Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waaswa Kufanya Kazi kwa Kushirikiana

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,175
1,028

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waaswa Kufanya Kazi kwa Kushirikiana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza makundi.

Ametoa rai hiyo Mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili Taarifa ya Bajeti ya 2023-2024 ya Ofisi hiyo.

Waziri Mhagama alisema, Kuna kila sababu ya kufanya maamuzi ya pamoja ya ushirikishwaji ili kuweza kupata mafanikio kwenye idara na vitengo, kama viongozi wenu wanavyofanya kazi vizuri kwa kushirikiana.

Aliendelea kusema kuwa hata kama inafikia wakati Mtendaji hayupo kwenye Idara au kitengo kuwe kuna Mtu anayeweza kufanya kazi kwa viwango na uwezo huo huo ili mambo yaweze kwenda vizuri.

“Tukifanya kazi kwa umoja na ushirikiano tukifanikiwa tuwe tumefanikiwa wote na tukianguka tujue tumeanguka wote na tujipange ili kujua sababu ya kuanguka na tuweze kujipanga." Alibainisha.

Aidha, Waziri Mhagama alisema anafarijika na utendaji wa kitaasisi na kuwaomba watumishi kuendelea kuimarisha utendaji wa kitaasisi ambao unatoa fursa kwa kila mtu kuwa ni sehemu ya mafanikio na ufanisi wa taasisi.

“Wale ambao Mnamadaraka kwenye Idara Vitengo au Taasisi zetu Muhakikishe Mnajenga moyo wa kukuza watumishi walio chini yenu, kwa kuwapa fursa ya kukua kielimu ndani ya ofisi, kukua kiujuzi na kukua kiubobezi." Alihimiza.

Alibainisha kuwa Watumishi wa umma ni rasilimali muhimu, ya kuendesha rasilimali nyingine na kusema kuwa ni lazima tuiratibu vizuri Rasilimali hiyi na kuilinda kwa nguvu zote ili kuweza kupata mafanikio tuliyoyakusudia.

Waziri alisema; Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa aliwahi kusema,” jambo muhimu kwa mfanyakazi si muda anaotumia kufanya kazi,bali kiasi cha kazi anachoweza kufanya katika muda aliopewa."

Alisema Kuna kila sababu ya kuanzaa kujipima wenyewe hasa katika kuelekea kuanza mwaka 2024, ili kujua kiasi cha kazi tuliyoifanya na ufanisi wake kila siku anayoshiriki kama mtumishi wa umma katika ofisi ya waziri Mkuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, amesema vikao vya wafanyakazi ni tamko la kisheria ambalo chimbuko lake ni Hayati Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Rais wa awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa katika tamko no 1 la mwaka 1970 linalohimiza ushirikishwaji kupitia Baraza la wafanyakazi.

"Baraza ni kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na Menejimenti na Ofisi ya Waziri Mkuu, tutaendele kuwa vikao hivi vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu ya miongozo.

Awali akitoa salamu Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa ameipongeza Menejimenti ya Ofisi ya Maziri Mkuu, kwa kutekele za Sera ya ushrikishwaji kikamilifu,

Chama cha wafanyakazi kinaamini hakuna haki bila wajibu, tunaangalia namna tunavyopata haki na namna ambavyo tunatekeleza wajibu katika kuhakikisha mipango iliyopangwa inakamilika sawasawa.
 

Attachments

  • 36e7b08cb3aea00bea4018475cecfda3.jpg
    36e7b08cb3aea00bea4018475cecfda3.jpg
    111.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom