Tanzania kuingia Uchumi wa Kati maana yake nini?

Oct 7, 2019
51
156
Jumatano tarehe 1 Julai, 2020 Benki ya Dunia iliitangaza rasmi nchi ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya muda ambao Tanzania ilijipangia katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025

Hakika hii ni jambo la kufurahiwa na kila mtanzania kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa, "Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya."

Licha ya Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati, lakini je ni wangapi kati yetu tunafahamu maana ya Tanzania kuingia uchumi wa kati?

Ni vema basi kujuzana maana ya hili ili watanzania tutambue nafasi yetu na wajibu wetu kama wananchi.

Benki ya Dunia (World Bank) sambamba na Umoja wa Mataifa (United Nations) zimeainisha vigezo vitatu ambavyo hutumika kuzipima nchi na kuzipa daraja la ufaulu kuingia katika uchumi wa kati na kuendelea

Tafsiri ya vigezo hivyo pia imehanikizwa na Ofisi ya Mwalikishi wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea, Zisizounganishwa moja kwa moja na bahari na Visiwa Vidogo, nchi zinaweza kuhitimu kutoka kuwa nchi zinazoendelea mpaka kufikia kuwa nchi zenye uchumi wa kati kwa vigezo vikuu vitatu.

Kwa upande wa Umoja wa Mataifa (United Nations) vigezo hivi vimeainishwa na Kamati kwa ajili ya Sera ya Maendeleo (Committee for Development Policy) kwa kifupi CDP ya Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC).

Vigezo hivi ni wastani Pato la kila mwananchi yaani 'Gross National Income' kwa kifupi GNI per capita kwa mwaka, Uwekezaji kwa watu 'Human Assets Index' kwa kifupi HAI na Kiwango cha uhimilivu wa nchi kiuchumi endapo itakumbana na majanga au mitikisiko ya nje yaani 'Economic Vulnerability Index' ambayo ni matukio yote yanayozorotesha uchumi kama vile vimbunga, magonjwa kama Covid 19, mafuriko na tetemeko la ardhi.

(1) WASTANI WA PATO LA KILA MWANANCHI
Wastani wa pato la kila mwananchi hutumika kupima ukuaji wa nchi kiuchumi. Wastani wa pato la kila mwananchi hupatikana kutoka katika pato la nchi kwa ujumla ambalo hujumuisha mapato yote ya nchi yaliyozalishwa na wakazi wa nchi husika na biashara mbalimbali za halali zilizomo ndani ya nchi hiyo sambamba na pato lililochumwa na raia wa nchi husika waliopo nje ya nchi. Jumla ya mapato yote hayo hugawanywa kwa idadi ya watu waliomo katika nchi husika kupata wastani wa pato la kila mwananchi katika nchi hiyo.

Kwa mantiki hiyo, wastani wa pato la kila mtanzania kwa mwaka ni sawa na kuchukua mapato yote ya ndani ya Tanzania kujumlisha na yale ya watanzania waliopo nje ya nchi na kisha kugawanya kwa idadi ya watanzania wote takribani milioni 59.

Benki ya Dunia hutumia kipimo kinachojulikana kama "Atlas Method" kupata pato la kila mwananchi katika nchi husika.

Hivyo basi kupitia kipimo hiki cha Atlas cha Benki ya Dunia, Tanzania imekuwa na wastani wa pato la kila Mtanzania linalofikia Dola za Marekani 1,044 na hivyo kuifanya Tanzania kuingia katika kundi hilo lenye kiwango cha kati ya Dola 1,036 mpaka Dola 4,045.

(2) UWEKEZAJI KWA WATU
Uwekezaji kwa watu hujumuisha maeneo makuu mawili ambayo ni elimu na afya. Katika elimu na afya kuna vitu kadhaa ambavyo hutazamwa kama vile, chakula, lishe, kiwango cha watu wazima wanaojua kusoma na kuandika, matarajio ya umri wa watu wazima na watoto wa umri chini ya miaka mitano hadi 14 kuishi, kiwango cha kalori kinacholiwa na mtu mmoja mmoja na kiwango cha udahili katika elimu ya msingi na elimu ya juu.

Kwa kuzingatia uwekezaji kwa watu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imeielekeza nchi katika malengo manane ambayo ni; mosi, nchi kuwa na chakula cha kutosha sambamba na usalama wa chakula hicho. Pili, elimu msingi bure ikiwa na lengo la kuondoa ujinga na kufikia ngazi ya elimu ya juu na mafunzo ambayo yatalenga kutoa rasilimali watu ya kiwango cha juu itakayoweza kujibu na kumudu changamoto za maendeleo katika ngazi zote nchini.

Tatu, dira inaielekeza serikali kuhakikisha kuwa nchi inafikia usawa wa jinsia na uwezeshwaji kwa wanawake katika maeneo yote ya mahusiano ya kijamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Lakini pia dira inaielekeza serikali katika kuhakikisha kuwa inaongeza upatikanaji wa huduma bora za msingi na zenye kutosheleza za afya na maji kwa watu wote sambamba na upatikanaji wa huduma za afya bora ya uzazi kwa watu wa rika zote.

Pamoja na hayo dira inaielekeza serikali kuweka mikakati thabiti ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa robo tatu ya kiwango cha sasa na ikielekeza matarajio ya watu kuishi yafanane na kiwango kilichofikiwa na nchi za uchumi wa kipato cha kati na kuondoa umasikini wa kiwango cha juu.

Kufanikisha azma hii serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye elimu kwa kuhakikisha sera ya elimu msingi bure bila malipo inatekelezwa kwa kila Mtanzania kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne.

Serikali inatoa kiasi cha shilingi Bilioni 23.8 kila mwezi kugharamia elimu msingi bure.

Mbali na hilo serikali imetumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 20 kukarabati shule kongwe 17 nchini ili kuziweka katika mazingira bora ya kufundishia.

Serikali pia inatoa wastani wa kiasi cha Bilioni 450 za Kitanzania kila mwaka kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
Uwekezaji huu katika elimu unalenga kujibu hoja zilizoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Katika afya serikali imefanya makubwa sana kwa kuongeza bajeti ya afya kutoka Shilingi Bilioni 30 mpaka Bilioni 270 kwa mwaka.

Serikali imeweza kujenga vituo vya afya 352 na hospitali 69 kote nchini huku nyingine zikiendelea kujengwa ikiwemo hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambayo ujenzi wake utagharimu shilingi Bilioni 16 ikikamilika.

Maana ya uwekezaji huu ni kwamba dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya zinaendelea kuongezeka na hivyo kupunguza pengo la upatikanaji dawa na vifaa hivyo.

Lengo la haya yote ni kumfanya Mtanzania afanye kazi kwa bidii ili hata anapopata changamoto ya kiafya aweze kupata huduma bora, stahiki na ya bei nafuu.

Mbali na vigezo hivyo katika afya na elimu vinavyotumiwa na Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa, Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa pia katika miundombinu wezeshi ya kiuchumi kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwana kufua umeme la Mwalimu Nyerere katika Bonde la Mto Rufiji ambalo linatarajiwa kuzalisha Megawatt 2115 huku likitarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi trilioni 6.5.

Ujenzi wa bwawa la kufua umeme utaenda kushusha bei ya umeme hivyo kufanya gharama za uzalishaji wa bidhaa viwandani kushuka na hatimaye bei za bidhaa kushuka na hivyo kuvutia zaidi wawekezaji.

Mbali na hilo, serikali imefanikiwa kupeleka umeme katika vijiji 9112 hadi kufikia mwezi Aprili kutoka vijiji 2018 mwaka 2015 na hivyo kubakiwa na vijiji 3,156 kati ya vijiji 12, 268 vilivyopo Tanzania.

