The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

I hope Kalaghe na wenzie wanajiandaa kujibu kuhusu hii issue wakija London
 
Nime paste mara kumi kwenye tovuti ya CCM hiyo link!!! Sijui wanafungua kusoma? Tovuti yenyewe haijawa up dated sijui toka wakati wa Sauoer's Darwin's Nightmare!
 
Hii ripoti ndio inayoleta mzozo maana kwa nini ripoti iandaliwe na WB halafu Serikali y Tz iwe na sauti ya kusema itolewe au isitolewe...!!

Ndiyo maana hata hao WB nawashuku kama wana nia safi. Kama ripoti ni yao (commissioned by WB), na kama wao walipinga kwa dhati ununuzi huo kwa nini wasingeitoa ripoti kwa wadau wengine wa maendeleo Tanzania, ikiwemo kuwapa Uingereza wenyewe? Uwazi wa WB uko wapi wakati ndiyo hao hao wanazungumzia utawala bora? Hao Barclays nao kwa nini wasiwajibishwe kama waliidanganya WB? Mbona mambo mengine WB hutukalia kooni mpaka tufuate wanavyotaka wao?

Kama Barclays nao walidanganya katika kutoa mkopo, huku wakijua wanachofanya si kweli HAKUNA SHERIA YA KUFANYA MKOPO HUO UWE BATILI, kwa hiyo TANZANIA ISILIPE na PESA ZILIZOTOLEWA ZIRUDISHWE?
BOT wanaweza kuwanyang'anya leseni BARCLAYS kama WALIDANGANYA?

WAANDISHI WETU WAWAFUATILIE WB nao TUWASIKIE WANASEMAJE, wafuatilieni na BARCLAYS.

Maswali kwa JK/JMT: Kama SFO watasema mambo shwari, hamna rusha au utata wowote sisi tutafanya nini? Tutaridhika tu?
Je, toka tuhuma hizi zilipojitokeza serikali yetu na vymbo vyake vya dola vimefanya uchunguzi kwa watu waliohusika kwa upande wa Tanzania? Kama bado, serikali ik tayari kufanya uchunguzi huo?
Serikali iliacha kuchukua/kununua sehemu ya mtambo uliobaki kwa vile waliona hawauhitaji au kwa vile hawakuwa na pesa au kwa vile walikujagundua kuwa ni ghali mno? Je, kwa kuacha kununua mtambo huo au mwingine usalama wetu wa anga (kijeshi na kiraia) uko salama kiasi gani?

Ndiyo maana NAPINGA suala la kudai kuna WAFADHILI wanaojidai wanataka KUISAIDIA JamboForum lakini tukata issues kwa Ung'eng'e, maana NDIYO HAO HAO wa "kuwakoma giladi?!" Tshwzkxxyq!

Huyo Anthony Mwongo (be'liar) naona ana kazi kwelikweli... kwani kazi kuhojiwa na polisi!!
 
"some people get everything,some people get nothing,
some people get hopes and dreams.
some people get ways and means,........
............................................aah aah aaah ..ah!! will survive"
like meshack ,shedrack and abednergo,thrown in the fire but never get burn"
 
Aksante sana DrWho kwa hiyo Link,nami nimeipitisha kwa baaadhi ya viongozi ili waone, kama Waingereza wametumia zaidi ya 2hrs kujadili Rushwa inayoihusu Tanzania,inakuwaje sie tunashindwa kuchukua hata nusu saa kujadili masuala hayo nyeti katika Bunge letu?Huyu Kiongozi wa serikali Bungeni anayepindisha majadiliano ya maana kama haya na yale ya Richmond na Barrick Minning co. anapaswa awajibishwe.Hivi tunaangaliwaje na hawa mnaowaita Wafadhili?
Huyu Muungwana anakuja London 02.17.07,Lazima mumuulize maswali kuhusu suala hili.Kumbukeni kuwa siku hiyo ni Jumamosi hakikisheni kwamba hatoki kwenda mpirani mpaka mmalizane nae.Ikiwa hamjiandai vizuri wataukwepa hata huo Mkutano,Hakikisheni kuwa mnapata Schedule mapema ili mjiandae kujadiliana nae.Hawa wenzetu hawana machungu, wanachowaza wao ni kutunisha mifuko yao na kuhakikisha kuwa wanawapatia vijana wao Elimu nzuri ili nao waje kutuongoza/kutuibia.Vijana wetu wanahangaika nyumbani kupata Elimu (imekuwa ghali mno) wakati akina Miraji wapo Havard kwa pesa ya Mlipa kodi!Haki Elimu wakisema mnawafungia.Jamani TUAMKE hakuna atakayeisemea Tanzania isipokuwa SISI.
 
blah blah za radar mmezisikia muungwana zomboko alipokuwa anaongea na wahariri...anasema anangojea uchunguzi wa uingereza kujua kama kuna mtu hapa bongo alikula cha juu kwenye hiyo deal mh..
 
Daily News Reporter
Daily News; Friday,February 02, 2007 @00:07

TANZANIA will demand refund from the British government if it is proved that the radar it bought from British Aerospace Systems five years ago was over-priced, President Jakaya Kikwete said yesterday.

He told editors during his monthly address to the nation in Dar es Salaam that the government was keenly following the investigation by London's Serious Fraud Office (SFO) on the 40 million US dollars (about 50bn/-) transaction.

President Kikwete said Tanzania wanted to know if the radar was over-priced as claimed, and if there are Tanzanian officials who received kickbacks to facilitate the purchase, he explained. He said his government would demand refund of any excess payment to BAE Systems because it was an agency of the British government.

"We didn't buy the radar from the streets. We shall lodge formal request for refund from the British government if it is proved that its agency inflated its price to squeeze extra money out of our poor country," he said. President Kikwete maintained that Tanzania was right to buy the radar and that it is a shame on Britain if executives of its arms supplier took advantage of the transaction to earn illegal income.

The transaction was brokered by a British middleman based in Dar es Salaam, who is alleged to have received a 12 million US dollars (15m/-) commission paid to his Swiss account in addition to 400,000 dollars (520m/- ) paid to his Tanzanian-registered company, Merlin International.

Meanwhile, President Kikwete said only true information on corruption and other crime should be volunteered to the government to facilitate quick action by law enforcement agencies.

He praised one informer, who led the police to arrest drug dealers. "He sent me a text message that I should call back because he had important information to give me. I called and he facilitated the arrest of drug dealers," explained the president.

He, however, said many volunteers gave anonymous information which could not be verified and they did not come forward to lead the investigation.

"The suspects mentioned in such information have their own rights as individuals. We can't arrest and charge them on the basis of text messages or anonymous letters," he explained.

In the wide-ranging discussion, President Kikwete said Tanzania was not bothered by being a member of both the EAC and the Southern African Development Community (SADC), because the latter was yet to form a customs union.

He said the dilemma of dual membership to regional groupings also faced Kenya, Uganda and all Southern African countries. "We are not alone in this--we shall decide what to do when SADC establishes a customs union."

Haya mbona na sisi htupatii hiyo mobile number yake?
 
Iwapo itabainika kudhulumiwa…
Tanzania kudai fedha za rada[/FONT
]Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema itadai fedha zilizozidi katika ununuzi wa rada iwapo uchunguzi utabaini bei waliyopewa ilikuwa ni ya dhuluma.
Hayo yalizingumza jana na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wahariri na waandishi wa habari waandamizi Ikulu kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo matokeo ya ziara yake Davos, Uswisi na Addis Ababa, Ethiopia.
Alisema Tanzania ina maslahi katika uchunguzi huo unaofanywa na Idara ya Kuchunguza Makosa ya Ulaghai (SFO) ya Uingereza, kama shirika la BAE System liliuza rada hiyo kwa bei ya juu tofauti na bei halisi na kama ilitoa kamisheni ya sh. bilioni 12 kwa mtu aliyefanikisha ununuzi huo.
Rais Kikwete alisema iwapo uchunguzi utabaini Serikali ya Tanzania ilidhulumiwa, itatuma maombi kwa Serikali ya Uingereza kudai fedha zilizozidi kwa kuwa Tanzania ilinunua rada hiyo kutoka shirika linalomilikiwa na serikali ya Uingereza na siyo kampuni binafsi.
“…Nitashangaa shirika la serikali ya Uingereza litadhulumu masikini kama sisi. Hili likithibitika tutawaomba angalau Serikali ya Uingereza iweze kutulipa kiasi cha ziada waturudishie. Kwamba shirika la serikali ya Uingereza kweli limeiibia nchi masikini!” alionyesha kushangazwa Rais Kikwete.
Tanzania ilinunua rada hiyo kwa sh. bilioni 42 (sawa na paundi za Uingereza milioni 28).
Rais Kikwete pia alisema maslahi mengine ya serikali ya Tanzania ni kwamba uchunguzi huo utasaidia kuwabaini waliohusika hapa Tanzania.
Alisema idara hiyo ya upelelezi ilikuja nchini na kumhoji wakala wa kampuni ya BAE Systems kuhusu kamisheni ili kupata ukweli wa suala hilo.
“…Ama na humu ndani nao kuna watu waliokula sasa hii nayo sisi tuna ‘interest’ kwa taarifa hiyo, lakini na sisi wenyewe tunaendelea... kwa hiyo siyo kwamba tuna ngoja na sisi tunafuatilia kwa umakini na ukaribu. Tumemsikia Claire Short akisema mashine hiyo ingenunuliwa kwa nusu ya bei.
“Mwenyezi Mungu watuthibitishie, wao si wanafanya uchunguzi watuthibitishie kweli mitambo ile tuliyonunua ni nusu ya bei iliyonunuliwa. Tutafungua madai rasmi, maana ni shirika la serikali asilimia 100 hana ubia na mtu. Ni shirika lao la silaha wenye kiasi kukubwa cha hisa ni serikali. Haya ndiyo sisi tunaendelea nayo kuyafuatilia,” alisema.
Akizungumzia suala la kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmonds alisema anachofahamu hawalipwi chochote na atawashangaa sana TANESCO kama watakuwa wanalipa malipo yoyote Richmonds.
Kuhusu sifa ambazo amezikataa, alifafanua kuwa alichosema kwa viongozi wenzake wa CCM ni kuwatahadharisha na sifa hizo kwamba zinaweza kuwafanya washindwe kufanya kazi au kushindwa kujua matatizo yanayowazunguka.
Alisema sifa zingine zinapaswa kuangaliwa kwa undani kwa kuwa zinaweza kumpumbaza kiongozi na kujiona ni kila kitu kwa kuwa watu wanamsifia na hatari yake, akitokea mtu kumkosoa ataonekana adui kumbe yeye ndiye anaeleza ukweli.
Wakati huohuo, Rais Kikwete amesema hoja kuhusu ubora wa vifaa vya tiba vya Taasisi ya Moyo Tanzania (THI) ni vyema wakaachiwa wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwa ndiyo wenye ujuzi.
Rais Kikwete alisema hayo baada ya kuulizwa swali kwamba Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Mama Salma Kikwete walitembelea hospitali hiyo na kutoa sifa kwa vifaa walivyona navyo, na kwamba wizara ilikuwa wapi kueleza ubovu wa vifaa hivyo hadi viongozi walipokwenda kutembelea.
Akijizu swali hilo alisema: “Mimi nadhani kila kitu tukiweke kwenye mizania ya dhamana na ujuzi wa mambo yalivyo. Wataalamu ni wizara. Wizara inadhani vifaa vile siyo vizuri sana lakini wewe na mimi tukienda pale tukiambiwa hapa ukilala moyo unauona. Hapa ukilala tunakupasua tu wewe na mie tunaweza kudhani hakuna vifaa vilivyo bora kushinda hivi.”
“Lakini akija anayejua, anakwambia vifaa hivi vya mwaka 47, wenzako siku hizi wana vifaa vya kisasa zaidi. Sasa kama mimi nisingependa hili, liwe la mjadala kati ya aliyoambiwa mke wangu na aliyoambiwa mzee Mwinyi na wanayojua wizara, mimi nadhani muende wizarani wawaambie, hebu tuambie ulichokiona wewe hapa kasoro yake ni nini? Lakini ukienda kumwambia mzee Mwinyi atasema nimekuta pale mambo mazuri kwelikweli.
“Mke wangu ataniambia Loh! Yaani wale sijapata kuona pengine ndiyo aina ya kwanza ya mashine aliyowahi kuiona na hana mfano wa nyingine ya kuilinganisha, lakini wizara wanao wataalamu. Tufanye kazi na wizara inayohusika kujibu maswali tulinayo kuliko tukachukua mifano hii ya viongozi hawa,” alitahadhirisha Rais Kikwete.
 
haya wasomi, hayo ndio maneno ya mheshimiwa rais wetu, angalieni kutokuwa wasemaji wa serikali ya tanzania, wengine tunawajua na mlishakuwa katika vyombo vya kutnga shria na sasa mko hapa.wakati mlipokuwa ndani ya chombe hicho mlishindwa hata kusema kwa kujipendekeza mkidhani siku moja unaweza kupewa cheo.
Kumbukeni nyie magalatia kuwa, CCM itamfuata mtu ambae anaonekana ana upeo, mvuto kwa wananchi na mwenye mwelekeo mzuri iwe kwenye siasa au kiutendaji.
Lakini nyie wote mnaopiga madongo serikali sasa, ndio nyie mlioshindwa maisha huku tanzania kwak ukimbilia nje na huku nyumbani mmeshindwa hata kujenga choo na ndio maana kila siku mnasema hawezi kurudi kwa kuwa hali ni mbaya, sasa kama hali mbaya ndio serikali ikupe pesa mfukoni?
Basi wewe kaeni huko ulaya ili muweze kupata hizo pound 55 ambazo queen anawapa.
ALUTA KONTINUA, MAPAMBANO NA MAGARATIA YANAENDELEA!
 
Hivi huyu rais anashauriwa na nani?

kwanza yeye kuzungumzia hii issue KWA UNDANI KAMA ALIVYOFANYA wakati bado kuna mambo ya kisheria yanaendelea huku UK inaweza kufanya kila kitu kiende na maji

Naona amekuwa so detailed katika maelezo yake na hii kama hao BAE SYSTEMS waki ijuwa itakuwa ni nzuri kwao kwani wanaweza kuobject matokeo yoyote ya SFO

Hiovi hao jamaa wa IKULU hawajui kama suala hili lishakuwa International na kuna ma lawyers wako stand by kama serikali itatoa matamko ya kujifunga
 
hivi kuna mtu ana video ya press conference aliyoifanya JK jana?
 
DrWHO

Unauliza huko bongo hawana haraka ya kitu kama hiki labda usubiri, unakumbuka wakati wa maandamano ya Rada tulipata habari kwenye magazeti kwanza kabla ya members.
 
We philomon,
kuwa muungwana huwezi kumwita ais wa nchi zomboko,unaweza kujipatia matatizo makubwa kwa kutaka kujifanya hujilikani ungali watu wanakujua, lakini awali ya yote sisi Watanzania na hasa watu kutoka afrika tumejaliwa kuwa na heshma kwa kumuheshimu mkubwa aliyekuzidi kiumri na hata yule ambae ni kiongozi wako.
Kumwita kiongozi wa nchi tena aliyechaguliwa na wananchi kwa zadi ya kura asilia 80 ni utovu wa nidhamu na nina shaka na heshima, hekima na busara zako.
Yawezekana hukuelelwa katika mazingira ya kitanzania na kama umelelewa basi tuna wasiwasi ulikosewa radhi na wazazi wako.Ushuair kwako ndugu philomon kwamba tupo hapa tukibishana kwa hoja, ambapo mengine yanakuwa fundisho kwa wenzetu wengine na sisi wenyewe kuweza kujipanua na uwezo kujua mambo mbalimbali iwe kukosea au kuelemisha.
Ninachokushauri tafadhari matusi ya kumtukana kiongozi wa nchi si vizuri, tunaingia katika mitandao ya wakenya na waganda, tean wao nchi zao zina matatizo lukuki tofauti na sisi, lakini hawatukani viongozi wao na wanabishana kwa hoja.
Sasa wewe matusi ya nini, kumbuka huyo Rais ni mtu mwenye familia yake na ndugu, jamaa na marafiki.si vizuri na wala si utaraabu hao jamaa au watoto zake kuona baba yao na sisi watanzania kuona rais wetu akidhalilishwa kwa matusi mazito kama yako.
Ombo langu kwako, tupishane kwa hoja ili tuweze kupata uweli wa mambo na mengine tunaweza kujifunza kutoka kwako wewe.
HILO NI OMBI,LAKINI NI FUNDISHO KWAKO!
 
MtoaUkweli, hapa umesema.. kweli jamani tuwe na ulimi mzuri.. lugha chafu hazifai kabisa ila unaweza kuyatukana matendo yenyewe kwa kupitia hoja.
 
point of correction mtoa ukweli,mimi hata sehemu moja sijawahi kutukana mkuu,na tafadhali acha kutisha watu kama una wajua ,au kusema nimelelewa nje...nafikiri neno "muungwana zomboko" si tusi,angalia dictionarry yako ya kiswahili kama utakuta tusi la hivyo..mbona watu walimuita mwalimu "mchonga" ,au mzee mwinyi rukhsa na lisiwe tusi?
sasa naona tunataka kudhibitiana mpaka uhuru wa kuandika especially baadhi ya watu wanaokulipa wanapoguswa...wewe vipi..unataka kusema kwa sababu muungwana alipata hiyo asilimia 80% ndio unataka hadi hapa tunyenyekee,,..mimi nilishasema hapa kuwa sisi ni wazalendo na hatumchukii rais ,..sisi tunarusha mawe tu kumfanya atawale vizuri..ushauri anaopata hapa ni wa moja kwa moja ...kama unataka kudhibiti hadi rais kuitwa nick names nenda fungua ile forum ya state house ,..tukija huko mta edit mnavyotaka...nakupa changamoto weka thread yangu yoyote niliyotumia matusi[ya nguoni]

mkandara usimsikilize mtoa ukweli,hakuna tusi lillotumika ,..muungwana zomboko si tusi its just name for wazee wa mjini kwenye vijiwe vya gahawa..tutupe mawe tu kaka ,hapendwi mtu ,inapendwa maisha bora tu!! we are results oriented...
 
Kumwita kiongozi wa nchi tena aliyechaguliwa na wananchi kwa zadi ya kura asilia 80 ni utovu wa nidhamu na nina shaka na heshima, hekima na busara zako.
Yawezekana hukuelelwa katika mazingira ya kitanzania na kama umelelewa basi tuna wasiwasi ulikosewa radhi na wazazi wako.

Mtoa Kweli

Sasa ndio unafanya nini; au hiyo sentensi sio tusi.

Anyway; Asilimia 80 ya kura za wizi, ahadi za uongo, ukandamizaji wa wapinzani, ubabe wa media, matumizi mabaya ya dola...NO WAY hastahili heshima ya 80%...not from me.
 
Hello there!
Nimekuwa nikifuatilia suala la rada kwa makini sana, hasa mimi kama wazalendo wengine wenye uchungu na nchi hii yenye rasilimali nyingi.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba rada ni moja ya vitu vikuu muhimu ambavyo serikali yake inafuatilia kwa karibu

Rais Kikwete alisema nchi maskini kama Tanzania kununua rada kwa bei ya juu kuliko bei yake halisi ni kuiumiza kiuchumi na kama kweli itathibitika kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa kitu cha kwanza kufanyika ni kuiomba serikali ya Uingerea iirudishie Tanzania fedha zilizozidi.

Inasemekana kuwa rada kama hiyo ilikuwa inagharimu kati ya Sh20 bilioni na Sh30 bilioni, hivyo kufanya Tanzania kupoteza zaidi Sh20 bilioni za Tanzania. Rada hiyo iliuzwa kwa Sh50 bilioni.

Katika mkutano huo ambao ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alitaja kitu kingine ambacho serikali yake inafuatilia kwa karibu juu ya ripoti hiyo ya uchunguzi iliyoundwa kuchunguza suala hilo nchini Uingereza, ni kupata uhakika kama kuna watanzania walihusika katika kula rushwa ya fedha za rada.

Ingawaje Rais Kikwete hakusema moja kwa moja hatua zitakazochukuliwa na serikali yake iwapo baadhi ya Watanzania watatajwa katika ripoti hiyo kuwa walihusika katika kula rushwa, dalili zinaonyeshwa kuwa watuhumiwa wa rushwa watafikishwa mbele ya sheria.

All in all:
>>Bado kichwa kinaniuma kwama inamaana mpaka sasa hajui orodha ya wakubwa serekalini waliohusika katika hilo sakata? Tena wengine wako secta nyeti ktk sirikali yake!!
>>Ok. Let's say kwamba wamebainika. Je ataweza kufata sheria kama anavyojikosha kwetu? What i mean is yeye kama mwenyekiti mpya wa ccm atakuwa na ubavu wa kuvunja mwiko na kumsweka mwenyekiti mstaafu wa ccm mbele ya hakimu?
>>Pia napenda kuuliza kwamba wakati huo akiwa waziri wa nje ali react vipi kama kweli anauchungu na walipa kodi?
>> Na hao walioko madarakani atawa action vipi wasiweze kukwamisha/kupindisha mlolongo wa justice.

Sorry for all above lakini, for sure i cant sense the light channels.
 
Tangu lini mwizi anataka heshima? Mwizi akikamatwa hupigwa mawe hadi kufa akibahatika ataokolewa sasa hawa wanasiasa wamekuwa wezi ni halali yao kukejeliwa. Waache wizi na Rushwa wataheshimiwa. Pesa za walipa kodi ndizo wanatumbua halafu wanataka heshima What a joke? hapa ni mawe tu tena ya usoni.
 
mtoa ukweli ,heshima haiombwi huja ."..na heshima ya kuitwa baba ni chakula mezani" hata watu muhimu kwenye historia kama mahatma gadhi,mwalimu nyerere,nelson mandela ,bob marley,haile selasie[rastafari]ets wameipata heshima kwa kuihangaikia na hawakuwahi kupigiwa debe ila mtu anajikuta anawaheshimu tu hata kama hataki atasifu kimoyo moyo...

uko wapi mtoa ukweli ? rudi umtetee "MUUNGWANA ZOMBOKO"
 
Back
Top Bottom