaka kukwepa hilo alitakiwa kuweka fedha zake Dubai zikiwa cash bila kuhusisha Benki za magaharibi.

Naona watu wanrushiana maneno kwamba baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa wezi haina maana CCM yote ni ya wezi.

Statement hii inakuwa ya kweli tu kama chama kinachukua hatua madhubuti kufuatilia tuhuma zinazotolewa na vyombo vya habari na mitandao ya Internet.

Kitendo cha Rais wa Serikali ya CCM na Mwenyekiti wa CCM MH Kikwete kuendelea kuwakumbatia wala Rushwa wezi wa fedha za umma watuhumiwa wa Rushwa na yeyey mwenyewe Binafsi kuhusishwa na Matukio ya mengi ya Kifisadi, kinatimiliza jambo moja tu.

CCM ni chama cha Maharamia.
Wewe msomaji wangu kama ni mwanachama wa CCM na hujawahi kufanya Uharamia wowote unatakiwa kujua hilo na kuchukua uamuzi wako binafsi wa kuachana na CCM au kuendelea kuitetea kwa hoja tete huku umeng'ang'ania mchuma wa Maharamia.

Hakuna utetezi wowoteule unwezao kubadiri sifa ya CCM ya kuwa chama cha Maharamia zaidi ya ule wa kuwawashia moto Maharamia ndani ya Chama na kuwapiga kabari za nguvu.
Kwa nini?
Kwa sababu sisi tulio nje ya Chama chenu tunaiona CCM kutoka kwa umbo lake na sura yake na umoja wake, kama kuna migawanyiko nyufa na tofauti mnazijua ninyi mlioko ndani na ni matatizo yenu huko huko ndani.
Sifa na heshima ya chama hamchagui ninyi kwa utashi wenu. Sifa na heshima ya chama mnaipata kwa kulinganisha maneno yenu na vitendo vyenu katika mzani wa kisiasa.
Manweza kuchagua namna ya kushughulikia matatizo yenu lakini hamuwezi kuchagua na kusimamia au kuelekeza namna sisi tusio wana CCM tunavyojisikia au tunavyotakiwa kujisikia kuhusu chama chenu.
Sisi tunaiona nyumba ya CCM kama nyumba ya wahuni wezi malaya na majangiri wanao tumia vipajiwalivyopewa namwenyezi Mungu kuangamiza urithi na uwezo wa vizazi vyao kujijengea nguvu za kiuchumi.
Sisi tunaiona nyumba ya CCM imejaa watu wengi kama soyo wote wenye Tabia kama ya Mama nguruwe ambaye hasiti kula watoto wake mwenyewe akijisikia kufanya hivyo.

Kila siku tunaona Maharamia kibao wakiingia na kutoka ndani ya mwenye nyumba ya CCM vile wapendavyo.
Kitendo hicho cha Maharamia kuingia na kutoka wakiwa vifua mbele kinatufanya tuamini kwamba nyumba nzima ya CCM inajari na kuthamini mchango wa Maharamia hao katika ujenzi wa utawala bora wa CCM.
Endapo mchango wa Mafisadi hauthaminiwi na CCM basi tungesikia Ngumi mateke Vibao na viminyo vikiendelea na baadhi ya mafisadi kutoka mkuku wengine wakiwa wametinga "Birthday Suit" tu.

CCM is a Party of Criminals.
 
..............Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Tanzania's anti-corruption bureau, which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to multi-million pound secret commission payments made by BAE.............

.........very clear............UCHUNGUZI.......identified the money!!!!.................halafu yeye anajikanyaga, badala ya kuelezea umepataje hizo pesa.........something will be revealed soon abt this.

Ni rahisi sana kuelezea pesa zako umezipataje......mtu akianza kujikanyaga na kutafuta wanasheria kuelezea..........mmmhh....
 
Kuhani Mkuu

kudos.....kadiri siku zinavyoendelea hapa JF unajenga hoja murua kabisa...si kama pale mwanzoni

anyway umemzungumzia watu watatu na Warioba, Mar Nyalali na Lubuva sidhani kama nyumba zao zinaingia ktika level ya kuitwa kasiri wachilia mbali hekalu

otherwise maneno mengine ni point sana mkuu
 
...mimi naona kule europe na marekani ili uweke pesa bank lazima uwe mfanyakazi ,mwanafunzi ama una haki ya kuishi hapo.

sasa imekuaje Chege afungue akaunti huko ???

