Kyoma
Senior Member
- Jun 2, 2006
- 101
- 89
vilaza wapo dodoma wanahemea per day,yaani inakatisha tamaa tulioibiwa hakuna hata mbunge mmoja ambaye angalau kachomekea neno hadi leo,wabunge wa uingereza wana uchungu utafikiri pesa iliyoibiwa ni yao wetu aah kimyaa wanaogopa kamati za chama na wale wa upinzani wanaogopa kunyimwa vitripu vya kuandamana na muungwana zomboka
Mzee Phillemon Mikael,
Ukifuatilia mienendo ya wanasiasa wengi wa nchi zetu masikini utakata tamaa ya maisha. Ni bahati mbaya tunawapata viongozi wenye vyeo bila ya kuwa na sifa za uongozi na watu wenye sifa za uongozi ambao hawana vyeo vya kuwapa nafasi ya kutumia sifa hizo kwa manufaa ya jamii zetu. Matokeo yake ni kwamba wenye vyeo wataendelea kuvurunda utawala wa jamii zetu, wakati wale wenye sifa bila vyeo wanalazimika kuendeleza uongozi wao kwa njia zisizo rasmi. Napenda kuwapongeza wadau wote wa jambo forum kwa kuendeleza uongozi katika njia hii isiyo rasmi. Ni matumaini yangu kuwa taasisi zetu zote (Bunge, Vyombo vya habari, Mahakama, Wanafunzi, Waalimu, Madaktari, wakulima, Wafanyakazi, Vyama vya siasa, wazululaji, changu doa, na wadanganyika wote) wataondoa ukungu uliogubika macho yao na kufuata nyao za Jambo forum
Kuongoza ni kuonyesha njia. Nakupongeza sana Mwana Kijiji kwa kuonyesha njia. Kitu ulichokifanya, sisi wa kwa Mfugwa Mbwa tunaita "Education for Liberation". Ni matumaini yangu kuwa wanafunzi wote wa nyumbani wataachana na "old fashioned tricks" za kugomea masomo. Migomo ilikuwa na mafanikio zamani wakati tunatawaliwa na viongozi waliokuwa na maono kuwa nchi haiwezi kuendelea bila kuwasomesha watu wake. Migomo haiwanyimi usingizi watawala wetu wa sasa. Nawashauri wanafunzi wawe wanapitia Jambo Forum ili wapate mbinu za kupambana na hawa waheshimiwa.
Nani kasema kuwa mataifa makubwa kama Uingereza na Marekani hayawezi kuzuiwa kutembeza ubabe na kuwakandamiza raia wa nchi masikini? Ukitaka kutumia mtutu wa bunduki utakata tamaa na huwezi kamwe! Lakini kumbuka haya mataifa yamefika hapa yalipo kwa sababu ya kutumia "bongo" na "Karamu". Ndio njia hiyohiyo inayoweza kutumika kuyasambaratisha. Mara nyingi wanaofanya ubabe, unyonyaji, na ukandamizaji ni viongozi wao wakishirikiana na watawala wetu wenye uwezo mdogo wa kuona mambo. Raia wengi wa hizi nchi hawakubaliani na matendo ya viongozi wao. Vivyo hivyo, raia wengi wa nchi zetu hawakubaliani na watawala wetu. Kwa mtindo huu wa Mwana Kijiji wa kuweza kuwasiliana moja kwa moja na raia wa hizi nchi katika wakati muafaka, tunaweza kuwaweka kiga, na kuwapiga kabali la nguvu hawa waheshimiwa wetu, hivyo kujikomboa. Bado naamini kuwa raia wa Uingereza/Marekani wana uwezo mkubwa wa kuzisimamisha serikali zao. Kinachotakiwa ni sisi kutoa somo kwa hao raia na likaeleweka.
Hongera sana Mwana Kijiji pamoja na wadau wote wa Jambo Forum