Nchimbi: Uhusiano wa Tanzania na Urusi kuboreshwa kunufaisha pande zote

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
IMG-20240222-WA0015.jpg

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa CCM, chini ya Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kudumisha uhusiano na urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi, ukilenga kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.
IMG-20240222-WA0017.jpg

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, ambapo amesisitiza kuwa kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kutaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake na kuufanya kuwa wa moja kwa moja zaidi.
IMG-20240222-WA0018.jpg

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Alhamis, Februari 23, 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, pamoja na kurejea kumbukumbu za uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Urusi, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambao mwaka huu unafikisha miaka 62, walizungumzia maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa kazi na Serikali za nchi hizo, chini ya uongozi wa vyama vinavyoongoza nchi hizo, Chama Cha Mapinduzi na United Russia, mtawalia.
IMG-20240222-WA0016.jpg

Kwa upande wake, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, mbali ya kumpongeza na kumtakia kila la heri Balozi Dk. Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, ameelezea uhusiano wa muda mrefu wa Urusi kwa Tanzania na nchi za Afrika, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambapo ilikuwa mojawapo ya nchi za mwanzo kuitambua Tanganyika huru, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Vladimir Vladimirovich Putin, na mazingira mazuri ya uwekezaji, biashara na uchumi ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Urusi iko tayari kuendelea kuenzi na kuimarisha uhusiano utakaonufaisha pande zote mbili.
 
WhatsApp Image 2024-02-22 at 16.22.02 (1).jpeg

Si tayari tumeshaolewa?
Au Urusi anataka kuwa mchepuko?
 
Nchi inayoishi kwa kusaidiwa kama Tanzania, Urusi haina msaada wowote kwa sababu na yenyewe ipo kwenye uchumi unaochechemea, huku wataalam wake wengi wakiwa wameikimbia nchi yao na kwenda nchi za Ulaya Magharibi na America kutafuta maisha.

Russia's Future Is Bleak

The breakup of the Russian Federation may seem to be a remote possibility, but a survey of “global strategists and practitioners” conducted by the Atlantic Council showed that a surprising 46 percent of the 167 persons who participated (including 49 percent of Europeans) expected Russia to become a failed state in the next ten years. Forty percent expected Russia “to break up internally for reasons including but not limited to revolution, civil war, or political disintegration.” Other analysts agree that Russia's decline is irreversible, but that first Russia might lurch into a dangerous fascist phase or even civil war before outright disintegration. Such declines would pose new sets of headaches for NATO and, in particular, its frontline states. For now, these scenarios remain in the arena of speculation. A failed state with thousands of nuclear warheads would be a dangerous combination.
 
Ila wewe jamaa jinga sana
 
CCM inaomba msaada wa urus kusaidiwa kwenye maswala ya kuisaidi serikali isiangushwe, kwa mujibu wa taarifa za kijasusi urus imekuwa ikizisaidia viongozi wa Afrika kuwalinda wasiondolewe madarakani kwa malipo ya kupewa rasilimali.
 
Back
Top Bottom