The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Huyu hawezi kujihudhuru hata siku moja, ana kiburi sana huyu Fisadi na sababu kubwa ya kiburi chake ni kutokana kuwa wakati akiwa mwanasheria mkuu alihusika moja kwa moja katika dili nyingi za wakuu Mafisadi, hivyo wanamuogopa sana hata kumwambia kitu, wakijua wakisema lolote anaweza kuleta noma muda wowote

Hawa jamaa si unajua wamefanya hii nchi kama ka mradi kao, na sisi tunaangalia na kusema eti ngoja 2010, mimi sijapata picha hapa solution ni hipi iliyobaki, kwa sababu kwa nchi kama zetu kura imeonekana sio solution, ukifuatilia yaliyotokea yenya baada ya Chama tawala kushindwa na sasa Zimbabwe, utaona kuwa kura za wanyonge hazisemi lolote kwa sasa
Hawa jamaa hawajiudhuru na kuiba watatuibia na kura wataiba watashinda na nguvu ya hoja imeshindwa na sheria inawabana maskini tu na kuwaacha matajiri, sasa hapa hakuna njia zaidi ya solution ya mwisho kabisa jamani

Mkuu huyu jamaa tukimkamata vizuri anaweza kutwambia kama hata na sisi tumeisha uzwa.

Kiburi alichonacho kinatisha sana maana nilimuona siku Lowassa anatimuliwa Ukuu akidai hiyo haikubaliki. Sijui kwa nini hawezi kwenda naye. Inabidi akimaliza wiki kabla hajajiuzulu tuanze kuandamana.

Otherwise hawezi kutuweka kwenye vyombo vya habari mbali mbali ni fedheha kwa watanzania maana sasa hivi dunia nzima inaweza kuelewa kuwa watanzania siyo waaminifu.

Halafu vile vile yule Mzee aliyechagua kukaa kimya inabidi naye atoke aongee chenge kama wmwanasheria hawezi kulala mitini na kitita hicho chote bila mkuu wa kaya kuwa na hata fununu.

Hivi hakuona mwenzake Tony juzi alivyowekwa kitimoto kwenye vyombo vya habari kuhusu rada?

Inabidi tufuatilie akisafiri kwenda nje waandishi wa habari wa nje wamuhoji maana historia inaonyesha yeye hupenda kuhojiwa na wazungu.
 
one moment
wonderfully he will ascend to power by 2010 in tsunami fashion,what comes in here is who is the dumbest??
......eeerr, Him and his cronies who at no time have shown mercy upon Tanzanians and will rapaciously pounce on them by all means, be it thru vote rigging!!
 
Unajua this is what i am talking about, habari za ukweli I mean hata ukiwa kipofu ukasomewa hii article, you can tell kwamba huu ni ukweli na sio blah! blah! blah! au abla! abla! za kawaida hapa JF.

Waziri Chenge, aliyekuwa mwanasheria mkuu na hatimaye kuwa waziri majuzi tu, ameyapata wapi haya mapesa? Aliwahi kufanya kazi nje? Akiwa mwanasheria mkuu serikali au vyombo vyetu vya usalama vilikuwa aware kuwa huyu mkuu ana mapesa kiasi hiki nje? na kwamba ni zake kihalali? I mean lets be fair, hzio hela nyingi sana kwa kiongozi mbongo kuwa nazo nje, sasa ni lazima iwekwe wazi alzipata lini?

Halafu ni kwa nini yeye anakuwa witness na sio mshitakiwa? Hapo bado sijaelewa?

Mkuu in less than six months itabidi kuwe na baraza jipya la mawaziri maana bado mafisadi wapo wengi tu ndani ya sirikali ya muungwana. Na sisi hapa JF kamwe hatulala mpaka kieleweke. Tumechoka kuambiwa Tanzania ni nchi maskini sana duniani wakati mafisadi wanakuwa mabilionea kupitia migongo ya walala hoi. Wote hawa tunawajua walikuwa hawana utajiri wowote, leo hii miaka michache wamekuwa mabilionea ni kipi walichokifanya kuweza kuwa mabilionea kama siyo kuifisadi Tanzania na Wananchi wake?

