Tanzania kuingia Uchumi wa Kati maana yake nini?

Seems ameumia sana na hii issue ya Middle Income.

Sidhani kama kuna mtu anahitaji kujua hizo "mboyoyo" kwa sasa!

Habari ya mjini ni kuwa MI hizo porojo zake ni inconsequential tu kwa sasa.
 
Kwa sababu mwanaume aliyekua amuoe amekuoa wewe.
We utakuwa shoga yake nini ndio maana unajua hayo mambo? sema umenifananisha mie kidume nataka nijiweke hapo kwa shangazi Fatma,nimemuelewa sana na naahidi kumuondoa stress zote.
 
Hongera serikali, hongera rais wetu kipenzi JPM.

Picha hizi hapa.

FB_IMG_15936344211148271.jpeg
FB_IMG_15936344102287425.jpeg
 
Tunatisha sana kwakweli,hapo Bwawa la Mwalimu Julius nyerere halijaanza kazi,kwakweli hatukamatiki...
 
Hiki ni kipimo kinachotumika kuonesha mapato yote ya Nchi yanayotokana na pato la mtu mmojammoja na biashara pamoja na yale yanayotokana na vyanzo vya nje. Ni kipimo kinachoendelea sana na Benki ya Dunia pamoja na Umoja wa Nchi za Ulaya katika kupima na kufuatilia utajiri wa Nchi na mchango wa Nchi wanachama kila mwaka.

Kipimo hiki ni mbadala wa kipimo kinachopima jumla mapato ya ndani " Gross National Product (GDP) kwa sababu kinaonekanana kuwa na usahihi zaidi katika kuonesha picha ya utajiri wa Nchi.

Benki ya Dunia kwa kutumia njia iitwayo " Atlas" hufuatilia utajiri wa Nchi nyingi Duniani ikiwemo Tanzania.Kipimo hiki huwza kubadilishwa na kuwasilisha utajiri wa Nchi kwa kutumia kizio cha Dola za Kimarekani.

Kipimo hiki cha "GNI" kinauonesha ukuaji wa Tanzania kama ifuatavyo:

Mwaka 2015 kilionesha ukuaji wa dola 980 sawa na 5.15% ukilinganisha na mwaka 2014 lakini Mwaka 2016 ukuaji ulishuka na kuwa dola 970 sawa na 0% ukilinganisha na mwaka 2015 japokuwa Mwaka 2017 ukuaji ulikuwa dola 970 asilimia za ongezeko zilikuwa 1.02%,taarifa za mwaka 2018 zinaonesha ukuaji ilifikia dola 1020 sawa na ongezeko la 1.03% ukilinganisha na mwaka 2017.

Taarifa zinadhihirisha kuwa mwaka 2017 ndipo Nchi ya Tanzania ilipoweka mipango madhubuti na malengo ya kuingia kwenye orodha ya Nchi za uchumi wakati mwaka 2025 lakini kufikia mwaka 2020 tayari Benki ya Dunia imedhihirisha kuwa Tanzania ina sifa za kuwa Nchi ya uchumi wa kati ambazo kwa mujibu wa kipimo cha GNI zina utajiri wa unaovuka dola 1006 yaani dola (1006 mpaka 3955).

Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki viongozi wake.
 
Habarini!
Sina elimu kabisa ya masuala ya uchumi, ni mwendo wa kusikia na kushabikia tu.
taarifa zinasema tumeingia uchumi wa kati jana, benki ya dunia (WB) nasikia ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Sijui maana ya uchumi wa kati,
sijui vigezo vya uchumi wa kati,
sijui faida za uchumi wa kati.

Hili jukwaa limejaa wabobezi wa kila namna, nina uhakika na hilo kwa 100%
naomba, ukiwa free of politics na vitu vingine, unipatie elimu kuhusu hili suala.

NB:
Kumuelimisha mtu ni ibada kubwa sana kwa mwenyezi Mungu!
ahsanteni sana!!
 
Wanabodi,

Uchumi unapimwa kwa vigezo vingi sana lakini vikubwa ni viwili ambayo Benki ya Dunia na IMF wanatumia navyo ni:

GNI(Gross national income) pamoja na GDP(Gross domestic product)

Kwa mujibu wa Taarifa ni kwamba GNI ya Tanzania imeongezeka na kufikia kwenye midhania ya viwango vya Benki ya Dunia ya uchumi wa kati.

GNI ni kitu endelevu

GNI au Gross national Income ni jumla ya mapato yote yanayoingia nchini au yaliyotengenezwa nchini na watu ambao ni Raia wa Tanzania au ambao sio Raia wa Tanzania

Mapato yanayoongelewa kwenye GNI ni kama ifuatavyo:

Haya mapato yanaongeza GNI na kuifanya kuwa kubwa hivyo kufanya Taifa la Tanzania kufikia uchumi wa kati

Foreign Aid au Misaada yote tunayopokea toka kwa wahisani toka nje. Hii misaada inaongezwa kwenye GNI na kuifanya ionekane GNI imeongezeka.

FD's (Foreign direct investment) huu ni uwekezaji wa moja kwa moja toka nje ,Thamani ya uwekazaji huu nayo inaongezwa kufanya GNI iwe kubwa

Pesa za Watanzania waishio nje au Makampuni ya Kitanzania yaliyo nje ya nchi ambazo pesa wanazituma moja kwa moja Tanzania. Hizi pesa nazo zinaongezwa kwenye GNI na kuifanya iwe kubwa.

Riba(Interest) pamoja na hisa ambazo nchi inapokea kwenye uwekezaji mbalimbali kwenye hati fungani za muda mfupi(bills) au hati za muda mrefu(Bonds). Hizi riba na hiza zinaongeza GNI na kuifanya iwe kubwa.

Mapato yafuatayo yanapunguzwa kwenye mahesabu ya GNI na kuifanya GNI kuwa ndogo au Yanaondolewa wakati wa mahesabu ya GNI.

Mapato yote ambayo wawekezaji wa kigeni waliopo Tanzania au Raia wa kigeni kipato wanachokipata Tanzania yanaondolewa kwenye kufanya mahesabu ya GNI.

GDP au Gross domestic product ni thamani ya bidhaa au huduma kwa bei ya soko kwa wakati huo. Hapa zinaongelewa thamani ya bidhaa au huduma zilizozalishwa kwa muda fulani mfano mwaka mmoja,Hizi ni bidhaa za ndani.

Kuna utofauti mwembamba sana kati ya GDP na GNI, GNI inachukua thamani na zile za nje

Benki ya dunia wanachofanya kupima uchumi ni kama ifuatavyo

GNI=GDP+ (Foreign aid,Foreign investment+interest+..............)

Je, GNI ya Tanzania imekua na kutufikisha uchumi wa kati?

Maswali yafuatayo ni muhimu kujua kama kweli tumefika uchumi wa kati

Je, uwekezaji toka nje umeongezeka Tanzania?

Je, mikopo na misaada imeongezeka Tanzania?

Je, uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani umeongezeka Tanzania?

Je, diaspora au watanzania toka nje wanaleta vipato nyumbani?

Katika awamu ya Tano ya JPM ni kweli kuna uwekazaji mkubwa sana kwenye SGR, barabara na sehemu kadhaa. Yote hayo yanaongeza GNI.

Kama Jibu ni ndiyo basi mambo mazuri.

Benki ya dunia wamegawa hivi vipato kwa madaraja matatu.

Low, Middle na High

Kuongezeka kwa GNI au kufika uchumi wa kati siyo kigezo kuwa maisha ya mtu mmoja mmoja yamekuwa mazuri au Nchi yetu siyo maskini.

Qatar ni moja ya nchi yenye GNI kubwa kutokana na visima vya mafuta au oil reserves.

Qatar kidogo GNI yao inafanana na Maisha ya Raia wake

Nchi kama kenya wao wapo uchumi wa kati siku nyingi lakini ni maskini wa kutupwa sana

Naomba tuendelee kujadili kwa lugha rahisi ili kuelimisha wengi juu na maana ya uchumi wa kati.

Nadharia za uchumi hasa GNI na GDP zina mapungufu yake mengi Sana. Mara nyingi nadharia hizi zinashindwa kuhusianisha ukuaji wa uchumi na Maisha ya mtu mmoja mmoja.

Wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia zaidi,Sisi wengine hatujasoma uchumi bali tunaelezea jinsi mambo yalivyo na yanavyofanyika World Benki na IMF

Watanzania wengi wanashangilia hasa wanasiasa sidhani kama wanaelewa maana halisi ya uchumi wa kati kwa hivi vipimo vya GNI vya Benki ya Dunia na IMF

Huu ni ushauri pia umetolewa na Mwana JF ambao nchi zao ziliingia matatizo kwa kufikia uchumi wa kati soma
Tanzania Chungeni mambo ya Eurobond
 
Mimi ninachofahamu ni kwamba tumeingia kwenye uchumi wa kati. Tuamini hivyo na tujiamini
 
Back
Top Bottom