BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
JESHI la Polisi nchini, limewataka watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwashambulia askari wanaobeba siliha kuacha tabia hiyo mara moja kwani sheria inamruhusu kutumia silaha hiyo kwa ajili ya kulinda uhai wake, uhai wa mtu mwingine na mali binafsi na za serikali.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ambapo amesema Askari Polisi wanapotekeleza majukumu yao wameruhusiwa na sheria kubeba silaha ili waweze kulinda Maisha ya watu na mali zao, kulinda Maisha yao na mali za serikali ikiwepo hiyo silaha.
“kumejitokeza mtindo wa baadhi wa watu ambao wamevunja sheria na wakati mwingine wanatenda uhalifu wa kujichukulia sheria mkononi, wanawashambulia askari akiwa amebeba silaha”
“Jeshi la Polisi linawataka watu wa aina hiyo kuacha hiyo tabia kwani askari ni binadamu kama binadamu mwingine na sheria inamruhusu kutumia silaha hiyo kulinda uhai wake, wa mtu mwingine na mali za mtu huyo na za serikali,” imeeleza taarifa hiyo.
NIPASHE