Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Kama kweli mh. rais ana dhamira ya dhati, tengua majina ya ajira hizi.

1. majina hayo yapo elfu 8, sio elfu 13 kama mnavyojitapa.

2. kuna majina yamejrudia. kuna kijana jina lake limejirudia mara 196.

3. Kuna waliomaliza kidato cha nne mwaka jana(2019) lakini wameajiriwa.

4. Kuna mwamba eti kaajiriwa kufundisha basic mathematics, history na kiswahili. Sijui amesoma chuo gani.

Msitufanye hatuna akili, tunajitambua.
 
Acha kuichafua serikali wewe, serikali haiwezi kufanya huo ujinga kama umekosa kwasababu una GPA ndogo acha tuliochaguliwa tukaanze kazi jumanne (1.12.2020)
 
Hawa jamaa wanatengeneza tatizo jingine ndani ya tatizo lililokuwepo la ukosefu wa ajira.
 
acha kuichafua serikali wewe, serikali haiwezi kufanya huo ujinga kama umekosa kwasababu una GPA ndogo acha tuliochaguliwa tukaanze kazi jumanne (1.12.2020)
Kakudanganya nani kigezo kilichotumika ni GPA?
 
kama haujachaguliwa kwaajili ya GPA yako ndogo tulia kabisa, usimgomanishe raisi wetu na wananchi, tena muache kabisa raisi wetu afanye majukumu makubwa ya kuijenga tanzania
Hapana sio GPA wala nini....kama haya majina nayoyaona mitandaoni yametoka kwa viongozi wa umma tena wa taasisi nyeti basi tunasafari ndefu...

Na Rais asipoliangalia hili nitakuwa na mashaka na anayokuwa anahubiri kila siku.

Penye ukweli tuseme....nimeona jina la mtu kurudiwa zaidi ya mara 100.
 
Kusema kweli mapungufu yaliyojitokeza kwenye hizi ajira ni mengi kupita maelezo. Kuna form four leaver wameajiriwa huku wenye sifa na vigezo stahiki wakiachwa. Wengine matokeo yao ya kidato cha nne ni kizungumkuti. Kuna wengine wameajiriwa na umri mkubwa kinyume kabisa na kigezo cha umri wa mwisho kuajiriwa serikalini ambacho ni miaka 45.

Tunaomba mheshimiwa Rais uingilie kati ili mchakato wa kuwapangia walimu vituo vya kazi uanze upya na mapungufu yote yaliyojitokeza yaondolewe.
 
Back
Top Bottom