Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,235
2,000
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ametangaza ajira za walimu 6,949 wa shule za msingi na sekondari pamoja na watumishi wa Afya 2,726

Nafasi hizi ni kujaza nafasi wazi kutokana na vifo, kustaafu, kuacha kazi au kuhamia sekta nyingine. Waombaji wanatakiwa kuomba kupitia tovuti ya tamisemi, ajira.tamisemi.go.tz kuanzia leo tarehe 9-23 mei, 2021

Maelekezo.
 • Maombi ya ajira za UALIMU , yamefunguliwa kuanzia tarehe 2021-05-09 hadi tarehe 2021-05-23
 • Maombi ya ajira za AFYA, yamefunguliwa kuanzia tarehe 2021-05-09 hadi tarehe 2021-05-23
 • Kama ni muombaji mpya bofya kiunganishi cha juu kulia "Jisajili" kuanza kuomba
 • Ingiza namba ya kidato cha Nne ikiwa na mwaka wa kuhitimu kama jina la mtumiaji na uingize nywila yako kuingia ndani ya mfumo.
 • Baada ya kufanikiwa kuingia ndani, tafadhali kamilisha maombi yako kabla ya tarehe ya mwisho
 • Maombi yasiyokamilika hayatafanyiwa kazi
 • Hakikisha kabla ya kutuma maombi umesoma na kuelewa vizuri tangazo lilotolewa
 • Bofya hapa ili ujisajili kwa ajili ya kutuma maombi
Kwa Msaada
Tafadhali piga simu namba : 026-2160210
 

Attachments

 • File size
  433.7 KB
  Views
  46

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
465
1,000
Baada ya serikali kutangaza nafasi za ajira za ualimu na afya,tunaomba tupeane uzoefu wa namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao ,vitu muhimu vinavyoambatanishwa nk

Wadau karibu tupeane uzoefu na Link ya kutuma maombi

Link ya maombi hii hapa(Mfumo wa Maombi ya Ajira)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom