ripoti ya cag

  1. K

    Watu Wamepoteza Mwamko wa Kusikiliza Ripoti ya CAG

    Ni takribani miaka mitatu sasa CAG amekuwa akitoa taarifa zilizojaa madudu ya ufisadi na rushwa pasi na mamlaka ikiwemo serikali kuchukua hatua yeyeote kukabiliana na tuhuma hizo kwa kipindi chote hicho. Imefikia hatua sasa wananchi wamepoteza kabisa imani ya kuendelea kusikiliza ripoti...
  2. ACT Wazalendo

    Ripoti ya CAG, Kazi Inaendelea ya Kufuja Fedha za Umma

    Maeneo kumi (10) muhimu katika Uchambuzi wa Ripoti ya CAG mwaka 2022/23. Kama ambavyo tumekuwa tukifanya kila mwaka, uchambuzi wetu mwaka huu utajikita kwenye mambo kumi (10) ambayo tunaona ni muhimu Watanzania kuyatambua na tutayatolea mapendekezo ili yaweze kuchukuliwa hatua. Katika...
  3. Roving Journalist

    Act Wazalendo inafanya uchambuzi wa ripoti ya CAG

    Act Wazalendo inafanya uchambuzi wa ripoti ya CAG https://youtube.com/live/NUZV2KCIntw?si=tEvs29-aBxTF6TT9
  4. Msanii

    Ripoti ya CAG. Tunaishia kupiga kelele na hatuna la kuwafanya. Kuna ukweli...

    Kibonzo cha msanii Massoud Kipanya kinafumbua fumbo lisilojadilika. Nani mwenye uthubutu? Hata Rais mwenyewe anaonekana kuvuta miguu kwenye kuwachukulia hatua wabadhirifu waliotajwa kuhusika na ukwapuaji wa fedha za umma. Tutafakari pamoja..... Je, tunajadili kama wananchi kwa lengo gani...
  5. Joram Mtanzania

    Kuna hasara mashirika ya umma kwa kuwa hakuna uwajibikaji

    Kitu kikubwa nilichogundua ni kuwa, Namna pekee ya Kuyaokoa mashirika ya serikali yanayo andamwa na hasara kubwa ni namna ya kupata waendeshaji wawajibikaji. Imekuwa ni kawaida sana Kipindi hiki cha Uongozi wa Rais Samia Watu kubadilishiwa vitengo tu badala ya kuwajibishwa. Utakuta Kiongozi...
  6. Kaka yake shetani

    Kila ripoti ya CAG inapotolewa ubadhirifu wa pesa ni mkubwa lakini pesa hizo mtaani na kwenye mzunguko hakuna

    Madudu na mawashawasha ya ripoti za CAG nyingi tunasikia ubazilifu mkubwa kila kona pesa ambazo zimetumika vibaya ila cha kushangaza huku mtaani hakuna mwenye pesa kwa wale mimi na wewe. Kipindi cha jakaya angalau tumeona pesa ilikuwepo na maisha kwenye mzunguko ukilinganisha JPM na Samia...
  7. Erythrocyte

    Ushauri: Ripoti ya CAG isirudiwe tena kusomwa hadharani, inatia hasira na kuleta manung'uniko, wanaotuhumiwa hawajawahi kukamatwa

    Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua. Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti...
  8. Heparin

    Ripoti ya Ukaguzi wa CAG kwa Mwaka 2022/23 kutua kwa Rais wiki hii

    MKUTANO wa Bunge la Bajeti umepangwa kufanyika kuanzia Jumanne ya juma lijalo. Pamoja na mambo mengine, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2022/23 itawasilishwa kwa mujibu wa sheria. Ibara ya 143 ya...
  9. Pfizer

    Azim Dewji: Siku za Nyuma ripoti ya CAG ilikuwa Siri. Wanaochezea pesa za miradi watungiwe Sheria kali

    Mfanyabiashara maarufu nchini, Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuruhusu mjadala wa ripoti ya CAG unaoendelea bungeni kuwa mjadala wa wazi, amesema uwazi huo utasaisia wezi wa pesa za miradi kuacha tabia hiyo Kwa upande mwingine...
  10. Pascal Mayalla

    Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika

    Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa...
  11. Petro E. Mselewa

    Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

    Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG). Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge...
  12. BARD AI

    Spika Tulia: Wabunge hawasemi uongo, Ripoti ya CAG inaonesha kuna ubadhirifu

    Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema kutokana na mjadala wa Wabunge kuonesha Halmashauri nyingi zina Ubadhirifu mkubwa, anapata wakati mgumu kusikia kauli za Mawaziri wakisema Wabunge wanasema uongo wakati taarifa za Kamati zinaonesha kuna ubadhirifu katika Halmashauri hizo. Akitolea...
  13. R

    Luhaga Mpina: Hakuna hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka Ripoti ya CAG itolewe Machi 2023

    Luhanga Mpina akitoa mchango wake amesema, amesoma taarifa ya CAG mwaka 2021, amesoma majumuisho ya majibu ya serikali na mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG, hakuna sehemu kwenye majumuisho ya mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG inayoonesha hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka...
  14. R

    Waitara: Wote waliothibitika kuiba fedha za serikali wanyongwe!

    Msikile Waitara akitema cheche hapa Asema watanzania wengi wanaisha maisha ya ufukara sana kiasi cha kushindwa hata kuwalipia ada watoto wao na kwenda kuomba msaada wa kufanikishiwa jambo hilo, akisema watumishi wa umma wote wanasomeshwa na watanzania na wana elimu ya kutosha, na kwamba...
  15. S

    TBC yakata matangazo Bunge likijadili ripoti ya CAG

    Shirika la Umma la TBC limekata matangazo ya Bunge muda huu wakati wabunge wakijadili Ripoti ya CAG, kwanini TBC chombo cha umma kizuie wananchi wasiangalie wabunge wakijadili ripoti ya CAG? Au ni maelezo ya Nape kuwalinda rafiki zake walioguswa na ripoti ya CAG?
  16. Roving Journalist

    Taarifa ya kamati kuhusu ripoti za CAG kwa hesabu zilizokaguliwa za serikali kuu na mashirika ya umma kwa mwaka 2022

    Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 3, leo Novemba 2, 2023. https://www.youtube.com/live/Px2Csdrfk20?si=ydhC7gCMmMBrjxso === TAARIFA YA KAMATI KUHUSU RIPOTI ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA HESABU ZILIZOKAGULIWA ZA SERIKALI KUU NA MASHIRIKA YA...
  17. tawakkul

    Wangapi wametumbuliwa na kushitakiwa kutokana na Ripoti ya CAG 2022?

    Habari wakuu, Hii ripoti ilisababisha mvutano mkubwa na mpaka wanaojitambua kutaka kulazimisha bunge kuijadili kabla ya muda wake. Hivi wale walichezea pesa zetu, kodi zetu kwa maslahi yao na familia zao wamechukuliwa hatua gani? Au ni siri na hatupaswi kufahamu? Tuliambiwa tusubiri bunge la...
  18. Burkinabe

    Spika Dkt. Tulia usijisahaulishe; Novemba ilee, tunasubiri mjadala wa wazi na huru Ripoti ya CAG

    Asalam Aleykum wapenzi wana JF. Ama baada ya salamu hizo, nitumie nafasi hii kumkumbusha Spika wa Bunge la JMT mh. Dk. Tulia Acson kuhusu ahadi yake aliyoitoa mnamo mwezi Aprili kuhusiana na mjadala wa Ripoti ya CAG iliyotolewa mwaka huu 2023. Dk. Tulia Acson katika kuwanyamazisha badhi ya...
  19. Msanii

    Ripoti ya CAG, je jeshi la Polisi, TAKUKURU wanatimiza wajibu wao?

    Mdhibiti na mkaguzi wa fedha za umma amekuwa anatoa ripoti za ukaguzi wa matumizi na mapato ya serikali na matumizi ya serikali. Kila ripoti imejaa ushahidi tena wa kitaalam namna ambavyo fedha ya umma imetumika ama kuchezewa kupitia vote mbalimbali zilizopitishwa na Bunge. Jambo la kushangza...
Back
Top Bottom