Jensen salamone
JF-Expert Member
- Sep 28, 2019
- 320
- 639
Kwanza nianze kwa kuwapongeza wizara ya Tamisemi chini ya waziri ummy, katibu mkuu na wote waliohusika kwenye mchakato mzima wa uchambuzi na utoaji ajira
Ofcourse wanastahili kupewa pongezi kwa kazi nzuri waliyofanya kwani kwa asilimia kubwa wametenda haki kwa waombaji hasa kwa kutoa kipaumbele kwa vijana waliomaliza vyuo na kukaa mtaani kwa muda mrefu. Mbali na kutenda haki pia wamejitahidi kuwa wawazi hususani kwenye kuainisha kiwango cha elimu kwa kila mwombaji kwa sababu kulikuwa na uvumi kwamba walimu wenye digrii hawaajiriwi lakini hivi sasa tumeshuhudia kwa macho wakiajiriwa.
Pamoja na pongezi hizo nzuri kuna mambo machache ambayo naona hayajaenda sawa kwenye mchakato wa hizo ajira nayo ni kama yafuatayo,
1. Kuna waombaji kiwango chao cha elimu kinaonyesha wamemaliza elimu ya digrii mwaka 2019 lakini index zao za kidato cha nne zinaonyesha wamehitimu kidato cha nne 2014 ambapo kwa kuzingatia mwaka wao wa kumaliza kidato cha nne kwa mujibu wa TCU ilibidi digrii yao ya kwanza ya ualimu waipate kuanzia 2020 kwani digrii ya ualimu minimum ni miaka mitatu kwa vyuo vyote nchini. Miongoni mwa waombaji hao ni wenye index zifuatazo
(i) S4463-0023/2014 -kuhitimu degree(2019)
(ii) S3065-0009/2013-kuhitimu degree(2016)
(iii) S1183-0035/2014- kuhitimu degree(2019)
(iii) S4507-0035/2014 -kuhitimu degree(2019)
(iv) S1229-0068/2014-kuhitimu degree(2019)
2. Mwombaji mwenye index no S4166-0038/2014 taarifa zinaonyesha hakufanya mtihani wa kidato cha nne
3. Watu wenye ulemavu (PWD's) walioajiriwa ni 145 kati ya 1000 maana yake ile 3% haijafikiwa kwani kwa idadi yao ilibidi waajiriwe angalau 208 ili kufikia lengo la 3%. Kwahiyo mnapokuwa mnaajiri ni vyema mkazingatia hilo kwa sababu PWD's tunaishi nao kwenye jamii zetu na tunajua wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutengwa, kudharauliwa na wengine huficha ulemavu wao kwa hofu ya kubaguliwa na hivyo huishi kwa taabu sana
4. Mwombaji mwenye index no S0660-1409/2019 haitambuliki kwenye baraza la mitihani (NECTA) kwahiyo ni vema mka link mifumo yenu na necta ili kasoro ndogo ndogo kama hizi sijirudie
5. Halmashauri ya muheza imepelekewa walimu wengi kulinganisha na halmashauri zingine. Kwahiyo ni vema mnapokuwa mnagawa walimu kuwepo na uwiano mzuri angalau kila halmashauri ipate watumishi kuliko kupeleka walimu wengi sehemu moja huku halmashauri zingine zikibaki na uhaba mkubwa.
Otherwise jitahidini kuomba vibali vya kuajiri walimu mara kwa mara kwakuwa bado tatizo la uhaba wa walimu ni kubwa kupita maelezo.