Tanga: Mkuu wa Mkoa awasimamisha kazi watumishi 4 Halmashauri ya Muheza, ubadhirifu na utendaji mbovu vyatajwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waliosimamishwa ni Ramadhani Mtingi (Idara ya ujenzi), Zainabu Mzindakaya (Mweka Hazina wa Halmashauri), Furaha Sarakikya (Idara ya Manunuzi) na Serapion Basgange (Afisa Elimu Sekondari).

Mkuu wa Mkoa Omary Mgumba amewatuhumu watumishi hao kutumia vibaya Fedha za Serikali na Usimamizi Mbovu wa Miradi ya Maendeleo na kuagiza TAKUKURU na CAG kuwahoji na kufanya ukaguzi wa miaka 3 wilayani Muheza.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kusimamishwa kazi na Waziri Innocent Bashungwa kwa utendaji usioridhisha.

========================

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ameagiza kusimamishwa kazi watumishi wanne wa Halmashauri ya Muheza kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo. Pia, ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuwahoji watumishi hao.

Mgumba ametoa maagizo hayo leo Jumatano Oktoba 19, 2022 wakati wa ziara yake wilayani Muheza ya kukagua miradi ya maendeleo.

Kusimamishwa kwa watumishi hao kumekuja ikiwa ni mwezi mmoja na siku 19 kupita tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nassib Mmbaga kusimamishwa kazi na aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo na utendaji kazi usioridhisha.

Watumishi hao waliosimamishwa ni Ramadhani Mtingi (Idara ya ujenzi), Zainabu Mzindakaya, Mweka hazina wa Halmashauri (DT), Furaha Sarakikya Idara ya Manunuzi na Ofisa Elimu Sekondari, Serapion Basgange "Tunaanzia na hawa wa nne na wengine kadri ninavyopata taarifa nitatoka na maelekezo na hawa sio wasimame kupisha uchunguzi maalumu lakini pia Takukuru uanze kuhangaika nao" ameagiza Mgumba

Pia, ameagiza Mkazi wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi maalumu kwa miaka mitatu mfululizo katika miradi yote ya maendeleo Wilayani humo. Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Zainab Bakari amesema kuwa amepokea maelekezo hayo akiahidi kuyatekeleza.

Mwananchi.
 
Kuwaonea, mbona Idara ya ardhi hakuigusa wakati huko ndiko uozo uliokolea wa Rushwa
 
Kuna surnames mbili hapo juu zipo very familiar, watoto hawa wameshindwa kuheshimu ubini wenye heshima, but ni still suspects siwezi kuwaambia chochote hadi court of law iamue kwanza
 
Back
Top Bottom