The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Yebo Yebo, jambo moja ambalo mimi sijalielewa ni huu uchunguzi wa SFO unatuhusu nini sisi? Uchunguzi wa SFO ni kwa manufaa ya Serikali ya Uingereza na hahusiani hata chembe na maslahi yetu sisi kama Taifa au wanunuzi!

Ni kwa sababu hiyo sioni kwanini viongozi wetu wasilingumzie jambo hili kwani Waingereza wenyewe wanalizungumzia, na uchunguzi wa SFO hautuzuii sisi kuanzisha uchunguzi wetu wenyewe. Wao wanaangalia kama BAE ilimlipa dalali Dola milioni 12 na kwa kufanya hivyo basi kuvunja sheria. Sisi uchunguzi wetu uwe ni

a. Ni kwa nini tulihitaji rada hii? Je tulikuwa na tishio gani la kijeshi lililolazimisha kununuliwa rada hii?
b. Kwa nini ilitugharimu kiasi hiki bilioni 50 wakati tungeweza kununua rada mpya kwa bei robo ya hiyo?
c. Ni nani aliyetetea ununuaji wa rada hii na mtu huyo amenufaika vipi?
d. Je, Serikali ya Tanzania imlipa dalali huyo pia na kama ilimlipa ni kiasi gani?
e. Ni mafanikio gani ya kimapato na kiutalii ambayo tumeyapata kwa kutumia rada hii?
f. Kama rada hii inaangalia theluthi moja tu ya nchi je hizo theluthi mbili zinaangaliwa na vyombo gani, na serikali itanunua rada nyingine mbili ili kukamilisha ulinzi wa anga?
g. Je bwana Vithlani amemlipa Mtu yeyote kutoka katika serikali ya Tanzania kwa kumpatia na kumwezesha dili hilo la BAE, na mtu huyo ni nani au ni akina nani?
h. Je sheria yoyote ya matumizi ya fedha za serikali imevunjwa?


NB:

Jamani nipeni hadi Jumatano, nitadraft kitu kama hicho sijui tutaiita barua au nini.. halafu tutaona tutakapofikia...
 
Wanabodi,

Kwa wataalam wa hizi e-mail... je, kuna uwezekano wa hizi e-mail pamoja na sahihi zake kwenda bunge la Uingereza?..
navyofikiria mimi upelelezi wa bunge lao unaweza kuchukua mkondo mwingine (dhidi ya Blair) ikiwa wananchi wa Tanzania kwa wingi wataliomba Bunge lao. Pia hao conservative watalipigia debe kwa sababu za kisiasa na hasa kumwangusha Blair kiasi kwamba swala hili litakuwa wazi zaidi kwetu. Uingereza wanaweza kabisa kutupa picha nzima ya uuzaji wa rada hii ikiwa uchunguzi utafikia kuwapa kibano BAE na pengine hawa jamaa watawataja wahusika wote. hadi sasa swala zima linaendeshwa kwa maslahi ya Uingereza lakini upo uwezekano wa bunge lao kuchukua mkondo mwingine.
Vyama vya Upinzani pia wanaweza kuungana pamoja na kuyaweka malalamiko yao kudai kama tutakavyofanya sisi. Tusitegemee ukweli kutoka TZ maanake kimila chetu kinasema huwezi kumwita mwizi ndugu yako kumtakia kifungo - hiyo ni roho mbaya!
 
Kwa nini sisi wenyewe Tanzania tusimpe kibano huyo middleman? Unafikiria yeye anapenda kuishi ulaya? Huyo ndio mwenye data zote akipewa kibano atasema kila kitu.
 
Kwa nini sisi wenyewe Tanzania tusimpe kibano huyo middleman? Unafikiria yeye anapenda kuishi ulaya? Huyo ndio mwenye data zote akipewa kibano atasema kila kitu.


I take the above as a joke but just know...Street justice doesn't apply in international business.
 
Yebo Yebo, jambo moja ambalo mimi sijalielewa ni huu uchunguzi wa SFO unatuhusu nini sisi? Uchunguzi wa SFO ni kwa manufaa ya Serikali ya Uingereza na hahusiani hata chembe na maslahi yetu sisi kama Taifa au wanunuzi!

MJJ

Bob hapo juu amejibu karibu sana na mtazamo wangu, e-mail kwa vyama vya upinzani kama Consev na Lib Dems zinaweza kuzaa matunda na pia kwenye bunge la UK. Basically, naunga mkono mbinu yoyote itakayoleta matunda...pia naona kwenye hiyo e-mail tuijumuishe pia Sky News, BBC, ITV, Channel 4 etc.
 
Kwenye website ya Waziri Mkuu wa Uingereza kuna mahali mtu anaweza kuanzisha petition na watu wakasaini petition hiyo. Hata hivyo kuna condition mbili aidha uwe ni Muingereza au Unaishi Uingereza kufanya hivyo. Ningekuwa UK ningeanzisha petition hiyo. Je kuna mtu yeyote aliyeko huko anayeweza kucreate petition na kutupa link watu tukaanza kumwaga sahihi!!?
 
naona humu ndani kuna tatizo la wenye kuijua fitna..petition ikienda kwa blair msidhani kutakuwa na tofauti

Fitna lakini kama mnaitaka lazima kuwepo kwa taarifa kamili na kama kuna mtu ana access ya hiyo deal then mtakuwa na mwanzo mzuri kwani mjue kuwa hakuna binadamu wabishi kama wazungu na kama mnashitaki kwao basi lazime ziwepo documents za kusupport hiyo petition na pili kuwepo kwa pressure kule Bongo kuanzia WORLD BANK mpaka USAID(UBALOZI WA AMERICA) kwani hao ndio wenye kutoa pesa zao kisha baada ya hapo mtazameni msemaje wa serikali ya Tanzania ambaye hatumjui atakavyo bwabwaja

Nadhani kuna umuhimu wa kuwa na details za kutosha kabla ya kuanza na hii petition ama sivyo mtachemsha
 
Wakati tukiendelea na Mjadala huu, nakuombeni wenzangu mnaokaa nje na hasa wale wenye uraia nje sote tujiunge na wenzetu kuweka sahihi zetu za kuunga hii petition ya Uraia wa nchi mbili..
http://www.tanzaniacyberzone.com/Petition/default.asp.. Shukran.

Kisha kuna hawa jamaa wa UN kitengo cha sheria sijui pia kama wanaweza kuwa na msaada ktk swala letu hili kama walivyotumia hawa cyberzone.. site yao ni hii hapa:-
http://www.un.org/law/ilc/index.htm
 
Majira nao wamekuja na habari hii leo...

Marekani kuchunguza kampuni iliyouza rada

*Yadaiwa kuwahonga maofisa wa nchi nyingine kwa staili mpya
*Walilipiwa hoteli, malazi na usafiri wakiwa 'peponi' Marekani
*Mtu wa kati aliyehusika akiri, kuanika mambo yote hadharani

Na Mwandishi Wetu

WAKATI mkataba wa kuiuzia Tanzania rada ukiendelea kuchunguzwa kwa tuhuma za rushwa, kampuni ya Uingereza ya BAE Systems, huenda ikaingia kwenye matatizo mengine, safari hii ikichunguzwa na Serikali ya Marekani, ikidaiwa kufanya vitendo vya rushwa nchini humo.

Katika sakata hilo jipya, gazeti la Majira limebaini kuwa kampuni hiyo inahusishwa na vitendo vyenye utata vinavyodaiwa kufanyika Marekani wakati wa mchakato wa kuingia mkataba na Serikali ya Saudi Arabia, ambao ulifanikishwa mwaka 2002.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, gazeti la The Daily Telegraph la Uingereza, lilieleza kuwa kuna taarifa za awali zinazoonesha kuwa kampuni ya BAE iliwalipia, maofisa kadhaa wa Serikali ya Saudi Arabia, gharama za hoteli, malazi na usafiri wakiwa Marekani, kitendo kinachohusishwa na rushwa, ili kuchagiza mkataba ambao ulifikiwa mwaka mmoja baadaye.

Gazeti hilo lilisema baadhi ya waendesha mashitaka Marekani tayari wameonesha shauku ya kutaka kuichunguza kampuni hiyo kutokana na tuhuma hizo.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hilo umeonesha kuwa tayari kikao kati ya maofisa wa uchunguzi wa Marekani na wenzao wa Uingereza, kutoka Kitengo Maalumu cha Kuchunguza Makosa ya Ulaghai (SFO), walishakutana mwaka jana.

Marekani ina uwezo kisheria wa kuichunguza kampuni hiyo ya Kiingereza kupitia sheria yake iitwayo " Foreign and Corrupt Practices Act."

Uchunguzi zaidi uliopatikana Uingereza unaonesha kwamba huenda wiki hii kwa kuanzia, Baraza la Congress la Marekani, likawaita maofisa wa BAE Systems na kuwahoji.

Mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo, alikaririwa na The Daily Telegraph akisema uwezekano wa maofisa hao kuhojiwa ni "asilimia 60." Mahojiano hayo yatafanywa na Kamati ya Masuala ya Huduma za Silaha ya Bunge hilo.

Kuna ushahidi mzito unaotilia shaka mwenendo wa kampuni hiyo na jinsi ilivyowakirimu maofisa hao wa Saudia.

Ushahidi uliopo mpaka sasa, lilisema The Daily Telegraph, unaonesha BAE iliwalipia maofisa wa Saudia gharama za hoteli, usalama na gharama nyingine kwa kipindi cha miezi sita, gharama zinazofikia, kwa wakati huo, pauni milioni 4. BAE ndiyo iliyolipia gharama hizo kupitia wakala maalumu.

Miongoni mwa malipo hayo yanayodaiwa kufanywa zimo pauni 130,000 zilizotumika kwa ajili ya usalama Julai, 2001 mjini Los Angeles na kiasi kingine cha pauni 257,000 kilichotumika Agosti, huku pauni 150,000 zikitumika kama gharama kwenye hoteli ya Beverly Hills Hilton. Ushahidi unaonesha gharama hizo zililipwa na BAE kupitia kampuni iitwayo Travellers World.

Ushahidi huo unaonesha gharama za aina mbalimbali na matumizi ambayo maofisa hao walizitumia wakiwa katika miji kadhaa ukiwamo Washington,D.C., ambazo zote zililipwa kupitia akaunti ya Travellers World na hati za malipo zilisomeka: "Gharama za malazi na huduma kwa ajili ya wageni maalumu."

Inadaiwa katika malipo hayo, mtu wa kati, alikuwa akitumika kuhakikisha kwamba risiti zote zilikuwa zikirejeshwa makao makuu ya BAE Systems.

Bw. Peter Gardiner, ambaye alipata kuwa mmoja wa waendeshaji wa kampuni ya Travellers World, alikiri kuwa malipo hayo yalikuwa yakifanyika kwa miaka kadhaa kabla ya kukoma, mara baada ya BAE kuingia mkataba mwingine Marekani.

" [Yule mtu wa kati] aliniarifu kuwa kuna mabadiliko yangefanyika, na hasa baada ya BAE kuingia mkataba na kampuni ya kimarekani ambao uliwataka wakurugenzi wa kampuni hiyo (BAE) kutojihusisha na shughuli zozote za chini kwa chini," alisema.

Bw. Alexandra Wrage, Rais wa taasisi ya Trace International ya Marekani, inayojihusisha na masuala ya kupinga rushwa, alipohojiwa alisema: "Hakuna sababu inayoweza kuifanya Idara ya Uchunguzi (ya Marekani) kutohoji juu ya suala hilo. Hilo limo ndani ya Sheria ya Kupambana na Rushwa ya Kampuni za Kigeni."

Kwa mujibu wa sheria hiyo ya Marekani, yeyote atakayepatikana na hatia anaweza kufungwa jela miaka mitano.

Kutokana na uchunguzi huo mpya, kampuni ya BAE imejibu kwa kusema: "Kampuni imeshangazwa na namna vyombo vya habari vinavyoyashughulikia kwa juhudi kuu masuala ambayo hayana msingi na hayana ushahidi."

Vyanzo kutoka ndani ya kampuni hiyo vinasema viongozi wa BAE hawaamini kama kweli Marekani inaweza kuzichukulia taarifa hizo kwa kuamua kufanya uchunguzi.

Mtendaji Mkuu wa BAE Systems, Bw. Mike Turner, anaonekana kujiamini na kusisitiza: "Kampuni yake iko tayari kutoa ushirikiano wote," kinasema chanzo kimoja.

Msemaji wa ubalozi wa Saudi Arabia, alikataa kuzungumza chochote kuhusu kadhia hilo na akawataka waandishi wakarejee taarifa ya awali iliyotolewa mwezi uliopita na Prince Mohammed bin Nawaf, Balozi wa nchi hiyo Uingereza.

Katika taarifa hiyo, Balozi alikaririwa akisema: "Ningependa kuweka bayana, kwamba Serikali ya Saudi Arabia haikubaliani na vitendo vyovyote vya rushwa au urasimu wa aina yoyote na itachukua hatua kali dhidi ya wote watakaokutwa na hatia ya kuhusika katika suala hilo kwa kupokea rushwa..."

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Tony Blair, amekwishasimamisha uchunguzi dhidi ya BAE kuhusiana na suala hilo la Saudi Arabia akisema hilo lingeathiri uhusiano mwema kati ya nchi hizo mbili.

Uchunguzi wa kampuni hiyo wa kuhusika na vitendo vya rushwa katika mkataba wa kuiuzia Serikali ya Tanzania rada, bado unaendelea, ingawa kumekuwa na wasiwasi kwamba huenda nao ukasimamishwa kwa sababu zile zile za kidiplomasia na kiusalama.

Hilo hata baadhi ya wabunge wa Uingereza walilihoji na Bw. Blair akakwepa kujibu.
 
Mimi siaminio katika Duo na ni matumaini yangu kwamba Serikali haitaingia kichwa kichwa kulete mambo ya u DUAL we need no DUAL .
 
Penye wengi haliharibiki neno, hii strategy ya kulianzisha nje ya nchi italipa cha msingi ni kuangalia modality ambayo itasaidia mkakati wetu kufanikiwa, kwani tukisema tupeleke waraka huu bunge letu itakuwa ni kazi bure

Nini kifanyike

1. UK kuna wabunge wanojua kupiga kelele, zitafute personal contacts kisha wapewe data, kwa kuwa wanamtandao mkubwa wanaweza kufukua zaidi kuwapa kibano hawa watawala wetu.

2. Zitafutwe contact za waandishi wa habari wa nje mahiri katika habari za africa tuwapigie kelele watusaidie, wakiandika mara mbili tatu ni kibano tosha kuwanyoosha watawale.

naomba kutoa haoja
 
Mgumu unaongelea Rada ama Dual maana kuna mchanganyiko wa mada sasa .Sijui hata DUAL imekujaje hapa . Hebu fafanua unaongelea nini Mzee Mgumu
 
Lunyungu,
Mshikaji inaonyesha wewe una kimeo fulani hapa...
sasa hawa watu wanaoishi nje mbona huwaulizi kwa nini wanachangia mada hizi!..Kwa uchungu gani waliokuwa nao ikiwa wao sio Watanzania?
Mshikaji unashindwa kuunganisha vitu na kufahamu kuwa hiyo dual inahusiana sana na wakazi wa Uingereza na ndiyo inayowapeni nyie nafasi ya kuweka sahihi ktk hiyo petition yenu ya Uingereza!.

Jamani nyie wabongo ama kweli roho za kikorosho haziwaishi.. Mimi nakuuliza wewe hapo!...
Una haki gani ya kuwa Mtanzania kuliko sisi hapa! Kama sio sheria mbovu za kidikteta hizo ambazo tunapingana nazo humu kuziondoa.
 
nadhanini muhimu kusubiri kujua matokeo ya uchunguzi wa SFO otherwise watu watachemsha na kama nilivyosema ni muhimu muwe na DATA za kutosha kussuport arguments

Upande wangu naona kuna GAPS nyingi tuu katika hili na hii inatokana na ukweli kuwa hakuna mwenye enough details na naweza kurepost tena maswali niliyo muuliza bwana Mwanakijiji

nitarepost after couple of minutes
 
@Mwanakijiji

nimefurahi kuona kuwa umetimiza ahadi yako ya kuwa utarudi humu siku ya AL-KHAMIS kuja kuweka mambo sawa na nafurahi kwa hili lakini pia ningependa kusema kuwa pamoja na kukubaliana nawe lakini nadhani kuba baadhi ya hoja ambazo itabidi nikujibu
HOJA NUMBER1

Hii nakubaliana nayo na sishangai kuwa haya yanatokea kwani kuna mambo mengi tuu ambayo wanasiasa na maofisa wa serikali walifanya maamuzi bila kufikiria maslahi ya Taifa au wananchi hivyo uko right katika hili...lakini sio sababu ya kurudia kosa

HOJA NUMBER 2

Serikali ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuita wachunguzi toka nje kitakuwa ni cha kushangaza kwani tunavyo vyombo vya kufanya kazi hiyo na kama vikipewa nafasi na uhuru huo vitafanya kazi yake sasa kuwaita Scotland Yard kuchunguza rushwa kwetu n aibu na inaonyesha jinsi gani ambavyo hatujiamini na hiii pia itazua kitu kinaitwa CONFLICT OF INTEREST baina ya yetu na Serikali ya UK.

Walio husika ni wahindi wenye uraia wa Uingereza na hakuna sheria inayowakataza kufungua off shore acounts be it in Swiss au Dominica republic hivyo itakuwa tunatafuta mchawi na kuwalaumu hao wahindi bure wakati wao wamekuja kutafuta dili na wakalipata sasahizi hoja zingine zinakuwa tu kuwa wanaojiita watoto wa mjini walikuwa wapi mpaka wakapigwa bao na wadosi?

Umezungumzia kuwa wahusika walikuwa akina nani ambao walishawishi serikali kununua hiyo RADA na walinufaika vipi? of course washawishi wanatoka sehemu mbali mbali Wizara ya ULINZI,wizara ya MIPANGO, wizara ya MAWASIALIANO, wizara ya FEDHA, IDARA YA ANGA a hawa matokeo yake wanapleka proposals zao kwa hao waheshimiwa then hapo ndipo wataamua kama pesa zipo basi wago ahead sasa kama unataka kujua hii inafanyika vipi then kuna umuhimu ukaelewa kwa nini wengine tunapigania TRANSARENCY KATIKA TENDA kwani bila hivyo ni ngumu hata kujua kuwa akina nani walikuwa shortlisted na kama BAE SYSTEMS walipewa je walipewa baada ya kuwashinda akina nani katika bidding? Je bwana MKJJ hili ulilinvestigate? na kama ungejaribu kulivutia muda then ungejua kwa nini waliamua kununua rada ambayo haitoshi thuluthi moja ya nchi kama ulivyosema na maybe ungeelewa kuwa cost ya kuimaintain hiyo RADA katika hiyo AFTER SALES SERVICE cost angezichukua nani na kwa estimates zipi?


HOJA C


Bwana MKJJ umtoa hoja kuwa serikali ya UK imonitor akaunti za Bwana Vilathni na Somaiya ili kujua kama kuna malipo yaliyofanyika kwa mtu yeyote mwingine na hususan afisa au kiongozi wa serikali ya Tanzania.

Sasa kwanza lazima uelewe jinsi gani mambo haya yalivyo kuwa complicated na hii inachangiwa zaidi ya mfumo wa banking huku UK na Europe kwa ujumla na hata kama kutakuwa na payments zimeonekana zilifanyika kisheria hao wahindi hawawezi kueleza mengi kwani kwanza hao Barclays bank wanaendeshwa na pesa nyingi za HARAM toka katika rogue states kama MYAMAR au BURMA,IRAN,ZIMBABWE na zinginezo na kwa taarifa tu ni kuwa hili hata ahao ma financial regulators hapa UK (FSA) hawezi kuligusa kwani punde wakiaanza tu basi ujue kuwa unaweza kuangusha serikali nzima ya UK ambayo of course imejaa wala rushwa kuanzia house of Lords mpaka huko Whitehall na kama huamini basi tazama kesi ya CASH FOR PEERAGE

pilikuna ma lawyer wako stand bay kuwalinda hawa jamaa ambao kusema ukweli ni kuwa hakuna kitu kitakachopatikana kwani pesa zitakuwa zimeshaingizwa either kwenye TRUST au STOCK MARKET AU KWENYE HEDGE FUNDS ambayo imewatajirisha jamaa wengi huko THE CITY na ndio maana WEALTH MANAGEMENT corporations kama GOLDMAN SACHS,MERRYLL LYNCH,CREDIT SUISSE FIRST BOSTON,BARCLAYS GLOBAL INVESTORS,LEGG MASON, JP MORGAN ASSET MANAGEMENT na kadhalika ...hao ni wajanja wa kuzificha pesa na ndio wanao lipia campaigns za akina BLAIR na LABOUR.....hivyo hiyo haiwezi peke yake kujenga hoja za kuwa akaunti ichunguzwe kaama wakithubutu kuanza hiyo witch hunt basi waingereza yatawakuta yaliyowakuta waamerika baada ya kuanza kunusa akaunti za WASAUDI matokeo yake waarabu waliamua kufanya Capital flight from USA to UK and CHINA na si kwamba wazungu wahawalijui hilo..wanalijua sana na ndio hiyo hiyo pesa ambazo zinaendesha uchumi wa nchi hizi

Vile vile usisahau kuwa serikali ya Tanzania hawawezi kuinchunguza BAE SYSTEM kwani kazi hiyo wanaifanya FSO ambao kama wakiwa na la zaidi then wanaweza kuwa SUMMON watuhumiwa kujibu mashitaka. Hilo la kutaka kuchunguza akaunti za watu mjomba nalo litakuwa ngumu kwani huku ulaya kuna suala zima la CONFIDENTIALITY na BANKING CODE na hii ndio mpaka leo waNIGERIA wameshindwa kupata pesa zote alizoziiba SANI ABACHA na waSWISI waliamua kuwapa hao WANIGERIA DOLA BILIONI MOJA kati ya dola zaidi ya bilioni 4 aliziiiba

Kwa hiyo ndugu yangu hiyo ni uphill task na itacheleweshwa na LAWYERS ambao wao they make a living out of kuchelesha mambo kama haya na sasa hebu niambie utaanza wapi na utamalizia wapi?Mfano mdogo ni kuwa Kampuni kubwa za law firm kama SKADDEN,ARPS,SLATEMEAGHER& LOM LLP & ASSOCIATES au CLIFFORD CHANCE unafikiri kinachowaaweka mjini ni kucheza na sheria na wanaweza kuzungusha hao mpaka kiama na ndio hao washaui wa hao ma middle men ambao unataka wahojiwe kwa hiyo huo ni mwamba

umewataja OBVIOUS viongozi lakini vile vile naweza kukujibu maswali yako kama ifuatavyo:


1.Rais Benjamin William Mkapa ambaye chini ya uongozi wake rada hii ilinunuliwa.

Lakini huoni kama kumshitaki Mkapa kama ni kutafuta scapegoat? kwani ukimpandisha BM kizimbani it means that TONI BLAIR also has to be there with BM but like the other loans for honours(or CHASH FOR PEERAGES) 'scandal', one major fly in the ointment; Blair was/is a lawyer. It's unlikely he'll ever be caught bang to rights on this kind of thing. And even so, he has a rather more serious crime to answer for, which is also unlikely ever to come to charges. it's not his sticky paws that are the issue, it's his paw print. Is he really directly culpable in this case, as he was a lawyer I'd be surprised if he didn't leave himself wiggle room which is opposite to our dear Mheshimiwa BENJAMIN WILLIAM MKPA who is a JOURNALIST by profession unless sijui kitokee nini but its a win win situation for BLAIR but not for MKAPA




2.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa wakati huo na Rais wa sasa Bw. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alitetea ununuzi wa rada hiyo. Na hata jana ametetea.


Hoja hii inajibiwa kuwa JK naye kwa taarfa yako alikuwa anafuata tu instructions toka kwa wakubwa zake akama ambavyo CLARE SHORT baadae ilibdi akubali matokeo na majibu ya JK juzi ni sawa kwa sababu hao jamaa wa FSO washampa njia nzuri ya kutokea kwa kusema kuwa uchunguzi bado unaendelea na kwa kweli angeropoka basi kama kuna kesi ya kujibu BAE SYSTEMS wangedai kuwa JK karopoka hivyo hawawezi kupata FAIR TRIAL...and this includes HAO WAHINDI akina SOMAIYA


3.Mwanasheria Mkuu wa Wakati huo Bw. Andrew John Chenge ambaye ni Waziri wa Miundo Mbinu wa sasa ambaye ofisi yake ilisimamia mkataba kati ya serikali na Bw. Saileth Vithlani


Hoja hii haikataliwi lakini ukumbuke kuwa naye anapelekewa recomendation toka wizara ya FEDHA na MIPANGO ambao kuishi kwao kunatokana na WORLD BANK..NA KAMA KWELI BWANA MWANA KIJIJI UNGETAKA KUJUA ZAIDI BASI NADHANI investigation yako ingelenga huko WORLD BANK ..ambao wanaofisi DAR na hapo WASHINGTON...lakini hili nalo waandishi wetu huko Dar wangemuuliza huyo rais wa WORLD BANK bwana Paul Wolfowitz ...amabye anahamu sana wanafunzi tanzania wawe na first class eductaion




and maybe we should have gone back to SQUARE 1

And the OBVIOUS QUESTIONS you should have asked is WHERE DID WE GET THE MONEY TO BUY THIS EQUIPMENT?



ASSUMPTIONS:


Now who are the donors/contributors of the aid money? Is it govts in the west or is it charitable organisations? If the latter there some political bargain/wrangling could result in Blair escaping personally unscathed. If the latter, they are duty-bound and presumably required by their own charter/constitution to persue the money or in other words kuchelewesha haki na hapo tena Ma-lawyer wataingia kuanza kuidadua constitution ambayo nadhani unaelewa kuwa iko pungufu

Now kwa upande wa BAE SYSTEMS...I see that it's small fry for them so it won't be the end of the world for them if they had to cough up the dough. But then they are duty-bound to their shareholders that they contest any claims of that nature.....UPO HAPO MWANA KIJIJI?

fURTHERMORE, The World Bank is involved, apparently. Isn't Wolfowitz very convenient its president these days? Now that's an old friend of Bush/Blair....




4.Prof. Mark Mwandosya aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi ambaye sasa ni Waziri wa Mazingira.

Huyu labda hii kwake isngekuwa na nguvu zaidi kwani naye anapata directions toka juu..unless unataka kumuuliza kuhusu hiyo project yake ya uwanja mpya wa ndege


5.Maafisa (wanasheria na washauri) wa Wizara husika ambao walihusika na mikataba hiyo.


SASA HAPA MWANAKIJIJI UMENENA lakini kama na yeye alikuwa anapewa DIRECTIVES ?

6.Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa wakati huo kwani rada hiyo ni ya matumizi ya kijeshi zaidi kuliko ya kiraia.

Kuna umuhimu walipa kodi wakajua KODI zao hawa wanajeshi wanazituia vipi na PROCUREMENTS ZA JESHINI ZINAENDAJE ....

7.Maafisa na Wanasheria waliohusika katika majadiliano hayo. Na hasa kama ni maofisa hao hao walioshiriki katima manunuzi ya Ndege ya Rais, Helikopta za Bell na Malori ya kijeshi.

hOJA HII inaendana zaidi na majibu yaliopo hapo juu


HOJA D

JK nilimshajibia na yeye alikuwa anasema hayo aliyo ambiwa na wakubwa zake yaani MKAPA ambaye alikuwa hawezi kupindua kwa BLAIR so its kesi ya kujaza maji kwenye gunia ....labda ungeuliza ule mkataba tuliosaini na waamerika kutumia anga ya Tanzania small print zake zinasemaje na so far umemnufaisha nani?

HOJA E

hii nilishakujibu kutumia mfano wa NIGERIA wanaohaha kuhusu pesa zilizoibiwa na ABACHA USWISI na nadhani unajua kuwa ISSUE ILIOPO hapa ni nani atapata WIGGLE ROOM...nadhani unajua kuwa post ENRON & KEN LAY maybe we as Tanzanians we can be a bit optimistic of a successful trial of corporate frauds..only in the west.... Incidentally, Ken Lay's death has now resulted in his conviction being set aside:

http://tinyurl.com/y9tpb5

Blair and Mkapa can always escape with a heart attack
 
DrWho, nashukuru kwa majibu yako hata hivyo maswali yangu bado yanabakia:

- Kwanini Tanzania iliamua kununua rada hii ya matumizi ya kijeshi na kiraia?

- Ni tishio gani la anga ambalo lililazimisha serikali kung'ang'ania lazima iwe ni rada hii? Ni nchi gani iliyotupa tishio hilo na kwanini Watanzania hawakuambiwa kuwa tunatishiwa kijeshi!?

- Ni kwanini rada hiyo imegharimu Dola milioni 40 wakati kuna mabenki na wafadhili wengine ambao walikuwa tayari kutusaidia kupata rada ya kiraia, ya kisasa na ambayo ingetupa usalama wa anga kwa bei ya robo ya hiyo?

- Katika ununuzi unaomhusisha dalali, dalali hulipwa aidha na mnunuzi au na muuzaji. Hadi hivi sasa dalali amekiri kupokea malipo ya dola milioni 12 toka kwa muuzaji. Je mnunuzi (Tanzania) alimlipa dalali huyo malipo yoyote, kiasi gani, na nje ya hizo Dola milioni 40?

- Je, kuna ofisa yeyote wa Tanzania ambaye amepokea malipo toka kwa dalali huyo nje ya nchi na maofisa waliohusika na ununuzi wako tayari serikali iwatake waidhinishe akaunti zao nje ya nchi zichunguzwe kujua pesa walizonazo humo zimetoka wapi?

- Wakati wa ununuzi wa rada hii aliyekuwa Waziri waa Mambo ya nchi za nje alitetea kwa kusema kuwa tunahitaji rada hii kwani itatuongezea mapato na kuongeza utalii. Je tangu rada hii inunuliwe ni kiasi gani kimekusanywa kwa sababu ya rada hii (tukikusanya mapato toka nchi zinazopita katika anga letu). Je ni watalii kiasi gani ambao wameongezeka sababu ya matumizi ya rada hii?

- Lengo la rada hii tuliambiwa na Rais Mkapa ni kuongeza usalama wa anga. Je kabla ya kununuliwa kwa rada hii ni ajali ngapi zimetokea au nusura kutokea angani, na kununuliwa kwake kumepunguza ajali hizo kwa kiasi gani?

- Rada hii tuliyoinunua ina uwezo wa kuangali theluthi moja tu ya nchi na hususan viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere na kile cha KIA. Ili kuweka ulinzi na usalama kwa nchi nzima tunahitaji rada nyingine mbili zenye uwezo kama huo. Je tuko tayari kununua rada nyingine kwa gharama hiyo hiyo kila moja ili kutimiza lengo la kuilinda anga letu na kutupa usalama? Tuko tayari kutumia dola milioni 80 kufanya hivyo?

- Kuna uhusiano gani kati ya kununua ndege ya Rais kwa karibu kiasi hicho hicho cha rada na kumtumia dalali yule yule, dalali ambaye anafanya biashara ya silaha na serikali yetu kwa muda mrefu? Ni nani anampa dili hizo dalali huyo na mtu huyo ananufaishwa vipi?

- Kama tumeweza kumfikisha mahakama Balozi kwa kughushi na kutumia vibaya nafasi yake na kununua nyumba ya ubalozi kwa bei ya chini wakati akitoa stakabadhi za kuonesha bei ya juu, ni kwanini hatufikiri kuwa kuna mtu katika serikali ambaye inawezekana kabisa amefanya jambo hilo kwenye rada? Mtu huyo ni nani?

- Uchunguzi wa SFO ni kwa ajili ya serikali ya Uingereza. Uchunguzi huo hata kidogo hautuzuii sisi kuanzisha uchunguzi wetu wenyewe. Je serikali iko tayari kufungua uchunguzi huru? Je kuna chombo chochote kinachoweza kuanzisha uchunguzi bila ya kutaka ruhusa kwa Rais?

Hayo ni maswali yangu na ya Watanzania wengine wengi.
 
capt.nai10501231404.tanzania_weapons_destroyed_nai105.jpg

A member of the Tanzanian police stacks confiscated weapons before they were set alight, Tuesday, Jan. 23, 2007 at the Lake Tanganyika stadium in Kigoma, 1,000 kilometers west of Dar es Salaam.

capt.nai10401231402.tanzania_weapons_destroyed_nai104.jpg

A member of the Tanzanian police starts a bonfire of confiscated weapons, Tuesday, Jan. 23, 2007 at the Lake Tanganyika stadium in Kigoma.

capt.nai10601231421.tanzania_weapons_destroyed_nai106.jpg

Spectators look on as a bonfire of confiscated weapons burns, Tuesday, Jan. 23, 2007 at the Lake Tanganyika stadium in Kigoma.

capt.nai10701231424.tanzania_weapons_destroyed_nai107.jpg


Wabongo wanatimka baada ya baadhi silaha kulipuka! (Picha zote na AP)

Good Job, Tanzania.. now.. tuliweza kuzikamata silaha hizo huko kigoma kwa msaada wa rada iliyoko Dar?
 
Back
Top Bottom