msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Waziri wa nchi, ofisi ya Rais-Tamisemi ameiagiza tume ya utumishi wa walimu 'TSC' kuandaa utaratibu wa kuanza kuajiri walimu kupitia halmashauri kwa niaba ya wizara ya ofisi ya Rais-Tamisemi.
Japo utaratibu wa kuomba hizo ajira bado haujafahamika lakini nadhani maombi yatakuwa yanatumwa moja kwa moja kwenye ofisi za tume ya utumishi wa walimu(TSC) zilizopo kwenye kila wilaya.
Baada ya utaratibu huu kuanza kutumika tutarajie rushwa kuwa moja ya kigezo kwenye upatikanaji wa ajira. Maana yake kama unatokea familia duni sasa sahau kupata ajira ya ualimu.
Najua kwa sasa naweza nisieleweke lakini ukweli ndio huo kwa sababu watumishi wa TSC nao ni binadamu wana ndugu zao. Je, unadhani wataacha kuchomeka ndugu zao wakupe ajira wewe mtu baki?
Tukumbuke kuwa ofisi za TSC zipo kila wilaya kwenye majengo ya halmashauri ambako kuna watendaji na maafisa wa idara mbali mbali na hawa watu wana fanya kazi kwa ukaribu sana. Sasa tuchukulie baada ya ajira kutangazwa, mkurugenzi wa halmashauri achomeke watu wake, DC achomeke watu wake, afisa mipango achomeke watu wake, afisa utumishi achomeke mtu wake, afisa elimu achomeke mtu wake, afisa ardhi achomeke mtu wake, afisa tehama naye achomeke wakwake katika mgawanyo kama huu ajira zitaishia kuwa za watu wa halmashauri na wenye ukaribu na watumishi wa TSC kwahiyo mtoto wa mkulima hatakuwa na nafasi ya kupata ajira tena.
Pia tukumbuke baada ya ajira kurudishwa TSC kuna vigezo vipya vitaibuka moja wapo kitakuwa kigezo cha kujitolea, ufaulu, chuo ulichosoma, umri, jinsia nakadhalika. Kimsingi vigezo hivi vitawekwa kimkakati ili kutengeneza mianya ya rushwa ili kwa yoyote atakayeshindwa kuvitimiza atoe pesa ili apatiwe ajira.
Sasa kwakuwa hili ni jambo la kitaifa na linagusa maslahi ya wananchi naomba kushauri mambo yafuatayo,
1. Namuomba waziri wa Tamisemi, ummy mwalimu asitishe mchakato huu kwani unaenda kutengeneza undugu, kujuana na rushwa kwenye ajira.
2. Nashauri utaratibu unaotumika sasa kuajiri walimu uendelee kama kawaida kwani kwa kiasi fulani umesaidia kupunguza kama sio kuondosha kabisa urasimu kwenye ajira. Na katika hili napendekeza pia utaratibu uliotumika kwenye ajira zilizopita wa kutumia kigezo cha mwaka wa kuhitimu chuo ndio uendelee kwani kuna vijana wamemaliza chuo muda mrefu na wameanza kukata tamaa hata kukosa matumaini kwa serikali yao.
3. Namuomba mheshimiwa Rais mama yetu Samia aliangalie hili kwa uzito wake kwani linaenda kumchonganisha yeye binafsi na serikali anayoiongoza kwa wananchi wake.
4. Namuomba mheshimiwa Rais atafakari upya na kurudisha usimamizi wa masula ya elimu kwenye wizara husika(wizara ya elimu) kwani mapendekezo haya ya waziri ni dalili kwamba TAMISEMI imeanza kuelemewa kutokana na mzigo wa kimajukumu iliyonayo ya kuhudumia sekta nyingi kwa wakati mmoja.
5. Kwakuwa waziri wa Tamisemi, ummy mwalimu alianza vizuri na hapa kati kati ameanza kulega nilikuwa nashauri amwombe mheshimiwa Rais ambadilishie wizara kabla mambo hayajaharibika kwa sababu huku anakotaka kwenda siko.
Mwisho kabisa natoa Rai kwa ndugu wazazi na vijana mnaotarajia kuomba ajira ya ualimu kukataa utaratibu huu kwani unaenda kuwaumiza zaidi badala ya kuwaponya. Hata mimi binafsi naupinga kwa nguvu zote kwani umewahi kutumika miaka ya nyuma na rushwa ilikuwa inatembea sana ndipo serikali ikabadili utaratibu wa kuajiri sasa nashangaa leo serikali inataka kuturudisha kulekule. Katika hili tuseme HAPANA kwa sauti kubwa