Polisi wamsaka aliyesalimisha silaha kanisani baada ya kuokoka

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
Polisi mjini Meru wanamtafuta mtu aliyesalimisha bunduki kanisani baada ya kutubu dhambi na kueleza kwamba ameokoka.

Kwa mujibu wa tovuti ya Taifa Leo imeandika kuwa jana Jumanne Februari 14, 2024 Polisi walipigwa na butwaa baada ya mchungaji Nathan Kirimi kufika katika Kituo cha Polisi cha Meru Central akiwa na bunduki aina ya AK47 na kueleza kwamba silaha hiyo ililetwa kanisani na muumini aliyekwenda kutubu dhambi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Imenti Kaskazini, Ezekiel Chepkwony amesema wakati Mchungaji Kirimi wa Huduma ya Jesus Winner alipofika kituoni hapo akiwa na bunduki hiyo walipatwa na mshangao.

Mchungaji huyo aliandikisha maelezo Polisi ambapo alisema kuwa wakati wa ibada ya Jumapili, kundi la waumini walikwenda madhabahuni wakitaka kumpa Yesu maisha, kisha walipiga magoti, naye kuwaongoza maombi ya toba.

“Kwa mujibu wa maelezo ya mchungaji huyo, baada ya ibada, mwanamume mmoja alimfuata na kumweleza kwamba alikuwa na ushuhuda na alitaka kusalimisha silaha,” amesema Kamanda Chepkwony kwenye mahojiano na Taifa Leo.

Ofisa huyo wa Polisi amesema bunduki hiyo inaonekana ilikuwa imefichwa mahali kwa muda mrefu au kufukiwa ardhini kwa sababu ilikuwa na kutu.
 
Hapo Polisi walitakiwa watoe pongezi na ushujaa kwa mchungaji na hata wakimpata mtuhumiwa wampongeze ikiwezekana waangalie maisha yake yalivyo kama yapo chini wampe mtaji
Mchungaji atakuwa aliweka nadhiri na mtu huyo kutomtaja,

Polisi watumie BUSARA kubwa kushughulikia issue hiyo Kwa USALAMA wa Mchungaji na USALAMA wa msalimisha silaha.
 
Duh! Hii habari inanikumbusha, niliwahi kuchora katuni/kibonzo kwenye gazeti moja hapa nchini ikionesha jambazi sugu likisema limeokoka mbele ya polisi wenye bunduki na kuwafanya polisi hao kushangaa mshangao mkuu na kudondosha bunduki zao chini wasiamini kuwa ni kweli jambazi sugu hilo limeokoka
 
Wataacha kuja kusema ukweli kwa Wachungaji.. na kuomba toba kimya kimya na kuyarusha kiujanja kwenye dustbin au poleni aunhata kuacha walipofukia.

Ila hawa watu hawana siri!!!.. na dude hata hawajakifanyia uchunguzi kwanza kimya kimya... Wajue ikoje imetumikaje. Kiwewe tu kitawaponza...
 
Polisi wako sawa, kitendo alichofanya kina legal implication, kanisani sio sehemu sahihi ya kusalimisha silaha, utaratibu kama huo ukiendelea mwingine anaweza kwenda kusalimisha silaha hospitali, shule au hata benki. Ikumbukwe polisi hakuna mambo ya baba mchungaji, inawezekana bunduki ikawa ni ya mchungaji na imetumika kufanya tukio mahali then mchungaji anaiwasilisha Polisi ku cover up.
 
Nafikiri Polisi wangetumia hii kama alama ya mfano, wangeitisha mkutano na waandishi wa habari wampongeze aliyesalimisha silaha na kuwasihi wengine wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha silaha zao pia.
The world is not black and white, but a more complicated gray.
 
Hiyo kaunti ndogo ya Imenti Kaskazini iliyotajwa kwenye habari ni Tanzania au Kenya?
 
Back
Top Bottom