Unaweza kufungua akaunti mahala ambapo, sio tu huna haki ya kuishi, pia hata huishi. Benki kama Citibank na Chase Manhattan pasi ya kusafiria inatosha. Sehemu kama Bank of America pasi ya kusafiria na kitambulisho kingine (wakati mwingine hata kadi ya kukopea hela) vinatosha.
 
Wakuu,

Poleni sana, ila angalieni msije mkapata ukichaa bure kwa kuumiza vichwa. Hawa viongozi wetu wana pesa nyingi sana nje. Kwa Chenge naamini ana account zingine zaidi ya hiyo ambayo wajanja wameigundua. Mnachosoma hapa ni just a tip of the iceberg.

Wengine wametumbukiza pesa zao nyingi kwenye majumba hasa hapa UK ambapo sheria za kununua nyumba na kumiliki ardhi ziko huru mno.

Balali aliwahi kusema kuna Watanzania kama 10 wana bilioni zaidi ya 200 ambazo zingetosha kununua NBC wakati ule inauzwa. Sasa ni miaka kama mitano imeisha, idadi yao imeongezeka, si ajabu hata pesa wanazoficha nje zimeongezeka.

Sijui tufanyeje, lakini taifa letu limevamiwa na linakuwa raped, hatuna nguvu hata ya kulinda mali zetu toka kwa majambazi zaidi ya kuja hapa JF na kupiga kelele. Tuendelee kuelemishana maana kadri watu wengi watakavyochukia ndivyo yatatokea yale yanayompa kichaa sasa Mugabe.

Hawa jamaa hata huruma hawana, wanataka kuiba pesa hata ambazo hawazihitaji. Ni uroho uliozidi kiasi.
 
Ni huzuni na masikitiko makubwa. Watanzania tunaibiwa na kufukarishwa na viongozi wetu wenyewe tuliowapa dhamana ya kutuondolea ufukara.

Je kwa nini hawa jamaa walioigundua hii $1m ya huyu mwizi tusiwape tenda ya kufichua hela zote za viongozi wetu nje ya nchi? (ukweli ni kwamba UWT wameshindwa) Huu ujambazi nadhani ulitokea wakati wa enzi za Mkapa baada ya JKN kufariki dunia. Je ni kweli hatujui mahali pa kupata hela($28m)za kusambaza umeme kwenye mikoa ya kusini kwa kupitia gridi ya taifa kama waziri alivyoliambia bunge? TZ tumekwisha!
 
Sijaona idea mbovu kama hii ya kumtaka ajiuzulu?? why??

Kwani yeye uwaziri amegombea wapi??

Kwanini msimtake rais aliyechaguliwa na Umma wa Watanzania kumtoa??

Chenge ameshasema "" Kamuulizeni rais kwa nini nimechaguliwa""

So hapa naungana na Chenge kwamba yeye asiulizwe kabisa kwa sababu kazi hiyo ni ridhaa ya rais. Full stop

Accountability accountability accountability! Rumsefeld didn't run for secretary of defense, did he? But he resigned....
 
Wadanganyika jamani!... ama kweli NDIVYO TULIVYO..
Hivi kweli mlikuwa na kijiimani kuwa Chenge hakuhusika na deal la Radar?..
Hivi kweli mnaamini kwamba viongozi wetu ni wasafi?... Nani kati yao mwenye wadhifa hana account nje!..
Na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kutoa account zake nje ktk report ya mali na mapato yake Bungeni..Hakuna! hata Sitta mwenyewe, wanazohesabu ni mali zao ndani Tanzania zinazojulikana na registered chini ya majina yao, sio wake zao, watoto wao na kadhalika...hata kama wao ndio wamiliki nje ya sheria.
Kumbukeni wote hawa wameruhusiwa kufanya biashara, hivyo wanazo account nje mbali kabisa na wizi wa pesa za serikali wanalindwa na sheria waliyoianzisha wenyewe.
Tumeibiwa toka enzi za Green bank na mashirika yote yaliyobinafsishwa yana hujuma ndani ayke hakuna hata moja lililobinafsishwa kwa faida ya nchi yetu. That is a fact na kutokubali hayo wakati hatuna ushahidi nje ya ukweli huo kunakamilisha dhana ya NDIVYO TULIVYO.. wepesi wa kusahau na Kusamehe! kama tulivyosamehe biashara ya Utumwa.
Jamani hawa viongozi wetu, wadhifa waliokabidhiwa ni mtaji toka wa kuanzisha biashara wakizuia mashirika mengine kutopata tender isipokuwa yale yatakayokubaliana na masharti binafsi - MTUKULA...

Mkandara, hakuna aliyedanganyika kama fisadi Chenge hajaifisadi Tanzania katika mikataba mbali mbali ikiwemo ya uchimbaji dhahabu na ule wa Rada, na hata hapa JF kuna ushahidi chungu nzima wa yeye kuitwa fisadi katika thread mbali mbali. Tatizo ni kwamba tulikuwa hatuna ushahidi wowote sasa tumeupata. Aeleze amekuwa katika sirikali miaka mingapi, amefanya biashara zipi na kwa muda gani kumuwezesha kuwa na bank account nono kiasi hicho.

Jamaa wanataka kumtumia kama shahidi nadhani kwa sababu bulungutu lilioingia kwenye account hiyo lilikuwa kubwa kuliko hiyo current balance ya $1,000,000 na labda yeye ndiye alikuwa mgawaji kwa mafisadi wengine ndani ya sirikali akina Mramba na wengine kama inavyoonyesha hapa Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began. Na kama utakumbuka fisadi Mramba alituambia kwamba, "Hata majani tutakula lakini lazima rada inunuliwe."

Kwa hiyo Wadanganyika hatukudanganyika na ndio maana tunakula sahani moja na mafisadi mpaka kieleweke. Ebo! Hapendwi fisadi Tanzania
 
Ni huzuni na masikitiko makubwa. Watanzania tunaibiwa na kufukarishwa na viongozi wetu wenyewe tuliowapa dhamana ya kutuondolea ufukara.

Je kwa nini hawa jamaa walioigundua hii $1m ya huyu mwizi tusiwape tenda ya kufichua hela zote za viongozi wetu nje ya nchi? (ukweli ni kwamba UWT wameshindwa) Huu ujambazi nadhani ulitokea wakati wa enzi za Mkapa baada ya JKN kufariki dunia. Je ni kweli hatujui mahali pa kupata hela($28m)za kusambaza umeme kwenye mikoa ya kusini kwa kupitia gridi ya taifa kama waziri alivyoliambia bunge? TZ tumekwisha!

Nurujami,

Hata serikali ya TZ wakitaka, wanaweza kugundua baadhi ya hizi pesa na zilikofichwa. Akina RO ndio kazi yao.

Ila kwenye hili na wao wamo sasa nani atakuwa tayari kumchunguza mwenzake? Hapa ni lazima wananchi tuwalazimishe. Wakiona chama chao kinaelekea kubwagwa, wataanza kusalitiana na kila mtu kujiokoa mwenyewe.

JK kama anataka kuwajua waliotuibia, naamini kuna vyombo vya dunia vinaweza hata kufanya kazi hii bure. Tatizo ni viongozi wetu hawataki kabisa hata kusikia. Si umeona EPA? Kila kitu kiko wazi lakini watu wanapiga dana dana tu.
 
Ni kichekesho kikubwa sana sisi huku JF kudiscuss acct ndogo ya Mh Chenge iliyoko Jersey kama investment acct. Hii ni acct ndogo sana inayohusu kununua shares mbalimbali Wall st, sasa je thamani ya hizo shares zake ikitajwa itakuwa vipi??

Also most of our senior govt officials have local accts hapo NBC, CRDB, Stanchart zenye thamani kubwa mno kuliko hiko kiacct kidogo.

Kabla sijasemwa kuhusu kutaja $1 mill kama kiacct kidogo, hapa nadiscuss relative, yaani kama kuna mtu ana $20 mill kwenye acct then $1 million ni ndogo in relative terms.

Hela zetu nyingi inasemekana zimewekwa South Africa, UK, Dubai.

Watu wa bank local wakiamua kufyatua matofali ya hawa viongozi patakua hapatoshi.

Jamani tatizo siyo udogo wa bank account hiyo!! Kama Chenge ni mwadilifu si angeshaanika ushahidi wa kipato chake kuonyesha kwamba yeye kuwa na bank account yenye $1,000,000 is not a big deal!

Angetwambia mshahara wake sirikalini, mapato yake ya biashara mbali mbali ikiwemo kusafirisha prawns, matunda, magogo n.k. katika nchi mbali mbali duniani(kama ana biashara yeyote) ambayo yamuwezesha kuweza kuwa na account nono kiasi hicho.

Hiyo bank aliyofungua account si ajabu walikuwa hawamjui kama ni waziri Tanzania, lakini waliona transaction za ajabu ajabu na kuamua kuifunga account hiyo ili kuchunguza kulikoni kama walivyosema hapa, Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Sasa kitu gani msichokielewa kuhusiana na suspicious transactions mpaka mtake kuonyesha Chenge kuwa na account ya kiasi hicho is not a big deal!? 😕

Duh! Wadanganyika jamani! hivi mlitaka awe na bank account inayoonyesha balance ya $100,000,000 au zaidi ndio muamini kama amefanya ufisadi!? 😕
Mnajuaje kama ana bank accounts nyingine katika nchi mbali mbali za magharibi zenye balance kama hiyo au hata zaidi? Hebu acheni hizo jamani!

Swali la kujiuliza ni je, ni mawaziri/former mawaziri wangapi katika sirikali ya Muungwana na fisadi Mkapa wana account katika mabank ya nje. Je, pesa katika bank accounts hizo zilipatikana kihalali? Je fisadi Mkapa naye ana bank accounts nchi za nje? kama jibu ni ndio zipo katika nchi gani na pesa katika bank accounts hizi zilipatikana kihalali? Je, Muungwana naye ni aje? naye ana mabulungutu yake yaliyosambazwa katika nchi mbali mbali duniani?
 
BAE corruption investigation switches to Tanzania

· Focus on £28m radar deal with East African state
· SFO's new director due to take over this month

David Leigh and Rob Evans The Guardian, Saturday April 12 2008

Following the uproar over its halted Saudi investigation, the Serious Fraud Office is expected to decide whether to bring fresh corruption charges against arms manufacturer BAE within six weeks, over a second arms deal, this time with Tanzania.

A minister from the east African state has denied that more than $1m (£507,500) in his offshore accounts came from BAE.

Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Tanzania's anti-corruption bureau, which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to multi-million pound secret commission payments made by BAE.

Chenge does not dispute the money in his Jersey accounts. But he told the Guardian: "The obvious inference [of the investigations] is that I have received for my benefit 'corrupt payments' from BAE. This is untrue."

He said he was only involved in minor aspects of the radar deal, which was promoted by other ministries and approved by the Tanzanian cabinet. His bank records, he said, would show investigators that "there is no connection to the BAE Tanzanian radar deal".

His US lawyer from Cleveland, Ohio, J Lewis Madorsky, added: "While the matters in question took place a number of years ago, we can state ... that any and all allegations of illegality, impropriety, misconduct and unethical behaviour made against our client are categorically and vigorously denied".

Investigators say Chenge could be a valuable witness. The target of their investigation is not him but BAE. The arms company made the commission payments to a local agent in Tanzania to promote the £28m radar sale, through an elaborate chain of offshore companies and a Swiss bank.

The agent has now left the country and is wanted by Interpol.

These developments come at a key moment in the BAE saga. A landmark high court ruling on Thursday said that the decision to drop the SFO's Saudi inquiry was wrong.

In a huge embarrassment for the British and Saudi governments, the court rejected the claims that the inquiry had to be closed down for reasons of national security and because lives would be at risk.

And it took the extraordinary step of naming Prince Bandar, the crown prince's son, as the man behind what it said could be characterised as an attempt to pervert the course of justice.

Former prime minister Tony Blair caused uproar by personally forcing a halt to investigations into the Saudi deal. The Guardian subsequently disclosed that £1bn had been paid into accounts controlled by Prince Bandar during the deal. Bandar says the payments were not improper.

Inspectors from the Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD) grilled British officials in London last week about their failure to get results from any of their BAE investigations. Britain signed up to an international treaty to outlaw bribery, but there have never been any prosecutions.

The Tanzania deal, although smaller in cash terms than the Saudi deals, is equally controversial: Tanzania is one of the world's poorest countries, and the UK government is paying more than £100m this year to help the heavily-indebted country's budget.

It was Blair again who forced the radar deal through the British cabinet, despite protests from the then international development secretary, Clare Short. She said the sale, for which Tanzania had to borrow yet more from a commercial bank, was corrupt and "stank".

A lengthy SFO investigation in the UK subsequently discovered that 31% of the deal's contract price had been diverted via Switzerland.

BAE transferred the money to a subsidiary, Red Diamond Trading, registered anonymously in the British Virgin Islands.

Red Diamond then moved the cash to a Swiss account in the name of a Panama company, Envers Trading Corporation. This entity had two Panamanian nominee directors. But it was secretly controlled by a Tanzanian middleman, Shailesh Vithlani, according to Dar es Salaam court papers.

Investigators are now checking whether Vithlani arranged to pass any money in turn to Tanzanian politicians and officials.

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Vithlani, who is of Indian extraction but holds a British passport, is listed as wanted by Interpol.

He has been charged by the Tanzanian anti-corruption bureau with lying to investigators, but has left the country. His whereabouts are unknown.

According to the charges, Vithlani falsely denied he was the owner of the Panama company, and falsely claimed he had only handled a separate commission of 1% on the deal.

The SFO's new director, Richard Alderman, former head of UK tax investigations, is due to take over this month. The SFO refused to comment yesterday.

BAE, which has previously denied wrongdoing, also declined to comment, or to explain its chain of offshore payments, other than to say "BAE Systems continues to fully co-operate with the SFO investigation" .

The company has recently launched an extensive public relations campaign and last week unveiled a report commissioned from a commercial consultancy, Oxford Economics, which claimed BAE was of key value to the UK economy.

Source: The Guardian, Saturday April 12 2008
 
Mnaonaje basi tumdunge mshale wa sumu wa kimakonde mgongoni kwani tukimtwanga risasi mlio utashitua majirani walio lala.

Apate fedha kwa fedheha lakini akose roho yake.
 
Kuhani Mkuu

...kudos.....kadiri siku zinavyoendelea hapa JF unajenga hoja murua kabisa...si kama pale mwanzoni ..otherwise maneno mengine ni point sana mkuu

Ndugu Ogah;
Kama mtu mwenye imani za Siasa Huria nimezoea - na naona ni bora zaidi - kuitwa majina tofauti sana na pongezi kwa sababu inanipa uhuru wa kuangalia mambo kivyangu badala ya inavyokubalika na walio wengi au wachache wa kundi fulani. Hata hivyo, ahsante.

Turudi kumtafuta Chenge ndugu yangu, letu moja. Bado yupo?
 
Mh. Chenge atueleze hizo pesa za offshore acc; zaidi ya U$1,000,000 alizitoa wapi?

BAE corruption investigation switches to Tanzania

· Focus on £28m radar deal with East African state
· SFO's new director due to take over this month

David Leigh and Rob Evans The Guardian, Saturday April 12 2008

Following the uproar over its halted Saudi investigation, the Serious Fraud Office is expected to decide whether to bring fresh corruption charges against arms manufacturer BAE within six weeks, over a second arms deal, this time with Tanzania.

A minister from the east African state has denied that more than $1m (£507,500) in his offshore accounts came from BAE.

Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Tanzania's anti-corruption bureau, which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to multi-million pound secret commission payments made by BAE.

Chenge does not dispute the money in his Jersey accounts. But he told the Guardian: "The obvious inference [of the investigations] is that I have received for my benefit 'corrupt payments' from BAE. This is untrue."

He said he was only involved in minor aspects of the radar deal, which was promoted by other ministries and approved by the Tanzanian cabinet. His bank records, he said, would show investigators that "there is no connection to the BAE Tanzanian radar deal".

His US lawyer from Cleveland, Ohio, J Lewis Madorsky, added: "While the matters in question took place a number of years ago, we can state ... that any and all allegations of illegality, impropriety, misconduct and unethical behaviour made against our client are categorically and vigorously denied".

Investigators say Chenge could be a valuable witness. The target of their investigation is not him but BAE. The arms company made the commission payments to a local agent in Tanzania to promote the £28m radar sale, through an elaborate chain of offshore companies and a Swiss bank.

The agent has now left the country and is wanted by Interpol.

These developments come at a key moment in the BAE saga. A landmark high court ruling on Thursday said that the decision to drop the SFO's Saudi inquiry was wrong.

In a huge embarrassment for the British and Saudi governments, the court rejected the claims that the inquiry had to be closed down for reasons of national security and because lives would be at risk.

And it took the extraordinary step of naming Prince Bandar, the crown prince's son, as the man behind what it said could be characterised as an attempt to pervert the course of justice.

Former prime minister Tony Blair caused uproar by personally forcing a halt to investigations into the Saudi deal. The Guardian subsequently disclosed that £1bn had been paid into accounts controlled by Prince Bandar during the deal. Bandar says the payments were not improper.

Inspectors from the Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD) grilled British officials in London last week about their failure to get results from any of their BAE investigations. Britain signed up to an international treaty to outlaw bribery, but there have never been any prosecutions.

The Tanzania deal, although smaller in cash terms than the Saudi deals, is equally controversial: Tanzania is one of the world's poorest countries, and the UK government is paying more than £100m this year to help the heavily-indebted country's budget.

It was Blair again who forced the radar deal through the British cabinet, despite protests from the then international development secretary, Clare Short. She said the sale, for which Tanzania had to borrow yet more from a commercial bank, was corrupt and "stank".

A lengthy SFO investigation in the UK subsequently discovered that 31% of the deal's contract price had been diverted via Switzerland.

BAE transferred the money to a subsidiary, Red Diamond Trading, registered anonymously in the British Virgin Islands.

Red Diamond then moved the cash to a Swiss account in the name of a Panama company, Envers Trading Corporation. This entity had two Panamanian nominee directors. But it was secretly controlled by a Tanzanian middleman, Shailesh Vithlani, according to Dar es Salaam court papers.

Investigators are now checking whether Vithlani arranged to pass any money in turn to Tanzanian politicians and officials.

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Vithlani, who is of Indian extraction but holds a British passport, is listed as wanted by Interpol.

He has been charged by the Tanzanian anti-corruption bureau with lying to investigators, but has left the country. His whereabouts are unknown.

According to the charges, Vithlani falsely denied he was the owner of the Panama company, and falsely claimed he had only handled a separate commission of 1% on the deal.

The SFO's new director, Richard Alderman, former head of UK tax investigations, is due to take over this month. The SFO refused to comment yesterday.

BAE, which has previously denied wrongdoing, also declined to comment, or to explain its chain of offshore payments, other than to say "BAE Systems continues to fully co-operate with the SFO investigation".

The company has recently launched an extensive public relations campaign and last week unveiled a report commissioned from a commercial consultancy, Oxford Economics, which claimed BAE was of key value to the UK economy.

Waungwana,
Nafikiri tusisahau wakati tunalichokonoa hili la Radar, kuwa huyu huyu CHENGE pia yumo kwenye ngebengebe za Richimond, EPA, Mikataba ya Madini n.k. He could be the bigest fish to catch, if TZ was to be serious about snaping others, but do they???
 
Wakati ule Muungwana alipokuwa anaandaa baraza jipya la Mawaziri katika mawaziri waliokuwa wakizungumziwa na Watanzania pamoja na hapa JF kwamba hawastahili kuwemo kwenye baraza jipya ni huyu fisadi Chenge, lakini Muungwana aliziba masikio, sasa ameumbuka tena hata kabla ya miezi sita.

This will be the shaky government we have ever seen since 1961
 
yani imefikia kipindi hata kufungua hii forum huwa naogopa, nakata tamaa, naumia
 
...Tuandike email ya pamoja kama kikundi na kumtaka aeleze alivyopata hiyo mihela ama sivyo ajiuzulu.

Enough with kulalamika, tumuandikie na tumueleze.Ikiwezekana tutume na fax pia.Na tuendelee na utamaduni huu.Pengine hata hajui kuwa kuna watu wa "pressure group" JF wanajua hizi habari.

Mnaonaje?

Chenge amehimili mi shinikizo mikubwa kuliko 'ki-email' cha watu wa kwenye mtandao! Kila la heri, japo nitaisaini.

Pendekezo moja tu: E-mail za Bunge sijui hata kama zinafika, manake hata ukijaribu kuandika 'nataka kuchangia kampeni yako' au 'nimegundua dhahabu kwenye jimbo letu,' huwa hawajibu! Hivyo ikishaandikwa labda itumwe nakala kwenye magazeti pia.
 
Mimi nadhani itabidi niache kabisa kufuatilia masuala ya serikali yetu kusema ukweli mtu unaweza kudata . Hivi vitu vinatia hasira sana na inaonekana dhahiri hawa watu hawasikii na wala hawajali watu wanasema nini ! Kwa sababu naona the situation is not getting better...
 
jamani hata nyerere ambae alikua raisi kwa zaidi ya miaka 20 alikua hana akiba kabisa ikabidi jeshi wamsaidie kujenga kanyumba pale butiama,huyu chenge ana zaidi ya billion moja shillings tena kaziweka marekani kwa kipindi kifupi tu? uwiiiiiii mwiziiiiiiii, eti na huyu ni kiongozi ktk serikali ya tanzania,wajameni tukishindwa kumpa justice huyu jamaa inabidi kumuondoa kabisa in any means necessary.
 
Back
Top Bottom