Rushwa imeifikisha pabaya TAMISEMI. Je, hawa viongozi wanaoiongoza wanapaswa kuwepo hapo?

Teleza1

Senior Member
May 16, 2020
134
250
Barua ya wazi kwa sekretarieti ya ajira na TAMISEMI

Ndg, Viongozi wenye dhamana inayohusiana na AJIRA hususani Ajira za ualimu Mimi kama Mtanzania wa kawaida mwenye akili timamu na ambae pia ni Mdau wa ELIMU Naiomba Ofisi yako iweze kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya majina ya waajiriwa wa Kada ya ELIMU Yaliyotolewa na Wizara yako pendwa na Nyeti ya TAMISEMI. Tarehe 27/11/2020 kuna baadhi ya majina ya waajiriwa yanaendelea kuwapatia watanzania TAHARUKI KUHUSU AJIRA ZAO

Naomba nizungumzie aina hizi za makosa yaliyofanyika kwenye AJIRA hizi ambazo mmeutangazia umma wa watanzaniaKuwa zilichambuliwa na walioajiriwa walikidhi vigezo na sifa. Rejea barua kutoka kwa KATIBU MKUU OFISI YA RAIS -TAMISEMI ya Tarehe 27 November, 2020 yenye Kichwa cha barua TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI PAMOJA NA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA

Makosa hayo nimeyaainisha hapa chini kama ifuatavyo;-

a) Waajiriwa ambao walihitimu kidato cha NNE 2019.

b) Waajiriwa ambao walipataufaulu hafifu wa daraja LA NNE kuanzia alama 30- 33

c) Waajiriwa ambao hawakufanya mtihani wa kidato cha NNE.

d) Waajiriwa Ambao vituo vyao vya kufanyia mitihani NECTA Haivitambui.

e) Waajiriwa ambao hawako kwenye orodha ya watahiniwa Wa mwaka husika kulingana na namba yake ya usajili wa kidato cha nne.

f) Waajiriwa ambao walisoma masomo tofauti na waliyopangiwa kufundisha kwenye ajira yao.

A). Waajiriwa ambao walihitimu kidato cha NNE 2019
Kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji elimu kubwa tunajua kuwa mhitimu wa kidato cha NNE mwaka 2019 Moja kwa moja atakuwa hajahitimu mafunzo ya ualimu iwe Astashahada, Stashahada au shahada ya Ualimu kwa Mwaka mmoja kwani ni dhahiri shahiri kuwa mhitimu huyu wa mwaka 2019 Matokeo yake aliyapata Mwanzoni mwa mwaka 2020 au Mwishoni mwa mwaka 2019 sasa kama hivyo ndivyo imekuwaje MTU huyu akaajiriwa mwaka huu 2020 ile hali hana mafunzo ya ualimu? Au waliosomea Ualimu wameisha mpaka TAMISEMI imeanza kuajiri waliosomea VETA kuja kufundisha shule za msingi na sekondari. Mfano wa waajiriwa hao ni hao hapa ambao ni baadhi ya wengi mliowaajiri;-

Ally Miraji Shalua S3838-0063/2019

Bakari Lauzi Bakari S3678-0064/2019

Mariam Said Dibwine S0208-0140/2019


Hao ni baadhi yao Ila wapo wengi sana na sababu ya wizara kuajiri hao ambao yawezekana hawana sifa za kuajiriwa sijazijua. Naomba ufafanuzi

B). Waajiriwa ambao walipata Ufaulu hafifu wa daraja la NNE kuanzia points 30-33.

Kulingana na miongozo ya Wizara ya elimu inasema wazi kuwa mhitimu wa kidato cha NNE anatakiwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Astashahada anatakiwa awe amepata ufaulu wa daraja LA kwanza hadi daraja la NNE LA points 28 lakini mwaka huu tumeshangazwa na kilichofanywa na TAMSEMI kuajiri wahitimu ambao walipata ufaulu wa daraja LA NNE LA points 30-33. Je, hapa tayari utaratibu ule wa awali ulikuwa umekiukwa au Sekretarieti ya ajira siku inaajiri ilikuwa imelala usingizi au ilirusha sandakalawe kwa waombaji wa ajira hizo?

Wafuatao ni baadhi ya waliopata ufaulu huo wa daraja LA NNE LA Points 30 hadi 33 ;-
A) ABDALLAH AHMED JIGWA S2732-0091/2019 alipata daraja LA NNE la points 31

B) BAKARI RAJABU KHALIFAN S1680-0064/2019 Alipata Daraja la NNE la points 30

C) FAUSTA SHAO ALEXANDRY S2019-0008/2019 Alipata daraja la NNE la points 32

D) DAVID LAMECK NDOSSA S1943-0147/2019 Alipata daraja la NNE la Points 33.
Hao ni baadhi ya wenye ufaulu hafifu ambao sasa wanaenda kuwafundisha wanafunzi wetu ili na sisi siku moja tupata wanafunzi Bora wenye umahili wa sayansi ya viumbe, sayansi ya Nyota n.k
Naomba ufafanuzi

C) Waajiriwa ambao hawakufanya mtihani wa kidato cha NNE
Kwenye orodha ya ajira hizo kuna MTU mmoja ambae Mimi nimembaini miongoni kwa wengine ambae hakufanya mtihani wa kidato cha NNE lakini Leo hii ameajiriwa na wizara yako shida iko wapi? Je, sekretarieti ya ajira iko sawa kwenye hili au lilikuwa ni takwa la kisiasa? Mwajiriwa huyo ni huyu hapa;-

Halima Saidi Mohamed P2735-0006/2019
Natambua kabisa inawezekana alijisajiri kurudia mtihani lakini hapa tena yanaweza yakaibua Maswali Mengi sana kama namba yake ni P ambayo inaonesha kuwa mtahini huyo alijisajiri kama mwanafunzi binafsi hivyo kupewa namba hii ndo ilikuwa Mara yake ya kwanza kutaka kufanya mtihani huo wa taifa ambao hakuufanya lakini Leo ameajiriwa na Anatarajiwa kwenda kazini kuripoti na kuwafundisha wanafunzi. Kwa tafsiri ya haraka haraka ametoka darasa la Saba na kwenda kufundisha.
Naomba ufafanuzi

D) Waajiriwa ambao vituo vyao vya kufanyia mitihani *NECTA haivitambui. Kuna baadhi ya waajiriwa ambao kwa namba ambazo zinawaelezea kwenye orodha ya ajira ukitafuta kwenye urodha ya shule unakuta namba hiyo ya mtahiniwa haipo yaani namba ya shule hiyo haipo na kama haipo inamaanisha mtahiniwa huyo ni HEWA kwani shule hiyo haipo Tanzania .
Mfano wa waajiriwa hao ni hawa hapa kwa baadhi hao kwani wako wengi;-

i) LUKAS EMMANUEL MTOI S1380-0852/2019

ii) PETRO ADRIANO KIOSHA S0566-1215/2019

iii) RAJABU STUART WILLIAM S0440-0963/2019

iv) SHOTO SOSTHENES NYANDA S1380-1058/2019
Naomba ufafanuzi kwanini mwajiriwa aweke namba ambayo haioneshi alisoma wapi elimu yake ya kidato cha NNE alafu pia TAMISEMI na sekretarieti ya Ajira ilitumia Matokeo kutoka wapi kumwajiri au kuwaajiri hawa inamaana hawapo wenye vyeti na sifa za ualimu kuajiriwa mpaka mkaajiri ambao wamedanganya mpaka vituo vyao vya kufanyia mtihani.

E) Waajiriwa ambao hawako kwenye orodha ya watahiniwa wa mwaka husika kulingana na namba yake ya usajili wa kidato cha nne.
Kuna baadhi ya waajiriwa wameoneshwa kwa namba za usajiri wa kidato cha nne Ambao ukiangalia orodha ya waliofanya mtihani mwako huo mhusika hayuko kwenye orodha hiyo kwa Tafsiri ya haraka ni kwamba mhusika hakufanya mtihani kwani hakusajiriwa. Mfano ni Mwajiriwa
SHAFII MOHAMMEND NAMKURUNG'UNDU S0738-0076/2019 Mwajiriwa huyu kwa namba hii ya usajiri inaonesha alisoma Shule ya sekondari Ridhwaa Seminary mwaka 2019 lakini cha ajabu mwaka huo kwenye shule hiyo watahiniwa walikuwa 61 Ila Mwajiriwa namba namba yake ilikuwa ni no 76. Kwa maneno mepesi mtahiniwa wa mwisho kwenye mtihani huo alikuwa mwenye no S0738/0061/2019 ila Mtajwa hapo juu namba yake ya Mtihani ni S0738/0076/2019
Kwa maneno na ushahidi huo hakukuwepo na mtahiniwa anaeitwa SHAFII MOHAMMED NAMKURUNG'UNDU.
Naomba ufafanuzi yeye alifanyia wapi mtihani wa kidato cha nne?

F) Waajiriwa ambao walisoma masomo tofauti na waliyopangiwa kufundisha kwenye ajira yao

Kuna baadhi ya waajiriwa kwenye orodha yako wameoneshwa kwenda kufundisha au kuandaa vifaa vya maabara ile hali MTU huyo hakufaulu somo lolote lile linalohusiana na Maabara yaani kama aliyasoma masomo hayo basi hakufaulu alipata alama F
Mfano ni Mwajiriwa David Lameck Ndossa S1943-0147/2019 Mwajiriwa huyu alifeli somo la Biology lakini Leo ameajiriwa kwenda kuwa Laboratory Technician Lugufu wasichana Sekondari Hata kama kuna kurudia Mwajiriwa alirudia mtihani lini na akafaulu lini? Maana ni mhitimu wa mwaka 2019?.

ZINGATIA
Kwenye orodha ya majina ya walimu waliopangiwa vituo vya Nazi Novemba 2020 kuna jedwali ambalo lina neno Applicant Id Nimejiridhisha pasi na shaka kwa waajiriwa ambao walifanya mtihani miaka ya 2009 na 2010 hii Applicant Id ni Index no ya Mwajiriwa ya mtihani wa kidato cha NNE .
Mfano
Abbas Juma Malungo S1222-0100/200

Abdallah Rajabu Dumwe S0811-0102/2009

Zuhura Musaka Majaliwa S0316-0238/2010
MAJINA HAYO PASI NA SHAKA YANASOMEKA HIVYOHIVYO KWA WAHUSIKA NA NAMBA ZAO ZA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NI HIYOHIYO.

Kulingana na maelezo hayo na ushahidi huu nilioutoa TAMISEMI HAIONI AJIRA HIZI ZINAIBUA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU *

1. Je, ni ajira kweli na walioorodheswa ni sahihi?
2. Hazijakaa kisiasa kwa sababu ya mapungufu yake? Maana tuliwahi kuambiwa kuwa Serikali ya awamu ya Tano inaangalia uchapaji kazi wa MTU na sio Vyeti.
3. Hamuoni kwa mapungufu haya na mengine ukafanyika uchunguzi wa wazi kuhusu ajira hizi?

4. Walioidhinisha ajira hizo wanalitakia nini taifa kwenye Tasnia ya Elimu?

5. Kwa makosa hayo ofisi na mishahara wanayolipwa hawa waliotoa ajira hizi hawaoni hawatutendei haki sisi walipakodi wa Nchi hii?

Wako,
Prof Hans
Mwalimu asiyekuwa na Kituo maalumu cha Kufundishia


Tafadhali soma
 

Teleza1

Senior Member
May 16, 2020
134
250
Hawa viongozi wa tamisemi watumbuliwe kabisa haiwezwkani wapokee rushwa halafu waanze kuedit kwa watu waliokula hela pia wazirimpya wa tamisemi aondoe baadhi ya wafanyakazi wa Tamisemi.
 

Teleza1

Senior Member
May 16, 2020
134
250
Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu...
Tangazo lilikuwa lipo sana applicant yeyote atakae jaza invalid numbers, application yake itakuwa nullfied and will not be processed(rejected). Sasa imekuwa hizo application ziwe proccessed wakati applicant amejaza invalid index number. Mmepokea rushwa namba zilizokuwa zinatumika kupokelea rushwa ntaziweka hapa na miamala yake
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,283
2,000
Kama kweli hakuna udanganyifu basi teknolojia ya tehama imewagombanisha waombaji na serikali.

Watu wa ICT wa idara iliyo husika na kuchuja na kutangaza waajiriwa hawakuwa makini wanastahili kuwajibishwa.

Hakuna proof reading baada ya uhakiki wa vyeti kisha kurekebisha namba za kuhitimu kidato cha nne wale waliokosea kujaza kabla ya kusambaza majina kwa umma?
 

Ahjumma

JF-Expert Member
May 19, 2020
460
500
Barua ya tamisemi inafikirisha sasa kwanini walichagua hao wenye makosa wakaacha watu makini waliojaza vizuri hizo ajira maana hao ni wazembe hawastahili hizo nafasi
 

dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
536
1,000
Uchambuzi wangu kuhusu ajira hizi zilivyozua gumzo; kwanza, inaonekana kutotolewa kwa ajira kwa muda mrefu kumepelekea watu kuwa sensitive na ishu za ajira kiasi cha kufuatilia kwa umakini na ukaribu ajira hizi.

Pili huenda imani wa watu kwa serikali imepungua kiasi cha kutokuwa na imani na idadi ya ajira zilizotolewa hivyo kuwa makini kujilidhisha kitu kilichoplekea kugundua makosa Au walio wengi wamechefukwa na mambo fulani fulani juu ya serikali yao hivyo kwenye kila kiletwacho na serikali watakuwa makini kutafuta makosa ili na wao wapate fursa ya kuinanga serikali yao.

Note: Hizi ni hisia tu hakuna uhalisia kwenye nilichoandika hapo juu
 

Ooh yes

Senior Member
Jul 31, 2020
140
225
Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu.

Ufafanuzi huo umetolewa leo katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI Jijini Dodoma mara baada kutokea hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu ajira mpya za walimu zilizotangazwa hivi karibuni.

Amesema ajira hizo zilitangazwa baada ya kukamilia kwa mchakato wa uchambuzi wa maombi ya ajira uliofanywa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora na tume ya utumishi wa walimu.

Mhandisi Nyamhanga amesema hoja kubwa ilyojitokeza ni kwa jina la Mwalimu mmoja kujitokeza katika kila ukurasa na kuonekana mara 196, badala ya mstari wa maelezo ya Jedwali (Sub- titles) lakini shule aliyopangiwa ni moja, pamoja na jina hilo kujirudia halikuchukua nafasi ya mwombaji yoyote ya walimu waliotakiwa kuajiriwa au kuathiri idadi ya waalimu waliotakiwa kuajiriwa na tayari marekebisho yamefanyika.

Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa Shule binafsi kupangiwa mwalimu, Serikali imekuwa ikiingia ubia na baadhi ya Shule binafsi ambazo hupokea wanafunzi wenye uhitaji maalum, shule hizo hupamgiwa walimu na kupewa ruzuku ya uendeshaji hivyo Shule ya Mwalimu Tutuba ilikuwa katika mchakato wa kuingia ubia na serikali lakini haukukamilika, hivyo Serikali baada ya kujiridhisha mwalimu aliyepangiwa katika shule hiyo amepangiwa katika shule ya sekondari Malagarasi.

Kwa upande wa wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017, 2018 na 2019 kupangiwa vituo vya kazi Mhandisi Nyamhanga ameeleza waombaji wa ajira walitumia mwaka wa kuhitimu chuo badala ya mwaka wa kuhitimu kidato cha nne ambapo waombaji 27 waliandika mwaka 2019, waombaji 27 waliandika mwaka 2019 na waombaji 13 waliandika mwaka 2017, Serikali ilihakiki vyeti vyao na kubaini kuwa waombaji hao walihitimu kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

Kwa kuongezea amesema kuwa Serikali imefuata utaratibu wa kuhakikisha Waombaji wote waliopata nafasi ya ajira wanazingatia vigezo vilivyotolewa katika tangazo la ajira ambapo lilifafanua kuwa mwombaji asizidi umri wa miaka 45.

Aidha Mhandisi Nyamhanga amewalekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakiki vyeti halisi vya waliopata ajira na kujiridhisha kabla ya kutoa barua za ajira, na kusisitiza kuwa endapo itabainika udanganyifu au kasoro za vyeti vya kitaaluma wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema Serikali imetoa ajira za waalimu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wametoa ajira 8000 na awamu ya pili watatoa kwa waalimu 5000 ili kupunguza malimbikizo ya mshahara kwa waalimu wapya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameweka wazi kuwa Serikali itahakikisha waalimu wote waliomba ajira kwa masomo waliyoomba yanaendana na masomo wanayoyafundisha.
Duh majanga
 

Nsam

Senior Member
Oct 25, 2018
188
250
Barua ya wazi kwa sekretarieti ya ajira na TAMISEMI
Ndg, Viongozi wenye dhamana inayohusiana na AJIRA hususani Ajira za ualimu Mimi kama Mtanzania wa kawaida mwenye akili timamu na ambae pia ni Mdau wa ELIMU Naiomba Ofisi yako iweze kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya majina ya waajiriwa wa Kada ya ELIMU Yaliyotolewa na Wizara yako pendwa na Nyeti ya TAMISEMI. Tarehe 27/11/2020 kuna baadhi ya majina ya waajiriwa yanaendelea kuwapatia watanzania TAHARUKI KUHUSU AJIRA ZAO.....

Mafala hawa wanakula tu kodi zetu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom