Mbio za silaha zinazoongozwa na Marekani zinaweza kuangamiza jamii ya binadamu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,029
1,051
1716186026440.png


Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Utafiti wa Amani Duniani ya Stockholm, matumizi ya jumla duniani katika mambo ya ulinzi kwa mwaka 2023 yalifikia dola za kimarekani trilioni 4.44. Tathmini hiyo ya mwaka ya Mwelekeo wa Matumizi ya Kijeshi Duniani ya Taasisi hiyo imehitimisha kuwa, kiasi hiki ni cha juu zaidi katika matumizi ya kijeshi kwa mwaka tangu mwaka 2009, na hakuna wakati ambao binadamu ametumia fedha nyingi kiasi hicho katika operesheni za kijeshi.



Bila shaka, viongozi wa dunia wanaweza kuwa na sababu nzuri ya maamuzi yao ya kuongeza dau katika ushindani wa kijeshi duniani, kwa kuwa mara nyingi kabla, wamekuwa wakihusika na mchezo wa kutupiana lawama huku wakiwa na nia dhahiri ya kulazimisha wajibu wote wa mbio za silaha kwa wapinzani zao wa kijiografia. Hata hivyo, data halisi zinaacha nafasi ndogo sana ya kuwa na sintofahamu, kwani Marekani inaendelea kuwa kiongozi asiyepingika duniani huku bajeti ya Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo ikifikia dola za Marekani bilioni 916. Kiasi hiki kikiongezwa na kile cha bajeti za ulinzi zinazoongezeka kwa kasi katika nchi kama Japan, Korea Kusini na Australia, ni wazi kuwa wajibu usiopingika wa dunia ya Magharibi katika mbio za silaha duniani utaonekana kidhahiri zaidi.



Mwelekeo huohuo wa wazi unaweza kufuatiliwa katika mbio za silaha duniani. Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Amani Duniani ya Stockholm, katika miaka mitano iliyopita, usafirishaji wa silaha kwa nje uliofanywa na Marekani umeongezeka kwa asilimia 17, na nafasi ya soko la silaha la Marekani duniani imeongezeka kutoka asilimia 34 hadi 42. Takwimu zinazohusu Jumuiya ya NATO nazo zinajieleza, kwani nafasi ya Jumuiya hiyo katika kutoa silaha kwa nchi za kigeni kati ya mwaka 2019 hadi 2023 imeongezeka kutoka asilimia 62 hadi 72. Makadirio mengi yanapendekeza kuwa Marekani na wenza wake wataendelea kuimarisha nafasi zao katika utoaji wa silaha kwa dunia nzima.



Licha ya madai mengi kwamba Marekani daima inapinga kueneza silaha za nyuklia, rekodi ya ufuatiliaji wa Marekani kuhusu kutoeneza silaha hizo inatia mashaka. Kwa mfano, uamuzi wa utawala wa rais wa Marekani Joe Biden wa kuipatia Australia nyambizi tatu zinazoendeshwa kwa nguvu ya nyuklia itakapofika miaka ya 2030 unaibua wasiwasi kuhusu hatma ya baadaye ya kutoeneza silaha za nyuklia.



Tathmini ya Taasisi ya Utafiti wa Amani Duniani ya Stockholm inaunganisha kwa usahihi ongezeko la masuala ya ulinzi na mapigano katika maeneo kama Ukraine na Palestina, na pia kuongezeka kwa mvutano katika maeneo mengine duniani. Uwezekano wa mwaka huu wa 2024 kuwa mwaka wa uamuzi wa kubadilika kutoka vita na migogoro na kuwa na amani na maridhiano ni mdogo sana, kwani hata kama migogoro inayoendelea duniani itamalizika, bado mbio za silaha duniani zitaendelea. Makombora ya kimkakati, nyambizi za mashambulizi, na ndege za mizigo zinazosanifiwa siku hizi zina uwezekano mkubwa wa kutumika kikamilifu katika miaka 15 hadi 20 kuanzia sasa, na zinaenda kupanga mandhari ya mkakati wa sunia kwa sehemu kubwa ya nusu ya pili ya karne ya 21.



Mwendelezo wa mbio za silaha unapaswa kuchukuliwa kama tu sio sehemu ya kutokuaminiana, mivutano na migogoro ya kijeshi, bali pia kama chanzo kikuu cha hayo yote. Katika dunia iliyojaa mifumo hatari iliyo tayari kutumika wakati wowote, matishio ya ajali na vita isiyo na sababu yanaweza kuwa makubwa zaidi. Pia kuongezeka kwa siasa za kijeshi duniani kunabadilisha uhusiano wa kimataifa kuwa mchezo usiokuwa na faida, ambapo lengo sio kutatua tatizo gumu, bali ni kumshinda mpinzani.
 
Back
Top Bottom