Maana ya hili ni kuwa uchumi wa vijiji unaenda kukua na hivyo kuleta athari chanya kwa mtu mmoja mmoja.

Kwa mfano kuna mikoa ambayo wananchi walikuwa wakivua samaki na kushindwa kuwahifadhi kwenye majokofu kabla ya kuwauza na hivyo kuingia hasara kutokana na samaki kuoza, kwa uwepo wa umeme kutawawezesha kuhifadhi samaki na hivyo kujiongezea kipato.

Sambamba na hayo, ujenzi na ukarabati mkubwa wa meli, upanuzi wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ujenzi wa barabara na madaraja kama vile Mfugale, Ubungo, Uhasibu, Pangani na Wami ni vielelezo vingine vya kukua kwa uchumi.

Ukiacha hayo, serikali imenunua ndege mpya takribani 9 kati ya 11 hizi zikiwa na lengo la kusafirisha na kuleta mizigo na watalii kutoka nchi zinazoongoza kutalii Tanzania.

Miundombinu hii yote inaufungua uchumi wa Tanzania na kuifanya kuwa nchi shindani kiuchumi barani Afrika.

(3) KIWANGO CHA UHIMILIVU WA NCHI KIUCHUMI ENDAPO ITAKUMBANA NA MAJANGA
Hiki ni kipimo cha mwisho ambacho hutumika kuipandisha nchi kuingia kwenye uchumi wa kati.

Kipimo hiki kinazingatia uwingi wa idadi ya watu (population size), kiwango cha bidhaa kinachosafirishwa, kilimo, misitu, uimara wa mazao na huduma zinazosafirishwa, idadi ya wanaoathirika na majanga ya asili kama Covid 19 na hata kuwa ama kutokuwa na uimara kwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo.

Katika hili tumeona namna Tanzania ilivyoweza kupambana na janga la Covid 19 wakati nchi nyingi za Afrika zikiyumba sana kutokana na janga hilo. Hii inatoa tafsiri ya uwezo wa uchumi kuhimili majanga.

Lakini pia tumeona Tanzania ikizalisha mazao ya chakula kwa wingi kama mahindi kiasi cha kuweza kuziuzia nchi za jirani kama vile Kenya na Zimbabwe hali ambayo inatoa tafsiri ya kuwa nchi ipo imara katika eneo la uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo.

Kwa ujumla Pato la kila mwananchi-GNI, Uwekezaji kwa watu-HAI na Kiwango cha uwezo wa uchumi kuhimili majanga-EVI ndivyo vigezo vinavyotumika kuzipima nchi na kuzipandisha huku GNI kikitumika na Benki ya Dunia kama kigezo kikuu na hivyo kwa kutumia kigezo hicho kilichopimwa kutumia njia ya Atlas Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati.

Umoja wa Mataifa wao hutumia vigezo vyote ambavyo pia vinathibiti kwa Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kama nilivyoainisha hapo juu.

Kuingia huku kwa Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kunatoa tafsiri kuwa Tanzania inaweza kufika mbali sana kiuchumi kama sisi watanzania tutaongeza bidii na maarifa katika kufanya kazi na pia kuwa wazalendo.

Tushangilie ushindi huu kwa kufanya kazi kwa bidii huku tukilinda mafanikio tuliyopata na kuongeza mafanikio mengine zaidi.

Wanabodi,

Uchumi unapimwa kwa vigezo vingi sana lakini vikubwa ni viwili ambayo Benki ya Dunia na IMF wanatumia navyo ni:

GNI(Gross national income) pamoja na GDP(Gross domestic product)

Kwa mujibu wa Taarifa ni kwamba GNI ya Tanzania imeongezeka na kufikia kwenye midhania ya viwango vya Benki ya Dunia ya uchumi wa kati.

GNI ni kitu endelevu

GNI au Gross national Income ni jumla ya mapato yote yanayoingia nchini au yaliyotengenezwa nchini na watu ambao ni Raia wa Tanzania au ambao sio Raia wa Tanzania

Mapato yanayoongelewa kwenye GNI ni kama ifuatavyo:

Haya mapato yanaongeza GNI na kuifanya kuwa kubwa hivyo kufanya Taifa la Tanzania kufikia uchumi wa kati

Foreign Aid au Misaada yote tunayopokea toka kwa wahisani toka nje. Hii misaada inaongezwa kwenye GNI na kuifanya ionekane GNI imeongezeka.

FD's (Foreign direct investment) huu ni uwekezaji wa moja kwa moja toka nje ,Thamani ya uwekazaji huu nayo inaongezwa kufanya GNI iwe kubwa

Pesa za Watanzania waishio nje au Makampuni ya Kitanzania yaliyo nje ya nchi ambazo pesa wanazituma moja kwa moja Tanzania. Hizi pesa nazo zinaongezwa kwenye GNI na kuifanya iwe kubwa.

Riba(Interest) pamoja na hisa ambazo nchi inapokea kwenye uwekezaji mbalimbali kwenye hati fungani za muda mfupi(bills) au hati za muda mrefu(Bonds). Hizi riba na hiza zinaongeza GNI na kuifanya iwe kubwa.

Mapato yafuatayo yanapunguzwa kwenye mahesabu ya GNI na kuifanya GNI kuwa ndogo au Yanaondolewa wakati wa mahesabu ya GNI.

Mapato yote ambayo wawekezaji wa kigeni waliopo Tanzania au Raia wa kigeni kipato wanachokipata Tanzania yanaondolewa kwenye kufanya mahesabu ya GNI.

GDP au Gross domestic product ni thamani ya bidhaa au huduma kwa bei ya soko kwa wakati huo. Hapa zinaongelewa thamani ya bidhaa au huduma zilizozalishwa kwa muda fulani mfano mwaka mmoja,Hizi ni bidhaa za ndani.

Kuna utofauti mwembamba sana kati ya GDP na GNI, GNI inachukua thamani na zile za nje

Benki ya dunia wanachofanya kupima uchumi ni kama ifuatavyo

GNI=GDP+ (Foreign aid,Foreign investment+interest+..............)

Je, GNI ya Tanzania imekua na kutufikisha uchumi wa kati?

Maswali yafuatayo ni muhimu kujua kama kweli tumefika uchumi wa kati

Je, uwekezaji toka nje umeongezeka Tanzania?

Je, mikopo na misaada imeongezeka Tanzania?

Je, uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani umeongezeka Tanzania?

Je, diaspora au watanzania toka nje wanaleta vipato nyumbani?

Katika awamu ya Tano ya JPM ni kweli kuna uwekazaji mkubwa sana kwenye SGR, barabara na sehemu kadhaa. Yote hayo yanaongeza GNI.

Kama Jibu ni ndiyo basi mambo mazuri.

Benki ya dunia wamegawa hivi vipato kwa madaraja matatu.

Low, Middle na High

Kuongezeka kwa GNI au kufika uchumi wa kati siyo kigezo kuwa maisha ya mtu mmoja mmoja yamekuwa mazuri au Nchi yetu siyo maskini.

Qatar ni moja ya nchi yenye GNI kubwa kutokana na visima vya mafuta au oil reserves.

Qatar kidogo GNI yao inafanana na Maisha ya Raia wake

Nchi kama kenya wao wapo uchumi wa kati siku nyingi lakini ni maskini wa kutupwa sana

Naomba tuendelee kujadili kwa lugha rahisi ili kuelimisha wengi juu na maana ya uchumi wa kati.

Nadharia za uchumi hasa GNI na GDP zina mapungufu yake mengi Sana. Mara nyingi nadharia hizi zinashindwa kuhusianisha ukuaji wa uchumi na Maisha ya mtu mmoja mmoja.

Wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia zaidi,Sisi wengine hatujasoma uchumi bali tunaelezea jinsi mambo yalivyo na yanavyofanyika World Benki na IMF

Watanzania wengi wanashangilia hasa wanasiasa sidhani kama wanaelewa maana halisi ya uchumi wa kati kwa hivi vipimo vya GNI vya Benki ya Dunia na IMF

Huu ni ushauri pia umetolewa na Mwana JF ambao nchi zao ziliingia matatizo kwa kufikia uchumi wa kati soma
Tanzania Chungeni mambo ya Eurobond
 
Uchumi wa mtu mmoja mmoja GNI per capital wetu ulikuwa unakuwa kwa kasi kipindi cha JK kati ya 2005-2014 toka GNI per capital 500$ mpaka 970 $ almost 80%. Na umekuwa unakuwa kwa taratibu between 2015-2020 from 970$ mpaka 1020 almost 6%.

Nini maana yake
1. Kipato cha mtanzania kiliongezeka zaidi kipindi cha JK kutokana na kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa Pesa kwenye nchi, kuwezeshwa kwa Private sectors and FDI kuongezeka.

2. Kipindi hicho Uchumi wa mfukoni wa Mtanzania ukiongezeka maradufu kuliko miundo mbinu ya serikali kama barabara , Ofisi za serikali, hospital Na mashule .. miundombinu mingi ilikuwa inategemea misaada hasa barabara Na kupelekea ukuwaji wake kuwa mdogo .msukumo mkubwa ulikuwa kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja huku wakiboresha miundombinu taratibu

3. Sasa alipoingia JPM amepiga U-turn. Now kuna ongezeko kubwa la miundombinu kama barabara, Ujenzi wa hospital, Shule, ununuzi wa ndege , SGR, Umeme Stigla, flyovers, meli, boats vivuko nk nk wakati uchumi wa mtu mmoja mmoja uneeendelea kupungua Na Kwa sasa unakuwa kwa asilimia 0-5% tu Na dalili zinaonyesha utaendelea kushuka na pengine kurudi tena kwenye GNI per capita ya 500 $ in next 5 years kama hatua stahiki hazitachukuliwa.

Nini Kifanyike:
1. Kuwa na uwiano wa kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na miundombinu ya Taifa, lazima vitu hivi vi balance ili twende pamoja.

2. Tunapoingia kwenye MIC tutegemeee kupungua kwa misaada, kwa hivyo ni lazima budget na vipaumbele vyetu vilenge pia kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuboresha upatikanaji wa huduma kama maji, chakula, dawa na umeme, ama sivyo kama mwelekeo unaoendelea wa sasa. Upo uwezekano wa huduma muhimu kama Afya, maji na umeme na hata chakula kuzorota wakati miundo mbinu kama barabara, miji mikuu, majengo kuimarika.

Kupanga ni kuchagua.

Adjustments.JPG
Adjustments.JPG
 
Wanabodi saalam!

Nchi imefikia uchumi wa kati kabla ya 2025, hii ina maana kasi yake ni kubwa sana.

Wamezingatia nini hata kutuweka hapo? Na je, ukuaji huu unaenda na maisha ya Mtanzania mmoja mmoja?

Maana huku mitaani hali ni mbaya kupitiliza huu uchumi kukua kunaangaliwaje!

Sina data kamili, lakini nakumbuka hawa hawa WB, walishaonesha kuwa toka 2016 uchumi wetu umeshuka toka 7.% uliokuwapo 2015 (mwenye kumbukumbu aniwekee)

Leo hii tumepanda mpaka uchumi wa kati! Nina shaka na hao wawakilishi wa WB waishio Tanzania. Kuna kamchezo kanachezwa kati ya serikali na hao. Muda utaongea.

CC: Pascal Mayalla, Mzalendo no2, na wengine. Leo mabebaru wapo upande wenu, nimeona comment ya mtu mmoja anasubiri tamko la IFM.

LEO MABEBERU WATAMU SANA
 
Tz iliingia huko toka 2018.Walingoja tuwe stable ndipo tutangazwe. Hata hiyo per capita ya mwanzo ili uwe middle income ($1036) tushaivuka. Sasa hivi tunasoma kwenye $1080 hivi!
 
Kwa huu uongo basi mabeberu naanza kuwapiga vita Tz ninchi maskini yakutupwa haina mbele wala nyuma watu wenye maisha mazuri niwabunge tu na marais na wanasiasa kwa ujumla ila siyo waananchi.
 
Very good analysis lakini pia utulivu,amani,ulinzi na usalama umechangia sana kufikia ngazi ya uchumi wa kati.jiografia ya nchi,uongozi bora na madhubuti, mapambano dhidi ya rushwa,ufisadi, ubadhirifu, mabadilko ya fikra kwa kuwekeza kwenye weledi,ubunifu na kufanya kazi kwa bidii, sera nzuri za fedha na uchumi/kodi, Mifumo ya TEHAMA kukusanya kodi na tozo mbalimbali nazo zimechangia kutufikisha hapo ikiwemo lugha moja ya kiswahili nchi nzima na matumizi mazuri ya raslimali za nchi.Kimsingi tumefika hapa kwa mchanganyiko wa vichocheo vingi zaidi ya vigezo rasmi vya Bretton institutions. Tuna nafasi ya kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu (Higher middle income country )ifikapo 2030 ili mradi tumekwishaingia kwenye ngazi hiyo, tukitumia vizuri raslimali zetu kwa uadilifu na umakini mkubwa.Anyway Mungu Mkubwa. Mungu Aibariki Tanzania. Mungu Ambariki Rais JPM amwongezee maisha,ujasiri,maono na uzalendo wa kuipenda nchi kwa Maslahi ya Taifa.Amen
 
Kama Rais Magufuli ameweza kutupeleka uchumi wa kati kwa miaka mitano tu ndani ya muda mfupi tutamfikia USA
 
Kama Rais Magufuli ameweza kutupeleka uchumi wa kati kwa miaka mitano tu basi haitachukua muda kumfikia USA

Hongera Magufuli
 
Wanabodi saalam!
Nchi imefikia uchumi wa kati kabla ya 2025, hii inamaana kasi yake ni kubwa sana

Wamezingatia nini hata kutuweka hapo, na je ukuaji huu unaenda na maisha ya mtanzania mmoja mmoja?

Maana huku mitaani hali ni mbaya kupitiliza huu uchumi kukua kunaangaliwaje!!

Sina data kamili, lakini nakumbuka hawa hawa WB, walishaonesha kuwa toka 2016 uchumi wetu umeshuka toka 7.% uliokuwapo 2015 (mwenye kumbukumbu aniwekee)

Leo hii tumepanda mpaka uchumi wa kati!!!
Ninashaka na hao wawakilishi wa WB waishio Tanzania
Kuna kamchezo kanachezwa kati ya serikali na hao. Muda utaongea

Haya,cc p mayalla, mzalendo no2, na wengine,leo mabebaru wapo upande wenu,nimeona comment ya mtu mmoja anasubiri tamko la Ifm.
LEO MABEBERU WATAMU SANA!!!
Mjinga mpe ukubwa ili ushibishe njaa.
Njia pekee ya kutaka wakitakacho ni kuendana na step
 
Anyway,labda hamna nchi iliyomo tena katika hilo kundi.

Na hii je?

Cha msingi ni kujiuliza tumepanda kwa kiasi gani kwa muda wote huu kufikia hatua tuliyopo sasa na sio kupiga mapambio tu.

1593674465859.png
 
mchumi na mwana sheria wapi na wapi?! huyu mama ni mwana siasa au ni mchumi au ni mwanasheria?! mbona huwa simwelewi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom