Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

nashukuru raisi wangu wa moyoni.hakika sarakasi hizi za utawala wa kibabe zitafika mwisho..muda si mlefu uhuru wa kweli utapatikana.
Rais!!!!! Rais gani huyo??? wala hajasema yeye ni Rais, hata utambulisho wake ni Dr. W. Slaa anakula bata ughaibuni baada ya hotuba yake ya mwisho pale Serena
 
Dr. Slaa hakuna haja ya kumpa pole kwa sasa bali kukumpongeza yeye na wenzake naanza kuona mbele ya safari kama mwanga utaonekana, safari ya haki lazima wachache wataumia kwa niaba ya wengine.

Dhuluma na uzalilishaji wanaofanyiwa viongozi wa CDM na upinzani kwa ujumla ni maandiko na alama ndani ya mioyo ya watu hususani kizazi kipya ambacho hakioni faida ya mfumo wa sasa wa utawala. Ninacho shukuru bado viongozi wa CDM wanatumia busara kubwa sana kuongoza kundi kubwa la walalahoi lakini iko siku watashindwa na walalahoi wataamua kivyao, tusifike huko.
Noel Kwai, Sikubaliani na wewe hata kidogo. Kizazi kipya kimegawanyika kuhusu hali ya kisiasa nchini. Hii imetokana na mifumo na namna jinsi vyama vya siasa vinavyoendeshwa na hususan ni sera zipi vyama vinasimamia. Ndani ya CDM unayoizungumzia tayari vijana wengi hawana imani tena na chama hicho na wala usimpotoshe Dr. Slaa akarudi bure badala ya kuendelea kula bata huko aliko.

CDM inatuhumiwa kwa siasa za ukanda hili halina ubishi. Mwanachama/Kiongozi ndani ya CDM ambaye si mwanakasikazini akitoa hoja inayokinzani na Mwenyekiti Mbowe ujue huyo atafukuzwa mara moja au mwanachama/kiongozi ambaye ni influential na inaonekana huko mbeleni anaweza kukiongoza chama kama si mwanakaskazini atafukuzwa mara moja. Waliofukuzwa kwa kuthubutu hayo ni pamoja na Chacha Wangwe, David Kafulira, Zitto Zuberi Kabwe, Mkosa Mali, Shibuda na endelea kutaja wengine unawajua. Kati ya hao hakuma mwanakaskazini badala yake wanazidi kuwa promote akina Lema na pumba zao, Mnyika, Mdee na wengine kana kwamba watanzania hawana macho. Kama kuna mahali CDMA ilikuwa na wafuasi wengi ni mkoa wa kigoma kwa sasa hali hiyo haipo kabisa pamoja na danganya toto za CDM kuhubiri uongo dhidi ya wanakigoma waliofukuzwa CDM.
 
Hivi unajua kama watu wanataka kukuibia alafu wakajua kuwa una bastola, hatua ya kwanza ni kuuawa ili usimzuru yeye hivyo ni bora usiwe nayo ili hata akitaka Mali kwako anaweza kuchukua alafu akakuacha
Mawazo gani haya sasa

Ukiwa na silaha ya moto kisheria huruhusiwi kuionyesha onyesha hovyo sasa watajua je kama unayo silaha?

Mwizi akija anaweza kukuibia hela, mali pamoja na kumgonga mkeo mbele zako na wakamaliza wakakufumua ubongo wako so usiwe na mawazo mgando kama hayo
 
Naombeni utaratibu wa kumiliki kabastola kwa sasa maana kipindi cha nyuma Nilichemka walaji walikua wengi.
 
Kumiliki pistol inahitaji umakini mkubwa sana na kwa dizaini ulivyoandika hiyo post ni wazi ukikabidhiwa hicho kitu unaweza ukajikuta umejiua. Achana na wazo hilo mkuu.
 
Kumiliki pistol inahitaji umakini mkubwa sana na kwa dizaini ulivyoandika hiyo post ni wazi ukikabidhiwa hicho kitu unaweza ukajikuta umejiua. Achana na wazo hilo mkuu.
Mkuu nipe maelekezo nimiliki chombo maana huwa napatwa sana na matukio ya kuvamiwa hasa kwenye biashara zangu
 
Mkuu ni process ndefu sana..... Inahitaji muda na fedha. Ngoja nikutag kwenye uzi unaozungumzia hizo taratibu.
 
Aaaah mimi ninayo Manati nne, Mishale seti tatu na Mikuki mitano vinatosha tu hakuna kukaa vikao na kamati hizo wala kupata leseni
 
Za asubuhi wanaJF. N siku nyingine tena mapambano yanaendelea. Tunapambana.

Nataka kumiliki bastola kisheria kwa ajili ya ulinzi binafsi kutokana na nature ya shughuli yangu.

1. Je, taratibu zake zikoje?

2. Gharama za kununua bastola zikoje?

3. Ipi bastola nzuri?

4. Kuilipia kwa mwaka ni TZS ngapi?

5. Mchakato mpaka unaimiliki unachukua muda gani?

6.Criteria au vigezo vya kuimiliki vikoje?

Naombeni mawazo yenu wakuu.

Asanteni.
 
Za asubuhi wanaJF. N siku nyingine tena mapambano yanaendelea. Tunapambana.

Nataka kumiliki bastola kisheria kwa ajili ya ulinzi binafsi kutokana na nature ya shughuli yangu.

1. Je, taratibu zake zikoje?

2. Gharama za kununua bastola zikoje?

3. Ipi bastola nzuri?

4. Kuilipia kwa mwaka ni TZS ngapi?

5. Mchakato mpaka unaimiliki unachukua muda gani?

6.Criteria au vigezo vya kuimiliki vikoje?

Naombeni mawazo yenu wakuu.

Asanteni.
Mkuu Si kila kitu tunaweza share hapa,kutokana na unyeti wake naomba ufike kwa mtu mwenye cheo cha msajili wa silaha pale polisi makao makuu ghorofa ya 5 utapata majibu yote.
 
Utaratibu mwingine utaupata Ofisi yoyote ya Mkuu wa Wilaya maana ndiyo watoa vibali vya kumiliki kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
 
Jamaa asubuhi asubuhi yote hii unaanza kuulizia upatikanaji wa bastola,vibaka walitikisa dirisha nini?
Hahaaaa.....kipindi hiki washauri wa kisaikolojia walitakiwa wawe wengi sana........mtu anaweza kumpiga mashine yeyote aliye mbele yake!

Nchi imetikiswa na inatikiswa

Dodoma a mfanyabiashara wa viroba alijiua baada ya biashara yake kuzuiwa na serikali,sasa hawa wa vyeti,bado wanaosumbuliwa na TRA usiku na mchana
 
Nenda kwenye maduka ya Tanganyika Arms yaliyo mkoani kwako au kama uko Dar unaweza kwenda kununua pale makao makuu ya jeshi Upanga.

Hapo watakutajia aina mbalimbali na kukupa uzishike na kuzikagua.

Kama kuna ambayo utaipenda unatakiwa kulipia full amount lakini huchukui silaha.

Baada ya hapo wanakupa fomu 1in 4 copies, ambayo utaenda nayo Serikali ya mtaa wako, Kamati ya usalama wa mtaa itakaa na kukujadili kama unastahili kupewa kibali na kama wameridhika Watasaini na kuzifoward hizo fomu katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo watazipitia na kukujadili tena na kama wameridhika na maelezo yako watazifoward katika Kamati ya Usalama ya mkoani na wao watakaa na kukuuta watakujadili tena na wataridhika basi na wao watazipeleka Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vile vile Uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya Usalama ya Mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya fomu kufika CPS wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyoilipia, Pamoja na kutabu cha silaha hiyo ambapo kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha kuna wengine imewachukua zaidi ya mwaka na wengine hata miezi 2 inategemeana na kujulikana kwako.

ANGALIZO: Bastola ni silaha ya kuua mtu siyo silaha ya kupewa kila mtu awe anaimiliki na ajibebe mfukoni kwenda nayo kwenye baa kutishia watu, hivyo Huko kwenye kuomba kibali si kila aombaye hupata. Labda silaha za kuwindia tu.

Nimeandika kadri zijuavyo, hivyo wataalamu wengine wataongezea. Kama kuna sehemu nimekosea nisahihishwe.
 
Back
Top Bottom