The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Mkandara sijui kama ulielewa nilichokuwa nakizungumzia?

kwa sababu hili lilikuwa ni swali amabalo nilikuwa naangalia scenarios kuhusu hii issue

ASSUMPTIONS:

Now who are the donors/contributors of the aid money? Is it govts in the west or is it charitable organisations? If the latter there some political bargain/wrangling could result in Blair escaping personally unscathed. If the latter, they are duty-bound and presumably required by their own charter/constitution to persue the money or in other words kuchelewesha haki na hapo tena Ma-lawyer wataingia kuanza kuidadua constitution ambayo nadhani unaelewa kuwa iko pungufu

Now kwa upande wa BAE SYSTEMS...I see that it's small fry for them so it won't be the end of the world for them if they had to cough up the dough. But then they are duty-bound to their shareholders that they contest any claims of that nature.....UPO HAPO MWANA KIJIJI?

fURTHERMORE, The World Bank is involved, apparently. Isn't Wolfowitz very convenient its president these days? Now that's an old friend of Bush/Blair....
 
Western bankers and lawyers 'rob Africa of $150bn every year'

Africa kept destitute as western firms shift cash to tax havens

Nick Mathiason in Nairobi
Sunday January 21, 2007
The Observer

More than $150bn a year is looted from Africa through tax avoidance by giant corporations and capital flight using 'a pinstripe infrastructure' of western banks, lawyers and accountants, according to the African Union.

This £75bn equivalent shortfall easily eclipses pledges made by leaders of the world's richest nations to increase aid and write off debt at the G8 summit in Gleneagles in 2005.

Such is the level of capital flight, revealed in studies by the African Union, that the poverty-stricken continent is now a net creditor to the rest of the world. It is estimated that about 30 per cent of sub-Saharan Africa's annual GDP has been moved to secretive tax havens, many under the jurisdiction of the British government.

The full scale of the plundering, in which western companies and financial firms are complicit, has come to light at the launch this weekend in Nairobi of a pan-African campaign group, the Tax Justice Network for Africa. The TJNA is to investigate multinational tax avoidance and abuses of tax havens by corrupt African politicians on a country- by-country basis, as well as lobbying global leaders to commit to a proper crackdown.

Alvin Mosioma, the TJNA's first coordinator, said : 'It is astonishing that the World Bank and International Monetary Fund have not researched capital flight and tax. Until now these issues have not been included within the debate on poverty alleviation. We will publish precise information about tax avoidance in African countries and focus on the role of multinationals. Our message is that tax justice will improve democracy.'

As multinationals' dubious tax practices come into focus at the World Economic Forum at Davos this week a report will reveal that, despite the global commodity boom over the past three years, African governments are missing out in increasing tax and royalties, and in some cases actually receiving less revenue from mining companies than before.

As production of copper, gold, nickel and platinum soars, research from Christian Aid will show that the Tanzanian government's revenue from gold fell by nearly a third once the rise in prices has been factored in. Zambia saw revenues from copper halve. Pressure from the IMF to privatise industries on advantageous terms to mining firms is responsible for the shortfall, say campaigners: 'The myth that tax rates have to be slashed to attract overseas investment needs to be challenged,' said Anna Thomas, Christian Aid's policy manager.

There is also concern at how socalled transfer pricing techniques - otherwise known as profit-laundering - are deployed by giant firms in extractive industries to massage down their profits.

While Britain's government has been praised for putting poverty alleviation at the top of the agenda, it faces criticism that it has done little to stamp out overseas tax abuses involving UK firms and for being the destination for money siphoned out of Africa by corrupt officials. Cross-border dirty money flows are conservatively estimated at $1 trillion annually.

But the Treasury said: 'The government has effectively tackled both corporate and personal tax avoidance structures time and again. The UK is driving efforts to reach international consensus to overcome problems with capital flight and tax evasion.
'The UK's extensive network of tax treaties with other countries assists revenue authorities in the detection and countering of tax evasion. The UK is committed to engage with other jurisdictions to strengthen international cooperation on this issue.'

The African Union estimates that more than 80 per cent of the annual $150bn looted from Africa finds its way to offshore financial centres. The Observer revealed in 2005 that the total stock of private wealth held in low-tax havens is $11.5 trillion. Meanwhile, compelling evidence from Ghana and Nigeria is emerging that pressure on these countries from the IMF and World Bank to reduce corporate taxes has forced many African countries to levy VAT on fuel, which is increasing desertification and global warming by forcing millions of people in poverty to abandon gas stoves and chop down forests for wood burning.

Nigerian academic NA Adebayo said: 'Imposing VAT on petrol and gas products has sparked infl ation in many countries as transport costs rise and is also leading to desert encroachment.'

http://www.taxjustice4africa.net

http://observer.guardian.co.uk/business/story/0,,1994976,00.html#article_continue
 
DrWHO,
Ulimwengu haujabadilika. Wakoloni walikuja Afrika kutafuta cheap raw materials na kuchota natural resources. They are still doing the same today under the guise of investments.
It is up to us to wake up to their game.
 
HATIMAYE baada ya kuwapo hisia kuwa huenda Serikali ya Uingereza ikazuia uchunguzi unaoendelea dhidi ya kampuni ya BAE Systems inayotuhumiwa kuhonga baadhi ya vigogo wa Serikali ya Tanzania wakubali kupitisha ununuzi wa rada iliyogharimu taifa mabilioni ya shilingi, Mwanasheri Mkuu (AG) wa Uingereza amevunja kimya kuhusu suala hilo.

Akikaririwa kupitia gazeti la Financial Times la Uingereza juzi, Lord Goldsmith, alilizungumzia suala hilo kwa kubainisha kuwa uchunguzi wa rushwa katika ununuzi wa rada na vifaa vingine vya kijeshi unaoendelea Tanzania, Romania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Cheki na Chile, hautasimamishwa.

Hisia kuwa uchunguzi wa rada ambayo Tanzania iliuziwa kutoka Uingereza huenda ukasimamishwa, ziliibuka baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Tony Blair, kukutana na Rais Jakaya Kikwete jijini London wiki iliyopita.

Bw. Blair amekuwa akionekana kuitetea kampuni ya BAE Systems kiasi cha kufikia hatua ya kutumia mamlaka aliyonayo kisheria, kusimamisha uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo, ambayo ilikuwa ikikabiliwa na tuhuma nyingine za kuhonga wanasiasa wa Saudi Arabia. Uchunguzi huo ulisimamishwa kwa kile Bw. Blair alichokieleza kuwa ni sababu za kiusalama na kidiplomasia.

Kutokana na hali ya mambo na hasa tamko la Bw. Blair na Rais Kikwete mara baada ya mkutano wao wa London, ambapo waliazimia kuongeza ushirikiano baina ya nchi zao, baadhi ya wanasiasa Uingereza walianza kujawa na hofu kuwa huenda uchunguzi wa rada ya Tanzania ukafikia mwisho kama ilivyokuwa kwa Saudia.

Mmoja wa walioonesha hofu yao bayana, alikuwa ni kiongozi wa chama cha Liberal Democrats, Sir Menzies Campbell, ambaye alidiriki kumhoji Bw. Blair siku alipohutubia Bunge la Makabwela na kumtaka atoe tamko kama uchunguzi wa Tanzania nao ungesimamishwa. Bw. Blair alikwepa kujibu swali hilo na kuacha tashwishwi zaidi.

Lord Goldsmith, ambaye amekuwa akilaumiwa tangu nchi yake ilipotangaza kuzuia kuendelea kwa uchunguzi wa Saudi Arabia, alithibitisha kuwa uchunguzi mwingine wa tuhuma za rushwa dhidi ya BAE Systems utaendelea.

"Ujumbe ulio wazi ni kwamba uchunguzi mwingine kuhusiana na kampuni za Kiingereza kutumia rushwa utaendelea, hata kama kulitokea matatizo sana baada ya kusimamishwa ule wa Saudi Arabia.

"Watu lazima waelewe, si BAE Systems wala kampuni nyingine yoyote ambayo iko juu ya sheria," alisema na akazidi kutetea kuwa kusimamishwa kwa uchunguzi wa Saudi Arabia ni uamuzi uliokuwa sahihi ingawa uliwagharimu sana.

"Ni suala ambalo limetugharimu sana, kwa sababu watu wametafsiri vinginevyo au wataendelea kulifasiri vibaya, wakimaanisha hatuna mkakati imara wa kupambana na rushwa," alisema Lord Goldsmith na kuongeza:

"Uchunguzi mwingine kuhusu tuhuma za BAE katika nchi za Romania, Tanzania, Jamhuri ya Cheki na Chile, utaendelea kwa nguvu zote."

Akizungumzia zaidi kuhusu uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu huyo alisema yuko tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa na Kitengo Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Ulaghai (SFO) iwapo atahitajika.

Wakati akisema hayo, taarifa ya kampuni ya BAE Systems imeeleza kuwa kampuni hiyo inafuata maadili katika mikataba inayoingia na hata wafanyakazi wake wanafahamu miiko waliyowekewa ya kutotoa wala kutumia rushwa katika mikataba ya biashara.

Tamko hilo pia lilisisitiza kuwa BAE haipendezwi na wala haina tabia ya kutumia fedha kuhonga wanasiasa, ingawa haikani kuwa ina ukaribu na baadhi ya wanasiasa, jambo ambalo inasema taarifa hiyo, ni la kawaida hasa kwa kampuni ambazo mteja wake mkuu ni Serikali na idara zake.

Taarifa hiyo bila kutaja moja kwa moja tuhuma zinazoikabili, ilizungumza kiujumla tu kuwa haihusiki na tuhuma inazohusishwa nazo na ikasisitiza kuwa inafanya kazi zake kwa kufuata misingi ya kimataifa na maadili ya kibiashara.

Katika hatua nyingine, tuhuma hizo za rushwa zimeifanya Serikali ya Uingereza izidi kubanwa mbele ya Kamati ya Utendaji ya Shirika la Kimataifa la Uhusiano wa Kiuchumi (OECD) lenye makao makuu yake Paris, Ufaransa.

Kutokana na mwenendo wake katika kushughulikia masuala ya tuhuma za rushwa dhidi ya kampuni zake, hasa suala la kuzuia uchunguzi wa Saudia, OECD, iliitaka Uingereza mbali ya sababu ilizoziwasilisha awali za utetezi, itekeleze majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wa jumuiya hizo.

Pia kamati hiyo imeamua kuujadili zaidi mwenendo wa Serikali ya Uingereza kwenye kikao kijacho Machi mwaka huu.

Rgds/MpigaKula
 
Maneno mazito wacha tuone . Ila my instinct were right kwamba JK sought to stop the investigation .
 
Baada ya kusimamisha uchungu wa Saud Arabia sidhani kama Blair na Goldsmith wana ubavu wa kusimamisha uchunguzi huu pia. Hautatusaidia sana sisi wabongo ila angalau tutakuja kuwa na uhakika zaidi kuwa katika hizo $ 12 ni ngapi zililiwa na kina nani...hata kama BM mwenyewe alikuwa wakina JK wakikanusha habari ndio imekwisha hakuna gazeti au yoyote atakayeweza kuchimba zaidi ya hapo.
 
Aisee!
Yetu Macho,Mzee! By the way update yako MPIGAKURA ni nzito.
 
*Wamsaka wakala wakidai aliwapunja mgawo
*Washangaa kusikia zilikuwa ni sh. bilioni 12

Na Mwandishi Wetu

SAKATA la rushwa katika ununuzi wa rada iliyonunuliwa na Tanzania mwaka 2002 kutoka kampuni ya British Aerospace (BAE Systems) ya Uingereza, limeingia katika sura nyingine baada ya kudaiwa kuwa baadhi ya vigogo waliohusika katika 'dili' hilo sasa wanahaha kumsaka wakala huyo, akidaiwa kuwatapeli.

Mshituko huo umekuja baada ya vigogo hao kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa 'kamisheni' waliyopewa wakati wa kufanikisha ununuzi wa rada hiyo, hailingani na kiwango cha sh. bilioni 12, ambacho wakala aliyekuwa akiwaunganisha alikaririwa kukiri kuzipokea kutoka BAE Systems.

Wakala huyo, aliyeelezwa kuwa karibu na wanasiasa wengi wa Tanzania, alikiri alipohojiwa na wachunguzi kutoka Kitengo Maalumu cha Makosa ya Ulaghai (SFO) cha Uingereza na kula kiapo mbele ya Hakimu wa Tanzania, akithibitisha kupokea fedha hizo ambazo ziliwekwa kwenye akaunti yake binafsi Uswisi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, imedaiwa kuwa wakala huyo tangu alipohojiwa na SFO, amekuwa akisakwa na vigogo hao wakitaka kujua undani halisi wa 'kamisheni' hiyo ya sh. bilioni 12 ya BAE.

Chanzo hicho kimeiambia Majira, kuwa hata hivyo, wakala huyo hayupo nchini kwa sasa.

"Inaelezwa kuwa hata ofisi yake imefungwa, kila watu wanapomuulizia kwa jamaa zake, wanaambiwa amekwenda India," kilisema chanzo chetu na kueleza kuwa ndiyo maana hata ile habari ya gazeti la The Guardian la Uingereza, iliandikwa kwa kuhojiwa rafiki yake, ambaye naye alikubali kuongea huenda kwa sababu wamekorofishana kibiashara.

"Wanahaha kumsaka, inaelekea walichoambulia wakati wa kuchagiza ununuzi si kile wanachokisoma sasa kwenye vyombo vya habari," kilisisitiza chanzo chetu ambacho kinafahamu kwa kina zaidi kuhusu sakata hilo la rada.

Akizungumzia vigogo hao, mpasha habari huyo aliiambia Majira kuwa sakata la rada lilihusisha viongozi wengi na kwa nyakati mbalimbali, kuanzia mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na hata naibu mawaziri, wengi wao wakiwa wastaafu kwa sasa.

"Hawa, hasa huyu ...(anamtaja Waziri mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu), ndiye aliyeshughulikia sana suala la rada na anajua mchakato wote.

"Yeye ndiye hasa aliyeratibu zile hatua muhimu. Sijui kama anaweza kupatikana. Najua hili ni suala nyeti, kila mmoja atakwepa na kukataa kuzungumza," kilisema chanzo hicho.

Kikizungumzia zaidi kuhusu uchunguzi wa SFO, kilisema kuna mambo mengi ambayo mawakala hao wameyaeleza na kukiri mbele ya wachunguzi hao.

Hata hivyo kiliwaasa wadau wote wa maendeleo nchini kuhakikisha kuwa suala la watu kutuhumiwa kuhusika katika rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, linapatiwa majibu sawia.

"Tujue, kwamba wale jamaa kutoka SFO wanachunguza kashfa ya rushwa si kwa faida ya Watanzania. Hata gazeti la The Guardian linaifuatilia sana habari ya rushwa katika rada kwa maslahi ya Waingereza wenyewe.

"Sisi tujiulize, tunachukua hatua gani kusaka ukweli wa viongozi wetu kudaiwa kuhusika katika sakata hilo? Nawaomba tuelekeze nguvu zetu katika hilo kwa sasa," kilisisitiza chanzo hicho.

Jana gazeti hili lilimkariri Mwanasheria Mkuu wa Uingereza, akisisitiza kuwa uchunguzi wa suala hilo nchini Tanzania utaendelea kufanyika kwa nguvu zote.

Rais Jakaya Kikwete ambaye Serikali yake imedhamiria kupambana na vitendo vya rushwa na ubadhirifu unaokwaza maendeleo ya nchi hii, alisisitiza akiwa London, Uingereza hivi karibuni, kuwa Serikali yake inafuatilia kwa karibu uchunguzi dhidi ya sakata hilo na hautaliingilia.

Kuhusishwa kwa viongozi waandamizi katika Serikali ya Tanzania katika mgawo wa 'kamisheni' ya sh. bilioni 12, ni suala ambalo sasa linazidi kuibua mjadala nchini na maoni ya wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani, ni kuwa Serikali ya Tanzania nayo inahitaji kujisafisha katika hilo, kwa kuunda tume huru.

Source http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2183
 
Mr. Lwelu*
Kuundwa kwa tume huru ni wazo zuri sana, lakini ninawasiwasi kwamba hiyo tume haita kuwa huru in reality kwasababu ambao wako involved wengi wao ni viongozi-Serikalini.
 
•
Sakata la ununuzi wa rada Vigogo wahaha Dar

Source: Majira 26/01/2007
 
•
Sakata la ununuzi wa rada Vigogo wahaha Dar

................................................

Rais Jakaya Kikwete ambaye Serikali yake imedhamiria kupambana na vitendo vya rushwa na ubadhirifu unaokwaza maendeleo ya nchi hii, alisisitiza akiwa London, Uingereza hivi karibuni, kuwa Serikali yake inafuatilia kwa karibu uchunguzi dhidi ya sakata hilo na hautaliingilia.

Kuhusishwa kwa viongozi waandamizi katika Serikali ya Tanzania katika mgawo wa 'kamisheni' ya sh. bilioni 12, ni suala ambalo sasa linazidi kuibua mjadala nchini na maoni ya wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani, ni kuwa Serikali ya Tanzania nayo inahitaji kujisafisha katika hilo, kwa kuunda tume huru.

Source: Majira 26/01/2007

Ngoja tuone kama TAKURU itaweza kumkamata hata mmoja. Tutaambiwa hakuna 'iota of evidence' na hata kama akibainika kwa kuwa na mali nyingi kesi ikipelekwa mahakamani DPP atweza kuifutilia mbali...

TAKURU KUTOINGILIWA kazi zao haitoshi kama sheria inayompa mamlaka DPP kufuta kesi ya jinai bila maelezo yoyote haifutwi au kufanyiwa marekebisho bado hii ni danganya toto.

Hata hivyo ni faraja kuona angalau kuna magazeti yanaweza kuandika hali halisi.

HIVI HUYU JAMAA (WAKALA) NDO YUKO BIZE KWENYE DILI ZA HELOKOPTA NA MAIVECO NINI, AU KESHATUKIMBIA?
 
Waliposema ni "Mtanzania" walitaka kumfanya kuwa awe wa kwetu. Hadi KLH News ilipoweka wazi kuwa huyu jamaa ni Muingereza na vikiunga Tanzania ana kwa kutimkia!! Tulipouliza humu tukaambiwa tuache BAE wafanye uchunguzi wao!! Kwenye nyongeza ya ripoti yangu maalum kufafanua niliwaambia ushahidi upo wa mara baada ya dili kukamilika viongozi kadhaa wa Tanzania na wasaidizi wao wa karibu walioshughulikia suala hili la rada walienda Uswisi na sehemu nyingine ambako walisaidiwa kufungua offshore accounts! Majina yapo na hadi namba za akaunti hizo zipo... Viongozi hao wanajulikana na miradi waliyoanzisha kutumia mapato hayo ipo inapendeza na kuvutia!!

Ila nani atoe ushahidi huo hadharani!! Njia pekee ni tume huru ya kuchunguza watu hawa.. tatizo ni nani awe wa kwanza kumfunga paka kengele? Mnafikiri wameanza kutafutana.. ngoja msikie watu wanaanza kuondoka kwa kiharusi!!!
 
Mjadala ambao umewaka sasa hapa na kila kona umepelekea mtoto wa Rais kutamka haya maneno .Nimeogopa sana kwa kweli baada ya kupatia mail hii na rafiki yangu mmoja . Nikaona nije hapa niwape hili nanyi mseme . Maana Tanzania ni yetu sote .Maneno yake hapo hapo chini .

On 1/23/07, S.B. Mkapa
Waste of time and money! How can one hujumu uchumi when what he is accused of swindling money from is still erect? I suggest they sell the building and make up for the difference. It would be a windfall! Biashara za kufurahisha donors hazina sera. Maandamano yanakuja!

A hungry stomach makes a poor political adviser!

I beg to differ with your analysis. Nobody has any proof that the radar was bought under dubious circumstances! Tuacheni ushabiki! If somebody made $12mil as a facilitator we should not blame anyone other than our own ignorance/stupidity for agreeing to the transaction in the first place.

We do not need SFO to tell us how dumb we are. The opposition marching just glamorizes the whole episode. Unafiki mtupu
!

Ninaomba na nyie mseme lenu kuhusiana na matamshi mazito maana mimi sina la kusema
 
Lyungu
hebu niweke waki kidogo

hiii ni email kati ya mtoto wa Rasi MKAPA na nani?
 
DrWho haya ni maongezi kwenye maongezi ya Rada na Kesi ya Mahalu kwa wanachama wa tanzanet sasa kuna jamaa najuana naye kanitumia majibu ya huyu kijana kwa wenzake wa kule .Mimi kwa kuwa si mwanachama huko basi nikaleta hapa ambapo mimi naweza kusikika .Haya ni majibu akitetea the whole episode yaani Rada na Nyumba Italia .
 
Kusema kweli hata simwelewi kabisa maanake anadai nyumba iuzwe turudishe fedha.. Nyumba gharama yake ni paundi za kiingereza 1.3/m na imenunuliwa kwa bei mara mbili na nusu ya gharama yake zaidi ya poundi 3/m hapa tutauza hiyo nyumba kurudisha gharama zipi?.

Pia swala la rada siji anaposema:- we should not blame anyone other than our own ignorance/stupidity for agreeing to the transaction in the first place.
Sielewi utajilaumu vipi kwa upoteaji wa USd 12/m ikiwa hakuna dubious circumstances ktk ununuzi.
Blame comes with Accountability
 
Mkandara nimesema nimeogopa baada ya kuona statement ya Mtanzania huyu .Yaani anadhani tunapoteza muda na anadhani uchunguzi ni haramu na sisi kusimama kidete ni punguani . Nataka ulingalishe hizi kauli na kauli za rais aliyepita hapo utaamini kwamba maji lazima yafuate mkondo maana hayawezi kuupanda Mlima. Nimeumia sana
 
Lunyungu,

Huyo kijana miaka na miaka ndivyo anavyoandika na kutukana.

Ni mtetezi wa sera za babake na anaona Watanzania wanaokosoa uongozi BWM kama wana njaa na ndio inawasumbua.

Mara nyingi akikutana na hoja nzito huwa anakimbia. Hawezi kuja hapa
kwenye JamboForum maana anaweza kukimbia baada ya siku moja.
 
Back
Top Bottom