Marekani kulipa Tanzania Msaada wa Shilingi Bilioni 980 Kusaidia Mapambano ya UKIMWI

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Serikali ya Marekani imesema itatoa Shilingi Bilioni 980 Ili kusaidia Tanzania kupambana na mambo ya Ukimwi Mwaka wa Fedha ujao wa 2024/25.

Swali.
Kwani Serikali Hamuwezi kuwa na vipaombele tofauti na hivi vya Ukimwi?

Yaani Bilioni 980 itaishia kwenye mambo yafuatayo,
-Semina na warsha
-Elimu Kwa Umma
-Posho
-Condom
-ARVs.

My Take
Vipaombele ambavyo havijengi uwezo ndio Mabeberu wanapenda sana Ili tuendelee kuwa tegemezi. Hii sio sawa.

==============
Serikali ya Marekani imepanga kuipa Tanzania kiasi cha fedha Tsh: Bilioni 980 kwa mwaka 2024/25 ili kusaidia kutekeleza vipaumbele vya Serikali kupitia Wizara ya Afya katika kupambana na VVU na UKIMWI hapa nchini.

Waziri Ummy amesema hayo leo Machi 25, 2024 wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya PEPFAR kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar Es Salaam.

“Tunaishukuru sana Serikali ya Marekani kwa kuendelea kuipatia Tanzania msaada kwa zaidi ya miaka 20 kwa ajili ya kupambana na Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI, ambapo kwa sasa watatusaidia Bilioni 980 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.” Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuyafikia makundi ambayo bado yana maambukizi mapya kwa kiwango kikubwa kama vile wasichana rika balehe na wanawake vijana (AGYW) pamoja na vijana rika balehe na wanaume vijana (ABYM).

Kikao hicho kimehudhuriwa na Balozi wa Marekani Nchini Mhe. Michael Battle na Mtendaji Mkuu wa PEPFAR Duniani Balozi Dkt. John Nkengasong ambapo kwa pamoja wamejadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano huo baina ya Tanzania na Marekani katika Sekta ya Afya.

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Michael Battle ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kufanya vizuri katika kufikia malengo ya asilimia 95 tatu.
 
Ila serikali yetu wachoyo sana hizo pesa lila leo wanakopa wanafaidi wenyewe huko ju wangekua mara mojamoja wanatugawia na sisi jameni yaani hali ngumu alafu wenzetu wanafaidi wenyewe tu.
 
Tangu lini msaada unalipwa?? Kama Hawa ndiyo Watanzania wapiga kura basi majizi yataongoza hii nchi mpaka basi
 
Back
Top Bottom