Walimu sita wanalazimika kufundisha zaidi ya Wanafunzi 700 Sekondari ya Mwabusalu-Meatu

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
WALIMU SITA, WANAFUNZI MIA SABA
Mwabusalu Sekondari, Meatu Simiyu
(Miaka 3, DIV I-0, II-7, III-14, IV-74, O-9)

Habari Gani Tanzania?

Shule ya Serikali ya Upili ya Mwabusalu (SLP 232) iliyopo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu inakabiliwa na uhaba wa walimu kwa miaka mingi sasa. Mwaka huu wa 2021 ina zaidi ya wanafunzi 730 na jumla ya walimu sita akiwemo mkuu wa shule. Walimu hao ni:

1. Judith Matatizo (HM) - Civics
2. Boniface Salama - English
3. Adolf Onesfori - History
4. Musa Peter - Maths, Physics
5. Thomas Godfrey - Geo, Kisw
6. Adam Kamendu - Bios, Chem

Tangu January 2021 mpaka shule zilipofungwa mapema tarehe 4, Juni, wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao ni zaidi ya 120 walikuwa wamejifunza wastani wa mada moja kwa kila somo. Cha kusikitisha ambacho pia ni cha kawaida kwa shule kama hizi ni kwamba kuna mikondo ambayo haijafundishwa kabisa lakini mitihani ya Mid-Term na Terminal wamefanya. Kwa mfano upande wa kidato cha kwanza:

1. Civics: Wamesoma mada 1 na bado haijaisha na hiyo ni kwa Form I A. Wale wa mkondo B hawajafundishwa kabisa tangu January. Hili ni somo la mkuu wa shule Bi. Judith Matatizo (Mtakumbuka kuwa Matatizo kwa kiingereza ni Problems, lakini hapa limetumika kama Proper Noun). Mkuu huyu hana muda kabisa wa kufundisha kwani yuko busy na majukumu ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu. Bila shaka anasubiri Mungu wa Israel kushusha Division I kama alivyoshusha Kware na Mana kutoka Mbinguni. Tatizo hapa ni Uhaba wa Musa huko Meatu.

2. English: Tangu January mwalimu aliingia darasani akafundisha "Family Tree" na akaendelea na hiyo mada mpaka mwezi wa tano wakafunga kwa ajili ya Terminal Break. Hili ni somo la Mwl. Boniface Salama. Sasa utata unakuja pale unapokumbuka kuwa somo la kiingereza lina vipindi sita kwa wiki kwa kila mkondo. Hii ni sawa na kusema inambidi mwalimu huyu afundishe zaidi ya saa 28 kwa siku ili kufundisha mikondo yote bila kupumzika. Kumbuka siku moja kwa hapa duniani ina saa 24. Ila kipengele cha Family Tree (Kinship) kwa miezi mitano? Hapo napo kuna shida sehemu.

3. History: Mada moja "Sources and Importance of Studying History" tangu January mpaka May. Hili ni somo la Bw. Adolf Onesfori.

TAMISEMI hebu fuatilieni hili kwani kwa upande wa Candidate classes hali ni mbaya sana. Lakini zipo shule zingine mbaya kuliko hii, kama alivyokiri Waziri Ummy kuwa zipo shule zaidi ya 1000 tangu zianzishwe hazijawahi kuwa na walimu wa Mathematics na Physics lakini wakati huohuo Mtangulizi wake Bw. Suleiman Jafo aliwahi kuiaminisha umma kuwa Walimu wako wengi na wa ziada na baadhi yao wakaanza kuhamishwa kwenda shule za msingi.

Linapokuja suala la walimu kunakuwa na siasa hewa nyingi, ahadi za kitoto zisizoisha, lakini kugeuza umma kama karakana ya wajinga fulani hivi. Shule za mjini zimejaa walimu wengi ambao wengine wana vipindi viwili tu kwa wiki nzima. Lakini huko vijijini hali ni mbaya na hakuna anayejali. Walimu wameshajikatia tamaa, wanafunzi wanaoshindwa kuhamia shule za mjini au kwenda zile za binafsi hawana namna isipokuwa kujikatia tamaa na kusubiri NECTA. Serikali nayo imeamua kujikatia tamaa na shule hizo. Hali hii si shwari kwa maana viongozi hawapeleki watoto wao huko na hivyo hawawezi kujua kuna shida gani huko. Kila mzazi anatakiwa kujijua na watoto wake.

JPM mwaka 2020 alitangaza zaidi ya ajira 13k, zikatoka ajira 8k zilizojaa uozo mtupu na mpaka leo zile 5k hazieleweki zilitoka lini au zinafanya nini huko store. Mama akatangaza replacement 6k ambazo zinachakatwa kwa sasa ili wale waliotoa chochote na wenye bahati na kujuana waajiriwe na wenye nyota za kitimoto kusubiri takataka bandani, lakini juzi hapa Mama tena akasema ametoa kibali cha ajira 3k ambazo hazieleweki zinakwendaje? Lakini hapohapo aliwahi kutoa ajira mpya 40k ambazo pia hazieleweki ziko wapi.... Kwa ujumla ni mchezo wa kitoto sana ukiangalia kuwa HESLB inazidi kuwapiga penalties wanaochelewa kurudisha mikopo ilihali ajira zenyewe ndo hizo za makaratasi juu ya gari.

KIPI KIFANYIKE?
Mama ulisema tusiishie kukosoa tu, bali tutoe na mwongozo au mapendekezo. Basi napendekeza haya yafanyike:

1. Kuliko kuahidi vijana u-DC na ukurungenzi huku majina tayari unayo, jenga shule kubwa moja tu kila halmashauri na uwakabidhi vijana waliomaliza vyuo mbalimbali kwenye halmashauri husika ili wajiajiri hapo. Walimu hao ndo watajua namna ya kupata wanafunzi na kuendesha shule kwa kujituma kwao. Fanya hivi ili vijana ambao ni zaidi ya laki moja waliohitimu mafunzo ya ualimu waweze kuitumikia taaluma yao lasivyo wasamehe madeni yao HESLB ili wakomae huko private schools kwa maisha yao yote ya ualimu maana mmeshindwa kuwaajiri kulingana na taaluma zao.

2. Fungia vyuo vya elimu kuacha kudahili wanafunzi wa sekta ya elimu kwa miaka 20 ili kutumia kwanza stock iliyopo mtaani hadi iishe. Wanafunzi wasome kuwa watu wengine tofauti na kuwa walimu.

3. Kuwepo na chuo kimoja tu cha walimu nchi nzima na kidahili wanafunzi kulingana na mahitaji ya walimu kwa mwaka husika. Wanaotaka kuwa waalimu waandaliwe tangu wakiwa mashuleni, na shule binafsi zitume maombi maalumu chuoni ili wanaopenda kutumikia shule binafsi wajaze form za ajira hukohuko kwenye shule husika.

4. Mikopo ya elimu ya juu isiwe na riba na serikali iwajibike kuwatafutie ajira wale wanaowapa mikopo pindi wanapomaliza masomo halafu watajilipa kidogokidogo kupitia PAYE.

5. Mwajiriwa wa shule binafsi awe na uwezo wa kuchukua pesa zake za NSSF muda wowote na kufanyia maendeleo yake na si kusubiri mpaka aache kazi au kustaafu. Lakini pia akaunti ya NSSF iunganishwe na akaunti ya benki ya mwanachama moja kwa moja kana kwamba anaweza kutoa pesa NSSF kwenda Bank and vice versa. Lasivyo kazi ya NSSF ifanywe na NMB ili kuepusha usumbufu.

6. Mtaala ubadilishwe, mada za kijasiriamali zifundishwe tangu shule za msingi na masomo ambayo si lazima kusomwa shuleni yafutwe na hivyo yaelekezwe tu na wazazi na mengine kufundishwa na walimwengu. Masomo kama ya Lugha, History, Literature, Dini na Civics yasiwe ya msingi. Wanafunzi wasome masomo ya Sayansi na Biashara. Hayo mengine watayasoma mtandaoni tu au maktaba wenyewe au kusimuliwa na wazazi wao na si kupoteza muda kuyasoma shuleni au vyuoni. Ifike muda tujaribu kuthubutu vitu vipya na si kukomaa na takataka zisizotuletea maendeleo yeyote.
____________________________
Mabango Hayaruhusiwi Hapa. Kumbukeni Kilichomkuta Chalamila.
 
Hili ni Zaidi ya Bango, Ujumbe Umefika na hii hali inaakisi Tanzania nzima. Kiukweli viongozi tulionao sijui wanafikirisha vipi vichwa vyao kuhusi hili Taifa. Siasa zimetawala mipango ya Maendelo kwa Taifa.
 
Ivi kwanini graduates waliosoma ualimu tu ndo wanaona Wana haki ya kuajiriwa serikalini kwenye hii nchi mbona graduates wa kada zingine Kama wahasibu, wanasheria n.k huwa SIONI wakitumia nguvu nyingi kuishinikiza serikali iweze kuwapa ajira?
 
Ivi kwanini graduates waliosoma ualimu tu ndo wanaona Wana haki ya kuajiriwa serikalini kwenye hii nchi mbona graduates wa kada zingine Kama wahasibu,wanasheria n.k huwa SIONI wakitumia nguvu nyingi kuishinikiza serikali iweze kuwapa ajira?
umemuelewa vzr mtoa mada?
 
umemuelewa vzr mtoa mada?
Nimemuelewa vizuri lakini uhaba upo sehemu nyingi Sana serikalini Kuna vijiji ,kata hazina watendaji, kuna zahanati hazina manurse ,daktari n.k kwaio kuja na hoja za uhaba wa shule kila siku ndo napoona graduates waliosoma ualimu Ni watu waohisi Wana haki Sana ya kuajiriwa serikali kuliko watu wa kada zingine.
 
Ivi kwanini graduates waliosoma ualimu tu ndo wanaona Wana haki ya kuajiriwa serikalini kwenye hii nchi mbona graduates wa kada zingine Kama wahasibu,wanasheria n.k huwa SIONI wakitumia nguvu nyingi kuishinikiza serikali iweze kuwapa ajira?
Mie sijaona ilo ulilo liona mkuu.
Ila pia hongera
 
Musa Peter kama namfahamu vile...

Ila Elimu yetu ina tatizo kubwa
 
Walimu hao ni:

1. Judith Matatizo (HM) - Civics
2. Boniface Salama - English
3. Adolf Onesfori - History
4. Musa Peter - Maths, Physics
5. Thomas Godfrey - Geo, Kisw
6. Adam Kamendu - Bios, Chem
Umepata ridhaa yao kuwaandika majina yao?
 
Ivi kwanini graduates waliosoma ualimu tu ndo wanaona Wana haki ya kuajiriwa serikalini kwenye hii nchi mbona graduates wa kada zingine Kama wahasibu,wanasheria n.k huwa SIONI wakitumia nguvu nyingi kuishinikiza serikali iweze kuwapa ajira?
Kwahiyo unataka walimu ndio wasemee wa sekta zingine kwani wao hawana midomo??
 
Ivi kwanini graduates waliosoma ualimu tu ndo wanaona Wana haki ya kuajiriwa serikalini kwenye hii nchi mbona graduates wa kada zingine Kama wahasibu,wanasheria n.k huwa SIONI wakitumia nguvu nyingi kuishinikiza serikali iweze kuwapa ajira?
Wasemee na wewe hao wengine. Mwalimu kajitolea kusemea wa fani yake. Wengine hawajazibwa midomo wala kufungwa mikono wasiandike. Zipo kada zinapenda kuneemeka kupitia "struggle" za wengine. Kila kada ipambane na hali yake kwanza na baade muunganiko ufuatie kupitia shirikisho la wafanyakazi kama lipo.
 
WALIMU SITA, WANAFUNZI MIA SABA
Mwabusalu Sekondari, Meatu Simiyu
(Miaka 3, DIV I-0, II-7, III-14, IV-74, O-9)

Habari Gani Tanzania?

Shule ya Serikali ya Upili ya Mwabusalu (SLP 232) iliyopo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu inakabiliwa na uhaba wa walimu kwa miaka mingi sasa. Mwaka huu wa 2021 ina zaidi ya wanafunzi 730 na jumla ya walimu sita akiwemo mkuu wa shule. Walimu hao ni:

1. Judith Matatizo (HM) - Civics
2. Boniface Salama - English
3. Adolf Onesfori - History
4. Musa Peter - Maths, Physics
5. Thomas Godfrey - Geo, Kisw
6. Adam Kamendu - Bios, Chem

Tangu January 2021 mpaka shule zilipofungwa mapema tarehe 4, Juni, wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao ni zaidi ya 120 walikuwa wamejifunza wastani wa mada moja kwa kila somo. Cha kusikitisha ambacho pia ni cha kawaida kwa shule kama hizi ni kwamba kuna mikondo ambayo haijafundishwa kabisa lakini mitihani ya Mid-Term na Terminal wamefanya. Kwa mfano upande wa kidato cha kwanza:

1. Civics: Wamesoma mada 1 na bado haijaisha na hiyo ni kwa Form I A. Wale wa mkondo B hawajafundishwa kabisa tangu January. Hili ni somo la mkuu wa shule Bi. Judith Matatizo (Mtakumbuka kuwa Matatizo kwa kiingereza ni Problems, lakini hapa limetumika kama Proper Noun). Mkuu huyu hana muda kabisa wa kufundisha kwani yuko busy na majukumu ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu. Bila shaka anasubiri Mungu wa Israel kushusha Division I kama alivyoshusha Kware na Mana kutoka Mbinguni. Tatizo hapa ni Uhaba wa Musa huko Meatu.

2. English: Tangu January mwalimu aliingia darasani akafundisha "Family Tree" na akaendelea na hiyo mada mpaka mwezi wa tano wakafunga kwa ajili ya Terminal Break. Hili ni somo la Mwl. Boniface Salama. Sasa utata unakuja pale unapokumbuka kuwa somo la kiingereza lina vipindi sita kwa wiki kwa kila mkondo. Hii ni sawa na kusema inambidi mwalimu huyu afundishe zaidi ya saa 28 kwa siku ili kufundisha mikondo yote bila kupumzika. Kumbuka siku moja kwa hapa duniani ina saa 24. Ila kipengele cha Family Tree (Kinship) kwa miezi mitano? Hapo napo kuna shida sehemu.

3. History: Mada moja "Sources and Importance of Studying History" tangu January mpaka May. Hili ni somo la Bw. Adolf Onesfori.

TAMISEMI hebu fuatilieni hili kwani kwa upande wa Candidate classes hali ni mbaya sana. Lakini zipo shule zingine mbaya kuliko hii, kama alivyokiri Waziri Ummy kuwa zipo shule zaidi ya 1000 tangu zianzishwe hazijawahi kuwa na walimu wa Mathematics na Physics lakini wakati huohuo Mtangulizi wake Bw. Suleiman Jafo aliwahi kuiaminisha umma kuwa Walimu wako wengi na wa ziada na baadhi yao wakaanza kuhamishwa kwenda shule za msingi.

Linapokuja suala la walimu kunakuwa na siasa hewa nyingi, ahadi za kitoto zisizoisha, lakini kugeuza umma kama karakana ya wajinga fulani hivi. Shule za mjini zimejaa walimu wengi ambao wengine wana vipindi viwili tu kwa wiki nzima. Lakini huko vijijini hali ni mbaya na hakuna anayejali. Walimu wameshajikatia tamaa, wanafunzi wanaoshindwa kuhamia shule za mjini au kwenda zile za binafsi hawana namna isipokuwa kujikatia tamaa na kusubiri NECTA. Serikali nayo imeamua kujikatia tamaa na shule hizo. Hali hii si shwari kwa maana viongozi hawapeleki watoto wao huko na hivyo hawawezi kujua kuna shida gani huko. Kila mzazi anatakiwa kujijua na watoto wake.

JPM mwaka 2020 alitangaza zaidi ya ajira 13k, zikatoka ajira 8k zilizojaa uozo mtupu na mpaka leo zile 5k hazieleweki zilitoka lini au zinafanya nini huko store. Mama akatangaza replacement 6k ambazo zinachakatwa kwa sasa ili wale waliotoa chochote na wenye bahati na kujuana waajiriwe na wenye nyota za kitimoto kusubiri takataka bandani, lakini juzi hapa Mama tena akasema ametoa kibali cha ajira 3k ambazo hazieleweki zinakwendaje? Lakini hapohapo aliwahi kutoa ajira mpya 40k ambazo pia hazieleweki ziko wapi.... Kwa ujumla ni mchezo wa kitoto sana ukiangalia kuwa HESLB inazidi kuwapiga penalties wanaochelewa kurudisha mikopo ilihali ajira zenyewe ndo hizo za makaratasi juu ya gari.

KIPI KIFANYIKE?
Mama ulisema tusiishie kukosoa tu, bali tutoe na mwongozo au mapendekezo. Basi napendekeza haya yafanyike:

1. Kuliko kuahidi vijana u-DC na ukurungenzi huku majina tayari unayo, jenga shule kubwa moja tu kila halmashauri na uwakabidhi vijana waliomaliza vyuo mbalimbali kwenye halmashauri husika ili wajiajiri hapo. Walimu hao ndo watajua namna ya kupata wanafunzi na kuendesha shule kwa kujituma kwao. Fanya hivi ili vijana ambao ni zaidi ya laki moja waliohitimu mafunzo ya ualimu waweze kuitumikia taaluma yao lasivyo wasamehe madeni yao HESLB ili wakomae huko private schools kwa maisha yao yote ya ualimu maana mmeshindwa kuwaajiri kulingana na taaluma zao.

2. Fungia vyuo vya elimu kuacha kudahili wanafunzi wa sekta ya elimu kwa miaka 20 ili kutumia kwanza stock iliyopo mtaani hadi iishe. Wanafunzi wasome kuwa watu wengine tofauti na kuwa walimu.

3. Kuwepo na chuo kimoja tu cha walimu nchi nzima na kidahili wanafunzi kulingana na mahitaji ya walimu kwa mwaka husika. Wanaotaka kuwa waalimu waandaliwe tangu wakiwa mashuleni, na shule binafsi zitume maombi maalumu chuoni ili wanaopenda kutumikia shule binafsi wajaze form za ajira hukohuko kwenye shule husika.

4. Mikopo ya elimu ya juu isiwe na riba na serikali iwajibike kuwatafutie ajira wale wanaowapa mikopo pindi wanapomaliza masomo halafu watajilipa kidogokidogo kupitia PAYE.

5. Mwajiriwa wa shule binafsi awe na uwezo wa kuchukua pesa zake za NSSF muda wowote na kufanyia maendeleo yake na si kusubiri mpaka aache kazi au kustaafu. Lakini pia akaunti ya NSSF iunganishwe na akaunti ya benki ya mwanachama moja kwa moja kana kwamba anaweza kutoa pesa NSSF kwenda Bank and vice versa. Lasivyo kazi ya NSSF ifanywe na NMB ili kuepusha usumbufu.

6. Mtaala ubadilishwe, mada za kijasiriamali zifundishwe tangu shule za msingi na masomo ambayo si lazima kusomwa shuleni yafutwe na hivyo yaelekezwe tu na wazazi na mengine kufundishwa na walimwengu. Masomo kama ya Lugha, History, Literature, Dini na Civics yasiwe ya msingi. Wanafunzi wasome masomo ya Sayansi na Biashara. Hayo mengine watayasoma mtandaoni tu au maktaba wenyewe au kusimuliwa na wazazi wao na si kupoteza muda kuyasoma shuleni au vyuoni. Ifike muda tujaribu kuthubutu vitu vipya na si kukomaa na takataka zisizotuletea maendeleo yeyote.
____________________________
Mabango Hayaruhusiwi Hapa. Kumbukeni Kilichomkuta Chalamila.
Hali hii sio huko tu..! hata huku kwetu pia ipo na imezoeleka kuwa kawaida...
 
Sasa TAMISEMI wafuatilie nini wakati wao wanajua kila shule ina walimu wangapi.

Serikali ndo chanzo cha hayo yote. Tena kwa makusudi.

Sijawahi kuielewa serikali yangu ya Tanzania. Inatumia nguvu kubwa kuandaa mitihani na usimamizi wake, wakati mwanafunzi huyo amepunjwa vipindi tangu chekechea hadi kidato cha nne kupitia upungufu wa walimu hasa shule za vijijini.
 
Hili ni Zaidi ya Bango, Ujumbe Umefika na hii hali inaakisi Tanzania nzima. Kiukweli viongozi tulionao sijui wanafikirisha vipi vichwa vyao kuhusi hili Taifa. Siasa zimetawala mipango ya Maendelo kwa Taifa.
Haya mambo hayawezi kubadilika bila kubadilisha mfumo wetu wa utawala. Achana na kubadilisha tume ya uchaguzi (najua CCM hii ndiyo hofu yao); wajaribu kubadilisha mfumo wa utawala. Tanzania yetu ni kubwa sana na siyo rahisi usimamizi wa mambo kama haya kufanywa na serikali kuu. Wakubali tuwe na system ya bottom top approach, na wananchi wapewe uwzo zaidi kuamua mambo yao. Hili la tatizo la kukosa waalim linaweza kuisha kabisa kama tutakuwa na mfumo mzuri wa kujitawala. Nchi igawanywe kwenye maeneo, na kila eneo lipewe uwezo wa kujisimamia kwenye mambo yake. Waalim wako wengi mitaani. Kila eneo likipewa uwezo wa kukusanya mapato, fedha zitatumika vizuri zaidi na wananchi watawawajibisha viongozi wao vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom