The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Mzee MMJ unajua kuwa huyu kijana wakati ule baba yake akienda US, na hasa NY na yeye alikuwa akihamia pale Waldorf-Astoria, na kulipiwa Presidential suite, yaaani dola 5,000 per night yeye mdogo wake na kijana wa Magani, rafiki yao, na hakuna mtu wa kuuliza ndio maana ana jeuri,


ila mwambieni asitone wabongo tuko kimya tunakusanya maovu tu iko siku inakuja wote watalipa pale Sanamu Monument, tena itakuwa mchana ili wananchi wote waone kwa macho yao Sadaaam Style, halafu tutarekodi kwenye cell phone mchezo wote!

Hela zetu walipa kodi!, only in bongo! Halafu tutawalipisha risasi zao kama Cuba!
 
Hey guys i am sorry but this topic sacks, and we better spend our time discuss our corrupted country. Its one thing to talk about Mkapa but to end up talking about his son relationship is out of line and personal. Tanzania most bof the time we dont know that much about other people business but we end up assume everything. Unless you have the fact dont be personal, because politicians family members are not fair game for attacks, we are better than that. This guy experience some stuff just like any other Tanzania in his age ... we need to stop focusing on family, personal, and assumptions. Be adviced
 
Mzee heshima yako,

Hatuna tatizo na experience ya maisha ya mtu yoyote, kama ni kweli wabongo wote at his age tuliiiba magari na kutaka ku-rape wanawake wasiotuhusu, and if we did try sisi kina yahe tusingekuwa hapa, yaani freeee!

Anapotuhusu ni pale anapotoa kejeli kwa wananchi, then he becomes a fair game, labda huko aliko hawajui kuchambua wajinga ila hapa kuna tulio-specialize na siasa za nguoni, hatupendi maisha personal ya mtu lakini ukitutukana wananchi then tutakujibu kwa lugha unayoonekana kuielea vizuri,

Mimi sijawahi kuiba gari kwa hiyo hayo maisha sijawahi kuya-experience, hawa watoto kina Steve wanajua kuiba magari maaana ndiyo tabia waliyofundishwa na wazazi wao kutuibia wananchi, samahani kama uko nao ila hapa hatupendi mchezo na mtoto wa mtu yoyote asiyejua kujiheshimu, na hata baba zao tunaweza kuongea siasa na kuingia kwenye ngozi zao ikibidi, ila anapoandika hiyo e-mail hapo juuu ni matusi kwa sisi wote wananchi na tutawajibu bila huruma, lakini samahani mimi siku-experience wizi wa magari, na kuiba za walipa kodi yaani wananchi!

Hiii ndiyo lugha anayoielewa huyo bwana mdogo ambaye unaonekana humfahamu, mimi nilifikiri ataishia kwenye mitaaa na ujinga wake kumbe sasa anataka kuuueneza mpaka kwenye mitandao tupo tunaowajua!
 
Hey guys i am sorry but this topic sacks, and we better spend our time discuss our corrupted country. Its one thing to talk about Mkapa but to end up talking about his son relationship is out of line and personal. Tanzania most bof the time we dont know that much about other people business but we end up assume everything. Unless you have the fact dont be personal, because politicians family members are not fair game for attacks, we are better than that. This guy experience some stuff just like any other Tanzania in his age ... we need to stop focusing on family, personal, and assumptions. Be adviced



one: how about you start working on your grammar and if you cant just post in swahili

two: thread is about former President's son talking some fart while he lives on tax payers money

three: as long as he is a was our former president his life and PERSONAL life will always in public doman and MKAPA's son is not immune
 
one: how about you start working on your grammar and if you cant just post in swahili

two: thread is about former President's son talking some fart while he lives on tax payers money

three: as long as he is a was our former president his life and PERSONAL life will always in public doman and MKAPA's son is not immune

DrWHO, please!
Unamsema mwenzako kwa grammar na wewe umefanya nini? Kwanza hiyo one, two and three ni nini?
"one": hiyo "and" umetumia ya nini? "cant just?" please man. Na kama nimekuelewa vizuri kiswahili hakina "grammar" ndiyo maana umemshauri atumie.
"two": you can not live on "tax payers money" but you can depend on. Note: taxpayers' money NOT tax payers money.
"three": as long as he was president or as long as he is former president na siyo hicho kimatumbi ulichoandika ambacho Mzee Mkandara amekupa tano.

Wote humu tunakosea hii lugha, kama unaamua kumcheka mtu jitahidi kidogo na wewe uwe makini. Hivi hao wafadhili mnaoota watasoma kwenye hii forum wataelewa nini? Mimi nashauri tuendelee na kiswahili chetu tu ili tueleweke.
 
DrWHO, please!
Unamsema mwenzako kwa grammar na wewe umefanya nini? Kwanza hiyo one, two and three ni nini?
"one": hiyo "and" umetumia ya nini? "cant just?" please man. Na kama nimekuelewa vizuri kiswahili hakina "grammar" ndiyo maana umemshauri atumie.
"two": you can not live on "tax payers money" but you can depend on. Note: taxpayers' money NOT tax payers money.
"three": as long as he was president or as long as he is former president na siyo hicho kimatumbi ulichoandika ambacho Mzee Mkandara amekupa tano.

Wote humu tunakosea hii lugha, kama unaamua kumcheka mtu jitahidi kidogo na wewe uwe makini. Hivi hao wafadhili mnaoota watasoma kwenye hii forum wataelewa nini? Mimi nashauri tuendelee na kiswahili chetu tu ili tueleweke.

Sam,
I was contemplating to do the same (asking DrWHO if his grammar looks any better) but thanks for taking care of that.
 
Sam

sam 19th January 2007 08:25 AM

Hivi hizo hesabu zenu mnazitoa wapi.
Serikali ya Tony ilitoa pound 28 mil ambazo ni sawa na US $40 mil.
Tukilipa $40 mil tutakuwa tumelipa mkopo bila riba. Na wao hawatakuwa wamepata faida yoyote.

sam 19th January 2007 09:59 AM

Sasa naona nimeanza kuelewa. Ni kwamba Barclay walitukopesha hela na serikali ya uingereza inatulipia.
Two more questions.
1. Hiyo Interest (4.9%) ni Simple Interest au ni Compound Interest?
2. How much do we have to pay as a country?


Kwenye ununuzi huu wa RADA kuna nchi zingine tatu ambazo wamenunua RADA kama yetu kwa 45% cheaper. Soma BOT Dar kuchunguzwa kwa tuhuma za wizi hapa:


........................The controversial multibillion military radar system, which Tanzania purchased from the UK-based British Aerospace Engineering at $40 million was of the same kind that three other countries bought at 45 per cent less cost.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=16939#post16939
 
kwa hesabu za haraka haraka 45% ya hiyo milioni 40 ni milioni 18! kama ni kweli kuwa nchi nyingine tatu zilinunua rada kama hiyo kwa kiasi hicho, mtu aniambie kwanini sisi tulinunua kwa karibu mara mbili ya bei waliyonunulia wenzetu. Ni sawa na mtu ambaye ametoka huku kijijini akienda pake Kariakoo na kuuziwa radio ya Panasonig (siyo panasonic) kwa shilingi 20,000 wakati mjanja wa Dar anainunua radio hiyo hiyo kwa shilingi 4000! waswahili watasema yaliyomkuta mtu wa Bush ni "kuingizwa mjini!"!!
 
Wabongo jamani!

Mimi narudi kwenye lugha yangu maanake sasa imekuwa swala la uandishi!...
Sam,
kama kweli wewe umeweza kusahihisha makosa huyo mfadhili atashindwa vipi kutoyaona uliyoyaona!..au ndio hiyo cant imekugusa kuwa hapa tunatumia cant language!
Ndugu yangu message imefika.. tusameheane!
Dr.WHO
Bado tano zako!..hakuna mpango wa kubebana hapa.
 
Jamani labda lugha za watu tuwaachie wenyewe, mbona yetu ni safi kwani kuna nini hapa au kuandika hiyo lugha ndio ushujaaa au u-intellectual wenyewe, maana nawaona wazee flani hapa sometimes huja na ung'eng'e mwingine unaouona ni wa kurudia kutoka kwenye magazeti na vitabu, sasa hubaki ninajiuliza kuwa yaaani ni nini?

Halafu mmoja akianza wengine hufuatilia nyuma kama kumbi kumbi, jamani mweeee! yaaani sisi zaramo unajua maana ya yes! Yes! ni Mzungu kala mafenesi, go mwali komtuguvula kumeso kalagha baho, nyie hayeni!

Vijana ushauri wa bure tunajua kuwa hapa hiii forum elimu ndipo alipoanzia na kuishia, basi tuoneeeni huruma waoga wa umende, andikeni lugha yetu, hao wageni kama wanaipenda sana hii forum basi wajitoleee kutafsiri hiii lugha ya kumkoma nyani, kwa kikwao, kilichoifikisha hii forum hapa ilipo ni ni lugha yetu taifa na hasa mawe, unajua mnawaponza watu hapa mpaka siku moja nikaona Mzee wangu JJ, naye kaja na kimombo, jamani aibu jamani vijana tupende lugha yetu aliyotupa Mwalimu, baba wa taifa, ndio huko makazini tukimwage inavyotakiwa lakini hebu tuwape nafasi wananchi waelewe kinachosemwa hapa, unajua nimegundua tatizo kubwa hapa ni kuwa wananchi wengi wachangiaji hawajiamini na hawaelewi urefu wa hii forum na uwezo wake wa kuwafikia na kuwagusa wananchi wa kawaida!

Tujiamini ndugu zangu, sijawahi kuona Kyoma au Nyamgluuu, wakiandika umombo, lakini hebu niambieni jinsi wanavyokuwa na mguso kwa hoja!
 
Jasusi,

Kosa letu ambalo linatufanya tuwe "wajinga" ni kuachilia vitu kienyeji. Lipumba na Mrema wameamua kuandamana (nguvu za soda) badala ya kufuata mkondo wa Sheria (Mahakama au Bunge) kufuatilia suala hili.

Unakumbuka wale Wazenji walimpelekesha Msekwa kiherehere kuhusu Mkataba wa Muungano?

Hilo ndilo lililotakiwa kufanyika hapa na si kukusanya vumbi la Morogoro road.

Ndio hakuja mtu kijijini mwangu kunihoji kama nahitaji Radar, lakini si vijimambo memgni tuu ambavyo vimetokea vikiongozana na tuhuma ambazo twazifungia macho siku ya kupiga kura lakini twawakasirikia wale Wazanzibari wanaodai kuuona maadnishi origino ya muungano na twawaita mafala?

Viongozi wetu na watendaji wameendelea kututumia sisi kama wajinga kujishibisha na kuvurunda. Same is being done by Foreigners. Is is our culture we have given them a proof a thousand times!

Steve mwacheni na mambo yake. Ana uhuru wa kubwabwaja sawa na mimi, Mzee ES, Mkandara na wengine. Yalisemwa mengi sana kuhusu watoto wa Nyerere, yakaja ya akina Abasi Mwinyi, wakapigiwa domo Marehemu Ipi, kesho itakuwa mtoto wa Sam.

Kupakana madongo hata kama kumo, tusiondoke kwenye suala nyeti ambalo ni kujadili hoja na si mtoa hoja!

Nasubiri Galfu Strimu iteguke, niende Rungwe na Rombo kuwakwida Mramba na Mwandosya!
 
Asalam Aleko*
Naomba kama kuna uwezekano tupewe hiyo website ya forum anayotumia huyo mtoto wa MKAPA.
Nimejaribu ku explore kutumia hiyo address ya tanzanet lakini what i found is different-dealing with domains.
 
Mzee Kishoka,

Kwenye hii forum hakuna mwiko, issue zinaendelea kukatwa hatujali mtoto ni wa nani, ila anaposomeshwa nje for 20 years na hela zetu walipa kodi, halafu akarudi na kutoa matusi hayo juuu, basi ni wajibu wetu kumsaidia kufikiri, na ninakuhakikishia kuwa akisoma hii thred hatarudi tena kusema ujinga,

Kitine alipumzishwa kwa sababu ya mkewe bro, ndio siasa, hakuna mipaka wote wanaomhusu mwanasiasa yoyote ni fair game publicly, hakuna mwenye shida na Steve hapa, tatizo ni vitendo na maneno yake, na hao wengine ni wakorofi lakini hawatukani wananchi, hapa amepewa majibu ya ujinga alioutoa na tunasonga mbele, hatutaki lectures zisizoisha, sisi hapa tunajua time na season, lakini hatukimbiiii issue hata siku moja!

Issue sio Steve, ila ni maneno yake na tabia za baba yake, maana zinafanana na the sad thing ni kwamba huyu baba yake aliwahi kuwa rais wetu, na bado wote wanatunzwa kwa hela zetu walipa kodi FULL STOP!
 
*Wamsaka wakala wakidai aliwapunja mgawo
*Washangaa kusikia zilikuwa ni sh. bilioni 12

SAKATA la rushwa katika ununuzi wa rada iliyonunuliwa na Tanzania mwaka 2002 kutoka kampuni ya British Aerospace (BAE Systems) ya Uingereza, limeingia katika sura nyingine baada ya kudaiwa kuwa baadhi ya vigogo waliohusika katika 'dili' hilo sasa wanahaha kumsaka wakala huyo, akidaiwa kuwatapeli.

Mshituko huo umekuja baada ya vigogo hao kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa 'kamisheni' waliyopewa wakati wa kufanikisha ununuzi wa rada hiyo, hailingani na kiwango cha sh. bilioni 12, ambacho wakala aliyekuwa akiwaunganisha alikaririwa kukiri kuzipokea kutoka BAE Systems.

Wakala huyo, aliyeelezwa kuwa karibu na wanasiasa wengi wa Tanzania, alikiri alipohojiwa na wachunguzi kutoka Kitengo Maalumu cha Makosa ya Ulaghai (SFO) cha Uingereza na kula kiapo mbele ya Hakimu wa Tanzania, akithibitisha kupokea fedha hizo ambazo ziliwekwa kwenye akaunti yake binafsi Uswisi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, imedaiwa kuwa wakala huyo tangu alipohojiwa na SFO, amekuwa akisakwa na vigogo hao wakitaka kujua undani halisi wa 'kamisheni' hiyo ya sh. bilioni 12 ya BAE.

Chanzo hicho kimeiambia Majira, kuwa hata hivyo, wakala huyo hayupo nchini kwa sasa.

"Inaelezwa kuwa hata ofisi yake imefungwa, kila watu wanapomuulizia kwa jamaa zake, wanaambiwa amekwenda India," kilisema chanzo chetu na kueleza kuwa ndiyo maana hata ile habari ya gazeti la The Guardian la Uingereza, iliandikwa kwa kuhojiwa rafiki yake, ambaye naye alikubali kuongea huenda kwa sababu wamekorofishana kibiashara.

"Wanahaha kumsaka, inaelekea walichoambulia wakati wa kuchagiza ununuzi si kile wanachokisoma sasa kwenye vyombo vya habari," kilisisitiza chanzo chetu ambacho kinafahamu kwa kina zaidi kuhusu sakata hilo la rada.

Akizungumzia vigogo hao, mpasha habari huyo aliiambia Majira kuwa sakata la rada lilihusisha viongozi wengi na kwa nyakati mbalimbali, kuanzia mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na hata naibu mawaziri, wengi wao wakiwa wastaafu kwa sasa.

"Hawa, hasa huyu ...(anamtaja Waziri mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu), ndiye aliyeshughulikia sana suala la rada na anajua mchakato wote.

"Yeye ndiye hasa aliyeratibu zile hatua muhimu. Sijui kama anaweza kupatikana. Najua hili ni suala nyeti, kila mmoja atakwepa na kukataa kuzungumza," kilisema chanzo hicho.

Kikizungumzia zaidi kuhusu uchunguzi wa SFO, kilisema kuna mambo mengi ambayo mawakala hao wameyaeleza na kukiri mbele ya wachunguzi hao.

Hata hivyo kiliwaasa wadau wote wa maendeleo nchini kuhakikisha kuwa suala la watu kutuhumiwa kuhusika katika rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, linapatiwa majibu sawia.

"Tujue, kwamba wale jamaa kutoka SFO wanachunguza kashfa ya rushwa si kwa faida ya Watanzania. Hata gazeti la The Guardian linaifuatilia sana habari ya rushwa katika rada kwa maslahi ya Waingereza wenyewe.

"Sisi tujiulize, tunachukua hatua gani kusaka ukweli wa viongozi wetu kudaiwa kuhusika katika sakata hilo? Nawaomba tuelekeze nguvu zetu katika hilo kwa sasa," kilisisitiza chanzo hicho.

Jana gazeti hili lilimkariri Mwanasheria Mkuu wa Uingereza, akisisitiza kuwa uchunguzi wa suala hilo nchini Tanzania utaendelea kufanyika kwa nguvu zote.

Rais Jakaya Kikwete ambaye Serikali yake imedhamiria kupambana na vitendo vya rushwa na ubadhirifu unaokwaza maendeleo ya nchi hii, alisisitiza akiwa London, Uingereza hivi karibuni, kuwa Serikali yake inafuatilia kwa karibu uchunguzi dhidi ya sakata hilo na hautaliingilia.

Kuhusishwa kwa viongozi waandamizi katika Serikali ya Tanzania katika mgawo wa 'kamisheni' ya sh. bilioni 12, ni suala ambalo sasa linazidi kuibua mjadala nchini na maoni ya wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani, ni kuwa Serikali ya Tanzania nayo inahitaji kujisafisha katika hilo, kwa kuunda tume huru.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2183
 
Back
Top Bottom