RC Mbeya asitisha Posho kwa Watumishi wote wa Halmashauri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesitisha utoaji wa posho kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani isipokuwa madiwani na kutaka zikatumike kukamilisha ujenzi wa shule tano za msingi ambazo miradi yake imeonyesha kusuasua.

Homera ametoa agizo hilo jana Septemba 22, 2023 baada ya kutorishiwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ilipokea fedha kutoka Serikali hali iliyosababisha kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi watumishi wanane wakiwemo walimu wakuu watano, wahandisi wawili na ofisa manunuzi.

“Ile asilimia 40 inayokwenda kwenye maendeleo na ile nyingine 60 za posho kuanzia sasa hazitatolewa kwa watumishi na badala yake zitaelekezwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya elimu isipokuwa madiwani pekee walipwe posho zao,”amesema.

Amesema katika asilimia hizo zinazotolewa na halmashauri kwa sasa watakaopata ni madiwani pekee lakini kwa upande wa watumishi zimesitishwa mpaka hapo miradi ya elimu itakapokamilika na wanafunzi kuanza kupata huduma.

Aidha ameagiza watumishi wote ambao wako kwenye kamati za ujenzi kutokusafiri kwenda nje ya mkoa mpaka hapo miradi hiyo itakapo kamilika katika Shule za Kasumuru, Mapinduzi, Luteba, Uhuru na Mababu Wilaya ya Kyela.

“Ndugu zangu tumuonee huruma huyu mama Rais Samia Suluhu Hassan anapotafuta pesa na kuleta lengo lake kuleta maendeleo kwa wananchi na kuboresha sekta ya elimu sasa inapofika halmashauri zote zikamilishe miradi mwezi June nyie mpaka sasa haijakamilika,” amesema.

MWANANCHI
 
Amekosea kesho yatamrudia yeye.Nashauri atumbuliwe yeye kwanza.
Anakamata wasanii kisa Nini.Ajitafakari.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Ni kwel kabisa sema uonevu tu.
Huu ni uonevu kwa Watumishi maana fedha za ujenzi wa madarasa kwa vyovyote vile zilitengwa kwenye bajeti na hazina uhusiano na posho za watumishi.

Nadhani Mh. Mkuu wa Mkoa atafakari upya agizo lake. Mambo kama haya hushusha sana morali ya kazi kwa watumishi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesitisha utoaji wa posho kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani isipokuwa madiwani na kutaka zikatumike kukamilisha ujenzi wa shule tano za msingi ambazo miradi yake imeonyesha kusuasua.

Homera ametoa agizo hilo jana Septemba 22, 2023 baada ya kutorishiwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ilipokea fedha kutoka Serikali hali iliyosababisha kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi watumishi wanane wakiwemo walimu wakuu watano, wahandisi wawili na ofisa manunuzi.

“Ile asilimia 40 inayokwenda kwenye maendeleo na ile nyingine 60 za posho kuanzia sasa hazitatolewa kwa watumishi na badala yake zitaelekezwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya elimu isipokuwa madiwani pekee walipwe posho zao,”amesema.

Amesema katika asilimia hizo zinazotolewa na halmashauri kwa sasa watakaopata ni madiwani pekee lakini kwa upande wa watumishi zimesitishwa mpaka hapo miradi ya elimu itakapokamilika na wanafunzi kuanza kupata huduma.

Aidha ameagiza watumishi wote ambao wako kwenye kamati za ujenzi kutokusafiri kwenda nje ya mkoa mpaka hapo miradi hiyo itakapo kamilika katika Shule za Kasumuru, Mapinduzi, Luteba, Uhuru na Mababu Wilaya ya Kyela.

“Ndugu zangu tumuonee huruma huyu mama Rais Samia Suluhu Hassan anapotafuta pesa na kuleta lengo lake kuleta maendeleo kwa wananchi na kuboresha sekta ya elimu sasa inapofika halmashauri zote zikamilishe miradi mwezi June nyie mpaka sasa haijakamilika,” amesema.

MWANANCHI
Kama nani?katibu mkuu utumishi au nani sasa ?hizo posho ni hisani au zipo kisheria na huyo RC ametoa wapi mamlaka makubwa hivyo ya kuondoa posho za watumishi
 
Sema miungu watu kila mtu kwa nafasi yake hata hao Walimu wakuu nao ni wakuda kwenye usimamizi wa hizo fedha
 
Back
Top Bottom