Watumishi wa Afya wasimamishwa kazi kwa kutofanya usafi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Ugalla kilichopo Kata ya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi baada ya kushindwa kufanya usafi katika maeneo ya hospitali.

Watumishi hao wamesimamishwa kazi leo Februari 16, 2024, ili kupisha uchunguzi kutokana na uzembe walioufanya wa kukitelekeza kituo hicho baada ya kufanya ziara na kukuta hali isiyoridhisha katika kituo hicho ambacho kimejaa nyasi na kutopata majibu ya kuridhisha.

Waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Nsimbo, Ofisa Manunuzi, Ofisa Tarafa, Mtendaji wa Kata ya Ugalla, Mtendaji wa Kijiji, na wengine watakaobainika kuhusika.

“Mmenileta hapa ili nipongeze kwamba mnafanya kazi nzuri? Au mlitegemea hapa mimi nije nifanye nini? na sasa hivi mnasema tupe masaa sijui mangapi tufanye usafi, wanini? wananchi wanaokaa huku ndiyo wanapaswa wafanyiwe usafi sio usafi ufanywe kwa ajili yangu mimi,” amesema Mrindoko.

Aidha, amesema sio sahihi kwa wananchi wanaoishi eneo hilo kukutana na nyasi katika kituo hicho cha afya kilichofanywa nyumba ya wadudu kama mchwa na wengine.

Source: Habari Leo
 
The higher the cheo the high kutumbukiwa.

Nawasikitikia Veo na weo kama walikuwa hawaivi na bwana diwani wataliwa vichwa mazima.

Afisa tarafa atachomoka mapema, atayajenga na DAS Kisha RAS na DAS wanamrudisha.

Afisa manunuzi kama alikuwa anawazunguka maboss kwenye chenji nae wanamla kichwa. Lakini kama alikuwa kinara wa kuwapa cross wakubwa watampambania kama mtoto wao.

DMO wakimchomoa, kama amethibitishwa ataondoka na LSSE yake kwenda kuhudumia watu hospital ya mkoa au kuwa mkufunzi vyuo vya afya au wizarani.

Nawalilia VEO na WEO Kuna mmoja ataangushiwa zigo Kwa kusilibwa na diwani.
 
Nani atatibu wagonjwa
Jibu la swali hilo jipatie mwemyewe kwa kujiiuliza: je kama radi ingelitokea ikawafyeka wote hao, nani angelitibu wagonjwa?

Ukiwa mtumishi wa serikali hautegemewi, bali wewe ndiye unayeitegemea Serikali kwa mishahara inayokulipa.

Ukiamua kutoroka ama kufukuzika ni sawa na kuchota kikombe cha maji ya bahari ukadhani kuna kutetereka kwa ujazo!
 
Back
Top Bottom