Tanzania yatumia zaidi ya shilingi bilioni 6 kutunza vyura 500 waliopelekwa Marekani

Lyagushki.jpg

Kupitia ukagauzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/2022 imebainika kuwa Vyura 500 bado wapo Marekani licha ya kumalizika kwa mkataba wa matunzo.

Serikali ilipeleka Vyura hao katika bustani za Bronx na Toledo ili kupisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha Umeme katika Bwawa la Kihansi miaka 22 iliyopita kwa mkataba ulioisha mwaka 2020 na ikaongeza miaka miwili hadi mwaka 2022.

CAG amesema pamoja na kuisha kwa mkataba huo, bado hakuna taarifa za kurejeshwa kwa Vyura hao Nchini huku idadi yao ya sasa ikiwa haijulikani.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,810
18,543
Ripoti ya CAG imebaini kuwa kwa miaka 22 (2000-2022), Tanzania imetumia TZS bilioni 6.69 kutunza vyura 500 iliowapeleka Marekani ili kuepuka hatari ya kupotea kutokana na utekelezaji mradi wa umeme wa Kihansi.

Hata hivyo, idadi yao kwa sasa haijulikani, na mkataba wa kuwepo Marekani umekwisha.
 
Mtapost sana haya Mambo ila nchi imejaa Mazezeta wacha wajipigie
 
Jamani tupo busy kukemea ushoga na usagaji hayo mambo sio kipaumbele chetu kabisa, waache wakae hata miaka 100
 
Kwahiyo hao chura hawakupata eneo lingine la kuhifadhiwa hapahapa Tanzania mpaka USA tu!???🤗
 
6,000,000,000/(22x365) unapata 747,198. Gharama ya kumtunza vyura 500 kwa siku USA

747,198/500=1494

Sh 1494 ni gharama ya kumtunza chura mmoja kwa siku USA. Mbona ni kama ya kawaida?
 
6,000,000,000/(22x365) unapata 747,198. Gharama ya kumtunza vyura 500 kwa siku USA

747,198/500=1494

Sh 1494 ni gharama ya kumtunza chura mmoja kwa siku USA. Mbona ni kama ya kawaida?
Kwa hiyo unaona ni sawa gharama hizo kupotelea nje? kwanini wasijengewa eneo jirani na Kihansi?
 
Kwa hiyo unaona ni sawa gharama hizo kupotelea nje? kwanini wasijengewa eneo jirani na Kihansi?
Kama wana Uwezo wa kuwajengea eneo jirani lenye vigezo vya UNESCO na hawakufanya hivyo hapo tutalaumu lakini kama hatuna Uwezo huo basi ni sahihi kuwapeleka USA
 
Vurugu za Simba na Yanga rais yupo mstari wa mbele. Ila hela zinaibwa anajidai kafunga swaumu
Jamani Rais nae kakemea wizi,tena kawaambia wezi ni ma stupid na Wapumbavu tena kasema live kwenye TV! Acheni kumuonea Mama wa Watu bure! Mnataka Mama awatumbuwe wezi alafu mumchukie Kama mlivyomchukia Mwendazake kisa kuyatumbua Mafisadi!!?
 
Vyura Wanakula Cash Halafu Wahuni Wanapigiemo Ooop Nchi Imefunguka Itakuwa Kama Bwawa
 
Yaani tuna wwkimbizi mpaka vyura
Hongera sana Tz kwa kuweza kuweka vyura kinyemela

Nearly 7b zimepotea kupitia kwa wajanja
Kweli watu wanapiga hela utafikiri wananusa
Screenshot_20230408_131437_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom