Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Je walio nje ya nchi wakija na miguu yao ya kuku wanafanyaje wakifika nchini mwao kwa likizo fupi?
 
wadau naomba mwenye majibu ya hili swali anisaidie,maana binafsi naona hayo siju wapi pa kununua,kusajiri na mengine ni additional tu.swali la huyu mdau ndo swali hasa.msaada jamani.
Cc,mbangaizaji,kitia ,mbu , zanziba na wengine

Unaweza kununua duka la silaha makao makuu ya jeshi upanga (mzinga) wao ni bei nafuu kidogo au Tanganyika Arms Karibu na Stesheni.
Ukinunua unaiacha Dukani unaondoka na risiti yako kwa ajili ya kufuatilia leseni ya umiliki wa hiyo silaha.
Ni vema ukimaliza nenda kituo cha polisi kikubwa: mfano pale central waone watu wa Arm licensing wakupe mahitaji yao kwa ajiri ya kupewa leseni.
Aanza na kufahamu eneo umaloishi na mjumbe wako, maana utaanzia huko hadi kupitia kamati za ulinzi na usalama zote kwa ajili ya clearance.
 
Ok ndugu ngoja nikupe utaratibu
Hatua ya kwanza nenda dukani kununua silaha uitakayo. Waweza kununua katika Duka la Jeshi au Tanganyika Arms pale nyuma ya stesheni kama upo Dar. Pia Tanganyika Arms wana Duka Arusha. Silaha nzuri na za kisasa zinauzwa Tanganyika Arms ila bei yao ni juu kidogo kwani zipo za kuanzia Ml.1.5 na kuendelea kutegemea na ubora wa silaha husika.
Ukishanunua unaiacha hapohapo dukani,wanakupa risiti na form za kuanzia process.
Hatua ya tatu unaenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kitengo cha IB. Ukifika pale Wizarani kwa ndani kulia utakuta kuna Tent,pale watakuchukua alama za vidole na wasifu wako.Baada ya siku 10 unaenda kuchukua karatasi inaitwa Police Clearance Certificate. Hii ni hati inayoonyesha kama una record yoyote ya uhalifu. NDIO maana walichukua finger prints zako ili ku-tress tabia yako. Ukiwa huna record yoyote mbaya ndio unapewa hiyo form,ni just page moja tu. Gharama yake ni tsh 2000 tu
 
Ukishapata hiyo Police Crearance Report ndio unarudi mtaani kwako ktk Serikali ya Mtaa. Kuna sehemu kwenye hizo form wanatakiwa wasaini Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa,agonge Muhuri na kuambatanisha Muhtasari wa Kikao cha Ulinzi na Usalama cha Mtaa. Hivyo Mwenyekiti ataita wajumbe wake mkae muongee,watakuuliza maswali ukiwa ' Hapo watajidai k
 
ikiwa ni pamoja na kuja nyumbani kwako kupaona. Ni lazima wakuombe rushwa hivyo jiandae na kama laki mbili na nusu maana watakwambia kikao hiki wewe ndio umekiitisha hivyo inabidi ukigharamie. Ukiwapa hiyo pesa unagongewa mihuri fasta ikiwa ni pamoja na kupewa huo muhtasari wa kikao ukiwa na majina ya wajumbe,namba zao za simu na saini zao.
Ukitoka hapo unakwenda Kata yako maana kwenye form Mao kuna Sehemu wanatakiwa wajaze,wapige Muhuri na kukupa Muhtasari wap. Ni kama ilivyokuwa Serikali ya Mtaa hivyo huko nako andaa mlungula.
 
Ukitoka Kata unakwenda kwa OCD wa Wilaya yako. Kumbuka hizo form unakuwa umeziambatanisha pamoja. OCD atakuhoji mawili matatu mfano kwa nini unataka kumiliki silaha nk,kuna sehemu anatakiwa asaini kwenye hizo form. Mlungula Polisi so suala la kuuliza hivyo jiandae.
Ukitoka hapo form unaziacha kwa OCD
 
OCD ndie atazipeleka Idara ya Usalama wa Taifa Wilaya. Wao watazipitia na watakupigia kukuhoji mawili matatu. Wakimaliza wanazirudisha kwa OCD.OCD na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya watakuita kwa mahojiano. Kutoka ulipoziacha kwa OCD mpaka upigiwe simu na Usalama wa Taifa inachukua kama miezi 3.
 
BAADA ya kikao cha Ulinzi na Usalama Wilaya ambapo OCD alishasaini,Mkuu wa Usalama Wilaya atasaini form zako kisha Mkuu wa Wilaya nae atasaini. Baada ya hapo form zako zitapelekwa kwa RPC atasaini, Mkuu wa Usalama Mkoa atasaini na kisha Mkuu wa Mkoa atasaini.
BAADA ya hapo form zako zitasonga mbele Makao Makuu ya Polisi zitasaini na wakubwa wa huko akiwemo DCI kisha Mkuu wa Usalama Taifa. Baada ya zoezi hilo ndio utaitwa na kupewa Barua ambayo utarudi nayo dukani uliponunua kwa uthibitisho kuwa upo safi. Dukani kuna simu watapiga ku-confirm then baada ya siku mbili tatu ndio watakuita na kukukabidhi Silaha yako. KWA kifupi ni zoezi linaloweza kuchukua kati ya miezi 9 mpaka miezi 12.
KAMA UNA swali uliza
 
OCD ndie atazipeleka Idara ya Usalama wa Taifa Wilaya. Wao watazipitia na watakupigia kukuhoji mawili matatu. Wakimaliza wanazirudisha kwa OCD.OCD na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya watakuita kwa mahojiano. Kutoka ulipoziacha kwa OCD mpaka upigiwe simu na Usalama wa Taifa inachukua kama miezi 3.
 
Hatimae Kama uliitaka kwa nia mbaya utakuwa umeshakata tamaa.


Aisee kwa mlolongo huo bora bei ishushwe sana.
 
Safi sana Mluhilamku, hizo ni hatua stahiki zinazotakiwa kufuatwa. Ila Kuna barua mbili, moja inaenda Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kuomba kupata kibali cha kumiliki silaha ikipitia kwa Mwenyekiti Wa Serikalini wa Mtaa na Kata. Ya pili ni ya mwajiri kukutambulisha
 
Kwa Wilaya zenye population kubwa zaidi ya huo muda mfano Dar, Arusha, Mwanza na Mbeya. Wilaya zake ni kubwa, mpaka watu wa Usalama wa Taifa wajihakikishie kuwa safi wa kupewa silaha ndiyo wanapeleka kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.
 
Back
Top Bottom