Wakati fisadi Mkapa akiwa Rais jamaa yangu aliwahi kuniambia kwamba fisadi alikuwa katika nchi moja ya magharibi akiangalia nyumba mbali mbali ili anunue. Sikumwamini nikamwambia ama alimfananisha Mkapa hamjui sawa sawa maana wakati huo wote tuliamini kwamba alikuwa ni Mr Clean, lakini kwa uchafu wake tuliokwishasikia hadi sasa, naamini kwamba aliyoniambia jamaa kuhusu Mkapa kuangalia nyumba mbali mbali ili achague ya kununua sasa naona yalikuwa na ukweli. Wakati kizungumkuti ndani ya Tanzania na Zimbabwe kikiendelea lupamba moto, muungwana yuko kwenye ziara China. Angekuwa na maadili angekatisha ziara ili akashughulikie matatizo yaliyoikabili sirikali yake na yeye kama Mwenyekiti wa AU, lakini kama mnavyojua siku zote msanii atakuwa ni msanii tu!

Labda anakuwa witness kwa sababu kupitia kwake wanaweza kuyajua mengi zaidi ya mshiko huo uligawiwa kwa akina nani wengine, si ajabu hata fisadi Mkapa alikatiwa mgao.

Mpaka kieleweke.

Alutta Continua!

 
lakini hizi mbona ni pesa kidogo sana,au watu wanatishika na hilo neno us dollar au pound sterling.
 
......eeerr, Him and his cronies who at no time have shown mercy upon Tanzanians and will rapaciously pounce on them by all means, be it thru vote rigging!!

yeah !!!!!!!!!!it sounds to some extents,but frankly call back 2005 .JK collected more than 80% this margine eliminates all ur allegations But i can join u hands if we predict tht either we tanzanians are dumbers or idiots to putting unmercy guys to power yet leting them enjoy thier life on power.Right??

Mimi nafikiri umefika wakati tuanze kujiuliza na kuji examine sisi wtzn ,hii si kitu ya kawaida .everything too much is harmful huku kuongea sana bila matendo nako ni harmful maana kutazaa taifa la wasemaji tu wasio na uwezo wa kutekeleza wanachokisema.Say little do more viceversa is unacceptable.
 
1.
Hivi kweli mnaamini kwamba viongozi wetu ni wasafi?... Nani kati yao mwenye wadhifa hana account nje!..

lakini hizi mbona ni pesa kidogo sana,au watu wanatishika na hilo neno us dollar au pound sterling.

Mkuu Bob,

Heshima mbele mkuu, sikweli kuwa viongozi wote ni wachafu, kama ambavyo sio wananchi wote tumelala usingizi kama wanaowachagua, na si kweli kuwa viongozi wote wana account nje, maana kuna ambao hata hawajawahi kutoka nje ya nchi,

However, baadhi ya viongozi wetu ni wachafu, tena sana, tuziruhusu facts zijiseme kama zinavyoanza kujisema zenyewe, kwenye hili la Chenge, kwa kweli ni aibu tena sana, huyu Chenge, amewahi kushika nafasi gani huko nje mpaka kuwa na hela kiasi hiki?

Mkuu wangu Katibu Tarafa, hebu soma gazeti la Forbes, uone ni wa-Marekani, wangapi kati millioni 245 wanazo hizo amount, tena bank zimekaa tu as a hard cash? Maana hata hao walionazo utakuwa robo tatu yake ziko in shares za stock, lakini sio hard cash, I mean something is not right na our political and legal system,

All and all, ni kwamba baadhi ya viongozi wetu ni wakatili kama sio makafiri, maana unawezaje kuwa na hela zote hizo bank USA, huku ukiona wananchi tena wa jimbo lako wanateseka kwa matatizo ambayo yanaweza kuwa solved na just dola 10,000 tu? Kwa wale manaofanya kazi bank au kwenye markets, hebu tuambieni hizi hela ambazo lazima Chenge, amezifunga kwenye CD, zinatoa interest kiasi gani kwa mwaka?

Halafu bado niko curious kama ni Chenge mwenyewe, aliyewaambia hao wachunguzi kuwa anzo hizo hela, au walimua-ambush? Najua kuna utaratibu wa uwt kumpa rais faili la any Tanzanian in advance ambaye anafikiriwa kupewa madaraka makubwa kitaifa, sasa how did they miss this Chenge's mega account?

Somebody need to answer haya maswali, unajua kuan viongozi kama watatu waliowahi kumwambia muungwana usoni, kabla ya uchaguzi kuwa asahau haitakuja kutokea yeye kuwa rais wa bongo, Nyang'anyi, Sarakikya, na huyu Chenge, wengine wamepigwa chini lakini yeye amesimama WHY?
 
Sasa tuache kulalamika, email yake hii hapa achenge@parliament.go.tz

Tuandike email ya pamoja kama kikundi na kumtaka aeleze alivyopata hiyo mihela ama sivyo ajiuzulu.

Enough with kulalamika, tumuandikie na tumueleze.Ikiwezekana tutume na fax pia.Na tuendelee na utamaduni huu.Pengine hata hajui kuwa kuna watu wa "pressure group" JF wanajua hizi habari.

Mnaonaje?


excellent idea, lets roll peeps,should we write him a letter as individually or as a group?...nina hasira nae huyu mdingi,nyie acheni tu!
 
Ni kichekesho kikubwa sana sisi huku JF kudiscuss acct ndogo ya Mh Chenge iliyoko Jersey kama investment acct. Hii ni acct ndogo sana inayohusu kununua shares mbalimbali Wall st, sasa je thamani ya hizo shares zake ikitajwa itakuwa vipi??

Also most of our senior govt officials have local accts hapo NBC, CRDB, Stanchart zenye thamani kubwa mno kuliko hiko kiacct kidogo.

Kabla sijasemwa kuhusu kutaja $1 mill kama kiacct kidogo, hapa nadiscuss relative, yaani kama kuna mtu ana $20 mill kwenye acct then $1 million ni ndogo in relative terms.

Hela zetu nyingi inasemekana zimewekwa South Africa, UK, Dubai.

Watu wa bank local wakiamua kufyatua matofali ya hawa viongozi patakua hapatoshi.
 
hiyo ni new jesey tu ana zaidi ya bilioni moja yani ana GIGA shilling 1 ama 1Gtsh
bado kwingine.

Ndio maana utakuta mwingereza kazi hafanyi ila analipwa fwedha ,unajua wanafanya je? wanamsubiri chege mauti yanamkuta harafu hizo pesa wanachukua wanalipa watu wao kilaini.
Harafu nini waafrika tulivyo waajabu utakuta pesa hizo hajui mtu yoyote ktk familia yake hilo nina 80%
 
Chenge ana biashara gani halali inayojulikana mpaka akaweza kuwa na $1m (£507,500) kwenye akaunti nje ya nchi? Uwezo wa kuhire an American lawyer anautoa wapi? Du yaani hata kabla ya yeye kuwa connected na hii scandal ya rada tayari kuna harufu kali ya wizi. Huyu jamaa miaka yoote anafanya kwenye public office hizo kama ni savings basi in total zilitakiwa labda ziwe $10,000. Kweli tunaliwa!!!!!!!

Biashara ya viongozi wetu ndo serikali..sasa tuone kikwete atasema nini sasa!!
 

excellent idea, lets roll peeps,should we write him a letter as individually or as a group?...nina hasira nae huyu mdingi,nyie acheni tu!


Sijaona idea mbovu kama hii ya kumtaka ajiuzulu?? why??

Kwani yeye uwaziri amegombea wapi??

Kwanini msimtake rais aliyechaguliwa na Umma wa Watanzania kumtoa??

Chenge ameshasema "" Kamuulizeni rais kwa nini nimechaguliwa""

So hapa naungana na Chenge kwamba yeye asiulizwe kabisa kwa sababu kazi hiyo ni ridhaa ya rais. Full stop
 
lakini hizi mbona ni pesa kidogo sana,au watu wanatishika na hilo neno us dollar au pound sterling.

usilete utani maana this is one billion, kwa mtu ambaye maisha yake yote ni civil servant, its lot of money. Huu mwaka wa shetani kwa CCM na mafisadi wake.
 
Hakuna Smoking Gun


Ni vigumu mno kwa mshahara wa serikali kupata hela kama za Chenge kwa uadilifu. Lakini sio kama haiwezekani. Kuna watu waadilifu wenye mali zinazozidi kipato chao. Pia tunaomshuku Chenge ndio tumebeba mzigo wa kuthibitisha kaiba, sio yeye ajieleze. Isitoshe hajashitakiwa, wala hachunguzwi huko UK, achilia mbali Bongo ambapo tunasubiri Waingereza watuambie 'tumemaliza uchunguzi na ile Radar tuliyo wauzia hatukutakiwa kuwauzia.'

Sidhani kama Chenge ni mwadilifu hata kidogo, lakini vipi akisema hizo hela amedunduliza toka aanze kazi baada ya kumaliza masomo UDSM? Na akaonyesha vibiashara vidogo viwili vitatu toka miaka ya sitini. Na marurupu ya Uwaziri na safari za nje toka aanze kupata vyeo. Na zawadi za hela na ng'ombe toka kwa marafiki toka miaka ya 60. Na hizo pesa kuzaa faidi benki toka siku ya kwanza alipoanza kazi kutokea shule UDSM? Kimahesabu haiwezekani?

Kuna watu waadilifu kama vile Warioba (nadhani aliyeandika ripoti ya rushwa labda muadilifu ) ambao sidhani kama wanakosa $1M benki. (Warioba kwa mfano ana muhekalu pale Mikocheni, kaanza kuujenga wakati ni AG). Marehemu Nyalali (nadhani uadilifu wake haujawahi kuswalishwa) lakini amejenga kathiri pale Masaki wakati ni CJ (ngazi ya cheo kinachoendana endana na AG). Na waadilifu wengine wengi tu, walioongoza Sheria, kina Lubuva (huyu kwa sababu ni Jaji na kwa kumuangalia maisha yake na familia yake nadhani ni msafi msafi), sidhani kama wanaishi kwenye vi geto na kuendesha vi-Volkswagen. Hizi mali wamezipata humo humo Serikali, labda kwa marupurupu.

Isitoshe Chenge hajashitakiwa. Mzigo bado haujahamia kwake kuthibitisha hakuiba. Na kwa vigezo tulivyo navyo mpaka hivi sasa tukienda nae mahakamani anatubwaga vibaya mno. (Wakina Kiula na Mlingwa si walishinda kesi wakati wanaendesha Ujenzi iliyo nuka rushwa kuliko wakati wowote katika kumbukumbu).

Kesi yetu kubwa hapa ni kutaka Chenge ajiuzulu kwa sababu kuna dalili dalili za ufisadi ambazo hazipendezi kwa kiongozi, tena aliyesimamia mikataba yenye utata. Lakini hatuna vidhibiti vya uhakika kwamba kaiba. Vita dhidi ya ufisadi tutapigana navyo sio kwa nguvu bali kichwa pia, ikiwa ni pamoja na kutangulia kujiuliza watajitetea tetea vipi hapa ili tujue tuje na gia gani. Vinginevyo watatuzidi kete.

Na mwisho, kumshangaa Kikwete kwa kukumbatia watu kama Chenge ni kutokumwelewa huyu Rais!
 
lakini hizi mbona ni pesa kidogo sana,au watu wanatishika na hilo neno us dollar au pound sterling.

ACHA UTANI!! kwa mfanya biashara kama mengi sita shangaaa akiwa nayo 1million usd..lakini chenge?? no way!!
 
wataalamu mie naomba mnisaidie ktk hili,mimi naona kule europe na marekani ili uweke pesa bank lazima uwe mfanyakazi ,mwanafunzi ama una haki ya kuishi hapo.

sasa imekuaje Chege afungue akaunti huko ???
 
umefika watanzania inabidi kuongea kwa sauti moja maana mtu aina hii siyo vyema kukaa kwenye serikali yetu. JK Vipi unasubiri uamshwe na nani kama sio wananchi.
 
I guess mnyika nayeye is on his way to a cool billion by 2015!
 
Nafikri barua hiyo ielekezwe kwa JK na sio Chenge kwani yeye alishasema.......muulizeni aliyenichagua!!
 
Back
Top Bottom